TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, February 1, 2014

Manji awawakia wanaomuandama Seif Magari

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewaonya wanachama na mashabiki wa timu hiyo wanaotishia maisha Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya imataifa wa klabu hiyo, Seif “Magari” Ahmed kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.

Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Manji amesema kuwa si suala jema kwa wanachama kumuhusisha Seif na matokeo ya timu hiyo ambayo kwa sasa imeshinda mechi moja na kutoka sare mechi moja katika mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya Tanzania Bara.
 
Manji amesema kuwa madai kuwa Seif siyo mwanachama halali  wa Yanga hayana msingi wowote na kuyaita madai hayo kuwa ni ya uzushi na yanaenezwa na maadui zao ambao hawaitakii Yanga mema.
Alisema kuwa hivi karibuni kumekuwa na madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu, taarifa za hujuma ndani ya timu ambazo zimewahusisha uongozi na baadhi ya wanachama jambo ambalo si la kweli.
Alifafanua kuwa ni haki kwa kwa nia njema kwa wanachama kuhoji mwenendo wa timu yao pale wanapoona-hairidhishi na ni wajibu wa wanachama kuchanganua mawazo merna na mabaya na siyo kumuhisha mtu kwa moja kwa moja kutokana na mtazamo hasi walionao.
 
“Ushindi au mwenendo mzuri  wa timu unatokana na viwango vizuri, nidhamu na ushirikiano wa wahusika wote, wachezaji, walimu, viongozi, wanachama na wapenzi kwa ujumla. Uongozi ulikutana na wachezaji, walimu, baadhi ya wanachama na wapenzi na kuyazungumzia na kukubaliana kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa wahusika wote na kuchukua hatua ya kubadilisha benchi la ufundi,” alisema Manji.
 
Aliongeza kwa kusema kuwa uongozi ulifika mbali zaid kwa kutoa adhabu na onyo kali kwa baadhi ya wachezaji walionyesha utovu wa nidhamu kwa kipindi kilichopita na kusikitishwa kuona kuwa baadhi ya wadau kwa kutumia vyombo vya habari wanachochea na kutengeneza uhasama ambao kwa kweli haupo ama kwa faida zao binafsiau kwa kutumiwa na watu ambao hawana nia njema kwa klabu.
Manji pia aliwaomba wadau wote wanamichezo na hasa wahariri wa michezo kudhibiti matumizi mabaya ya watu au vyombo vya habari yanayochangia sana kuzorotesha michezo nchini.

No comments:

Post a Comment