Katibu
 Mtendaji wa  Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk 
Suleiman (kushoto) . akifafanua jambo  kuhusu  filamu  ya  MV spice 
 Islander. Kulia ni Katibu  Mtendaji  wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce 
 Fissoo. 

Katibu 
 Mtendaji  wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce  Fissoo(kulia) akifafanua 
jambo  kuhusu  filamu  ya  MV spice  Islander . Kushoto ni Katibu 
Mtendaji wa  Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk 
Suleiman  . 
 
 
Katibu 
 Mtendaji  wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce  Fissoo(kushoto) akipeana 
mkono na Mwakilishi wa kampuni ya kutengeneza filamu  ya  Steps,  Moses 
 Mwanyilo (kulia).Katibu Mtendaji wa  Bodi ya Sensa ya Filamu ya 
Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman (kushoto) akipeana mkono  kulia 
Mwakilishi wa kampuni ya kutengeneza filamu  ya  Steps,  Moses  
Mwanyilo. 
(Picha na Magreth Kinabo)
………………………………………………………………………………
Na Magreth  Kinabo – Maelezo
 Viongozi
  wa Bodi za Filamu  wa Tanzania Bara na Zanzibar wametoa ushauri  kwa 
wasanii nchini  kuacha kutumia majanga halisi kwa ajili ya kutengenezea 
filamu Kibiashara.
Kauli
 hiyo imetolewa jana na viongozi  hao , wakati wa kikao cha  kati ya 
 Katibu  Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce  Fissoo  na  Bodi ya
 Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman  na Mwakilishi 
wa kampuni ya kutengeneza filamu ya Steps,  Moses  Mwanyilo 
 kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Akizungumza
 katika kikao hicho, Bi.Fissoo   alisema  kampuni hiyo imetengeneza 
 filamu  ya  MV Spice  Islander kwa  kuchukua picha halisi za ajali ya  
MV spice,ambayo iliwasilishwa katika ofisi yake Novemba 2013 kitendo 
ambacho ni kinyume na sheria , taratibu na kanuni  za utengenezaji wa 
filamu.
Alisema
 filamu hiyo ilichukua picha halisi ya ajali hiyo, hivyo ofisi yake 
ilimwandikia barua mtengenezaji huyo kuwa ibadilishwe, lakini aliomba 
ashiriki kikao na bodi. Hata hivyo aliitwa mara nne kwa ajili ya kikao 
na bodi hiyo  lakini hakushiriki  badala yake alileta marekebisho ya 
 filamu hiyo mara tano ambayo bado yalikuwa na kasoro hizo. 
 Naye
 Bw. Suleiman    alisema filamu hiyo ni muhimu . Hivyo alimtaka 
mtengenezaji huyo kutoingilia uhuru wa mtu, jamii na Serikali na kutaka 
filamu hiyo ifanyiwe marekebisho, hivyo ni vema wasanii wakawa wabunifu 
kutengeneza  filamu zinazogusa  bila kutumia  uhalisia wa janga na 
majina halisi.   
Aliipongeza
 bodi ya filamu  ya Bara kwa ushirikiano waliouonesha kwa kuwa filamu 
ikataliwa Zanzibar na Bara inakataliwa kwani  kazi kama hiyo 
iliwasilishwa Zanzibar na ilikataliwa kwa kuwa ajali iliyotokea si 
sherehe, bali itatonesha  vidonda vya watu walioathirika.
Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni hiyo alikiri kosa hilo na aliahidi kufanya marekebisho katika filamu hiyo.

No comments:
Post a Comment