TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, September 24, 2014

ARTEL YATOA VITABU KWA SHULE YA SEKONDARI SHIBULA MWANZA.

DSC05496[1] Meneja Airtel Kanda ya Ziwa Raphael Daudi (Kushoto) na Afisa
  Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Juma Kasandiko
  wakiwa wameshikilia kitabu baada ya  makabidhiano ya vitabu vya shule   ya Sekondari Shibula vyenye thamani ya shilingi millioni moja na nusu   vilivyotolewa na Airtel chini ya mpango wake wa Airtel Shule yetu.
DSC05493[1]Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Juma
  Kasandiko (kulia)  akimkabithi vitabu  mkuu wa shule ya shule ya
  Sekondari Shibula James Chisanda vilivyotolewa na Airtel chini ya
  mpango wake wa Airtel Shule yetu,
DSC05501[1]
DSC05502[1]Waalimu wa shule ya Sekondari Shibula wakifurahia vitabu mara baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Airte kukabithi vitabu hivyo chini ya mpango wake wa  Airtel shule yetu ambapo shule hiyo imepokea   vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi millioni moja   na Laki tano DSC05505[1]Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shibula wakifurahia vitabu vya
  sayansi walivyokabidhiwa na Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel,
chini ya mpango wa Airtel  shule yetu Airtel ilikabithi vitabuvya sayansi vyenye thamani ya shilingi millioni moja na nusu kwa shule hiyo DSC05418[1] DSC05419[1]Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shibula wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa halfa ya kupokea msaada wa vitabu kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Press Release
  Airtel yatoa vitabu kwa shule ya sekondari Shibula Mwanza
  Mwanza, Jumanne 23 Septemba 2014, Wanafunzi wa shule ya sekondari
Shibula iliyoko Mkoani Mwanza wamefaidika na vitabu kupitia mradi wa
  Airtel shule yetu  ambapo Airtel imetoa msaaada wa vitabu vya sayansi
  vyenye thamani ya shilingi milioni moja na Laki tano
  vitakavyowawezesha wanafunzi hao  kupata elimu bora.
  Kwa zaidi ya miaka 10 sasa mpango huu wa Airtel shule yetu umekuwa
ukisaidia  shule za sekondari kwa kuwapatia nyenzo muhimu kma vile vitabu, vifaa za kufundishia , madawati, kuboresha majengo ya shule
  lengo likiwa ni kuboresha ubora katika kutoa  elimu nchini.
  Akiongea wakati wa hafla ya kikuabithi vitabu Meneja Mauzo wa Airtel
kanda ya Ziwa Bwana Raphael Daudi alisema “ Airtel imewekeza kiasi cha   kutosha katika kusaidia malengo mkakatika katika sekta ya elimu kwa   kushirikiana na serikali katika kutoa elimu bora. Kwa kupitia mradi wa   Airtel Shule yetu tumeweza kuzifikia shule zaidi ya 1000 zilizoko   katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuwapatia vifaa vya kujisomea na kupunguza changamoto za uhaba wa vitabu huku tukifanikiwa  kupunguza   uwiano wa kitabu kwa mtoto kutoka  watoto 6 kwa kitabu kimoja hadi   watoto 2 kwa  kitabu kimoja.
  Leo tunatoa vitabu vya  masomo ya sayansi ikiwemo Hisabati Fizikia,
  Kemia na Baiologia kwa shule ya Shibula sekondari tukiamini utachangia  katika kuongeza kiasi cha ufaulu na kuchochea wanafunzi wengi kujiunga   na masomo ya sayansi. Tutaendelea na jitihada hizi katika kuboresha   sekta ya elimu na kuhakikisha tunazifikia shule nyingi zaidi nchini   aliongeza Daudi. 
 
  Kwa upande wake  Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemema Mkoani
Mwanza Juma Kasandiko ameishukuru Airtel kwa msaada wa vitabu kwa
  shule za sekondari zilizoko mwanza na kuwaasa wanafunzi kutumia muda   wao kujisomea na kuacha tabia ya utoro shuleni na kwa kufanya hivyo   kutasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo na Mwanza kwa  ujumla.
  Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Shibula Bwana   James Elias Chitanda alisema” Napenda kuwashukuru Airtel kwa kutoletea   msaada huu wa vitabu shule ni hapa, vitabu ni nyenzo muhimu katika   kuongeza maarifa na ujuzi hivyo vitabu hivi vitasaidia kuhamasisha   wanafunzi wengi kujisomea  na  kuongeza upeo, vitawasadia walimu   kuandaa masomo yao na kuwahamasisha wanafunzi wengi kujiunga na masomo   ya sayansi na kuongeza idadi ya wanasayansi  kwa ujumla.Tunatoa wito   kwa makampuni mengine kujiunga na kuchangia katika sekta ya elimu
  kwani ina mahitaji na changamoto nyingi.

No comments:

Post a Comment