TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, September 21, 2014

WATOTO ZAIDI YA WANNE KATIKA MANSPAA YA ILALA IMESADIKIWA KUFANYIWA VITENDO VYA KIKATILI JIJINI DAR ES SALAAM

Picha ya maktaba, Mtoto akionekana  akinusa harufu nzuri ya ua, Watoto wapo katika hatari ya kufanyiwa ukatili na watu wenye tabia mbaya hivyo wanapaswa kulindwa kwa kila namna ili kuepukana na vitendo hivyo.

KILA siku wastani wa watoto watano wananajisiwa katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kaimu Katibu Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Gladnes Munuo alisema hayo jijini hapa juzi wakati wa uzinduzi wa ripoti ya pili ya utafiti kuhusu unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.

Alisema kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Willy Sangu ubakaji ulipungua mwaka 2013 lakini katika robo ya kwanza ya mwaka 2014 uliongezeka ambapo idadi ya waliohudumiwa katika hospitali ya Amana baada ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia ni 310.

Alisema kwa mujibu wa Ofisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha ‘One Stop Centre’ kilichopo katika hospitali hiyo, Eva Mbilinyi vitendo vya ubakaji vipo kwa kiwango cha juu hali inayodhihirishwa na takwimu za wanaohudumiwa katika kituo hicho.

Alisema tangu kituo hicho kizinduliwe mwaka jana kimepokea matukio 253 ya unyanyasaji wa kijinsia ambapo kesi 35 zilifikishwa mahakamani hadi Juni 10.

No comments:

Post a Comment