Shuhuda
 aliyenusurika kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote 
miwili, Mariam Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya 
meza na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya 
kimataifa ya amani iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam 
kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu
Mwanamke
 albino Mariam Stanford aliyepoteza mikono yake yote miwili wakati 
iliponyofolewa na majahili asiowajua Oktona7, 2008 ameitaka serikali 
kuwanyonga wote wanaopatikana na hatia ya kuua albino nchini.
Alisema
 hata adhabu ya kifungo cha maisha haiwatoshi kwa jinsi wanavyosababisha
 maisha ya mashaka na yenye uchungu kwa walemavu wa ngozi.
Akiongea
 kwa uchungu huku hapa na pale akitulia kwa kuzidiwa na machozi kiasi 
cha kushidwa kuzungumza Stanford ambaye alisema wakati akikatwa mikono 
yake alikuwa na mimba ya miezi mitano na ambayo ilitoka alisema majahili
 hao si wa kusamehewa.
 
Alisema akiwa mama wa familia kitendo cha kumuondolea mikono yake 
kimemfanya kuwa tegemezi hali ambayo inaongeza maumivu juu ya maumivu 
ambayo anayo ya kunyanyapaliwa na jamii.
Alisema
 hayo wakati akitoa ushuhuda katika adhimisho la siku ya amani duniani 
iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es 
Salaam.
Alisema
 japokuwa Tanzania inaelezwa kuwa nchi ya amani wananchi wake wenye 
ulemavu wa albino hawana amani kutokana na kuwindwa kama digidigi. 
Alisema kwa sasa Tanzania ni kisiwa cha matatzio kwa kundi hilo ambalo 
sasa linajificha na wala kutokujua kesho ikoje au siku hiyo ikoje.
Mke
 wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, akilia kwa uchungu baada 
ya kusikia shuhuda kutoka kwa mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa 
mikono yote miwili, Mariam Stanford (hayupo pichani) ambaye hadi sasa 
anapewa matunzo na Shirika la Under The Same Sun.
Alisema
 ni vyema jamii ikawatazama na kuwasaidia kwa kuhakikisha kwamba 
wanasaidia kuwafichua watenda maovu hao hasa ikizingatiwa kwamba watu 
wenye albinizimu ni watu na watu kama watu wengine na hawawezi kuwa 
chanzo cha utajiri kwa binadamu wenzao.
Alisema
 anatamani kuona waliotiwa hatiani wakiuuawa hadharani au hata watu hao 
nao kukatwa viungo vyao ili watambue jinsi isivyofaa kuwafanyia binadamu
 wenzao matendo hayo.
Alishukuru
 taasisi ya Under the Same Sun kwa kumsaidia toka aliponyofolewa mikono 
mpaka leo na kuhimiza serikali kuona namna ya kuwasaidia waliokatwa 
viungo vyao ili waweze kusihi maisha ya kawaida.
Mkurugenzi
 Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akimfariji mke
 wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, wakati wa maadhimisho ya 
siku ya kimataifa ya amani duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi
 mmoja hivi karibuni jijini Dar.
Pamoja
 na kuomba watu hao wanyongwe Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali George 
Masaju aliitaka jamii kutambua kwamba sheria ya kuua anayeua ipo lakini 
inakabiliwa na mashindano na wanaharakati huku watoa ushahidi 
wakishindwa kuisaidia mahakama kufikia maamuzi katika kesi za maalbino.
Alisema ni wajibu wa wananchi kusimamia amani kwa kuhakikisha wanaisaidia serikali kutekeleza wajibu wake.
Balozi
 wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu akisoma ujumbe kwa niaba 
wa umoja wa mabalozi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani 
duniani.
Naye 
Balozi wa Uturuki nchini alisema kwamba Ali Davutoglu amesema kwamba 
ujenzi wa kituo cha maalbino Bagamoyo utaanza hivi karibuni ili 
kuwapatia nafasi wananchi hao kuwa katika hali ya kawaida.
Kituo hicho ambacho kitakuwa na uwezo wa kuchukua watu 500 na kuwa chemchem ya maarifa kwa watu wenye albinizimu.
Katika
 adhimisho hilo watoto wenye albuinizim walitoa shoo ya nguvu 
iliyowafanya watu mbalimbali kujimwayamwaya katika eneo la wazi na kutoa
 zawadi kwa vijana hao.
Aidha
 bendi ya vijana ilitumbuiza na kwaya ilikuwepo kutoa ushaiwishi wa 
kuelewa umuhimu wa amani huku wazungumzaji wengine wakitaka wanasiasa 
kuhudhura maadhimisho hayo na kupeleka ujumbe kwa wananchi ambao 
wanawasikiliza.
Katika
 adhimisho hilo wanasiasa waliokuwepo ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa dar 
es salaam, Madabida, Kaimu katibu Mkuu NCCR-Mageuzi Faustin Sungura na 
Naibu katibu mkuu CUF Magdalena Hamis Sakaya ambaye pia ni mbunge wa 
viti maalumu Tabora.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Masaju, akizungumza kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar.
Mgeni
 rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya 
na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid (wa pili kushoto), Mratibu Mkazi wa 
mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la 
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia), Makamu 
Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi, kwenye 
picha ya pamoja na binti mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono 
yote miwili, Mariam Stanford (kushoto).
No comments:
Post a Comment