Washiriki
 wa Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2014, wakimsikiliza Afisa Mfawidhi,
 Nisalile Mwangoka aliyekuwa akiwapa maelezo juu ya upimaji wa wageni 
wanao ingia nchini kupitia viwanja vya ndege unavyofanyika kutumia 
mashine maalum iitwayo ‘Walk Through Thermoscaner’, iliyopo uwanja wa 
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati warembo 30 wanaowania 
taji la Miss Tanzania walipotembelea uwanja huo na kujifunza mambo 
mbalimbali . Warembo hao wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa 
ndani kwa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini. 
 Mashine hiyo ikionekana kufungwa juu kuelekea usawa wa kuingilia abiria wanaowasili tka nje ya nchi.
 Namna inavyoonekana baada ya kipimo kuchukuliwa 
 Nisalile
 Mwangoka akionesha kifaa cha zamani cha upimaji ugonjwa wa Ebola 
ambacho kimeelezwa kuwa licha ya ufanisi lakini kilikuwa kinaweka foleni
 kwa abiria tofauti na hicho kipya.
 Meneja
 wa Usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), 
Kisusi Makomondi akiwapa maelezo washiriki hao wa shindano la Miss 
Tanzaniua 2014 juu ya shughuli mbalimbali za uwanja huo.
 Warembo wakianza ziara 
 Camera man wa True Vision John Lymo akiwajibika uwanjani KIA.
 Warembo pia walipata fursa ya kutembelea kikosi cha zima moto uwanjani hapo. 
 Warembo hao baada ya kutembelea Uwanja wa Ndege KIA waliwasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Mkuu
 wa Wilaya (DC) wa Arumeru, Nyirembe Munassa Sabi,akiwa na warembo baada
 ya kuwapokea ambapo walitarajiwa kufanya ziara ya kutembelea vivutio 
vya utalii hifadhi ya Arusha na Namanga katika mpaka wa Tanzania na 
Kenya.
No comments:
Post a Comment