RE: FOR IMMEDIATE RELEASE
SERENGETI FIESTA YABISHA HODI MORO MJINI
Morogoro-Tanzania-September 21st/2014  
Wakati tamasha la Serengeti Fiesta likitimiza wiki ya saba huku 
likizunguka na wasanii katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kutoa 
burudani ya aina yake, hakika kazi hiyo haikuwa rahisi kwani zaidi ya 
mikoa saba bado inalisubilia kwa hamu kubwa tamasha hilo la Serengeti 
Fiesta kwa mwaka 2014.
Baada ya umati mkubwa kujitokeza katika mji wa Iringa, tamasha 
la Serengeti Fiesta sasa linabisha hodi mjini Morogoro, si kwa mikono 
mitupu bali likiwa na kundi la wasanii nyota zaidi ya 12 wa muziki wa 
kizazi kipya watakaopanda jukwaani hapo leo katika Uwanja wa Jamhuri.
Tulipata nafasi ya kuzungumza na Stamina ambaye ni msanii wa 
muziki wa bongo fleva hapa mjini Morogoro naye alikuwa na haya ya 
kusema, “Nina furaha sana kwakuwa tamasha la Serengeti Fiesta litakuwa 
hapa mjini siku ya Jumapili na kama kawaida sitawaangusha mashabiki 
wangu. Nataka kuwapa shoo bora ambayo kamwe hawataisahau. Napenda 
kuwahakikishia kuwa msikose kuja katika shoo hii muhimu, njooni mmuone 
kijana wenu jukwaani akifanya mambo adimu.
Mbali ya tamasha hilo, kutakuwa na matukio kadha wa kadha kama 
bonanza la soka na dansi la Fiesta ambapo washindi watapata fursa ya 
kutua Dar es Salaam kushuhudia shoo ya mwisho ya Serengeti Fiesta 
inayotarajiwa kufanyika Oktoba 18, mwaka huu.
Wasanii wengine watakaotumbuiza katika tamasha hilo 
litakalofanyika katika Uwanja wa Jamhuri ni Afande Sele, Weusi, Ney wa 
Mitego, Vanessa, Linah, Young Killa, Bue, Makomando, Ommy Dimpoz, Mo 
Music, Baraka Da Prince, Y Tony na Joh Maker.
“Tulikuwa na shoo yenye mafanikio makubwa mjini Iringa na ni 
matarajio yangu kwamba mashabiki wetu wa Morogoro watazidi wale wa 
Iringa pia napenda kutumia nafasi hii kuwahakikishia wakazi wa Morogoro 
na viunga vyake kuwa shoo kabambe itaporomoshwa na wasanii wakali wa 
muziki wa bongo fleva na mengine mengi mazuri kutoka na SBL, hivyo 
msikose,” alisema Rugambo Rodney-Brand Manager Serengeti Premium Lager
Mwaka huu, tamasha la Serengeti Fiesta limevuta hisia za watu 
wengi toka katika kila kona ya mikoa yote ambayo tamasha hilo lilipita 
kwani watu wengi walijumuika nalo huku likiwa na kaulimbiu ‘Sambaza 
Upendo’ .

No comments:
Post a Comment