JUMUIA ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi, mkoa wa Arusha, imezindua
 rasmi  kikundi cha Vicoba cha mkoa huo kama kikundi cha mfano ili
 kuhamasisha wananchi kujiunga na kuanzisha Vikoba kila eneo ili kuinua
 hali zao za uchumi..
 
Uamuzi huo wa kuanzisha Vikoba, ulifikiwa mwishoni mwa kikao cha
 baraza la wazazi mkoa kilichofanyika wilaya ya Karatu na kuazimia mkoa
 kuwa na kikundi ncha vikoba cha mfano ili kuvutia ngazi zingine za
 jumuia hiyo kuanzia wilaya hadi vijiji kuanzisha vikoba.
 
Katibu wa jumuia ya wazazi mkoa wa Arusha, Daniel Mgaya, amesema
 katika kutekeleza maazimio ya kikao hicho cha baraza ,mkoa umeunda
 uongozio wa muda ikiwa ni hatua ya maandalizi ya kukamilisha katiba ya
 Vikoba, ili kuweza kuhudumia wanachama wake .
 
 Mgaya,amesema kupitia vikoba wanachama wataweza kubuni miradi
 mbalimbali ya kiuchumi nna hivyo kuboresha maisha yao na kwa kutambua
 kuwa vikoba ndio njia rahisi ya wananchi kuinua maisha.
.Amesema kikao cha baraza kiliwateua, Lodamini Mollel, kuwa mwenyekiti, Emanuel Loi Katibu, Aman Nassary kuwa mweka hazina ,huku Rehema Mohamed, Zaituni Kiobya Edward Seneu, Zakaria Mlyanga, na Josephine Shayo ,wakichaguliwa kuwa wajumbe .
 
 Mgaya,amesema kuwa pia baraza hilo la wazazi mkoa limemchagua, John
 Danil son Pallanyo,ambae ni mjumbe wa baraza hilo mkoa na taifa
 kusimamia mfuko huo.
 
Amesema baraza limeweka  kiwango cha hisa cha shilingi 15,000, ambazo
 zitakuwa zikitolewa kila wiki ambapo mfuko wa jamii utachangiwa
 shilingi 150,000 kila wiki  mara tatu.
 
 .Lengo lakuanzishwa kwa vikoba ni kuinua maisha ya wanachama ,na kwa
 kupitia  kikundi hicho cha mkoa wanachama watakuwa na uwezo wa kubuni
 miradi ya kiuchumi na pia watapata  elimu ya ujasiriamali na hivyo
 kuboresha vikoba vitaklavyoanzishwa ngazi mbalimbali mkoani Arusha. .

No comments:
Post a Comment