Mkurugenzi
  wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa Chama cha 
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila akionesha barua za 
kuomba vibali vya kufanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini. 
 Mkurugenzi
 wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa Chama cha Demokrasia
 na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila (kushoto), akizungumza katika 
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu maandamano ya 
chama  hicho yatakayoanza kesho nchini kote kupinga Bunge Maalumu la 
Katiba linaloendelea Dodoma. Kulia ni Kada wa Chadema, Aron Mashuve na 
Mwanasheria wa chama hicho, John Malya.
 Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene  akimkaribisha Kigaila kuzungumza na wanahabari.
 Mwanasheria wa Chadema, John Malya akifafanua baadhi ya vipengere  vya sheria kuhusu ruhusa ya kufanya maandamano.
  Mwanasheria  wa Chadema, John Malya akiwa na kada wa chama hicho, Aron Mashuve.
 =========================================
 CHAMA
 cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesisitiza kuwa migomo  na 
maandamano yasiyokoma nchi nzima yapo palepale na kwamba yanaanza rasmi 
kesho kwa kishindo kikubwa na hakuna mtu wa kuyazuia kwani ni haki yao 
kikatiba.
Chadema
 kimesema lengo la maandamano hayo ni kuishinikiza Serikali ya Chama Cha
 Mapinduzi (CCM), kitoe tamko la  kusitishwa Bunge Maalum la Katiba 
linaloendelea mjini Dodoma huku likifuja fedha za wananchi.
Kauli
 hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Organizasheni na 
Mafunzo wa chama  hicho, Benson Kigaila wakati  akizungumza na 
wanahabari Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni.
“Maandamano
  yaliyotangazwa na Freeman Mbowe si ya kwake ni maazimio ya Mkutano 
Mkuu wa Chadema uliofanyika Septemba 14, mwaka huu.
“Tunasisitiza
 kuwa maandamano na migomo isiyokoma nchi nzima yapo palepale, lengo 
letu ni kuishinikiza Serikali isitishe Bunge la Katiba kwani  mkutano 
mkuu uliazimia jambo  hilo baada ya kuona kuwa kinachofanyika Dodoma 
hakitatupa Katiba Mpya, bali fedha za wananchi zinatafunwa bure”alisema.
Aidha,
 alisema maandamano yao yapo kisheria ambapo katika Katiba  ya nchi, 
 maandamano ni haki sheria namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 
kifungu cha 11 kifungu kidogo cha 1 inaruhusu jambo hilo.
Kigaila
 aliongeza kuwa sheria hiyo inataka waandamanaji  kutoa taarifa ndani ya
 saa 48 kabla ya na si kuomba kibali taratibu ambazo wao wameshazipitia.
“Natoa
 mwito kwa  Watanzania wote wakatae ufisadi unaofanywa na Bunge Maalumu 
la Katiba. Kilichoko Dodoma ni kumaliza fedha ambazo zingetumika 
kujengea nyumba za walimu au hata zahanati katika maeneo mbalimbali 
nchini,”alisema .
Kigaila
 alisisitiza kuwa wamepata barua kutoka Jeshi la Polisi kuwataka 
kusitisha maandamano lakini hawatasitisha  kwa sababu, sababu za katazo 
hazina mashiko na hazijanukuu kifungu chochote cha sheria.
Alisema licha ya wao Chadema, maandamano yao hayo yamepata baraka kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi  (Ukawa).
Mkurugenzi
 huyo wa organizasheni wa chama hicho alisema maandamano hayo 
yanafanyika katika ngazi ya majimbo, wilaya na mkoa, ambapo kwa mkoa 
yataanzia maeneo tofauti kuishia  ofisi za mkuu wa mkoa husika na kwa 
wilaya yatakwenda kwa mkuu wa wilaya husika.
Alisema
 maandamano hayo  kila mahali yataanza asubuhi, huku kwa mikoa mitatu ya
 kanda ya Dar es Salaam yataanza keshokutwa Jumatano.
Kwa
 upande wale Mwanasheria  wa chama hicho, John Mallya alisema sababu 
nyingine iliyotolewa na polisi kuwa maandamano  hayawezi kufanyika kwa 
sababu kesi iliyofunguliwa Saedy Kubeinea ya kupinga Bunge hilo ipo 
mahakamani kuwa  haina mashiko kwa kuwa Chadema ni taasisi 
inayojitegemea na inamaamuzi yake ya kichama.
No comments:
Post a Comment