Kaimu
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasirimali Watu wa Wizara ya Habari, Vijana, 
Utamaduni na Michezo Bw. Titus Mkapa akimkaribisha Mwenyekiti wa timu ya
 Wizara HUM Sports Club (hayupo pichani) ili atoa salama za wachezaji 
kwa mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo 
leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
 wa Timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (HUM Sports 
Club) Dkt. Margareth Mtaki akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kuwaaga 
wachezaji wa timu hiyo inayotarajiwa kuondoka kesho kuelekea mkoani 
Morogoro kwa ajili ya mshindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam. 
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga na 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel.
Naibu
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa 
Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo wakati wa hafla ya kuwaaga 
wachezaji wa timu hiyo inayotarajiwa kuondoka kesho kuelekea mkoani 
Morogoro kwa ajili ya mshindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam. 
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga.
Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba 
Nkinga akimkabidhi zawadi Mwanamichezo aliyeiletea Wizara ushindi katika
 mashindano ya SHIMIWI na Meimosi mwaka jana Bibi. Niuka Chande. 
Mchezaji huyo aliibuka mshindi katika michezo ya Draft na kurusha Tufe 
na kuiletea Wizara vikombe viwili. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa 
Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Timu ya Wizara
 Dkt. Margareth Mtaki.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. 
Sihaba Nkinga akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Rais wa Shirikisho 
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi leo jijini Dar es Salaam 
wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Wizara hiyo wanatarajia 
kwenda mjini Morogoro kesho kwa ajili ya mashindano ya SHIMIWI 
yatakayoanza kuanzia tarehe 27 septemba hadi Oktoba 11.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. 
Sihaba Nkinga akiwa amenyanyua juu Kikombe cha ushindi wa kwanza kwa 
mchezo wa Draft katika mashindano ya SHIMIWI mwaka jana ambacho 
kilinyakuliwa na mchezaji watimu ya Wizara ya Habari Bibi. Niuka Chande 
(mwenye taki suti nyeusi)kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo 
Profesa Elisante Ole Gabriel akifurahia
aadhi
 ya wachezaji wa timu ya HUM Sports Club wakitoa salaam za timu yao kwa 
mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
 na Michezo hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya 
kuwaaga wachezaji wa timu hiyo wanakwenda mjini Morogoro kushiriki 
mashindano ya SHIMIWI yanayotarajiw kuanza tarehe 27 mwezi huu na 
kumalizika tarehe 11 Oktoba.
Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba 
Nkinga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na 
wachezaji wa timu ya Wizara 
………………………………………………………………….
Na Anitha Jonas – Maelezo
Timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waaswa 
kuwa mfano katika mashindano ya SHIMIWI ikizingatiwa kuwa ipo chini ya 
Wizara inayo simamia michezo nchini.
Wito huo umetolewa leo jiji Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa 
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi Sihaba Nkinga 
wakati Timu hiyo ikiagwa rasmi kwa ajili ya kuelekea Mkoani Morogoro kwa
 kushiriki mashindano ya SHIMIWI 2014 yanayotarajiwa kuanza tarehe 27 
Septemba hadi tarehe 11 Oktoba.
Bibi Sihaba pia amewataka wanamichezo hao kuwa na nidhamu katika
 michezo, kuzingatia sheria na kanuni zinazoongoza michezo 
watakayoshiriki na kujituma kwa lengo la kuleta ushindi.
“Kumbukeni kuwa ninyi ni Watumishi wa Umma hivyo mnapaswa 
kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma katika kutelekeza dhamira ya 
mashindano hayo”.Amesema Bibi Nkinga.
Kwa upande mwingine Bibi Sihaba amewashukuru wadhamini 
mbalimbali wakiwemo Platinum Credit Ltd,Starmedia 
(Startimes)TFF,WaterCom (T) Ltd na Mohamed Enterprise kwa kushirikiana 
na Wizara kuinua michezo kwa kuchangia vifaa mbalimbali vya michezo ili 
kufanikisha mashindano hayo.
Naye Mwenyekiti wa Timu Dkt. Margret Mtaki ameushukuru uongozi 
wa Wizara kwa kuwapa ushirikiano mzuri katika kufanikisha maandalizi ya 
Timu kwa kuwapatia vifaa vya kutosha katika michezo yote.
Pia Mwenyekiti ameahidi kuwa Timu itazingatia nidhamu ya hali ya juu na kujituma ili kuelete ushindi wa kishindo kwa Wizara.
Aidha, Mshindi wa Mchezo wa Drafti na Kurusha Tufe katika 
Mashindano ya SHIMIWI 2013 na Mashindano ya Mei Mosi 2014 Bi. Niuka 
Chande amekabidhiwa zawadi ya sh. 300,000 na cheti cha kutambua mchango 
wake katika michezo hiyo na kuiletea Wizara ushindi.
Timu ya Wizara mwaka huu inajumuisha jumla wachezaji 55 amabao 
watashiriki michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu,Riadha,Mpira wa 
Pete,Drafti,Karata, Bao na Kuvuta Kamba.
No comments:
Post a Comment