.Mwenyekiti
 wa Halmashauri ya wilaya ya.Mpanda Yasini Kibiriti akifungua kikao cha 
Baraza la Madiwani kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Wilaya ya 
Mpanda. 
Diwani
 wa Viti Maaalum Tarafa ya Mwese inayojumisha Kata za Kapalamsenga Ikola
 na Karema yenyewe akichangia kwenye kikao cha Madiwani wakati wa kikao 
hicho wengine ni madiwani wa Halmashauri hiyo.
………………………………………………………………………….
Na Kibada Kibada-Katavi
Zaidi ya shilingi milioni 80 zimetengwa na  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya maabara ya Sayansi vilivyojengwa katika shule za  Sekondari  zilizoko kwenye  Halmashauri hiyo.
Hayo
 yamelezwa na Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  Yasini 
Kibiriti wakati akifungua kikao cha kwanza cha Baraza  la Madiwani  kwa 
mwaka 2014/2015 kilichofanyika  kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halamsahuri
 hiyo.
Akizungumza
 katika Kikao hicho Mwenyekiti Kibiriti ameeleza ujenzi wa maabara kwa 
Halmashauri ya Mpanda uko vizuri sana  kwani wameishakamilisha ujenzi na
 fedha hizo zilizotengwa ni kwa ajili ya ukamilishaji ikiwa ni pamoja na
 kununua vifaa vitakavyotumika kwenye nmaabara hizo.
Akaongeza
 kuwa hadi kufikia oktoba 15 mwaka huu anaimani watakuwa wamekamilisha 
kila kitu na kwa Halmashauri za Mkoa wa Katavi Halamshauri ya Mpanda 
inaonekana kufanya vizuri katika ukamilishaji wa ujenzi wa maabara 
ingawa haipongezwi kwa juhudi inazozifanya katika kutekeleza kwa wakati 
maagizo yanayotolewa na Viongozi wa juu  wa serikali  kuanzia ngazi ya 
Mkoa na Taifa.
Mhe,
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  
aliagiza ujenzi wa Maabara kwa shule zote za sekondari   na ifikapo 
mwezi novemba mwaka huu kila Halmashauri iwe imekamilisha ujenzi 
huo,akawagiza wakuu wote wa Wilaya na Mikoa ambao hawatakamilisha ujenzi
 wajiondoe wenyewe kwa upande wa   Halmashauri ya Mpanda wao 
wamefanikiwa kukamilisha ujenzi huo.
Katika
 ujenzi huo  zaidi ya shilingi milioni 560 zimetumika kujenga maabara 
nane zenye vyumba viwili viwili  kwenye shule za Sekondari 
Mpandandogo,Karema,Ilandamilumba,Ikola,Mwese,naMishamo maabara zote hizo
 ziko vizuri kweli kweli tofauti na inavyozungumuziwa na watu kuwa 
Halmashauri iko nyuma katika utekelezaji wa ujenzi wa maabara siyo 
kweli.
Awali
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda Estomih Chang’ah alieleza 
changamoto inayoikabili Halmashauri katika utengenezaji wa barabara za 
Halmashauri hiyo kutokana na wakandarasi kutokuwa na Vifaa vya kutosha 
hali inayofanya ucheleweshaji wa kukamilika kwa barabara kwa wakati.
Chang’ah
 akaeleza wakandarasi wengi wanapokuja kuomba kazi kwenye Halmashauri 
hawakamilishi kazi zao kwa wakati ,ambapo wanatakiwa kutekeleza kazi zao
 kwa wakati lakini ajabu bado unakuta wanaomba msaada wa kusaidiwa vifaa
 vya ujenzi wakati walishapatiwa kazi  kwa mjibu wa mkataba wanatakiwa 
wakabidhi kazi siyo kuomba msaada tena wakusaidiwa vifaa vya 
kukamilishia kahiyo kule waliko pewa kazi.
Wakiongea
 katika kikao hicho Diwani wa Kata ya Kapalamsenga Moses Joseph alieleza
 kuwepo ucheleweshaji wa kusambaza kifusi kwenye barabara ya 
Kapalamsenga Ifume kazi inayofanywa na mkandarasi ambaye  aliingia 
mkataba na Halmashauri lakini kazi hiyo inaonekana kusuasua na 
haifahamiki lini ataikamilisha.
No comments:
Post a Comment