TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, September 25, 2014

TIMU YA KATA YA MKOLANI FC IMEIBUKA BINGWA WA KOMBE LA MEYA 2014 NA KUNYAKUWA BAJAJI NA SHILINGI MILIONI 1.5


 

 Baadhi ya Waamuzi waliochezesha michuano hiyo,

 Baadhi ya Viongozi mbali mbali wakijiandaa kutoa zawadi kwa washindi wa michuano hiyo.

 Baadhi ya Timu Zilizoshiriki

 Jukwaa la Pespsi ambalo lilitumika kufanya matangazo Uwanjani





   Wakazi wa jiji la Mwanza waliofurika kushuhudia Fainali hizo.

 
 
 

 Wakazi wa Jiji la Mwanza wakifuatilia kwa Makini Mchezo wa Fainali

 

 Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, pamoja na Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz (wa kwanza kulia), wakifuatilia kwa Makini Fainali hiyo.

 Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz kulia akiangalia kwa Makini Mpambano wa Fainali

 Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz(kulia) akitafakari jambo wakati mpambano wa Fainali ukiendelea


 Wasanii wa kundi la Bujora Traditional Group la jijini Mwanza wakionyesha vitu vyao kwa Mashabiki wa Soka waliofurika katika Uwanja huo wa Nyamagana jijini Mwanza.

 

  Wasanii wa kundi la Bujora Traditional Group la jijini Mwanza wakionyesha vitu vyao kwa Mashabiki wa Soka waliofurika katika Uwanja huo wa Nyamagana jijini Mwanza.

 
  Wasanii wa kundi la Bujora Traditional Group

 Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz(kulia) akitafakari jambo wakati mpambano wa Fainali ukiendelea

  Wasanii wa kundi la Bujora Traditional Group


  Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz(kulia) akifafanua jambo wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi

 
 

 Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula, akifafanua jambo wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi


 Katibu Mkuu wa TFF  Selestine Mwesigwa, akifafanya jambo wakati wa Fainali za Michuano hiyo.


 Zawadi ya Bajaji almbayo ilishindaniwa

 Shabiki wa Soka akiponyesha ukereketwa wake

 Timu zikiingia Uwanjani katika mchezo wa Fainali.


  Mkurugenzi wa My Way Entertainment , Paul Mganga(kushoto) akifuatilia Fainali muda mfupi kabla ya mpambano kumalizika, kushoto ni zawadi ya Vikombe vya washindi.


 Kiatu cha Dhahabu ambacho kilikuwa Gumzo kwa Wachezaji jijini Mwanza Meya Cup

 Wachezaji wa Mkolani wakipongezana
Kocha wa Timu ya Mkolani, Wandiba Wandiba, akiinuliwa juu baada ya Timu yake kuchukua ubingwa wa Michuano hiyo

 Mashabiki wa Mkolani wakipagawa baada ya timu yao kuibuka kidedea

 Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula (kulia) akiongoza viongozi kueelekea kutoa zawadi(Kati kati ni mwenyekiti wa Chama cha mpira wilaya ya mwanza Jackison Songora)

 Askari Polisi akionekana kuweka Ulinzi mkali kwenye Bajaji ambayo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya zawadi kwa timu iliyoibuka mshindi


  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua moja ya kumbukumbu kwa ajili ya habari

  mwenyekiti wa Chama cha mpira wilaya ya mwanza Jackison Songora, akifafanua jambo baada ya Fainali kumalizika.


 Wachezaji wa Timu ya Mirongo (Wenye njano) wakisubiri kupokea zawadi ya Mshindi wa Pili

 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua moja ya kumbukumbu kwa ajili ya habari


 mwamuzi bora kutoka Kituo cha Alliance, David Albert aliyepata zawadi ya  Sh laki mbili
Meneja Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nicolaus Coetz akikabidhi zawadi ya mfungaji bora kwa  Paulo Godfrey

TIMU ya Kata ya Mkolani FC Mwishoni mwa juma imeibuka mabingwa wapya wa Kombe la Meya 2014 baada ya kuichapa timu ya Kata ya Mirongo bao 2-1  (jumamosi iliyopita) katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Awali katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ulioanza mapema saa 8:00 mchana kwa timu ya Sokoni FC kuichapa Mnadani FC bao 3-0 na kuibuka mshindi wa tatu wa michuano hiyo huku magori ya Sokoni yakifungwa na Joseph Mwajalila dakika 33 kwa penati na Salimu Hamis dakika 39, 51 na kuwapa tiketi ya ushindi wa tatu.

Fainali hiyo iliyoshuhudiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TFF  Selesitine Mwesigwa, muasisi wa mashindano hayo Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza, Stanislaus Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Mwanza (MZDFA), Jackson Songola na Katibu wa MZDFA, Nasibu Mabrouk.

 Ndikilo alisema kwamba mashindano hayo yamewasaidia  vijana kuonyesha vipaji vyao, hivyo ni vyema sasa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwatumia vijana walionesha uwezo kuunda timu ya Mwanza City FC kama ilivyofanya Jiji la Mbeya.

“Ni bora mkaunda timu ya Mwanza City FC ili kushiriki ligi na huenda ikatinga ligi kuu Bara kama walivyofanya wenzetu wa Mbeya na sasa timu ya Mbeya City FC inashiriki ligi kuu, kwani timu zetu kongwe katika Mkoa huu za Toto FC na Pamba FC zimeonekana kuishiwa mbinu na kufanya vizuri ili kurejea ligi kuu,”alisema.

Katika mchezo huo mkali wa vuta ni kuvute kilishuhudia timu hizo zikienda mapumziko zikiwa hazijafungana na kipindi cha pili mchezaji Siraji Juma aliwainua mashabiki kwa kuandika bao la kwanza na bao la pili likifungwa na Paulo Godfrey huku katika hekaheka ya kuokoa mpira ulioelekezwa langoni mwake akijikuta akijifunga na hadi mwisho wa mchezo wadau wa michezo walishuhudia timu ya Mkolani ikitawazwa kuwa mabingwa kwa kuinyuka Mirongo Fc bao 2 - 1.
Mashindano hayo ya kombe la Meya 2014 yaliyodhaminiwa na Kampuni ya kutengeneza vinywaji vya Pepsi (SBC), Ndikilo alikabidhi bingwa timu ya Mkolani FC zawadi ya kombe, fedha tasilimu Sh milioni 1.5, medali ya dhahabu na Bajaji ya mizigo yenye thamani ya Sh milioni 4.5, mshindi wa pili alinyakuwa Sh milioni 2, kombe dogo na medali ya fedha.

Timu ya Sokoni FC iliyoibuka mshindi wa tatu ilijinyakulia fedha tasilimu Sh milioni 1, medali ya shaba na kombe dogo, mfungaji bora Paulo Godfrey akiwa na bao nane na kunjinyakulia kiatu cha dhahabu na Sh laki mbili, mwamuzi bora kutoka Kituo cha Alliance ilichukuliwa na David Albert na kupata Sh laki mbili huku timu ya Kata ya Mahina FC ikipata Nidhamu bora na Sh laki mbili.

No comments:

Post a Comment