=================================================== 
 SERIKALI YAWATAKA WASIMAMIZI NA WADADISI WA UTAFITI WA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI KUZINGATIA WELEDI.
Na. Mwandishi wetu – Kilimanjaro.
24/9/2014.
Aidha, imewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya, madakatari na  wafanyakazi wa vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini  kutoa ushirikiano kwa wadadisiwatakaoendesha utafiti huo ili waweze kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika maeneo yao kwa lengo lakupata taarifa sahihi zitakazofanikisha utafiti huomuhimu kwa maendeleo ya taifa.
Waziri wa 
Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akizungumza wakati akifungua 
mafunzo ya siku 27 kwa wakufunzi na wadadisi  kutoka  Tanzania Bara na 
Zanzibar  watakaoendesha  utafiti huo  amesema kuwa wakufunzi, wadadisi 
na wataalam  hao wanayo nafasi kubwa  ya kufanikisha upatikanaji wa 
takwimu sahihi zitakazotoa taswira halisi ya utoaji wa huduma ya afya 
nchini kwa mwaka 2014/2015.
Amesema utafiti huo utaiwezesha serikali kutathmini utekelezaji wa mipango mbalimbali na kufikia malengo iliyojiwekea kitaifa na kimataifa kwa kuboresha na kuendelea  kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wake.
Amesema 
Serikali imekuwa ikitekeleza programu mbalimbali  za kuboresha huduma za
 afya na maisha ya Watanzania kwa kupitia Mikakati ya Kimataifa na 
Kitaifa ikiwemo ile ya Malengo ya Milenia ya Mwaka 2015 na Mpango wa 
Maendeleo wa Miaka Mitano (2011 -2016).
Dkt. Seif 
amesema katika juhudi hizo  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imekuwa na
 jukumu la kusimamia programu mbalimbali za afya na kufuatilia 
utekelezaji na utoaji wa huduma za afya nchini.
Amesema kumekuwa na maboresho makubwa katika sekta ya afya hadi kufikia mwaka 2013 ambapo takwimu zinaonyesha kuwepo kwa  vituo  6767 vya kutolea huduma ya afya nchini , hospitali 256, vituo vya afya 701 na zahanati 5810.
“Nyote ni mashahidi kuwa toka kipindi hicho mpaka sasa serikali imeendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi wake,sasa tuna huduma ya kuzuia maambukizi ya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ambayo inapatikana  katika vituo vyote vinavyotoa huduma za mama mjamzito” Amesisitiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumzia mafunzo hayo amesema kuwa washiriki watakaofaulu na kukidhi vigezo vilivyowekwa  watashiriki katika zoezi la kukusanya takwimu za utafiti huo  kwa kipindi cha miezi minnekuanzia  tarehe 13 Oktoba 2014 .
Amesema utekelezaji wa utafiti huona mafunzo hayo unafanywa
 kwa pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Wizara ya Afya na Ustawi
 wa Jamii – Tanzania Bara, Wizara Afya – Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu 
Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na Shirika la ICF International 
la Marekani ambao pia wanatoa ushauri wa kitaalamu katika kufanikisha 
utafiti huo.
 Dkt. Chuwa amefafanua kuwa utafiti huo utahusisha ukusanyaji wa takwimu katika sehemu za kutolea huduma za afya kwa lengo la  kufahamu utayari wa vituo vinavyotoa huduma za afya na huduma bora za afya kwa wananchi. 
 Aidha amezitaja huduma zitakazoguswa na utafiti huo kuwa ni pamoja pamoja
 na Huduma za Afya ya Uzazi, Afya ya Watoto, Maradhi ya Kuambukiza kama 
vile Kifua Kikuu, UKIMWI, Malaria pamoja na Maradhi yasiyo ya kuambukizakama vile magonjwa ya Kisukari na Moyo.
  Amefafanua kuwa lengo la kufanyika kwa utafiti huo ni kuiwezesha serikali
 kujua ni kwa namna gani vituo vinavyotoa huduma ya afya vimejipanga 
kutoa huduma bora ya afya kwa kuangalia upatikanaji wa huduma 
mbalimbali, vifaa, dawa, miundombinu na rasilimali watu kwa kada 
mbalimbali. 
Naye mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Ibrahimu Msengi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema kuwa mkoa huo unaendelea na juhudi za kuboresha huduma  za afya zinazotolewa katika vituo vya  afya pamoja  kwa lengo la kuboresha hali ya maisha ya wakazi wa Kilimanjaro na kukuza pato la mkoa huo.
Amesema mkoa umeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya afya iliyopo
 ili iweze kuakisi ukuaji wa Pato la Mkoa na mahitaji ya wananchi katika
 kupata  huduma za afya zilizo bora kulingana na ongezeko la idadi ya 
Watu.
Amefafanua kuwa utafiti huo umekuja wakati muafaka ambapo mkoa huo na mikoa mingine nchini inahitaji kuboresha huduma za afya katika vituo vyotevya kutolea huduma.







No comments:
Post a Comment