Rais
 wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa  Martina 
Maurizio (kulia), akiwaelekeza jambo wachezaji wa mchezo huo walioko 
kambini Dar es Salaam jana. Wachezaji sita wa timu hiyo wanatarajia 
kuondoka Septemba 28 mwaka huu kwenda nchini Albania kushiriki 
mashindano ya dunia ya mchezo huo.
Wachezaji hao sita wakiwa wameshika bendera ya timu hiyo. Kulia ni  Rais wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa  Martina Maurizio.
Katibu
 Mkuu wa Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo Tanzania (TASMA). Dk. 
Nassoro Matuzya (kushoto), akimpima uzito mchezaji, Ramadhan Jangle 
ikiwa ni maandalizi ya mashindano hayo. 
 Dk. Nassoro Matuzya (kushoto), akimpima presha mchezaji, Heri Msukile. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Mwalimu wa mchezo huo, Max (kulia), akimfua Master Dhabiti Athuman Msawila. ‘Master Hugu’ 
 Mchezaji
 Ramadhan Hassan (kulia), akikwepa kwanja la Heridini Mwinyiheri wakati 
wakiendelea na mazoezi katika Klabu ya Yanga Jangwani jana.
Wachezaji Hamisi Magigo (kushoto) na Master Dhabiti Athuman Msawila. ‘Master Hugu’  wakirushia makonde katika mazoezi hayo.
Dotto Mwaibale
WACHEZAJI sita wa timu ya  Karate wanatarajia kuondoka nchini kwenda Albania kushiriki mashindano ya dunia ya mchezo huo.
Washiriki
 hao tayari wamefanyiwa vipimo vya afya zao pamoja na uzito Dar es 
Salaam jana na Dk. Nassoro Matuzya ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha 
Wataalamu wa Tiba za Michezo Tanzania (TASMA).
Kikosi hicho cha watu 20 kinatarajiwa kuondoka nchini Septemba 28 kuelekea nchini humo kwa mashindano hayo.
Akizungumza
 na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho la Dunia 
la mchezo huo (UPAM) Profesa  Martina Maurizio alisema wachezaji hao 
wataungana  wataungana na wenzao kutoka Mwanza, Unguja na Arusha ambapo 
utafanyika mchujo ili kupata timu ya taifa.
Alisema
 wachezaji hao wapo kambini  na wamepata mafunzo ya kutosha na hivyo ni 
lazima warudi na ushindi pamoja na kuitangaza Tanzania duniani.
“Watanzania
 wengi bado hawajaupa kipaumbele mchezo huu jambo linalofanya usahaulike
 lakini watajitahidi kuufanya mchezo huo ukubalike hapa nchini kama 
ilivyo kwa nchi nyingine.
Maurizio alimpongeza Mkurugenzi wa Princecasino kwa kujitolea kwa hali na mali kudhamini safari hiyo.
No comments:
Post a Comment