Meneja
 wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza 
Bw. Felician Ncheye, akiwakaribisha na kuwatambulisha wawezeshaji kwa 
washiriki wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo
 katika masuala ya masoko na Tehama kwa mameneja na waandishi wa habari 
takribani 60 kutoka Redio jamii mbalimbali nchini, yanayoendelea kwenye 
kituo cha habari na mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
Na Mwandishi wetu, Sengerema
SHIRIKA
 la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema 
litaendelea kusaidia kuimarika kwa redio za jamii nchini kwa kuwa ndio 
nyenzo muhimu za maendeleo ya wananchi kwa kuwapa sauti katika huduma na
 shughuli zao.
Kauli
 hiyo imetolewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa 
UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa mameneja 
na watendaji takribani 60 kutoka Redio jamii mbalimbali nchini, mafunzo 
yanayofanyika kwenye kituo cha Redio Sengerema FM.
Katika
 mafunzo hayo watendaji hao watafunzwa masuala ya Tehama na utafutaji wa
 soko kwa lengo la kufanya redio hizo kuwa endelevu na kujiendesha 
zenyewe kwa kuweza kutekeleza miradi yake na kuendelea kushirikiana na 
wananchi.
Mafunzo
 hayo ni utekelezaji wa mradi wa miaka mitatu wa kuwezesha redio za 
jamii nchini unaoendeshwa na UNESCO baada ya redio hizo nyingi kusaidiwa
 kuanzishwa katika miaka ya karibuni.
Afisa
 Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph 
akizungumza na Mameneja na waandishi wa habari kutoka redio tisa za 
jamii wanaohudhuria mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika 
masuala ya masoko na matumizi ya Tehama yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA
 na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na 
Utamaduni (UNESCO). Kushoto mgeni rasmi Ofisa mdhani kutoka Wizara ya 
Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya 
usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed.
Kwa
 mujbu wa Yusuph mradi wa SIDA ambao umekuwa ukitekelezwa kwa kipindi 
cha miaka mitatu umeshughulika na uboreshaji wa redio hizo ili kuzipatia
 uwiano na pia kuziwezesha kutumia Tehama kuhabarisha wananchi pia 
kutokana na mafanikio yaliyopatikana mradi huo utaendelea kwa miaka 
mingine mitatu.
Ametaja
 mafanikio hayo kuwa yamepatikana kwa ushirikiano wa Redio za jamii 
pamoja na shirika hilo hali iliyofanya kuyavuta mataifa mengine 
kuchangia kwa ajili ya kuendelea kuzijengea uwezo redio za jamii kupitia
 shirika hilo.
Ameongeza
 kuwa kufanikiwa kwa redio za jamii nchini Tanzania katika mradi huu wa 
SIDA kumefanya mashirika mengi yanayotaka kufanyakazi na wananchi wa 
kawaida kukimbilia UNESCO kutambua redio za jamii ambazo zinaweza 
kufanyakazi nayo.
Mradi
 huo wa Tehama unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na
 kuratibiwa na UNESCO ni sehemu ya mradi wa UNESCO katika nchi saba za 
Afrika , Tanzania ikiwamo.
Baadhi
 ya Mameneja na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali za jamii 
wakimsikiliza Bw. Al Amin Yusuph kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo 
yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema 
Telecentre mkoani Mwanza.
Katika
 mafunzo hayo yanayofanyika mjini Sengerema, elimu inatolewa kwa wakuu 
wa vituo na waandishi wa habari kutoka redio Micheweni FM, Orkonerei FM,
 Pambazuko FM, Mtegani FM, Kahama FM, Redio FM, Kyela FM, Fadeco Radio 
na Pangani FM.
“Kuna
 mambo mengi yamefanikiwa.. kikubwa zaidi kumpa nafasi mwananchi 
kujieleza na kueleza matumaini yake..” alisema Yusuph ambapo aliongeza 
kwamba kutokana na mradi huo kufanikiwa zipo nchi na mashirika ambayo 
yapo tayari kuchangia uimarishaji wa redio za jamii nchini.Hakuzitaja 
nchi hizo
Alisema
 kutokana na mafanikio yaliyopo ya redio hizo kuwa karibu na jamii, SIDA
 kwa kushirikiana na UNESCO wametengeneza programu hiyo ili kuwezesha 
kuwepo kwa matumizi ya mtandao katika kukusanya habari, kuziboresha na 
kuzitumia kwa manufaa ya wananchi.
Ofisa
 mdhamini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar 
na Mjumbe wa bodi ya usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed, 
akitoa baraka zake tayari kuanza mafunzo ya siku tano ya
 kuwajengea uwezo katika masuala ya masoko na Tehama mameneja na 
waandishi wa habari takribani 60 kutoka redio za jamii mbalimbali 
nchini, yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema 
Telecentre mkoani Mwanza.
Alisema
 kutekelezwa kwa mradi huo ni utekelezaji wa azimio la Windhoek la mwaka
 1991 linalohimiza matumizi ya redio jamii katika kuboresha maisha ya 
wananchi kutokana na kuonekana dhahiri kwamba wananchi wanapokuwa na 
nafasi ya kujieleza wanaweza kufanya makubwa zaidi.
Akifungua
 mafunzo hayo Ofisa mdhamini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na
 Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi redio jamii Micheweni, 
Ali Mohamed aliwataka mameneja na watendaji wa radio hizo kutekeleza 
ushauri wa UNESCO ikiwa na pamoja na kutekeleza maagizo ya utengenezaji 
wa vipindi vya vijana ili kupata nafasi ya kushindania nafasi moja ya 
upendeleo kwenda Paris , Ufaransa mwakani kwa tamasha la redio za jamii.
Aidha
 aliwataka watendaji kuwa makini katika kazi zao kutokana na serikali 
kuweka mazingira sahihi ya uendeshaji wa radio hizo kwa manufaa ya umma.
Mkufunzi
 wa darasa la mameneja wa redio mbalimbali za jamii Mkurugenzi Mtendaji 
wa ASMET, Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha mafunzo ya siku tano ya namna 
ya kuingiza kipato pamoja na kutafuta masoko kwa ajili ya kuendeleza 
vituo vyao yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na kuratibiwa na Shirika la 
Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yanayoendelea 
kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre mkoani 
Mwanza.
Baadhi
 ya mameneja wa redio mbalimbali za jamii wanaohudhuria mafunzo ya siku 
tano ya masoko na ujasiriamali yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na 
kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni 
(UNESCO).
Meneja wa kituo cha redio Orkonerei FM, Bw. Lucas Kariongi akihoji swali kwa mkufunzi wakati wa mafunzo hayo.
Mhasibu
 wa kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre, Bw. George 
Tumbo akiongaza washiriki wenzake katika kazi za vikundi wakati wa 
mafunzo hayo.
Afisa
 Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph 
akiendesha mafunzo ya matumizi ya Tehama kuwajengea uwezo wa kuweka 
kumbukumbu za vipindi na kukusanya vyanzo vya habari kwa kutumia 
“Tablet” kwa waandishi wa habari wa redio mbalimbali za jamii 
yanayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa 
na shirika la UNESCO yanayoendelea kwenye kituo cha Redio Sengerema 
mkoani Mwanza.
Afisa
 Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph 
akitoa maelekezo ya matumizi ya “TABLET” katika kuhifadhi na kuandaa 
habari kwa kutumia kifaa hicho.
Pichani juu na chini ni washiriki wa mafunzo hayo wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Teknolojia mpya ya “TABLET”.













No comments:
Post a Comment