Bunge
 Maalum la Katiba limependekeza muundo wa uongozi wa Serikali utakuwa na
  Makamu watatu wa Rais wa Jamhuri Muungano  wa Tanzania.
 Kauli
 hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mwenyekiti wa  Kamati ya Uandishi wa
 Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Andrew Chenge wakati akiwasilisha  Rasimu 
ya Katiba inayopendekezwa  wakati wa kikao cha arobaini na mbili cha 
Bunge hilo.
 Amesema
 kuwa katika mapendekezo hayo mgombea mwenza ndio atabaki kuwa  Makamu 
wa Kwanza wa Rais, na kwa upande wa Rais wa Zanzibar atakuwa Makamu wa 
Pili na Waziri Mkuu atakuwa Makamu wa tatu wa Rais.
 Amesema
 kuwa Kamati hiyo ya uandishi imeona ni busara mgombea mwenza kuendelea 
kuwa Makamu wa Rais kwa kuwa  itakuwa rahisi kwake kukaimu uongozi kama 
itatokea bahati mbaya Rais aliyemadarakani  hatakuwepo kwa namna moja au
 nyingine kwani ataendeleza ilani za mwenzake kuliko atakavyokuwa wa 
kutoka Zanzibar kama kutakuwa na vyama viwili tofauti vinatawala.
 Kwa
 upande wa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa pili , Chenge amesema kuwa 
hatua hiyo itasaidia kuimarisha muungano kwani kiongozi huyo ni kiungo 
muhimu katika kudumisha Muungano.
 “Suala 
 la Rais wa Zanzibar kuwa Makamu ni la msingi kwa kuwa ni kiungo muhimu 
ikizingatia historia ya nchi tangu mwaka 1964 muungano ulipoasisiwa 
ilikuwa hivyo hadi mfumo wa vyama vingi ulipoanza mwaka 1992,” alisema Mhe. Chenge huku akiongeza kuwa anakuwa hivyo kwa nafasi yake.
 Ameongeza kuwa Waziri Mkuu anakuwa Makamu wa Tatu kwa mujibu wa Cheo chake. 
No comments:
Post a Comment