
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba 
wamelazimisha sare ya mabao 2-2- na Wagosi wa Kaya, Coastal Union katika
 mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania bara uliomalizika jioni 
hii uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Simba chini ya kocha Patrick Phiri
 walianza mpira wakilishambulia mara kadhaa lango la Coastal na katika 
dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza Mnyama aliandika bao la kuongoza 
kupitia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na kiungo mkongwe, Shaaban 
Kisiga ‘Malone’.
No comments:
Post a Comment