TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, September 21, 2014

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YAPILI MHE. ALI HASSAN MWINYI KATIKA MKUTANO WA 22 WA AQRB

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akihutubia wataalamu mbalimbali wanaoshiriki katika mkutano wa 22 wa Elimu endelevu ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi jijini Dar e s salam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akitoa hutuba yake katika mkutano huo jijini Dar es Salaam.


Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi wapili kutoka kushoto akimshukuru Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa (AQRB) Dkt. Ambwene Mwakyusa.

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akikabidhi cheti kwa mwanafunzi bora wa Insha kutoka Mkoa wa Dodoma Consolata Chidabile. Kulia ni Waziri wa Ujenzi akishuhudia tukio hilo.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi katikati akiangalia moja ya tiles mara baada ya kufungua mkutano huo.

Washiriki mbalimbali wa Mkutano wa 22 wa Elimu endelevu ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi jijini Dar e s salam wakisiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi katika mkutano huo.

Msajili wa bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB),  Arch. Jehad  A. Jehad  akitoa hotuba yake.


Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya  pamoja na wanafunzi walioshinda katika shindano la Insha kutoka mikoa mbalimbali.
 (Picha kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Ujenzi).
=========================================== 

Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi amezungumzia kuridhishwa kwake na utendaji wa Bodi ya Usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi nchini (AQRB).

Akizungumza katika Mkutano wa 22 wa Elimu endelevu wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi jijini Dar Es Salaam, Mzee Mwinyi amesema ni wajibu wa bodi hiyo kuhakikisha utekelezaji endelevu wa taratibu za mienendo ya kitaalamu dhidi ya  usajili wa wataalam hao nchini unazingatiwa kwa viwango vya ubora.
“Nimeridhishwa na Kitendo cha Msajili wa Bodi hii kuwafutia leseni Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi 86, waliokiuka miiko ya utekelezaji wa taaluma hii, hivyo endeleeni kulisimamia hili ili kuhakikisha taaluma hii haipati dosari”,amesisitiza Rais Mstaafu Mwinyi.
Aidha, Rais Mstaafu Mwinyi amewataka watendaji na wataalam wa fani hiyo kupiga vita rushwa na ubadhirifu ili kuhakikisha jamii inapata majengo yaliyo bora na ya kudumu kwa muda mrefu na kuwataka wale watakaokiuka maadili ya taaluma hiyo wadhibitiwe kwa mujibu wa sheria.
“Siku za hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia  majengo mengi yanaanguka nchini na hii inasababishwa na wataalam kutokufuatilia kikamilifu katika maeneo yao ya kazi na kusababisha hasara na watu kupoteza maisha.
Katika hatua nyingine Rais Mstaafu Mwinyi ameipongeza AQRB kwa kuandaa mashindano ya insha kwa shule za Serikali kuhusu taaluma hiyo ambayo yatahamasisha wanafunzi  kusoma masomo ya Science na kuongeza wataalam hao nchini.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Bodi hiyo kwa kazi  nzuri za Ubunifu Majengo zinazofanywa na wakandarasi nchini na kuwataka kushirikiana na taasisi mbalimbali za ndani na  nje  ya nchi ili kubuni majengo yaliyo bora na yatakayodumu kwa muda mrefu.
Waziri Magufuli amebainisha kuwa zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 150 zimetengwa ndani ya mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kusaidia wataalam wa fani hiyo wanaomaliza masomo yao.
Naye, Msajili wa Bodi hiyo Bwana, Jehad A. Jehad amesema kuwa zaidi ya wataalam elfu moja (1000), wamesajiliwa tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo mwaka 1998 na kuiomba Serikali kuanzisha vitivo vya taaluma  hiyo katika vyuo vikuu mbalimbali nchini ili kukidhi haja ya wataalam elfu themanini na tano (85,000) ifikapo mwaka 2025.
Mkutano huo wa siku moja unaowakutanisha wadau mbalimbali wa ujenzi nchini una lengo la kajadili ‘sheria ya manunuzi namba 7 ya mwaka 2011 na athari zake katika mazingira ya ujenzi.

No comments:

Post a Comment