JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI 
“PRESS RELEASE” 
TAREHE                26.09.2014.
- MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI WILAYA YA MBOZI.
 
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA BHANGI JIJINI MBEYA.
 
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI WA VWAWA MJINI 
WILAYA YA MBOZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWILE LISBON @ MANGEU (25) 
ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI 
WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUMKAMATA KWA TUHUMA ZA 
KUVUNJA NA KUIBA KATIKA NYUMBA YA MTU MMOJA AITWAYE BRIGATE SICHALWE, 
MKAZI WA VWAWA MJINI.
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
 24.09.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO MAENEO YA FLORIDA VWAWA 
MJINI, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. AIDHA, 
TAARIFA ZA AWALI ZINADAI KUWA MAREHEMU ALIKUWA MHALIFU MZOEFU NA ALIKUWA
 AKISAKWA NA POLISI KWA MUDA MREFU KUTOKANA NA KUTUHUMIWA KWA VITENDO 
VYA UVUNJAJI NA KUIBA KATIKA MAENEO MBALIMBALI.
 KATIKA CHUMBA ALICHOKUWA AKIISHI 
MAREHEMU, KUMEPEKULIWA NA KUKUTWA MAGODORO MAWILI YALIYOTAMBULIWA KUWA 
NI YA WIZI. HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI. MWILI 
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA – MBOZI.
 TAARIFA ZA MISAKO:
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA 
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHRISTOPHER GEOFREY 
(23) MKAZI WA MBALIZI AKIWA NA MISOKOTO MITATU YA BHANGI SAWA NA UZITO 
WA GRAMU 15 IKIWA KWENYE GANDA LA SIGARA.
 MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO
 ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 25.09.2014 MAJIRA YA SAA 16:30 JIONI HUKO 
MAENEO YA MSITU WA KILIMO, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA 
MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA 
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA 
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA 
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI 
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
 Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA. 

No comments:
Post a Comment