TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, September 25, 2014

MANGULA AFUNGUA OFISI MPYA YA CCM-CHATO

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula katikati akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Ofisi ya CCM wilaya ya Chato. Wengine katika picha ni Mbunge wa Chato Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Geita Said Magalula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma.

 Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula kulia mara baada ya kumpokea katika kata ya Buseresere Mkoani Geita. Kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ndugu Joseph Msukuma

 Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula juu ya gari akihutubia mamia ya wakazi wa Buseresere mara baada ya kuwasili katika eneo hilo.

 Wananchi wa Buseresere wakimsiliza Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipopita kwenda kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Mangula

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akisalimiana na baadhi ya wananchama wa CCM katika kata ya Bwanga wilayani Chato mara baada ya kusimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili ya Ufunguzi wa Ofisi Mpya ya CCM wilaya ya Chato.

 Taswira ya Jengo jipya la Ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Chato ambalo ilikuwa ni ahadi ya Mbunge wa Chato ambaye pia ni waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akihutubia wananchi wa Bwanga waliofika kumsalimia wakati akiwa njiani kuelekea Chato ambapo alizindua jingo jipya  la Ofisi hiyo ya kisasa.

 Kijana wa Kikundi cha Ngoma cha Chato akionyesha umahiri wake wa kuzungusha ringi la Tairi la baiskeli kwenye mboni yake ya jicho hali iliyowashangaza wananchi wengi waliofika.

  Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kulia akifurahia jambo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula.



Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akivuta utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Chato ambayo ilikua ahadi ya Mbunge wa Jimbo hilo. Picha na Mpiga Picha Wetu


=====================================================================



Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula amempongeza Mbunge wa Jimbo la Chato Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na utekelezaji mzuri wa wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye jimbo lake.
Mheshimiwa Mangula alitoa kauli hiyo mara baada ya kufungua rasmi jengo la ofisi ya CCM Wilaya ya Chato ambalo liliahidiwa kujengwa na Mbunge huyo.
Mangula aliongeza kuwa CCM inajivunia mafanikio hayo ambayo ni hazina kubwa kwa taifa na kukijengea chama heshima kubwa ndani na nje ya nchi.

“Magufuli kama anavyoitwa jembe amefanya kazi kubwa ambayo kila mtu anaiona, miaka ya nyuma aliwahi kuahidi kuwa mtu atatoka Mtukula hadi Mtwara kwa usafiri wa Tax lakini hakuna ailiyeamini, leo hii hilo linawezekana”

Ndugu Mangula aliongeza kuwa wakati alipokuwa   Mkoa wa Kagera miaka ya 90s, hali ya Barabara nchini hata hapo Chato ilikua mbaya sana, ilimlazimu kutumia siku mbili hadi tatu ili kufika Njombe lakini leo hali ni tofauti kutokana na miundombinu kuboreshwa sana.

Aidha, Ndugu Mangula amepongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa haraka katika sekta ya Elimu jimboni hapo kwani kutoka shule moja hadi shule zaidi ya 120 ni jambo la kujivunia sana.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chato Dkt. John Pombe Magufuli  alieleza kuwa Chato imetoka mbali sana kimaendeleo kwani hapo mwanzo ilikua kijiji ikapiga hatua na kuwa Kata na kwa sasa ni Wilaya jambo ambalo ni la kujivunia sana.

Mbunge huyo aliongeza kuwa Jimbo hilo kwa sasa limepiga hatua kubwa sana katika Sekta ya Mawasiliano,umeme,maji na miundo mbinu ya barabara ambapo awali maendeleo hayo hayakuwepo.
“Nakumbuka kipindi cha nyuma kulikuwa na basi moja tu ambalo lilikuwalikifanya safari zake kuelekea Mwanza, na likikuacha basi huwezi kusafiri tena, lakini kwasasa mabasi zaidi ya 40 yanapita hapa kwenda sehemu mbalimbali ikiwemo Uganda” alibainisha Mheshimiwa Magufuli.

Mheshimiwa Magufuli aliongeza kuwa kwa upande wa Sekta ya elimu jimbo hilo limepiga hatua kubwa kwani kwa sasa kuna shule za sekondari zaidi ya 30 na shule za msingi 131.

Pia alitaja mfano wa barara ambazo zinatengezwa katika jimbo lake kwa kiwango cha lami kuwa ni pamoja na barabara ya kutoka Bwanga  kuelekea Biharamulo na Bwanga Uyovu ambazo zinajengwa na Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi ili kurahisisha maendeleo ya kiuchumi jimboni hapo,”alifafanua Magufuli.

Mheshimiwa Magufuli aliwaahidi wakazi wa Buseresere na Bwanga kuwa kero yao ya kukosa maji na mipango miji ataiwasilisha Serikalini haraka iwezekanavyo ili kuweza kushughulikiwa.

No comments:

Post a Comment