- IBARA 186 ZA TUME ZABORESHWA
 - IBARA 41 MPYA
 - IBARA 47 ZA TUME ZABAKI KAMA ZILIVYO
 - IBARA 28 ZA TUME ZAFUTWA
 
Na Mwandishi wa MAELEZO-Dodoma
Bunge Maalum la Katiba 
limependekeza jumla ya Ibara 274 katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania inayopendekezwa.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini 
Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum Mhe. Andrew 
John Chenge wakati akiwasilisha Bungeni Rasimu ya Katiba inayopendekezwa
 katika Kikao cha Arobaini na mbili.
Amesema kuwa wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba inawasilisha Bungeni Rasimu Katiba inayopendekezwa iliwasilisha Ibara 271.
Mhe. Chenge amesema kuwa baada ya 
kupitia Rasimu Katiba ya Tume walifanikiwa kupata Ibara 274 ambazo ndio 
wanapendekeza ziwemo katika Katiba mpya ijayo.
Ameongeza kuwa kati ya hizo 
zilizopendekeza na Bunge Maalum la Katiba 233 zimetokana na mapendekezo 
ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyowasilisha Bungeni mwezi Machi mwaka
 huu.
Amesema kuwa katika Ibara 47 kati 
ya zote za Tume 47 hazikufanyiwa marekebisho badala yake zilibaki kama 
zilivyopendeza wakati Ibara 186 ndio zilifanyiwa maboresha na 
marekebisho kwa ajili ya kuziboresha na wajumbe wa Bunge Maalum la 
Katiba.
Mhe. Chenge ameongeza Bunge hilo limeongeza Ibara 41 mpya na kufuta 28 zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
 Rasimu ya Katiba inayopendekeza 
na Bunge Maalum la Katiba ina sura mpya mbili mpya ambayo ni ardhi 
,maliasili na mazingira na sura inayohusu Serikali ya Mapinduzi ya 
Mapinduzi, Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawakilishi.

No comments:
Post a Comment