Wasanii
 wa muziki wa Bongofleva Ommy Dimpo na Vanessa Mdee a.k.a Vmoney 
wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa mashabiki wa tamasha
 la Fiesta 2014  lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Samora mkoani 
Iringa,huku miluzi na shangwe zikisikika kila kona ya uwanja.Tamasha la 
Fiesta linatarajiwa kufanyika kesho mjini Morogoro katika uwanja wa 
Jamuhuri ambapo wasanii mbalimbali wa bongofleva watatumbuiza.
Baadhi ya Mashabiki wakishangqweka.
 Msanii
 Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva,Selemani Msindi 
a.k.a Afande Sele Mfalme wa Rhymes,akiimba kwa hisia kubwa juu ya jukwaa
 la tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Samora 
mkoani Iringa.
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye tamasha hilo la Fiesta 2014 ndani ya Samora mjini Iringa hapo jana.
Anajiita
 Rais wa Manzese,jina lake la kisanii anajiita Madee kutoka kundi la TIP
 TOP CONECTIONs,akiimba mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Iringa 
waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa 
Samora hapo jana.Tamasha la Fiesta kesho linatarajiwa kufanyika ndani ya
 uwanja wa jamuhuri mkoani Morogoro.
Wakazi wa mji wa Iringa waliojitokeza ndani ya tamasha la Fiesta wakishangweka kwa raha zao.







No comments:
Post a Comment