TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, August 18, 2014

Kinondoni yatwaa ubingwa ARS 2014.

 Naibu katibu mkuu wa wizara ya habari ,utamaduni na michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akimkabidhi kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars 2014 nahodha wa timu ya wasichana ya Temeke Fatuma Issa baada ya kuibuka mabingwa. naeshudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso. 
 Makamu mwnyekiti wa chama cha soka cha wanawake Tanzania Rose Kisiwa akimkabidhi kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars 2014 nahodha wa timu ya mkoa wa kisoka Kinondoni Fred Mazuri  Baada ya kuibamiza Ilala 5 – 3, Jumapili jijini Dar-es-Salaam. 
Wachezaji wa timu ya mkoa wa kisoka ya Kinondoni wakishangilia ubingwa wa Airtel Rising Stars 2014 baada ya kuifunga timu ya Ilala 5 – 3, Jumapili jijini Dar-es-Salaam.

Kinondoni yatwaa ubingwa ARS 2014
Timu ya Kinondoni wavulana imetwaa uchampioni wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars kwa kuifunga timu ngumu ya Ilala 4-2 kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya sare ya 1-1 katika muda wa kawaida wa dakika 90.

Mechi hiyo iliyotanguliwa na shamra shamra za maandamano na halaiki, ilikuwa yenye upinzani mkali na baada ya kosa kosa za hapo na pale Kinondoni walipata goli katika dakika ya 31 kupitia kwa Kassim Kitwana kwa shuti kali la mbali lililomshinda mlinda mlango wa Ilala Sulum Siasa. 

Goli hili lilibadili kasi ya mchezo huku Ilala wakitafuta goli la kusawazisha na juhudi zao zilifanikiwa kuzaa matunda katika dakika ya 40 baada ya kutoke piga ni kupege golini mwa timu ya Kinondoni na mchezaji hatari Juma Yusufu kufunga kwa huti la karibu.

Kipindi cha pili kilianza kwa kushambuliamba kwa zamu lakini hakuna timu iliyofanikiwa kupata goli la kuongoza hadi dakika ya mwisho. Ndipo refa akaamua kumaliza ubishi kwa penati.Katika penati tano, Kinondoni walifunga kupitia kwa Abdul Malangali, Milaji Gwangaya, Omri Rashid na Abubakari Nuru wakati Kassim Kitwana alipaisha. Kwa upande wa Ilala waliofanikiwa kufunga ni Abdul Bitebo na Rashid Mohamed wakati Maisala Adam na nahodha wa timu Shaban Zuberi walikosa.

Akifunga fainali hizo za taifa za Airtel Rising Stars, mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Professor Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Naibu Waziri wa wizara hiyo Mheshimiwa Juma Nkamia, aliipengeza kampuni ya Airtel kwa kujitokeza kusaidia maendeleo ya soka hapa nchini.

Alitoa wito kwa vijana kuzingatia nidhamu katika michezo na kujituma ili kupata mafanikio na kusema kuwa katika dunia ya leo soka ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi. Pia alisema kuwa kufanikiwa kwao kutaiwezesha Tanzania kufahamika zaidi kimataifa. Naye Mkurungenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso amesisitiza nia thabiti ya kampuni yake kuendelea kudhamini mashindano ya vijana ya Airtel Risig Stars.  

No comments:

Post a Comment