TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, February 12, 2012

Upandaji miti kwa jumuiya ya wazazi kwa mkoa wa Arusha


Katibu wa Jumuiya ya wazazi katika chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Arusha Bi Anna Kiromo akipanda mti katika shule ya msingi mkombozi ikiwa kama ni njia mojawapo ya kuhifadhi mazingira ndani ya umoja huo. (PICHA NA GLADNESS MUSHI WA -ARUSHA)
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa wanafuraia jambo mara baada ya umoja huo kupanda miti jijini hapa
Mmoja wa viongozi katika chama hicho naye akiweka kumbukumbu ya mti katika eneo hilo la shule ya mkombozi kaloleni

NA GLADNES MUSHI- ARUSHA
VIONGOZI wa dhebebu la Ah madiyya nchini wamewasihi waiislamu wenzao kote nchini ,kuungana na kuomba dua la amani kuiombea nchi ili kuepusha matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani , ambayo yamekuwa yakienda kinyume na maandiko matakatufu yaliyopo kwenye Quran .
Wakizungumza kwenye kongamano la amani lililofanyika mwishoni mwa wiki katika msikiti Ah madiyya jijini hapa,walidai kuwa hakuna maagizo ya mwenyezi mungu yanayotoa mamlaka kwa kikundi ama mtu yoyote kutekeleza mauaji dhidi ya waumini wa dini nyingine.
Kiongozi mkuu mwenye cheo cha Amiri na mbashiri mkuu wa jumuiya ya waislamu wa Ahmadiyya nchini,Tahir Mohmood Choudhly aliwaomba waislamu kote duniani kuungana na kulaani vitendo vya kinyama vinavyofanyika kote duniani hususani nchi chenye uislamu kwa madai ya kutaka haki.
Aliwaomba watanzania kuwalilia wananchi wote waliouawa kutokana na machafuko mbalimbali yanayoendelea katika nchi za uislamu na kukilaani kikundi kidogo wa wanamigambo cha Boko haramu nchini Nigeria, kinachotekeleza mauaji kwa kisingizio cha kufuata maagizo ya uislamu yalioko kweneye Quruan.
‘’sisi waislamu tufike mahali tuelezane ukweli kwani matukio mengi ya uvunjifu wa amani yakiwemo kujilipua yanasababishwa sana na waumini wenzetu ,hakuna maandiko yanayoagiza dini ya kiislamu iteketeze dini nyingine ‘’alisema Choudhly.
Aidha aliongeza kwa kuwataka viongozi wa madhehebu ya dini nchini kusimama imara katika kutetea amani na kujiepusha na uchochezi,kwani taifa linawategemea sana katika kuepusha machafuko yanayoweza kuibuka.
Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi kuheshimu viongozi waliopo madarakani na kuacha kupinga kila kitu kinachotamkwa na kiongozi aliyeko madarakani, badala yake watoe mchango wa kusukuma maendeleo ya taifa hadi utakapo fanyika uchanguzi mwingine.
Naye Sheikh mkuu wa Ahamadiyya kanda ya kaskazini,Mzafara Ahamad,alisema kuwa lengo la kongamano hilo lililowashirikisha viongozi mbalimbali wa madhehebu mbalimbali ya dini ya kiislamu nchini ni kutoa mada ya kuomba amani .
Alisema kuwa kongamano hilo lilienda sanjari na uzinduzi wa msikiti huo wa Ahmadiyya muslim Jamaint uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 70 kwa ajili ya ukarabati ulioanza mwishoni mwa mwaka jana.
Kwa upande wa sheikh mkuu wa Aha madiyya mkoa wa Morogoro,Bakari Kaluta,aliwataka viongozi wa dini nchini kutawala kiuadilifu huku wakiongozwa na mwenyezi mungu katika mahubiri yao na kuacha kuwa sehemu ya kuleta mitafaruku ya kidini.
Ameyasihi madhebebu ya dini kuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano ya kuomba amani ,kwani bila hivyo nchi itaelekea kubaya kwakuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitumia vibaya maandiko matakatifu kwa kuhubiri uvunjifu wa amani kwa maslahi yao binafsi.
Naye meya wa jiji la Arusha ,Gaudence Lyimo aliyekuwa mgeni rasimi katika kongamano hilo,aliyasifu madhehebu ya dini ya kiislamu kwa kuandaa kongamano hilo la kuomba amani ,aliwatia moyo viongozi hao kuwa serikali inatambua mchango wao na inawaungamkono kwa jambo hilo.
Aliwasihi viongozi hao wa dini kuwa sehemu ya serikali katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa amani inapatikana kwa kila mtu hapa nchini na duniani kote.

A normal girl from Newark, NJ who became the first ever female to break the records in the charts, she made a breakthrough with such a VOICE the world had never heard before, Whitney Elizabeth Houston, not her colour, background, gender neither financial constraints could hold her back, there is a LOT to be learnt from this ALL TIME LEGEND, a simple mistake in life can have it all, she was among the most respectful, beautiful, humble, no words could define her Amazing character that she hold high attached to God's worship and praise, but sooner or later a creature came into her life and all gone wrong, Whitney she lost it all because she had true LOVE which unfortunately cost her lifetime, it is a GREAT LESSON, she has left a LEGACY for all of us to learn from and be more careful, more focused and on top off all not to sacrifice our inner self and connection with Lord for the sake of a wicked soul, She tried her best to find herself back but the wicked media which always made infamous rants from her mistakes and staggering moments could not let her to, perhaps it was too much for her to be able to hold onto maybe, one thing for sure I know all Angels are beautiful but at least I am sure for now not only when my day comes I will meet beautiful Angels but also one with strikingly, amazingly, absolutely GREATEST VOICE OF ALL TIMES, Whitney Elizabeth Houston

Mchezaji Haroub Canavaro wa timu ya Yanga akijaribu kumzuia mshambuliaji wa timu ya JKT Ruvu wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo jijini Dar es salaam. Mshabuliaji wa Yanga Davis Mwape ameipatia timu hiyo goli la kuongoza lililodumu mpaka mpira ulipomalizika na kufanya na kufanya timu ya Yanga kutoka kifua mbele kwa goli matokeo ya 1-0.
Wachezaji wa timu ya Yanga na JKT Ruvu wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Timu zikiingia uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo wa ligi kuu ya Vodacom.

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiwa meza kuu na Rais wa Zanzibar Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mh Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM Mh Wilson Mkama kabla ya kuanza kwa mkutano wa Halmashauri Kuu leo katika jengo la White House la Makao Makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo February 12, 2012

Mdhamini wa timu ya Yanga ya Jangwani jijini Dar es salaam Mama Fatma Karume akizungumza katika hafla ya timu hiyo kuimiza miaka 77 tangu kuanzishwa kwake iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock na kuhudhuriwa na wanachama na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu, huku mgeni rasmi akiwa Dk. Fenella Mkangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na michezo anayeonekana kulia katika picha kushoto ni baadhi ya wazee wa Yanga. Mama Fatma Karume alisema Yanga ni mzee wa miaka 77 lakini katika michezo anaweza kukimbia kwa kasi ileile ya kimichezo, hivyo akamuomba mola ili klabu hiyo izidi kupata mafanikio katika michezo.
Mgeni rasmi katika hafla ya timu ya Yanga kutimiza miaka 77 Dk Fenella Mkangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na michezo akizungumza katika hafla hiyo, huku Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga akifurahia jambo, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadik Meck Sadik na kushoto ni mdhamini wa Yanga Mama Fatma Karume.
Katibu Mkuu wa Yanga Selestini Mwesigwa akipiga mamombi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo kulia ni George Kavishe Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadik Meck Sadik.
Wadau kutoka Peacock Hotel wakijadiliana jambo ili kuhakikisha sherehe hiyo inafana zaidi.
Ancle Hashim Lundenga kulia ndani kama unavyomuona akiwa ametulia kitini Kutoka kulia ni Kocha mkuu wa Yanga Kostadin Papic shabiki mkubwa wa Yanga Emmanuel Mpangala na Kocha msaidizi wa timu hiyo mwenye (Mzuka Mwingi) Fred Felix Minziro wakifuatilia mambo mbalimbali katika hafla hiyo.
Kulia ni wanachama wa Yanga Mh. Mudhihir Mudhihir kulia na Jaji Mkwawa wakiwa katika hafla hiyo jana uziku.
Mashabiki ha wa pia walikuwepo kuipa tafu klabu yao.
Kundi la THT likitumbuiza katika hafla hiyo
Hii ndiyo mandhari ya ukumbi inavyoonekana katika picha

· Yashusha Gharama za m-pesa kwa 75%
· Kiwango cha kuongeza salio kwa m-pesa nacho chaongezwa hadi 25%
Kampuni ya huduma za simu za mkononi inayoongoza nchini leo imetangaza kwa mpigo kwa wateja wake nchini jumla ya ofa 4 zitakazowafanya kuzidi kufaidika, kuwezeshwa na kufurahia zaidi huduma za Vodacom m-pesa.
Wateja wa m-pesa sasa wamepunguziwa gharama za kufanya miamala kupitia huduma hiyo ambapo sasa kila muamala utagharimu Shilingi 50 ikiwa ni punguzo la asilimia 75. Wakati huo huo Vodacom ikiongeza kiwango ambacho mteja anaweza kununua muda wa maongezi kupitia huduma hiyo ya m-pesa hadi asilimia 25 kutoka asilimia 10 ya sasa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza amesema”Tunatambua ni kwa kiwango gani huduma ya m-pesa imekuwa ya umuhimu kwa maisha ya kila siku ya Watanzania, hivyo ni jambo la muhimu pia kwetu kuwapatia ofa zinazoakisi matumizi yao na kuyafanya kuwa rahisi na nafuu zaidi.” “Hii ndio dira yetu kwa mwaka huu na kuendelea” Alisema Bw. Meza.
Ofa nyengine iliyotangazwa na kampuni ya Vodacom Tanzania ni inayomwezesha mteja wa m-pesa sasa kuweza kutuma kiasi cha chini zaidi cha fedha cha shilingi 500 kupitia simu yake ya mkononi. Bw. Meza ameielezea ofa hii kuwa inalenga kuhakikisha kila Mtanzania bila kujali hali yake ya kiuchumi anafaidika na huduma bora,salama, ya uhakika na kuaminika ya m-pesa.
Aidha, pamoja na ofa hizo, kampuni ya Vodacom imezindua pia promotion ya m-pesa ambapo jumla ya Shilingi 480 Milioni zitashindaniwa na wateja kadri ambavyo wanavyotumia huduma ya m-pesa.
Katika promosheni hii wateja 100 watakuwa wakijishindia zawadi ya fedha taslimu za kitita cha Shilingi 50,000 kwa kila mshindi kupitia droo zitakazochezeshwa kila siku huku droo kuu ya kila mwezi kwa miezi mitatu ikitoa mshindi wa Shilingi 10 Milioni. Promosheni hiyo itadumu kwa siku tisini kuanzia Februari 13, mwaka huu.
“Dhamira yetu ni ya dhati kuhakikisha wateja wetu wanakuwa na furaha wakati wote na huku tukiwawezesha kadri wanayotumia huduma ya MPESA. Tutaendelea kuboresha mfumo wa m-pesa sambamba na huduma zinazopatikana katika MPESA ili izidi kuendana na mahitaji halisi ya maisha ya kila siku ya wateja.” Alisema Bw. Meza.
Kupitia huduma ya m-pesa mteja anaweza kufanya malipo kwa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo kununua umeme – LUKU, kulipia DAWASCO na DSTV. Aidha huduma ya m-pesa inaweza pia kutumika kulipia tiketi za usafiri wa ndani wa anga kwa mashirika ya ndege ikiwemo Precision Air na Coastal Air, kulipia ada za shule, kuweka na kutoa fedha katika akaunti ya benki ya CRDB na huduma nyengine nyingi.
Hakuna shaka huduma ya Vodacom m-pesa ndiyo huduma ya kibenki kupitia simu za mkononi inayoongoza nchini ikiwa na mtandao mpana wa mawakala zaidi ya 18,000 walionena nchi nzima mijini na vijijini na inayokua kwa kasi. Ubora na umashauri wa huduma hii unaifanya kampuni ya Vodacom kuzidi kung’ara na kuongoza soko la huduma za simu za mkononi nchini.

Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Azam lililochezwa Februari 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 67,548,000.
Jumla ya watazamaji 19,257 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 117 kwa kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000 kwa VIP A.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 10,303,932.20 kila timu ilipata sh. 13,182,800.34, uwanja sh. 4,394,266.78.
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,757,706.78, TFF sh. 4,394,266.78, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,197,133.39, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 439,426.78 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,394,266.78.
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. wamuzi wa akiba sh. 30,000, tiketi sh. 4,350,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 1,347,990,280 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 1,555,420.

Kamati ya Ligi imeagiza mchezaji Patrick Mafisango wa Simba aandikiwe barua ya onyo kutokana na kumsukuma mwamuzi Isihaka Shirikisho baada ya kumuonesha kadi nyekundu mchezaji mwenzake Haruna Moshi kwenye mechi kati ya Simba na JKT Oljoro.
Nayo klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya washabiki wake kurusha makopo ya soda na chupa za maji wakipinga uamuzi wa mwamuzi Shirikisho kumtoa kwa kadi nyekundu Haruna Moshi.
Wachezaji waliopigwa faini ya sh. 500,000 kila mmoja baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kutokana na kupiga ambapo pia wanakosa mechi tatu za ligi kwa mujibu wa Kanuni ya 25 ni nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa na Cyprian Lukindo wa Villa Squad.

Waamuzi watatu na kamishna mmoja wameondolewa kuchezesha na kusimamia mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na kuonesha upungufu katika uchezeshaji na usimamizi.
Uamuzi huo ulifanywa na Kamati ya Ligi iliyokutana jana (Februari 11 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine ilipitia taarifa za waamuzi na makamishna wa VPL ambayo leo (Februari 12 mwaka huu) inaendelea katika raundi ya 17.
Peter Mujaya wa Mwanza aliyechezesha mechi namba 101 kati ya JKT Ruvu Stars na Yanga amefungiwa kwa miezi 12 kwa mujibu wa Kanuni ya 26(a) ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kushindwa kumudu mchezo huo, hivyo kupata alama za chini.
Naye Isihaka Shirikisho wa Tanga ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa VPL msimu huu kwa kushindwa kumudu mchezo namba 105 kati ya Simba na JKT Oljoro. Moja ya udhaifu alioonesha ni kushindwa kumuadhibu mchezaji Patrick Mafisango ambaye alimsukuma baada ya kumuonesha kadi nyekundu Haruna Moshi wa Simba.
Mwamuzi mwingine aliyefungiwa kwa miezi 12 kwa mujibu wa Kanuni ya 26(a) ni Kennedy Mapunda wa Dar es Salaam aliyechezesha mechi namba 107 kati ya Villa Squad na Simba. Moja ya udhaifu wa Mapunda ni kushindwa kumpa kadi nyekundu Fred Cosmas wa Villa Squad baada ya kumuonesha kadi ya pili ya njano.
Pia waamuzi wasaidizi Michael Mkongwa wa Iringa na Kudura Omary wa Tanga waliochezesha mechi namba 112 kati ya Yanga na Mtibwa Sugar wameondolewa katika mechi zilizobaki za VPL kwa kutokuwa makini. Mwamuzi wa mechi hiyo Ibrahim Kidiwa amepewa onyo.
Waamuzi wengine waliopewa onyo na kutakuwa kujirekebisha ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam aliyechezesha mechi namba 92 kati ya Moro United na Yanga, na mwamuzi msaidizi wa mechi ya Simba na Coastal Union, Issa Malimali wa Ruvuma.
Kamishna wa mechi namba 112 kati ya Yanga na Mtibwa Sugar, Mohamed Nyange ameondolewa katika orodha ya makamishna kwa mechi zilizobaki za VPL kutokana na ripoti yake kuwa na upungufu.

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Mwenyekiti Msataafu CCM Ali Hassan Mwinyi amewataka wananchi wa Jimbo la Uzini kutofanya makosa kumchagua Mgombea wowote wa Chama cha Upinzani badala yake wamchague Mgombea wa CCM Mohammed Raza Daramsi ambaye ndiye mgombea anayefaa kwa ajili ya maendeleo yao
Mwinyi ameyasema hayo katika kiwanja za Manzese Uzini wakati alipokuwa akifunga kampeni za CCM katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Jimbo hilo
Amesema Mohammed Raza ni Mpenda maendeleo na anayejali watu hivyo wananchi wa Uzini wana kila sababu za kumchagua Mgombea huyo wa CCM ambaye anawazidi sifa wagombea wote wa vyama vya upinzani
Ameongeza kuwa kama watamchagua Raza matatizo ambayo yanalikabili Jimbo la Uzini yatakuwa yamepata suluhisho la kudumu kutokana na dhamira ya dhati iliyojengeka katika nafsi ya Mgombea wao na Chama chao
Ameyataja matatizo ambayo yanalikabili Jimbo hilo kuwa ni pamoja na Maji Safi na Salama, Elimu na Afya na kudai kuwa yanaweza kupata suluhu iwapo Raza atachaguliwa
Mwinyi ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewasisitiza mamia ya wananchi hao waliohudhuria katika kampeni hizo kutekeleza ahadi ya Chama kwa kumchagua Raza kama ambavyo Uongozi wa CCM ulitekeleza ahadi ya wananchi hao kwa kumsimamisha mgombea huyo ambaye alikuwa chaguo lao
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Balozi Seif Idd amewataka wananchi hao kutochezea bahati waliyoipata ya kumchagua Raza kwani ni mtu mwenye upendo na kuwajali wanyonge.
Mjumbe huyo ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar amesema kuwa ikiwa Raza ameweza kusaidia wananchi wa Majimbo mbali mbali wakiwemo wa Jimbo lake hapana shaka Raza atakuwa na juhudi zaidi ya kuwasaidia wananchi wake mwenyewe
Kwa upande wake Raza amesema atahakikisha anawapatia maendeleo wananchi wa Jimbo la Uzini pale watakapomchagua na kuweza kuwa nao kwa bega katika kusimamia Ilani ya CCM
Amesema Ilani ya CCM ndiyo ilani ambayo inatekelezeka kwa maendeleo ya wananchi wa Jimbo hilo hivyo waendelee kumuunga mkono kwa kumpa kura ambazo zitamfanya awe Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ili awatumikie
Wananchi wa Jimbo la Uzini watapiga kura kesho kumchagua Mwakilishi wa Jimbo hilo ambapo jumla ya Wagombea Watano wa Vyama mbali mbali vya siasa nchini wanagombea nafasi hiyo iliyoachwa kufuatia kifo cha Mwakilishi wa Jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment