TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, March 21, 2013

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAM CHADHAMINI FAINALI YA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13



CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAM CHADHAMINI FAINALI YA TAIFA  MISS UTALII TANZANIA  2012/13

Chuo Kikuu cha Dar es salaam ni miongoni mwa taasisi mbalimbali nchini zilizoitikia wito wa kudhamini fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 ikiwa ni baada ya kupata taarifa ya kuwapo kwa mapungufu mbalimbali ambayo yamepelekea kusogezwa mbele fainali zake kutokana na upungufu na ufinyu wa bajeti kiasi cha shilingi milioni 170 zilizotokana na kushindwa kwa baadhi ya wadhamini kutimiza ahadi zao.
udhamini huo ambao unalenga moja kwa moja kwa washindi, ni pamoja na kulipiwa gharama za ada ya masomo katika musimu wa 2013/14  kozi ya uandishi wa habari  katika chuo kikuu cha dar es salaam ,school of journalism and mass communication( sjmc).
akizungumza jijini dar es salaam kuhusu udhamini huo , rais wa miss utalii tanzania, gideon chipungahelo alisema kwamba ni jambo la kupendeza kwa kuwa kuna  ufinyu wa bajeti katika kukamilisha fainali za taifa za miss utalii tanzania.
“tunashukuru kuona taasisi kama chuo kikuu cha dar es salaam kinajitokeza kuunga mkono juhudi za miss utalii tanzania katika harakati za kufanikisha fainali za taifa za miss utalii tanzania 2012/13 ambazo zinalenga kuutangaza utalii wa tanzania, ikiwa ni pamoja na chuo kikuu cha dar es salaam ambacho kina historia ukilinganisha na vyuo vingine katika ukanda wa afrika mashariki na kati, hivyo nazidi kusisitiza kwa wadau, taasisi na makampuni binafsi kujitokeza kuunga na kusaidia juhudi hizi ili fainali za mwaka huu ziwe tofauti na fainali za miaka ya nyuma” alisema chipungahelo
Na kuongza kwamba ahadi kwa wadau na wapenzi wa mashindano haya iko pale pale, kwa kuwa dhamira ipo na nia ya kulifanya shindano la Miss Utalii Tanzania kuendelea kuwa bora na lenye mafanikio makubwa kuliko jingine lolote nchini na afrika iko pale pale, na hili litadhihirika wakati wa fainali kuu ya mashindano  mwishoni mwa mwezi huu, hivyo wadau,wafanyabiashara, makampuni binafsi na ya umma, hasa ya kizalendo watakaojitokeza siku hiyo watashuhudia burudani ya aina yake kutoka kwa Warembo mbalimbali wanaowakilisha Mikoa yao,na wawakilishi wa Kanda za Vyuo Vikuu Tanzania bara na Zanzibar.

Miss Utalii Katavi akionekana mwenye Furaha wakati akipozi kwa ajili ya Picha















No comments:

Post a Comment