TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, April 24, 2013

“TWANGA PEPETA” KUNOGESHA TAMASHA LA WASUKUMA NA WAKEREWE” CCM KIRUMBA NA NANSIO UKEREWE APRIL 27 NA 28.

Mkurugenzi Msaidizi wa My Way Entertainment, Rose Mwita(Kulia) akifafanua jambo kuhusiana na Tamasha la Kihistoria la Makabila ya Sukuma na Kerewe, linalohusu Vyakula vya Asili, Ngoma na Tamaduni za Makabila hayo, linalotarajiwa kufanyika tarehe 27 CCM Kirumba Mwanza na Tarehe 28 Uwanja wa Mongella Ukewrewe Mwezi Huu, Kushoto ni Afisa Habari wa Kampuni ya My Way Entertainment, Osbert Chusu,(Picha Kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Bendi pendwa Tanzania, Twanga Pepeta Internatinali, inatarajiwa kuporomosha bonge la shoo ndani ya Jiji la Mwanza na Mji wa Nansio Ukerewe katika viwanja vya CCM Kirumba na Nansio Ukerewe katika tamasha la kihistoria la utamaduni wa msukuma na mkerewe linalotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi Tarehe 27-04-2013 na Jumapili tarehe 28-04-2013 kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka usiku.
Akiongea jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya MyWay Entertainment Rose Mwita Marwa, alisema bendi ya Twanga Pepeta imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii na maendeleo ya vijana kupitia Muziki. Hivyo, burudani ya bendi hii na burudani nyinginezo zitakazokuwepo ili kuhamasisha wakazi wa Mwanza na Ukerewe kuhudhuria kwa wingi.
Rose alisema, “Tamasha hili linalenga kuhamasisha jamii ya msukuma, mkerewe na makabila mengine kuenzi mila na tamaduni. Vilevile, jamii na falimia zilizopo ndani na nje ya mikoa yao zikumbuke nyumbani na kutembelea wazee mara kwa mara”.
Aliendelea kueleza kwamba, zaidi ya watu 3,000 na familia zao, watahudhuria kwa wingi tamasha hili la kihistoria huku wakipata fursa ya;-
·        Kusikia historia ya msukuma na mkerewe kwa kina toka kwa wazee wanaotoka sehemu mbalimbali hasa kwenye familia za watemi wa Kisukuma na Wakerewe.
·        Kuona maonyesho ya zana za kale za jadi zilizotumiwa na makabila haya mawili.
·        Kuona na kucheza ngoma zote za asili ya msukuma na mkerewe pamoja na vikundi tofauti tofauti vya ngoma za asili na sanaa za makabila mengine.
·        Kula aina zote za vyakula vya asili ya msukuma na mkerewe.   
·        Kunywa vinywaji vyote vya asili ya msukuma na mkerewe.
·        Kupata burudani toka kwa wasanii wa kizazi kipya kutoka Dar es Salaam.
Vilevile alisema, wamewaalika viongozi wa serikali yetu, viongozi wa dini zote, wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya mkoa wa Mwanza, viongozi wa asasi zisizo za kiserikali za serikali na wanafunzi kutoka vyuo na shule mbalimbali katika mkoa wa Mwanza.
Tumejipanga vizuri katika kufanikisha siku za historia za makabila yote Tanzania kila mwaka tukianza na makabila ya ukanda wa kaskazini, likifuata Tamasha la Wahaya June 29, tukiwa na lengo la kuhamasisha jamii kuenzi mila na na kukumbuka na kuzipeleka familia nyumbani.
Tamasha hili limedhaminiwa na;-
Balimi Extra Lager, Safari Lager, Pepsi, Star TV, Radio Free Africa, JB Belmont Hotel, Mwanza Institute, Toyo na La Kairo Investiment.



No comments:

Post a Comment