TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, September 17, 2014

Benki ya Exim yaingia ubia kuongeza ufanisi katika udhibiti wa majanga

 Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kutangaza kuingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka na Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto).
 Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (watatu kulia) akibadilishana hati na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (wapili kulia) wakati benki hiyo ilipoingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa Ndani, Bw. Goerge Binde na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto).
 Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (kushoto) akibadilishana hati na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (kulia) wakati benki hiyo ilipoingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM)
Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kutangaza kuingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa Ndani, Bw. Goerge Binde, Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (wapili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa Benki ya Exim, Bw. George Shumbusho (wakwanza kushoto) na Mwakilishi toka Hymans Robertson  Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto)

BENKI ya Exim Tanzania imeingia ubia na kampuni ya StraitsBridge Advisors (SBA) ya nchini Singapore, kampuni itoayo huduma za kifedha kwa ajili ya kutoa huduma ya kitaalam katika masuala ya udhibiti wa majanga ijulikanayo kama Enterprise – Wide Risk Management (ERM), itakayoiwezesha benki hiyo kuongeza ufanisi katika udhibiti wa majanga. 

Akizungumza katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala alisema, ili Benki ya Exim iongeze ufanisi katika eneo la udhibiti wa majanga imesaini makubaliano na kampuni ya SBA ambayo itashirikiana na kampuni ya Hymans Robertson (H&R) ya London kuipa benki ujuzi mkubwa dhidi ya majanga inayokutanayo na kutumia fursa mbali mbali zinazojitokeza kibiashara.

Alisema kuwa ikiwa inazaidi ya miaka 92 ya uzoefu katika utoaji huduma hizo, Hymans Robertson ikishirikiana na SBA itaisaidia benki kuongeza ufanisi wake katika eneo la udhibiti wa majanga yaani Enterprise-Wide Risk Management (ERM).

“ERM inatoa muongozo katika masuala ya udhibiti wa majanga, ambayo moja kwa moja inahusisha matukio yanayoiusisha benki (majanga na fursa), kuyachunguza kwa kuyaangalia na kujua ukubwa wa athari zake na kufuatilia uendeleaji wake.

“Kwa kutambua na kwa umakini kuangalia na kufanyia kazi majanga na fursa, muongozo bora wa ERM utailinda benki na kuwajengea thamani wamiliki, wafanyakazi, wateja na wadhibiti,” alisema Bw. Lusala.

Alibainisha kuwa, mafanikio ya benki yoyote yanatokana na uwezo wa benki hiyo kuweza kufanya uwiano katika ya majanga yanayolandana na shughuli zake za kibiashara dhidi ya gharama za kudhibiti majanga mbali mbali.

"Kwa hiyo, benki yetu inatarajiwa kuutekeleza utaratibu huo wa ERM, ikiwa ni pamoja kuangalia maendeleo yake na utumiaji wa profaili ya benki ya majanga ili iweze kutuongoza katika ufanyaji wa maamuzi katika masuala yote ya kimkakati na yasiyokimakakati.

"ERM itahakikisha kuwa matokeo yatokanayo na jitihada za benki hayapotei kwa hasara zinazoweza epukika, au majanga," aliongeza.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Hymans & Robertson (H&R) Bw. Maurice Kilavuka alisema kampuni yake inafuraha kupata fursa ya kufanyakazi na Benki ya Exim katika safari yake ya kufikia ubora zaidi hususani katika masuala ya udhibiti wa majanga.

"Tunayofuraha kubwa kupata fursa hii ya kufanyakazi na Benki ya Exim ikiwa katika safari yake ya kufikia ubora zaidi hususani katika masuala ya udhibiti wa majanga. Ushirikiano huu unadhihirisha uelewa walionao Benki ya Exim juu utaalamu unaopatikana toka kwa wataalam wa StraitsBridge & Hymans Robertson. Tutafanya jitihada kubwa na kuiwezesha benki kuwa na mfumo bora duniani katika masuala ya udhibiti wa majanga yaani Enterprise Risk Management (ERM).

StraitsBridge Advisors pamoja na Hymans Robertson, imekuja mifumo mbali mbali madhubuti ya jinsi gani ya kudhibiti majanga ikiwa ni pamoja na majanga katika masoko, majanga katika mikopo, ALM, uwekaji bei katika utumaji fedha, Usimamizi na Upangaji wa Mtaji, na Usimamizi wa Fedha. Hii bila Bila ya shaka itakuwa ni nyenzo ya benki kuweza kujenga mfumo madhubuti wa udhibiti majanga,” Bw. Kilavuka alisema.

No comments:

Post a Comment