TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, May 1, 2015

WAKUU WA TAASISI ZA TAKWIMU WA NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA JIJINI DAR !

 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) nchini Tanzania Dkt.Albina Chuwa akifungua Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala la wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam. Kongamano hilo la siku 2 linajadili namna Bora ya uendeshaji wa Taasisi za Takwimu na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za masuala ya Takwimu Barani Afrika.
(Picha Zote na: Aron Msigwa –MAELEZO
 Mtendaji Mkuu wa  Taasisi ya  Takwimu ya Bara la Afrika Bw. Joseph ILboudo akizungumza na watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala lililowahusisha wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi  za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam.
 Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Takwimu Barani Afrika (AFRISTAT) pia mtaalam wa Takwimu kutoka nchini Cameroon Bw. Martin BALEPA akiwasilisha mada kuhusu namna nchi za Bara la Afrika zinavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kutumia takwimu sahihi.
 Bw. Andry Andriantseheno kutoka UNECA akiongoza kongamano hilo la siku 2 la  watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu wa nchi za Afrika linalojadili masuala ya Uongozi na utawala na leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania wenyeji wa mkutano huo.
 Baadhi ya watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala linaloendelea jijini Dar es salaam.
Watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la Kimataifa la siku 2 linalojadili masuala ya Uongozi na utawala wa taasisi za takwimu Barani Afrika linaloendelea jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment