TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 9, 2016

SOMA HABARI NA MATUKIO HAPA

Posted: 08 Jan 2016 01:00 PM PST
Mr. Mbwana Aly Samatta-2nd from left receiving an Award as the African Player of the Year based in Africa during an event that took place in Abuja, Nigeria on 7th January, 2016

C:\Users\malaler.FOREIGN\Documents\English header.jpg

Press Release


The Tanzania Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation wishes to inform the world and all football fans that Mr. Mbwana Aly Samatta, the African Player of the Year based in Africa is a citizen of Tanzania and not of Botswana or Tunisia as was reported by NBC Sports.com and several other international media. 

Mr. Samatta is one of the star players of the Tanzania national team (Taifa Stars) currently playing for TP Mazembe Club in the Congo DRC.

The Tanzanian icon was announced by the Confederation of African Football (CAF) as the African Player of the Year based in Africa in an event that took place in Abuja, Nigeria on 07th January, 2016. Mr. Samatta becomes the first player from East Africa to win the prestigious title.

The Ministry takes this opportunity to thank Mr. Samatta for placing Tanzania on the international football stage and congratulate him for the victory well deserved. 

Issued by:
Government Communication Unit
Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation
8th January, 2016
Posted: 08 Jan 2016 10:45 AM PST
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Studio ya Muziki na Filamu mara alipowasili katika viwanja vya Studio ya Rahaleo Mjini Unguja wakati wa ufunguzi wa Studio ya Muziki na Filamu leo ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akiwaangalia wasanii walipokuwa wakitoa burudani yao  mara alipowasili katika viwanja vya Studio ya Rahaleo Mjini Unguja wakati wa ufunguzi wa Studio ya Muziki na Filamu leo ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya  ufunguzi rasmi wa Studio ya Muziki na Filamu uliofanyika leo katika jengo la zamani la Studio Rahaleo Mjini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Studio za Muziki na Filamu Bakari Shomari alipotembelea Studio ya kurikodia Muziki baada ya kufanya ufunguzi rasmi  uliofanyika leo katika jengo la zamani la Studio Rahaleo Mjini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wiazra ya habari Utalii Utanmadunu na Michezo Dkt. Ali Mwinyikai alipotembelea moja ya Studio ya kurikodia Muziki baada ya kufanya ufunguzi rasmi  uliofanyika leo katika jengo la zamani la Studio Rahaleo Mjini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52,(wa pili kushoto)Meneja wa Studio za Muziki na Filamu Bakari Shomari
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine wakiwaangalia wasanii wanavyorekodi wakiwa Studio wa Muziki wa Audio alipotembelea Studio za Kurikodia Filamu na Muziki  leo katika jengo la zamani la Studio Rahaleo Mjini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52
  Baadhi ya wananchi na wasanii waliohudhuria katika sherehe za Ufunguzi wa Studio za Muziki na Filamu leo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar waliohudhuria katika sherehe za Ufunguzi wa Studio za Muziki na Filamu leo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi  wengine wakiangalia Moja ya Filamu iliyooneshwa leo wakati wa ufunguzi rasmi wa Studio ya Muziki na Filamu,mara baada ya kufanyika ufunguzi huo  leo katika jengo la zamani la Studio Rahaleo Mjini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52
 Msanii maarufu Makombora alipokuwa akisoma risala kwa niaba ya wasanii wenzake leo wakati wa ufunguzi wa Studio ya Muziki na Filamu leo,uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Sheinikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake kwa wasanii katika sherehe za ufunguzi wa Studi ya Muziki na Filamu katika Jengo la zamani la Studio ya Rahaleo Mjini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52
Baadhi ya Viongozi na Wasanii maarufu wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Studio ya Muziki na Filamu  uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein leo katika Jengo la zamani la Studio Rahaleo Mjini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Ikulu.
Posted: 08 Jan 2016 09:48 AM PST

Can You Spare a Few Moments to Nominate for an Award a Deserving Member of Our Diaspora?
 

DICOTA once again is inviting you to Dallas, Texas from April 28th to May 1st, 2016 to journey along, as we “Leverage the Tanzanian Diaspora Capacity”  with Awards instituted to shine the spotlight on the best practices and to reward impact, innovations and community development efforts in different sectors.


The process begins with nominations, which are then screened for eligibility and correct category placement. Take this opportunity to nominate a deserving someone in the Tanzanian Diaspora community for one of the prestigious awards.

  1. Go to https://www.surveymonkey.com/r/V5J3QM3 submit your nominations by 11:59 PM CST on Sunday, January 31, 2016.
  2. Final voting process for the top three finalists in each category which determines the DICOTA 2016 Award winners begins on Monday, February 15, 2016 and ends on Thursday March 31, 2016.

Who said we don’t know how to cheer up our own people?
Click here to see DICOTA 2014 Nominations and winners information.

Thank you,

Awards Committee
Posted: 08 Jan 2016 09:21 AM PST

Posted: 08 Jan 2016 08:40 AM PST
M2

Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa akimkabidhi  Balozi wa Namibia nchini aliyemaliza muda wake, Mhe. Japhet Isaack  zawadi ya ramani ya  Tanzania iliyochongwa kwenye mti wa mpingo  ili aendelee kuikumbuka Tanzania  atakapoondoka. alozi alikwendaofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 8, 2016 kuaga.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekuaana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Namibia ambaye anamaliza muda wake, Bwana Japhet Isaack.
Akizungumza na Balozi  Isaack leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaa, Waziri Mkuu ameshukuru Balozi huyo na  kumumwomba  waendeleze uhusiano mwema   ulipo baina ya nchi hizi mbili ambao ulianza tangu enzi za kugombania uhuru ili  kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizi mbili.
“Namibia ni  nchi yenye uchumi uanaokua haraka, na mmefanikia katika baadhi ya sekta , hivyo ningependa  Tanzania ijufunze kutoka kwenu hasa katika sekta za Utalii, Afya, na Elimu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Pia, alitumia fursa hiyo kuwakaribisha  raia wa Namibia kuja kuwekeza nchini  katika maeneo mbalimbali ikiwemo  viwanda  na kuendeleza maeneo ya ukanda maalum ya uwekezaji (EPZ) ili kuongeza thamani ya mazao pamoja na kutatua tatizo la ajira nchini.
Kwa upande wake,  Balozi  Isaack  amesema kwa kipindi alichokaa Tanzania amejifunza mengi, na amefurahishwa  ambavyo Waziri Mkuu pamoja Serikali kwa ujumla  inavyofanyakazi kwa kasi na kwa mafanikio makubwa.
“Hongera, ninafurahishwa na unavyofanya kazi  hongera sana”, alisema Balozi Isack. Pia, amefurahi sana kipindi chote alichokaa Tanzania kwani kimekuwa na matukio mengi yenye kumbukumbu  nzuri kwake.
Balozi Isack   ameomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe ili zishirikiane zaidi katika masuala mbalimbali ya kukuza uchumi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
IJUMAA, JANUARI 8, 2016.

Posted: 08 Jan 2016 08:26 AM PST
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS




TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU ZOEZI LA KUHAMISHA WAKAZI WA MABONDENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

Utangulizi

Nchi yetu ina kingo za mito na mabonde na maeneo mengi hatarishi ambamo watu wanaishi kinyume cha sheria, huku wakiharibu mazingira na kuhatarisha maisha yao.  Kutokana na uhaba wa makazi, hali ni mbaya zaidi katika mabonde ya Jiji la Dar es Salaam, hasa bonde la Mto Msimbazi.
Serikali za awamu zote, zimekuwa zikifanya jitihada za kuwaondoa wakazi wa maeneo ya mabondeni wanaoishi katika maeneo hayo kinyume cha sheria lakini mafanikio yamekuwa si ya kuridhisha. 

Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo moja ya misingi yake mikuu ni utii wa sheria za nchi, imeanza jitihada za kuwaondoa wakazi hawa. Tuliamua kuanza na Bonde la Mto Msimbazi kwasababu ndiko kwenye watu wengi na athari kubwa.Sababu zetu kuu za kufanya zoezi hili ni kusafisha mabonde na mito katika jiji la Dar es Salaam na mazingira yanayozunguka ni:-

  1. Kunusuru maisha ya wananchi wanaoishi katika mazingira hatarishi. Eneo la Bonde la Mto Msimbazi lilitangazwa kuwa ni eneo hatarishi kuishi binadamu tangu mwaka 1949 na baadaye 1979.

  1. Kupanua uwezo wa mito ya Dar es Salaam ili kupitisha maji ya mvua kwa kasi kubwa, hivyo kupunguza uwezekano wa kutokea mafuriko na maafa wakati wa mvua nyingi;
  2. Kuzuia milipuko ya magonjwa, hasa ya kipindupindu, hasa wakati wa mvua;


  1. Kuzuia eneo hilo kuendelea kutumika kama maficho ya wahalifu na uhalifu;

  1.  Kutoa nafasi kwa Serikali kuandaa na kuendeleza eneo hilo kwa mujibu wa sheria za nchi na mipango miji;
Utaratibu wa Zoezi

Kabla ya nyumba kubomolewa, taasisi hizi zinashirikiana kuhakiki iwapo nyumba anayokaa mkazi ina nyaraka za umiliki na vibali vya ujenzi na iwapo nyaraka hizo zina uhalali wowote. Nyumba ambazo zimethibitika kuwepo katika maeneo yasiyostahili ndio zinawekwa alama X kuashiria kwamba wakazi wanapaswa kuhama au kubomoa. Baada ya hapo, mkazi hupewa muda wa kubomoa na kuhama mwenyewe. 

Kutokana na utaratibu huu, sehemu kubwa ya nyumba zinazobomolewa ni zile ambazo watu wamekwishaamua kubomoa wenyewe. Baada ya hapo, alama huwekwa kuonyesha mpaka wa bonde. Katika zoezi hili, imebainika kwamba sehemu kubwa ya wakazi wa maeneo ya mabondeni ni wapangaji huku wamiliki wakikaa sehemu nyingine salama. Serikali pia imeweka Dawati la Malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Tathmini ya Zoezi

Jana, terehe 7 Januari 2016, Mawaziri watatu (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI; na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais; pamoja na Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii), walifanya mkutano wa kutathmini zoezi la kuhamisha wakazi wa mabondeni katika Jiji la Dar es Salaam.  

Mkutano huo ulipokea ripoti ya timu ya wataalam wa Wizara mbalimbali, inayoongozwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, ambayo, pamoja na mambo mengine ilibainisha kwamba sehemu kubwa ya kubaini makazi yaliyojengwa kinyume cha Sheria katika Bonde la Mto Msimbazi imekamilika. Ripoti ilieleza kwamba, hadi sasa, wananchi katika nyumba 774  wamehama na nyumba hizo kubomolewa. Ilielezwa pia kwamba kabla ya mkazi kuombwa  kuhama, uhakiki kuhusu uhalali wa makazi anayoishi hufanywa. Kutokana na uhakiki huo, jumla ya wakazi 20 walikuwa na hati halali za makazi na wakazi 119 walikuwa na leseni za makazi za muda mfupi. Hawa watu hawakuhamishwa. Mawaziri walipokea maelezo kuhusu changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika zoezi hilo.  Baada ya tafakuri na mjadala, Mawaziri hao walitoka na msimamo ufuatao, kama uamuzi wa Serikali: -

1.      Zoezi la kuwaondoa wananchi waishio katika bonde la Mto Msimbazi (eneo hatarishi) litaendelea kwa utaratibu ambao hautaleta mateso na usumbufu kwa wananchi;

2.      Katika awamu hii, zoezi litajikita katika Bonde la Mto Msimbazi tu.

3.      Kwa wakati huu, watakaohitajika kuhama ni wale tu ambao makazi yao yamo NDANI kabisa ya bonde, kwenye miteremko ya kuingia bondeni na kwenye KINGO za mto;

4.      Wale watakaokuwa na nyaraka halali walizopewa na mamlaka za umma, zilizowamilikisha na kuwaruhusu kujenga katika bonde hilo, hawatahamishwa bila kupewa sehemu nyingine za kujenga. Na watumishi wa umma waliowamilikisha maeneo hayo watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria;

5.      Serikali, ndani ya siku tatu zijazo, itaanza zoezi la kuzoa kifusi na kusafisha maeneo ambapo ubomoaji umefanyika.

6.      Serikali itaheshimu amri za mahakama kuhusu mapingamizi yaliyowekwa na baadhi ya wakazi wa mabondeni lakini pia itafuatilia kesi hizi ziishe haraka ili taratibu zinazofuatia zifanyike;

7.       Serikali itawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wake wanaoendesha zoezi hili kinyume na misingi ya sheria zinazotekelezwa, na kinyume na misingi ya haki na uwazi, ikiwemo wanaoweka alama za X zaidi ya mita zilizowekwa kisheria. Limeanzishwa dawati la malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kupokea malalamiko au maswali kuhusu zoezi hili.


8.      Nyumba na majengo ya miaka mingi, yaliyokuwepo miaka mingi kabla ya kutungwa kwa Sheria zinazotekelezwa kwa zoezi hili, hayatabomolewa isipokuwa tu pale maisha ya wakazi yapo hatarini. Wanaoishi katika makazi hayo watapewa miongozo ya hatua za kuhifadhi mazingira na kujiokoa na maafa;

9.      Serikali haina dhamira ya kubomoa mahoteli makubwa ya siku nyingi yaliyo karibu na fukwe katika maeneo ya Masaki. Wamiliki wa mahoteli haya watapewa masharti na miongozo ya kuhifadhi mazingira kwa mujibu wa Sheria.


10.    Serikali inaweka uratibu wa karibu zaidi miongoni mwa taasisi zake ili hatua za utekelezaji wa sheria za nchi zisiwe chanzo cha taharuki katika jamii.

11.  Serikali haina dhamira ya kuwatesa wananchi wake kwa kuwalazimisha kuhama katika makazi yao bila sababu za msingi. Lakini pia Serikali haiwezi kuruhusu wananchi waendelee kukaa katika maeneo ambayo ikinyesha mvua kubwa maisha yao yapo hatarini. Itakumbukwa kwamba katika mafuriko ya mwaka 2011, wananchi 49 waishio mabondeni walipoteza maisha. Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Hali ya Hewa, mwaka huu zinatarajiwa kunyesha mvua kubwa kuliko zilizowahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.

12.  Serikali inafuatilia kwa karibu kwa mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya taarifa za wananchi wanaohitaji msaada maalum wa kibinadamu.

Suala la Mchungaji Getrude Rwakatare

Mkutano ulipokea taarifa kuhusu suala linaloongelewa sana la nyumba ya Mchungaji Rwakatare.  Ilielezwa kwamba Mchungaji Rwakatare amejenga nyumba yake pahali ambapo amezuia mtiririko wa mto kwa kujaza kifusi ili kupata eneo zaidi katika eneo la miti ya mikoko, kinyume kabisa na Sheria tatu muhimu.  Pia ilielezwa kwamba tangu wakati ujenzi unaanza jitihada za kumsimamisha zilifanyika na mamlaka za Serikali za Mitaa lakini ikashindikana kutokana na sababu mbalimbali. Pale Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira lilipoingilia kati na kutaka kuibomoa nyumba hiyo, Baraza lilishtakiwa mahakamani. Wakati kesi inataka kuanza kusikilizwa, mwanasheria mdogo wa Baraza, yeye mwenyewe bila kuagizwa wala kuwaarifu wakubwa zake, mnamo tarehe 11 Mei 2015, aliingia makubaliano na mawakili wa Mchungaji Rwakatare kwa niaba ya Baraza ya kuondoa kesi hiyo mahakamani na kukubali, kwa niaba ya Baraza, kutombughudhi kabisa Mchungaji Rwakatare.  Makubaliano hayo yalisajiliwa na Mahakama kama hukumu tarehe 13 Mei 2015. Mwanasheria huyo alificha makubaliano hayo kwa miezi mitano hadi Oktoba 2015, yalipogundulika na mtumishi mwingine wa Baraza. Mkutano ulielezwa kwamba Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kufuata taratibu zote, alishaagiza kufukuzwa kazi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mwanasheria huyo. Mwanasheria huyo alifukuzwa kazi siku ya juzi tarehe 6 Januari 2016 na taarifa zake zimekwishafikishwa TAKUKURU. Vilevile, Ofisi ya Makamu wa Rais, iliiagiza Baraza kufungua shauri mahakamani la kuomba “makubaliano” kati yake na Mchungaji Rwakatare yawekwe pembeni kwasababu yalipatikana na njia ya udanganyifu. Shauri hilo lilifunguliwa tarehe 29 Disemba 2015.

Kuhusu Karakana ya Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Kasi (DART)

Mkutano pia ulijulishwa kuhusu hoja inayozungumzwa kwamba wananchi wanaondolewa katika maeneo ya kuishi mabondeni lakini mradi wa DART umeachwa. Mkutano ulielezwa kwamba Sheria ya Mazingira (kifungu 57 (2)) inatoa nafasi ya kutolewa ruhusa kwa miradi/shughuli zenye maslahi ya taifa kufanyika katika maeneo ya mabondeni, na kwamba Waziri mwenye dhamana ya mazingira anaruhusiwa kutoa miongozo ya namna ya shughuli hizo zinavyoweza kufanyika bila kuathiri mazingira. Mradi wa DART ulipata kibali hicho na una mkataba na Baraza la Mazingira kuhusu hatua za hifadhi ya mazingira zinazopaswa kutekelezwa katika mradi huo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
08.01.2016
Posted: 08 Jan 2016 06:04 AM PST
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha wakati alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga aliliagiza Jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakaye kiuka kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji wakati linaenda katika tukio lolote la uokoaji pamoja na kuzima moto. Pia aliitaka Jeshi hilo kuongeza kasi ya kukusanya mapato katika vyanzo vyake mbalimbali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kushoto) akitoa taarifa ya utendaji wa Jeshi lake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliliagiza Jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakaye kiuka kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji wakati linaenda katika tukio lolote la uokoaji pamoja na kuzima moto. Pia aliitaka Jeshi hilo kuongeza kasi ya kukusanya mapato katika vyanzo vyake mbalimbali

No comments:

Post a Comment