TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, July 27, 2016

G.S.M YAKAMILISHA UZINDUZI WA MASHINDANO YA R.P.C CUP LINDI 2016 UWANJA WA ILILU:

 Kikosi cha Timu ya Raha Leo
 Kikosi cha Timu ya Mtanda
 Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa Ndemanga (Kushoto) Akiwa na Mgeni Rasmi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, R.P.C Renatha Mzinga, wakati wa Uzinduzi wa Michuano ya Kombe la R.P.C CUP LINDI 2016, kwenye Uwanja wa Ilulu Mkoa wa Lindi tarehe 28/7/2016. Fainali ya Michuano ni 25/8/2016 katika Uwanja huo.(Picha Zote na Fungwa Kilonzo)
 Mkurugenzi wa Mashujaa Fm Radio, na Mratibu wa Michezo ya R.P.C CUP LINDI 2016, Shaaban Mpalule, akiwagawia  Mashabiki Furana mbali mbali  za G.S.M na T-Mark Tanzania, wakati wa Uzinduzi huo.
  Mkurugenzi wa Mashujaa Fm Radio, na Mratibu wa Michezo ya R.P.C CUP LINDI 2016, Shaaban Mpalule, akiwagawia  Mashabiki Furana mbali mbali  za G.S.M na T-Mark Tanzania, wakati wa Uzinduzi huo.
 Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
===================================

-R.P.C RENATAHA MZINGA AZINDUA KWA MBWEMBWE.
-DC LINDI AIPONGEZA KAMPUNI YA GSM
-MASHABIKI WATAKA GSM IFANYE MICHEZO HIYO KILA MWAKA.

Na: Mwandishi wa Miss Demokrasia Tanzania.

Kampuni ya GSM Tanzania, wauzaji wa Pikipiki za GSM na Magodoro ya kisasa ya GSM, leo jumatano 28/7/2016 imekamilisha uzinduzi wa Michuano ya Kombe la R.P C Cup LINDI 2016, ambayo lengo lake ni kuwaweka Vijana karibu na Jeshi la Polisi pamoja na kuwapa Elimu mbali mbali Madereva kuhusiana na Usalama barabarani ususani vijana waendesha Bodaboda na ilianza 13/7/2016 kwenye Uwanja wa Ilulu.
katika uzinduzi huo GSM ambao ni wadhamini wa Jumla katika michezo hiyo kwa Upande wa Jeshi la Polisi katika mikoa ya Lindi, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma, ilipongezwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa Ndemanga kwa kuweza kujitokeza kusaidia mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kwa mkiwango kisichoridhisha ikiwa ni pamoja na kukosekana na vifaa vya michezo pamoja na furana kwa Wageni mbali mbali.

 Aidha wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo Kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi, Afande R.P.C Renatha Mzinga, alisema kuwa wanaishikuru Kampuni GSM kwa mwaka huu kujitokeza kusaidia michezo hiyo ambayo hata hivyo bado kuna upungufu wa vifaa mbali mbali vya michezo ikiwemo mipira ya kuchezea.

"Mashindano ya Mwaka huu ni Mazuri na yameonyesha kuwa tofauti na miaka ya nyuma, pengine ni kwa kuwa yamejitokeza makampuni kama hawa GSM, Halotel na BIG BON, kwa kweli kunachangamoto nyingi sana kwenye hii michezo, na hata timu za mwaka huu zimeonekana kujiandaa vizuri kwa ajili ya kuwania zawadi siku ya Fainali, Niwapongeze wadhamini wote waliojitokeza kusaidia kwa namna moja na nyingine, kile kidogo walichotupatia kwetu ni kikubwa sana, kwa maana kimeonekana kuleta utofauti na miaka ya nyuma, hivyo nichukue fulsa hii kuwaomba hawa wadhamini kuweza kukumbuka kutusaidia kwenye hii hatua ya mwisho ambapo inaonekana vifaa bado havijatimia kama hii Mipira, Sare za Waamuzi na Zawadi zingine kwa ajili ya Timu, pamoja na kwamba tumepata vikombe lakini tunatakiwa pia kuwapa zawadi zingine ili kuonyesha tofauti ya mwaka huu na miaka ya nyuma, niwashukuru GSM kwani hawa wamejitokeza hatua za mwisho mwsiho lakini wametuwezesha leo kupendeza uwanjani, mashabiki wamevalia na watu mbali mbali furana zao, kwa kweli ninawapongeza sana, wasiishie mwaka huu tu bali wayachukue na kuyafanya mashindano kuwa ni ya kwao kila mwaka" alisema R.P.C Renatha Mzinga.
Aidha michuano hiyo imezidi kushika kasi na kufikia jumla ya michezo 27 ambayo tayari imechezwa katika kuwania kinyang’anyoro cha ubingwa  mwaka huu.
Wachezaji wa timu mbali mbali wamezidi  kuonyesha uwezo mkubwa katika michuano hiyo ambayo inashirikisha jumla ya timu 18 kutoka kata zote za Mkoa wa Lindi.

Katika hatua hii michezo ambayo imechezwa na matokeo ni kama ifuatvyo, Mtanda A imefanikiwa kuifunga Mitandi kwa 1-0, Matopeni 1-0 Wailes, Mnazi mmoja 2-0 Mbanja, Nachingwe 0-0 Msinjaili, Rahaleo 2-1 Mtanda B, Rasibula 2-1 Tandangongoro, Mingoyo3-0 Chikonji, Mtandi 5-1 Kitumbikwela, Makonde 5-0 Mikumbi, Polisi 1-1 Matopeni, Mnazi Mmoja 4-1 Mtanda A, Msinjaili 8-0 Wailes, Mtanda(B) 2-1 Mbanja, Rahaleo 2-0 Chikonji, Rasibula 2-0 Nachingwea, Mikumbi 2-0 Tandangongoro.

MIchezo mingine ni Mingoyo 0-Kitumbikwela. Makonde 1-0 Polisi, Mitandi 1-1 Mnazi Mmoja, MAtopeni 3-0 Msinjahili, Mtanda(A)1-1 Mbanja, Wailes 2-5 Nachingwea, Kitumbikwela 3-4 Chikonji, Polisi 0-1 Mikumbi, Mnazi MMoja 0-0 Mingoyo, Msinjahili 0-3 Makonde, Mitandi 2-0 Mbaja, MAtopeni 2-2 Nachingwea, na Mtanda 2-3 Raha Leo.

Michezo hiyo inaendelea tena kesho(leo) ambapo Wailes wataikaribisha timu ya Tandangomgoro katika mchezo wa kwanza na mchezo wa pili Mtanda (B) wataikaribisha Kitumbikwela kwenye mchezo wa pili majira ya saa kumi jioni.

mashindano yameendelea kuwa kuvutio kikubwa kwa wakazi wa mkoa wa lindi kutokana na wenyeji kujitokeza kuzishangilia timu za kata zao ambazo zinawania uchampioni huo wa kombe la R.P.C Renatha Mzinga.

Zawadi ambazo mpaka sasa zimetolewa na GSM ni pamoja na Filimbi, Stopwatch, Soksi, Mabegi, Kofia, Sare  na Viatu kwa ajili ya Waamzuzi, pamoja na zawadi ya Soksi kwa Wachezaji ambao wanafanikiwa kufunga magoli matatu katika mechi moja, ambapo badala ya kuondoka na mpira umewekwa utaratibu wa kuwazawadia Soksi kila anapotokea mchezaji amefunga mabao matatu.

Kiasi cha Shilingi Milioni Mbili tayari Kimetumika Mpaka sasa kutoka Kampuni ya GSM ambazo zimetumika kulipa Posho za Waandishi wa Habari wanaoendelea kuripoti matukio hayo kila siku na zingine zimesaidia kununua vifaa hivyo kwa ajili ya Waamuzi na zawadi za kila siku kwa wachezaji.

katika kiasi hicho kutoka GSM pia kimesaidia kununua Filimbi na Stop Watch kwa ajili ya Makocha wa Timu zote zinazoshiriki ligi hiyo ya R.P.C CUP LINDI mwaka huu.

katika hatua nyingine kampuni ya T-Mark Tanzania ambao pia ni miongoni mwa wawezeshaji wadogo wameweza kusaidia  Furana za kwa ajili ya Vikundi vya Uhamasishaji.

Kilele cha Michuano hiyo ni tarehe 25 ya mwezi wa nane ambayo itakuwa siku ya kilele cha siku ya Polisi Day.

Mashindano haya yanaandaliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Afande R.P.C Renatha Mzinga kwa ushirikiano na Mashujaa Fm Radio chini ya Wadhamini Wakuu Big Bon na GSM Wauzaji wa Pikipiki za GSM na Magodoro ya GSM,wadhamini wadogo ni CxC Tours & Safaris, Halotel, T-Marc Tanzania, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Issa Ndemanga, Miss Demokrasia Tanzania, MPALULEBLOGS: na Pimak Limited.

 Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
 Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
 Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
 Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
 Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
 Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
 Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
 
   Mkurugenzi wa Mashujaa Fm Radio, na Mratibu wa Michezo ya R.P.C CUP LINDI 2016, Shaaban Mpalule, akiwagawia  Mashabiki Furana mbali mbali  za G.S.M na T-Mark Tanzania, wakati wa Uzinduzi huo.
Kikosi cha Timu ya Kata ya Raha Leo, Kikishangilia Bao la kwanza
 DJ'S Machachali, Dj Kizo, akifanya Vitu vyake wakati wa Uzinduzi huo
 Wakati wa Mapumziko
 Mashabiki wakiwa wamejificha kivuli kwenye Miamvuli ya GSM wakati mchezo ukiendelea
  Watoto ambao ni wakeleketwa wa Soka na Wajanja wa G.S.M wakifurahia Vipeperushi vyenye Nembo ya Bidhaa za G.S.M, kama Piki Piki na Bidhaa Zingine, Vipeperushi vilivyogawiwa kwa Mashabiki Wote UWanjani humo.
Kikundi cha Ushangiliaji (Vijana) ambao walionyesha Staili ya Pekee katika Kushangilia kwa Kuvaa Nguo za Kike, maarufu kama Dela ambazo ziliwaonyesha kana kwamba wao ni Watoto wa Kike, waliokuwa wakizunguka Uwanja huku wakionyesha Mbwembwe ikiwemo kutikisa Nyonga, Viuno, na Vidole Juu, na kuwaacha MAshabiki kwa Vifijo, nderemo na Kelele za Mara kwa Mara kwa kile walichokuwa wakifanya Vijana hao wakati wote wa Mchezo, aikujulikana walikuwa mashabiki wa Timu gani.
 Majukwa yakionyesha utulivu wakati wote wa mpambano
 Timu zikiendelea kuchuana kusaka pointi tatu Muhimu
 Viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu wakifuatilia kwa Makini Mpambano huo huku wakivalia Furana za GSM
 Paparazi akiwa kazini
 Watu wa Huduma ya Kwanza (First AID) wakiwa eneo la Uwanja huo
 Rahaleo wakishangilia Bao la Pili
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa Ndemanga,(kushoto) na KAmanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, R.P.C Renatha Mzinga, wakifuatilia kwa makini Mpambano huo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, R.P.C Renatha Mzinga, akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa Ndemanga, Muda Mfupi kabla ya Uzinduzi huo

No comments:

Post a Comment