Na Mwandishi Wetu
MBUNGE    wa Jimbo la Lindi Mjini, Salum Baruany amewashauri watu waliowahi    kusoma katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania kushirikiana katika    kufanikisha tamasha la kuchangia maendeleo ya elimu kwa ajili ya mikoa    hiyo.
Baruany    aliyasema hayo juzi katika kikao cha maandalizi ya tamasha la   kuchangia  maendeleo ya elimu kwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma   kilichofanyika  Ukumbi wa Imasco, Temeke jijini Dar es Salaam.
Akiwa    mmoja wa waalikwa wa vikao hivyo vya kila wiki, Baruany alielezea    kukunwa kwake na ubunifu wa baadhi ya wanafunzi walioamua kuwahamasisha    wenzao kukumbuka walikotoka kielimu, kwa lengo la kuwainua wengine.
“Nawapongeza    sana. Ni wachache wanaoweza kukumbuka walikotoka, hasa kielimu. Hapa    mmelenga, mikoa ya kusini iko nyuma kielimu, naamini wa kusaidia    kupandisha hadhi ni ninyi wenyewe mliosoma kule na wadau wengine    wanaoguswa na suala hili.
“Msikate    tamaa, mtafanikiwa. Cha msingi ni kuwashirikisha na kuwashawishi    wengine waliosoma ana kuwa karibu na mazingira ya kielimu ya mikoa hii.    Nchi hujengwa  na wananchi wenye moyo, nanyi kwa kuguswa    kwenu, naamini elimu ya kusini itainuka kwa sababu ni vigumu mtu mmoja    mmoja kuchangia na bado maendeleo ya kweli yakaonekana, bali kupitia    mshikamano kama wenu,” alisema mbunge huyo.
Naye    Mratibu wa tamasha hilo, Asanterabbi Mtaki, licha ya kumshukuru  mbunge   huyo kwa nasaha zake, aliwataka wadau wa elimu nchini kuungana  na   waliosoma mikoa ya kusini ili kufanikisha azma ya kuiinua kusini    kielimu.
“Tangu    awali tumeelezea hali ya elimu ya mikoa ya Kusini, kwa kweli si nzuri    na inahitajika nguvu ya ziada, ndiyo maana tumeungana kuhakikisha    tunafanikisha kitu kwa ajili ya shule za kusini na wanafunzi wake, hasa    yatima, walemavu na wasiojiweza ili wapate haki ya kupata elimu bora,”    alisema Mtaki.
Alisisitiza    kuwa, kasi ya maandalizi ya tamasha hilo inaridhisha na kuongeza  kuwa,   nafasi ya waliosoma kusini kuchangia mawazo bado ipo, hasa  kupitia  vikao  vya kila mwisho wa wiki vinavyofanyika ukumbi wa Imasco.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Mohamed Mpinga  (kushoto) akimshukuru Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo  baada   ya kupatiwa na TBL msaada wa fulana na kofia vyenye thamani ya sh.  mil.  10 kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama   yatakayofanyika mkoani Kagera kuanzia Oktoba 3-8, mwaka huu. Hafla hiyo   ilifanyika Dar es Salaam juzi.Na Gladness Mushi, Arusha      Taasisi  ya maendeleo ya jamii hapa   nchini (CDTF) imefanikiwa kutoa msaada wa  kimaendeleo, ambapo imechangia   zaidi ya milioni 43 kwa ajili ya ujenzi  wa madarasa mawili pamoja na   ofisi ya walimu wa shule ya walemavu  iliopo katika eneo la Ilboru Mjini   hapa      Akizungumza  na vyombo vya habari mara  baada ya kukabidhi  vyumba hivyo vya  madarasa  pamoja na ofisi ya walimu  ambayo itatumika   kwa watoto hao  ambao ni walemavu Mkurugenzi wa  taasisi hiyo Bw Hendry  Mgingi alisema  kuwa watoto ambao ni walemavu kwa  kuwa nao wana nafasi kubwa sana ndani ya jamii ya watanzania     aidha   aliendelea kusema kuwa wao kama  taasisi ya maendeleo wamefikia uamuzi   huo mara baada ya kuona kuwa  watoto ambao ni walemavu wana nafasi  kubwa  sana  ya kuweza  kusaidika  hata kama wanaulemavu wa aina  mbalimbali.      aliongeza kuwa kama jamii ya watanzania itaweza kuwasaidia watoto hao ambao ni walemavu basi wataweza kufanya hata idadi ya wanafunzi ambao wana ujuzi mbalimbali kuongezeka kwa hali ya juu sana hapa  nchini.     "unajua   endapo kama baadhi ya taasisi  zitaweza kuona mchango ambao wanao hawa   watoto walemavu basi hawa  watoto wataweza kukua kwa kiwango cha hali  ya  juu sana na hata kama  hawataweza kufanya kazi ngumu basi wanaweza   kufanya kazi ambao ni raisi  na hivvyo kusaidia jamii katika kutatua   tatizo la ajira"aliongeza Bw  Hendry       hataivyo  alisema kuwa  walemavu  wanaweza kuibua mambo mbalimbali ikiwa ni  pamoja na kuweza  kutengeneza  ajira ambazo zimo kwenye jamii kwa kuwa  mpaka sasa baadhi ya  walemavu  wameonekana kuwa wabunifu wa hali ya juu  sana.     alisisitiza  kuwa  ubunifu huo ambao  wanao baadhi ya walemavu utaenda sanjari na  upokeaji  wa vipaji kutoka  kwa walemavu hao ambapo kama jamii ya leo  itaweza  kuwasaidia ni wazi  kuwa kazi mbalimbali za walemavu zitakubalika  na  jamii ya  watanzania.     'leo kuna    baadhi ya walemavu ambao wapo tu lakini cha ajabu ni kwamba bado    hawajaweza kusaidika lakini huu ndio wakati muafaka wa kila mwananchi    kuweza kuwasaidia hawa walemavu kwa kuwa kwa kutowasaidia basi asilimia    kubwa ya walemavu hao wanashindwa kutimiza ndoto za kuondokana na    umaskini"alisema Bw Hendry.     Alimalizia  kwa kusema kuwa walemavu  hao wanatakiwa kuhakikisha kuwa elimu ambayo  wanapata wanaitumia vema  katika kazi zao na  masomo kwa kuwa ili napo  waweze kufanikiwa ni lazima  kwanza kuwepo na mipango mikakati ya elimu  bora. 
Maandali ya kuujenga Mkoa mpya wa Njombe
Jamii    maskini kwa kawaida huwa na vipaumbele vingi. Matokeo yake ni   kushindwa  kuvitekeleza. Wananchi wa mkoa mpya wa Njombe ambao ni   wachapa kazi  kweli kweli wameikataa falsafa hiyo na wamejiwekea   vipaumbele vichache  na vya uhakika ili kuujenga mkoa wao. Vipaumbe vya   wananjombe ni:    
1.       Elimu-    Kwa kujitolea wananchi wa vijiji na kata za Katulila, Madobole, Miva,    Lusitu, Mtila, Mbega, Matola, Luponde, Itulike, Ramadhani, Kihesa,    Utalingolo, Ihalula, Nolle, Mamongoro, Makowo, Ng’elamo, Yakobi,    Igominyi, Idunda, Idihani, Lugenge na Kiyaula wameamua kujikita katika    suala zima la elimu kwa shule za awali, msingi na sekondari.  Majenfo mzuri ya ya kisasa yako katika hatua mbali mbali. Ombi lao ni waalimu wa kutosha.     
2.       Afya:    Ili kuimarisha afya wananchi hao wako katika mpango wa kuwa na   zahanati  katika kila kata. Tayari kwa kujitolea wameanza ujenzi wa   zahanati  hizo. Ombi lao ni kupatiwa wauguzi wa kutosha.
3.       Kilimo:    kutokana na hali ya hewa nzuri ya nyanda za juu kusini, wananjombe   hawa  wamejizatiti katika kilimo cha chai, mahindi, viazi mviringo na   misitu  ya mbao.    
4.       Miundombinu:  kwa    sehemu kubwa wananjombe wamejitahidi sana kutengeneza barabara za   ndani  na wanaamini ni kwa barabara nzuri wataweza kufaidika na  fursa zitokanazo na migodi ya machimbo ya chuma na mkaa wa mawe ya Mchuchuma na Liganga
  Rais  wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi Dk Ali Mohammed  Shein  jana amefanya  uteuzi wa nyadhifa mbali  mbali katika Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar.   
Kwa  mujibu wa  taarifa iliyotolewa na  Katibu wa Baraza la Mapinduzi na  Katibu Mkuu  Kiongozi Dk Abdulhamid  Yahya Mzee Rais amewateuwa Sheikh  Saleh Omar  Kabhi kuwa Mufti Mkuu wa  Zanzibar,Sheikh Khamis Haji Khamis  kuwa Kadhi  Mkuu wa Zanzibar ambapo  Sheikh Hassan Othman Ngwali kuwa  Naibu Kadhi  Mkuu wa Zanzibar. 
Aidha  Dk Shein  amemteuwa Muumin Khamis Kombo kuwa  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa  Mashtaka  Zanzibar,Khalifa Hassan Choum kuwa  Kamishna wa Vyuo  vya  Mafunzo  Zanzibar, Abdulrahman Mwinyi Jumbe kuwa  Mshauri wa Rais  Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi .Pia Mwinyi Jumbe ni  Mwenyekiti wa Bodi  ya  Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar. 
Vile  vile Rais  amewateuwa Balozi Mohammed Ramia  Abdiwawa kuwa Mshauri wake  katika  mambo  ya Ushirikiano wa Kimataifa na  Uwekezaji. Ramia aliwahi  kuwa  Balozi wa Tanzania Nchini Sweden na India  pia alikamata nafasi  mbali  mbali za Uwaziri katika Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar. 
Burhani  Saadati  Haji ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais  Ardhi,Nyumba na  Maendeleo ya  Makaazi. Kabla ya Uteuzi huo Burhani  aliwahi kuwa Waziri  wa Kilimo pia  Waziri wa Ardhi,Maji na Nishati.Pia Dk  Shein amemteuwa  Issa Ahmed  Othman kuwa Mshauri wa Rais Utalii. Issa  aliwahi kuwa  Mwenyekiti wa  Kamisheni ya Utalii Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza juzi
 Hatimaye    lile shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Mara katika maswala ya    utalii, litafanyika Ijumaa ya tarehe 07/10/2011, katika ukumbi wa  Bwalo   la Magereza mjini Musoma, ambapo takriban warembo 15 watapanda  jukwaa   moja kuchuana kumpata muakilishi wa mkoa katika mashindano yan  Miss   Tourism Lake Zone yatakayofanyika baadae mwezi december.       Kampuni ya  Stoppers Entertainment inayoandaa mashindano hayo,   imejipanga kuyapa  hadhi mashindano hayo ambapo warembo mbali na kupita   jukwaani,  watashiriki katika shughuli za kijamii, kuimba na kucheza   ngoma za  makabila ya mkoa wa Mara.     Hata hivyo waandaji wamewaomba  wadhamini  kuendelea kujitokeza kudhamini  shindano hilo, kutokana na  kugusa utalii,  utamaduni na uchumi wa nchi  yetu, yote kwa minaajili ya  kuitangaza  Tanzania.     Shindano la Miss Tourism Mara 2011,  litasindikizwa na  burudani kutoka  kwa  Ditto na Linah wote kutoka  jumba la vipaji THT. Pia burudani za  ngoma za asili zitakuwepo.
Na Mwandishi wetu    
TIMU ya Leaders Club imeisambaratisha timu ya Bongo Movie bao 1-0  katika mchezo maalum wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Leaders Club jana.    
Mchezo huo ulikuwa mkali na wa kusisimua kutokana na wachezaji wote kuonyesha viwango vya hali ya juu.    
Leaders Club ikiongozwa na Doyi Moke,  Adam    Sapi, Christopher Semi, Baraka, Makoye, Juma Pinto, Idd Janguo, Abdul    Tall, Michael, Kibwana Matephone na Charles Nyarusi walitawala mchezo    huo ambao ulivuta mashabiki wengi kutoka kona mbali mbali za jiji.     
Bongo    Movie iliongozwa na Jacob Steve, (JB), Masoud Bitebo, Steven Nyerere   na  Vincent Kigosi ‘Ray’ ilishindwa kumudu kasi ya timu ya Leaders.    
Baada    ya kosa kosa nyingi, Leaders Club ilipachika bao la ushindi kupitia   kwa  Juma Tall kufutia ushirikiano mzuri na Adam Sapi na Juma Pinto.    
Bao    hilo liliwachangaya zaidi Bongo Movie ambao walipoteza ‘network’    uwanjani na kuanza kumvamia mwamuzi kila wakati wanapocheza faulo.    
Tofauti na mchezo wa soka, mchezo huo ulionekana kuwa wa upande mmoja zaidi kutokana na uwezo mkubwa wa Leaders Club.    
Baada    ya mchezo, timu ya Bongo Movie iliondoka mapema uwanjani hapo tofauti    na awali kwani mara kadhaa huwa wanadumu uwanjani hapo kwa vinywaji  na   vitafunwa vingine.
 Na mwandishi wetu     
 NA  MAGRETH  KINABO – MAELEZO    
 WIZARA YA Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imejipanga kwa makini   ili kuhakikisha kuwa maeneo yote ya wazi yanarudishwa kwa wananchi ambapo matumizi yake yatakuwa kwa manufaa ya watanzania wote.
Aidha  wizara hiyo imesema kuwa itatoa muda maalum kwa watu wote walivamia maeneo  hayo kuondoka  wenyewe  na  utakapokwisha muda uliopangwa  itakuja kubomoa hivyo hakutakuwa na msamaha.(hakuna cha msalie mtume).
Kauli hiyo ilitolewa (leo) na Makamu Mwenyekiti  wa Kamati ya   Bunge  ya Ardhi na Maliasili na Mazingira, Abdulkarim  Shah, wakati akifunga maonesho ya  kuadhimisha    miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ya wizara hiyo yaliyofanyika  kwenye   viwanja vya Mashujaa, Mnazimmoja, jijini Dares Salaam.
Shah alitoa kauli hiyo ikiwa ni matazamio ya  miaka 50 ijayo ya wizara hiyo huku akisema maeneo hayo  yamepangwa kwa faida ya wananchi wote. 
“Napenda kusisitiza kwamba  taaluma ya  upangaji    miji inahitajika kutiliwa maanani na serikali haitakubali mipango  hiyo   kubadilishwa matumizi kiholela. Natoa rai hii kwa jamii  kushirikiana  na  serikali kulinda maeneo ya wazi yaliyoko katika maeneo  yao,” alisema  Shah. 
Aliwataka watendaji husika hasa wa halimashauri kutobalidilisha  matumizi ya ardhi .
Aliongeza    kuwa wizara hiyo imeandaa mikakati ya kuwa na mipango shahidi ya    uendelezaji miji itakayokidhi mahitaji ya idadi kubwa zaidi ya watu    watakaoishi mijini. 
Pia  kuwa    na mipango itakayowezesha ujenzi wa miji nadhifu, ya kisasa na    endelevu,kuzijengea uwezo halimashauri kusimamia na kudhibiti    uendelezaji wa miji na kuwa na mipango ya matumizi ya ardhi kwa kila    eneo la makazi nchini. 
“    Wizara imedhamiria kuongeza kasi ya upimaji wa ardhi nchini kwa    matumizi mbalimbali pamoja na kupunguza gharama za upimaji, ambapo nchi    itakuwa imejenga kituo cha kupokea na kusambaza picha za saltillite,    vituo vingi zaidi cha upimaji vitajengwa,” alisema.
Makamu Mwenyekiti huyo  aliongeza kuwa wizara hiyo itaanza kutunza kumbukumbu za upimaji  na ramani kwa kutumia teknolojia ya kisasa, ambapo sasa inatumika  mikoa 15 baadae itakuwa mikoa yote  hadi wilayani kulingana na uwezo wa bajeti.
Alisema ili kuwawezesha wananchi kutumia ardhi kama mtaji  wizara    itahakikisha kuwa mashamba ya wananchi vijijini kote nchini    yanabainishwa yanapimwa na wamiliki wake wanapewa hatimiliki za kimila.
Alisema kwa upande wa Shirika la   Nyumba  la Taifa(NHC)  limejipanga    kujenga nyumba 150,000 katika kipindi cha miaka 50 ijayo na kujenga    nyumba kwa ubia kwa kuwashirikisha wawekezaji wengine.
Rais   Jakaya Kikwete akiongea na Waziri wa mambo ya  Nje na Ushirikiano wa   Kimataifa Mh Bernard Membe na maofisa wengine leo  wakati akiondoka  New  York kurejea nyumbani baada ya  kuhitimisha ziara yake ya Marekani   ambapo alihudhuria mkutano wa 66 wa  Umoja wa Mataifa na wa Diapora   jijini New York na Virginia, Washington  DC.
Picha na Ikulu
Rais   Jakaya Kikwete akiagana na Mbunge wa Bukombe Profesa Kahigi huku    Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii wa Zanzibar Mh Juma Duni Haji    akiangalia leo wakatiakiondoka   New York kurejea nyumbani baada ya  kuhitimisha ziara yake ya Marekani   ambapo alihudhuria mkutano wa 66 wa  Umoja wa Mataifa na wa Diapora   jijini New York na Virginia, Washington  DC.
IMBA YASHINDA 1-0 DHIDI YA MTIBWA SUGAR YA MANUNGU
Mshambuliaji   wa timu ya Simba Emmanuel Okwi akishangilia huku akiwa amembeba   mchezaji mwenzake Amri Kiemba, mara baada ya kufunga goli  dhidi ya timu   ya Mtibwa Sugar ambao mpaka mpira unakwisha hawakupata goli, katika   mchezo wa ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo mpira   umekwisha na Simba wameshinda goli 1-0.    Ulikuwa ni mchezo mgumu kwa  pande zote kwani wamekuwa wakishabuliana na  kukosa magoli mara nyingi  pande zote huku magolikipa wakijitahidi kuzuia  mipira ya hatari.    Simba wamepata penati dakika za nyongeza hata hivyo beki wa timu hiyo   Victor Costa amekosa penati hiyo baada ya golikipa wa timu ya Mtibwa   Sugar Dida kupangua mpira huo. 
KIjana   Mpondela ambaye amevaa skafu nyekundu katikati akishangilia kwa nguvu   na mashabiki wenzake wakati timu ya simba ilipopata goli la kuongoza   dhidi ya Mtibwa Sugar. 
Mchezaji   Emmanuel Okwi wa Simba akikokota mpira mbele ya mabeki wa timu ya   Mtibwa Sugar kabla ya kufunga goli  katika mpambano huo. 



No comments:
Post a Comment