TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, February 24, 2012

Serikali yawaagiza wakaguzi wa ndani wa hesabu kuhakikisha kuwa matokeo ya utekelezaji wa miradi yanalingana na thamani ya fedha iliyotolewa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah akifungua mkutano wa siku tatu wa wakaguzi wa ndani wa Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa leo jijini Dar es salaam wenye lengo kuwaelimisha juu ya marekebisho ya Sheria ya Fedha Sura 348 ya juni 2010 yaliyopelekea Wizara ya Fedha kuanzisha Idara ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali(Internal Auditor General Division) ambayo pia inajukumu kusimamia na kuboresha ukaguzi wa ndani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekrietarieti za Mikoa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah na baadhi ya wakaguzi wa ndani wa Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa baada ya ufunguaji wa mkutano wa siku tatu wenye lengo kuwaelimisha juu ya marekebisho ya Sheria ya Fedha Sura 348 ya juni 2010 yaliyopelekea Wizara ya Fedha kuanzisha Idara ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali(Internal Auditor General Division) ambayo pia inajukumu kusimamia na kuboresha ukaguzi wa ndani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekrietarieti za Mikoa ulianza jana jijini Dar es salaam.
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Serikali imewaagiza wakaguzi wa ndani wa Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa hesabu za miradi yote ya maendeleo katika maeneo yao ya kazi inakaguliwa ili kuhakikisha kuwa inatoa matokeo mazuri yanayolingana na thamani ya fedha kwa matumizi yanaliyofanywa.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa wakaguzi wa ndani wa Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mkutano wa siku tatu wa wakaguzi wa ndani wa Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa unalenga kuwaelimisha juu ya marekebisho ya Sheria ya Fedha Sura 348 ya juni 2010 yaliyopelekea Wizara ya Fedha kuanzisha Idara ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali(Internal Auditor General Division) ambayo pia inajukumu kusimamia na kuboresha ukaguzi wa ndani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekrietarieti za Mikoa.
Alisema kuwa ni wajibu wa wakaguzi kuanzia serikali kuu hadi Serikali za mitaa kuhakikisha kuwa miradi zaidi ya maendeleo inakaguliwa na taarifa kuifikia Wizara ya Fedha mapema ili hatua muafaka ziweze kuchukuliwa kwa lengo la kuboresha dosari zinazojitokeza ili miradi inayopelekwa katika jamii inasaidia e kuleta maendeleo yaliyokusudiwa na wananchi.
“Ni wajibu wenu katika kuongeza uwajibikaji na uwazi katika usimamizi wa matumizi ya rasilimali za umma , ili Serikali iweze kupata thamani ya fedha zinazotumika na kuboresha huduma kwa jamii “ alisema Khijjah.
Aidha Katibu Mkuu huyo aliwaagiza kuwa wakaguzi hao wa ndani kujielimisha zaidi kwa kusoma miongozo mbalimbali ya ukaguzi wa ndani na namna ya kuweka kumbukumbu vizuri ili kufanya kazi ya ukaguzi katika viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.
Alisema kuwa hatua hiyo itawasaidia kuwa watendaji wazuri na wanaotoa taarifa zinazoonyesha ukweli halisi wa matumuzi ya fedha na rasilimali za wananchi kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Khijjah alisema kuwa Serikali ilianzisha Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kupitia marekebisho ya Sheria ya Fedha Sura 348 yaliyopitishwa na Bunge Juni ,2010 kwa lengo ya kuimarisha utendaji na uwajibikaji katika udhibiti na usimamizi wa matumizi ya rasilimali za umma na utawala bora.
Mkutano

Waziri wa wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu usitishwaji wa matangazo ya Televisheni kwa kutumia Technolojia ya analogia na kuhamia teknolojia ya utangazaji ya dijitali ambao utasitishwa rasmi tarehe 31 Disemba mwaka 2012 saa sita kamili usiku. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Frorens Turuka.
(Picha na Anna Itenda - Maelezo)

World class football stars made the dreams of four lucky football fanatics from across East Africa come true in the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ Celebrity Finale last night and football icon Jay Jay Okocha showed why he is ‘so good they named him twice’ as he helped his partner hit the jackpot and win USD50K!
The episode kicked off with the four footballing heroes, Jay Jay Okocha, Marcel Desailly, Rigobert Song and Kalusha Bwalya, stepping out onto the pitch to pick their team mate. The Tanzania nation waited with baited breath to see which excited top scorer from the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ mobile phone game got partnered with each celebrity footballer as they together took on the challenge to a life changing some of money.
It was Kenyan businessman James Nderitu from Nairobird who bagged Nigerian football icon Jay Jay and together went on to win USD50K. James has succeeded in business, succeeded in being partnering with a world class hero and succeeded in winning the Celebrity Finale! Speaking of his epic win, James said, “Winning makes me feel on top of the world – the whole experience, starring in the show and meeting Jay Jay – has been is a real dream come true.”
In classic hero style, Jay Jay gallantly donated his share of the winnings to the other three contestants in recognition of their incredible efforts on the show, so they took each took home just over USD8K .
Commenting on his experience of taking part in the show, Jay Jay said: “It was an incredible experience to be a part of, meeting the contestants, the audience and the hosts. This episode was filled with everything - drama, tears and laughter. Taking part you feel an amazing pressure, something that I did not expect to feel out on the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ pitch. I am delighted that I came through for my team mate, he put in a great performance too and hitting the final target on the Guinness® Money Wall meant we secured a truly life changing amount of money for him.”
Together the duo saw off tough competition, so who are the other knowledgeable football fans that are now the envy of football lovers across East Africa?
  • The top scorer from the East Africa region was ICT officer, George Otieno from Mombasa who was paired up with his dream football partner, former French international, Marcel Desailly
  • Stepping up to represent Tanzania was bachelor of commerce and Liverpool FC fan, Hance Kimola from Kinondoni, Dar Es Salaam who was teamed up with his ultimate football hero, former Cameroonian international, Rigobert Song
  • Back for a second time and ready to show off his knowledge on behalf of Uganda was radio journalist, Patrick Ogua from Arua, who was standing alongside Zambia’s great ever footballer, Kalusha Bwalya
All four contestants battled the mobile phone game leader board and demonstrated that they knew the offside rule from the free kick rule and their Pele from their Ronaldo, but in this Celebrity Finale it was the chance for their football heroes to take centre stage as they went head-to-head on the physical challenges to see if they could get their partners to the final round.
The footballers were on fire throughout the episode with some incredible displays of skill, some closely fought rounds and some extravagant celebrations from former Cameroonian international Rigobert Song. But it was James and Jay Jay who worked together to see off the other teams and secure themselves the chance to take on the Guinness® Money Wall.
The Guinness® Money Wall had defeated many teams throughout the series, but the question on everyone’s lips was, would a member of Nigeria’s ‘Dream Team’ have the skill to beat the wall?
It was a fantastic team effort for the duo with James correctly answering all the questions and Jay Jay demonstrating some phenomenal skill as he worked his way up the targets. The tension in the studio was immense when they had one target left and just one final ball. And as you would expect, Jay Jay delivered and hit the target when it counted, securing the pair the jackpot and earning himself the honour of being the first ever player on the show to hit target six!
Please remember to drink responsibly – 18+.

Balozi wa kinywaji cha Redds Original Akimkabidhi kifurushi cha zawadi mbalimbali Mkurugenzi wa kampuni ya ASSET Intateiment Asha Baraka kwaajili ya maadhimisho ya kipindi cha siku ya wapendanao Duniani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri masuala ya Jumuiya ya Madola, Umoja wa Mataifa na Afrika na Mazingira ( Parliamentary Under Secretary responsible for Africa, United Nations, economic issues, conflict resolution, and climate change) wa Uingereza Bw Hendry Bellingham wakishuhudia Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernad Membe akiweka saini sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hegue kuhusu makubaliano kati ya nchi hizo mbili juu ya taratibu za kukabadhiana watuhumiwa wa uharamia na mali zilizokamatwa katika matukio ya uharamia katika bahari kuu leo February 23, 2012 Lancaster House, London. (PICHA NA IKULU)
Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernad Membe akiweka saini sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hegue wakibadilishana hati za mikataba mara baada ya kusaini.

Mchezaji Ilunga (kushoto)wa Jamhuri ya Kiodemokrasia ya Congo akichuana vikali na mchezaji Hussein Javu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars wakati wa mchezo wao wa kirafiki unaofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam jioni hii. Mchezo huo ulikuwa ni kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya mapambano ya timu hizo kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini, ambapo Taifa Stars itakutana na Msumbiji na RDC Congo itakutana na Sychelies, mpaka mpira unamalizika hakuna timu iliyopata goli hivyo matokeo ya timu hizo mpaka mwisho yamekuwa 0-0 kwa timu zote.
Kocha wa timu ya Taifa Stars Jan Paulsen akimuelekeza jambo Aggrey Morris mchezaji wa timu hiyo kabla ya mchezo huo kuanza kwenye uwanja wa taifa.
Wachezaji wa Timu ya RDC Congo na Taifa Stars wakisalimiana kabla ya mchezo huo kuanza kwenye uwanja wa taifa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Lancaster House jijini London jana February 23, 2012 kijiunga na viongozi wa nchi mbalimbali katika mkutano wa kujadili mstakabali wa nchi ya Somalia ambayo imekuwa katika misukosuko kwa zaidi ya miaka 20 ambapo jumuiya ya kimatifa ikiongozwa na Uingereza imepania kumaliza matatizo mbalimbali katika nchi hiyo ikiwemo kutokuwa na serikali inayoeleweka, uharamia, ugaidi pamoja na kujaribu kurudisha amani.
PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Lancaster House jijini London jana February 23, 2012 kijiunga na viongozi wa nchi mbalimbali katika mkutano wa kujadili mstakabali wa nchi ya Somalia

MUIGIZAJI filamu nyota nchini, Charles Magali maarufu kwa jina la Mzee Magali, atachezesha mechi ya soka ya kuamua mbabe kati ya wasanii wa vichekesho wa Dar es Salaam na Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba. Kwa mujibu wa mratibu wa mechi hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Brayance Promortes, Pearson Samwel, Mzee Magali amechaguliwa kuwa mwamuzi baada ya kupendekezwa na wasanii wa pande zote. “Mzee Magali amekuwa kivutio kikubwa kwa wasanii wa Mwanza na hata nilipowaambia wachekeshaji wa luninga wa Dar es Salaam kwamba refarii atakuwa msanii huyo, wamefurahi sana,” alisema Samwel. Alisema kuwa nyota huyo wa filamu nchini amekubali kupuliza filimbi katika mechi ya kumaliza ubishi juu ya wasanii gani wanaweza kusakata soka kati ya wa Dar es Salaam na Mwanza ‘rock city’. Samwel alisema kuwa viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa Machi 3, mwaka huu, vitakuwa sh. 5,000 katika jukwaa kuu na sh 2,000 mzunguko. Mratibu huyo ameongeza kwamba, kampuni inayoratibu mechi hiyo ipo katika mchakato wa kutafuta mgeni rasmi. Wasanii kutoka Dar es Salaam watakaoshuka uwanjani ni Kingwendu, Sharo Milionea, Mboto, Senga, Pembe, Bambo, Mtanga, Mau, Ringo na Chilly. Wengine Defender, Zimwi, Muhogo Mchungu, Masele, Erick, Kiuno na Hawa, ambao watawasili Mwanza mwishoni mwa mwezi huu kujiandaa kucheza na wapinzani wao. Timu ya wachekeshaji wa Mwanza inaundwa na Babu Mkombe,Sharobaro wa Kihaya, Mchele, Chugu, Ngosha, Brother K, Mama Brandina, Msimbe wa ukweli,Okech Okech, Kafuku Kaukananga, Mzee Dude, Itagata, Malapulapu, Choko na Tengambili. Wasanii wengine watakuwepo siku hiyo ni Tatu Mkate wa Arusha, Avodia Tolu, Mrefu kwenda chini na Jully Tax, ambao wamepania kuwafunga wachekeshaji wenzao wa Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akipata Maelezo Kuhusu Upakuwaji wa Makontena katika Bandari ya Zanzibar kwa Mkuu wa Mipango{ZPC]Ali Haji Haji wakati wa Ziara yake yakutembelea Miradi ya Maendeleo, Kulia Kaimu Mkurugenzi wa Bandari Bw Msanifu Haji Mussa na Maofisa wa Bandari ya Zanzibar[Picha na Ali Meja]

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanueli Nchimbi (kulia) akizungumza na Rais wa Kituo cha Utamaduni na Uhusiano wa Kiislam kutoka nchini Iran Dkt. Mohammed Basheir Khurrqmshad (kushoto) mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine Rais huyo ameahidi kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Iran katika sekta ya utamaduni na michezo ikiwemo kusaidia kuleta makocha wa mchezo wa riadha. (PICHA NA ARON MSIGWA WA MAELEZO)
Benjamin Sawe na Ismail Ngayonga
Kitengo cha Habari
WHVUM.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel John Nchimbi ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuanza utekelezaji wa kupatiwa kocha wa mchezo wa riadha ikiwa ni mkataba wa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Dk. Nchimbi aliyasema hayo (leo) alipokutana na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran Dk.Mohammad Bagher Khurramshad jijini Dar es Salaam ambapo alisema hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa mkataba wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Iran.
Alisema nchi ya Iran imekuwa ni moja kati ya nchi yenye makocha bora na wenye uzoefu katika mchezo wa riadha kwa miaka mingi na kusema ni wakati muafaka kuichangamkia ofa hiyo.
“Nchi ya Iran ina makocha bora wa mchezo wa mbio za riadha sasa ni wakati muafaka kwa Chama cha Mchezo wa Riadha kuichangamkia ofa hii ili mchezo huu uweze kuiweka nchi katika ramani ya michezo duniani’’.Alisema Dr. Nchimbi.
Kwa Upande wake Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran Dk. Khurramshad alisema Iran itaendelea kuisaidia Tanzania katika sekta ya Michezo,Utamaduni na Sanaa ikiwa ni kuboresha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
“Huu ni mwanzo tu wa makubaliano ya mkataba lakini tutaendelea kuisaidia Tanzania katika sekta za utamaduni na sanaa kama tulivyokubaliana katika mkataba baina yetu”.Alisema Dr.Khurramshad
Serikali ya Tanzania na Jamhuri ya Kiislam ya Iran mwezi uliopita zilitiliana saini mkataba wa ushirikiano katika sekta za Utamaduni na Sanaa ambapo kwa upande wa Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi na upande wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran iliwakilishwa na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Dk.Khurramshad.
Katika mkataba huo uliosainiwa Jijini Tehran moja kati ya makubaliano ni pamoja na ushirikiano katika sekta ya Utamaduni na Sanaa ambapo Serikali ya Tanzania iliombwa na ilikubali kuandaa Wiki ya Utamaduni wa Tanzania nchini Iran.

Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa taarifa kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kwanza la Africa kuhusu Uendeshaji, Changamoto na Fursa katika Uhifadhi wa Mbuga za Wanyamapori na Maeneo yaliyohifadhiwa (The 1st Pan-African Conference on Sustainable Tourism Management In National Parks and Protected Areas: Challenges and Opportunities).
Kongamano hilo la siku Tano limepangwa kufanyika katika Kituo ya cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) tarehe 15 hadi 19 Oktoba 2012. Washiriki wapatao 300 kutoka nchi mbalimbali wanatarajia kuhudhuria.
Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO) kufuatia mkutano wake (UNWTO General Assembly) ambao ulifanyika nchini Korea 2011. Katika Mkutano huo Tanzania pia ilichaguliwa kuwa mjumbe katika Baraza la Utendaji (Executive Council) la Shirika hilo, nafasi ambayo itakuwa nayo hadi mwaka 2015.
Kongamano hilo la Oktoba 2012 ni la kwanza na la aina yake litawakuwakutanisha wahifadhi na wadau wa sekta ya Utalii ili wajadili namna ya kufanikisha uhifadhi na utalii duniani. Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo kutokanana na sifa nzuri na uzoefu ilio nao katika kuanzisha na kuendeleza hifadhi za Taifa.
Tanzania inategemea kupata manufaa kutokana na Kongamano hilo kwani washiriki watapata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini na hivyo kuvitangaza warudipo makwao. Pia watanzania watapata fursa ya kuuza huduma mbalimbali kwa wageni watakaohudhuria Kongamano hilo, kama vile malazi, chakula, burudani na usafiri.
Faida nyingine ni kuwa, washiriki kutoka Tanzania watapata fursa ya kubadilishana ujuzi na ueledi na wenzao watakaotoka nchi mbalimbali duniani.
Wizara inatoa wito kwa wanachi, wafanyabiashara na wadau wote kujiandaa ipasavyo ili kunufaika na ujio huo wa Kongamano hilo la kimataifa nchini.
Taarifa mbalimbali zitaendelea kutolewa kuhusu maendeleo ya maandalizi ya Kongamano hilo.
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Uzinduzi wa kumbu kumbu ya mwanzilishi wa skauti Ulimwenguni bw Robert Baden PowelL na mkewe Bi. Oliva Powell(lady baden powell)kimkoa umefanyika leo na kilele ni siku ya tar.25 ya mwenzi huu kwenye viwanja vya sheikh Amri Abeid jijini hapa kwa maonyesho na matamasha kote nchini.
Hayo yamesemwa nakamishina mkufunzi mkuu wa taifa bi Margareth Olumbe wakati akisoma risala ya maskauti wa kike hapa Arusha na kusema kuwa girl guide hapa nchini ilanzishwa mnamo mwaka 1928 na girl guide 9 na walijiita 1st Kilimanjaro na walikuwa na uhusiano na mke wa gavana wa wakati huo ukaingia ukimya wa muda mrefu na guiding haikusikika hadi 1934 mke wa gavana Lady Mack alianzisha kampuni nyingine Dar es-salaam na ikaitwa 1st Dar –es-salaam kampuni na ilikuwa na wazungu tu baadae alianzisha first dar-es-salaam Brownes na ilkuwa mchanganyiko.
Kuna changamoto nyIngi kubwa zinazowakabili girl guide hapa mkoani na taifa kwa ujumla zikiwemo kuwatoa watoto katika tabia hatarishi kuwa raia wema,wazazi ambao wangesaidiana nasi wamekuwa na shughuli nyingi na wengine hawafikiki hata na watoto wao,mwitiko wa wananchi
Akatoa ombi kwa mgeni rasmi ambaye alimwakilisha mlezi wa skauti wa kike hapa nchini mama Salma Kikwete bi Pendo Laizer kutoka(CASEC) kuwa awe mlezi wa girl guide wa arusha na mgeni huyo kukubali kuwa mlezi na kuwatafutia wafadhli wakukisaidia girl guide mgeni huyo aliambatana na mgeni kutoka nchini uingereza bi jill Nicholson na Yona .M.Mziba kutoka kitengo cha polisi jamii mkoani hapa

Na Gladness Mushi - Arusha
Tanzania inajipanga vizuri kutekeleza sera ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto wa kitanzania katika kutoa elimu ya awali hapa nchini na kuwa kila shule itatakiwa kuwa na shule ya awali kwani maandalizi tayari yalikwishaanza kwa walimu wa cheti kuwa ndio wafundishaji wa elimu hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi Dr.Shukuru Kawambwa wakati akiongea na vyombo vya habari katika jukwaa la kwanza la kitaifa linalo jadili utungwaji sera ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto jukwaa hilo lililo andaliwa na banki ya dunia kupitia shirika la bennian la marekani inayofanyika jijini hapa.
Dr.kawambwa alisema kuwa kuangalia sera za maendeleo ya awali ya mtoto ni jambo ambalo serekali inajipanga nalo na kuwa inalipa umuhimu mkubwa ndiyo maana umeona mawaziri mbali mbali kutoka wizara za Elimu,Fedha,ofisi yawazirimkuu(Tamisemi),Afya na Maendeleo ya jamii jinsia na watoto na kuwa sera ya makuzi na malezi ni tofauti na sera nanipana zaidi kuliko sera ya elimu ilyopo hapa nchini kwa sasa.
'Unapoanza kuwekeza katika kuandaa sera na mafunzo ya awali kwa mtoto inamaana kuwa unamjali na kumthamini na kugundua vipaji vya watoto na huko ndiyo kujenga msingi wa awali wa mtoto ili anapoanza elimu ya msngi teyari anakuwa na msingi imara'.alisema Kawambwa
Alisema kuwa serekali njia iliyosawa hawajapotea kwani elimu ya kiwango cha chini inatolewa japo haikuwa inapewa kipaumbele lakini sasa tunaangalia uwezekano wakuanza kutoa chakula kwa shule zetu zote japo si kwa mwaka huu na hii inatokana na ukosefu wa fedha na akalishukuru shirika la chakula ulimwenguni (WFP)kwa kutoa chukula kwa baadhi ya shule za jamii za kifugaji hapa nchini na mafaniko meyaona kwani shule hizo viwango vimepanda.

No comments:

Post a Comment