TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, March 11, 2012

MNYAMA SIMBA ASHINDWA KUUNGURUMA MWANZA,

Mchezaji wa timu ya Simba Felix Sunzu akimtoka beki wa timu ya Toto Africa ya Mwanza katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii, Mpira umekwisha na hakuna timu iliyofanikiwa kupata goli katika dakika tisini matokeo yamekuwa 1-1. Kocha Milovan ameipongeza timu ya Toto Africa kwa kucheza vizuri, wao walitaka kushinda lakini hawakuweza kufanya vizuri.
Wachezaji wa Simba ta Toto Africa ya Mwanza wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Kikosi cha timu ya Toto Africa ya Mwanza kikiwa katika picha ya pamoja.
Timu zikiingia uwanjani tayari kwa kukipiga katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.

Na Mwandishi Wetu MALKIA wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando, naye atakuwa miongoni mwa waimbaji watakaopamba tamasha la nyimbo za Injili litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Alex Msama, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo chini ya Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, Muhando amethibitisha kushiriki tamasha hilo. "Katika tamasha la Pasaka mwaka huu ndipo Rose Muhando atapata fursa ya kutambulisha albamu yake ya nne ya Utamu wa Yesu ambayo haijawahi kuzinduliwa tangu aikamilishe," alisema Msama. Albamu ya Utamu wa Yesu inabeba nyimbo saba ambazo ni Utamu wa Yesu uliobeba jina la albamu hiyo, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia. Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawa Sawa. Msama alisema pia Muhando ataimba pamoja na Anastazia Mukabwa wa Kenya aliyeshirikiana naye katika albamu ya Vua Kiatu, na baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu. "Mpaka sasa tunaendelea na mazungumzo na waimbaji wengine mahiri wa muziki wa Injili, lakini Muhando atakuwepo na Mukabwa atakuja na kundi la waimbaji wake," alisema Msama. Albamu ya Vua Kiatu inabeba nyimbo nane ambazo ni Vua Kiatu uliobeba jina la albamu hiyo, Ee Mungu, Usiwe Manamba, Nzizilela, Nishike Mkono Bwana, Wanaokudharau na Mfalme. Mbali na Mukabwa, wengine waliothibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka ni Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho wa Dar es Salaam, kundi la Glorious Celebration na Atosha Kissava kutoka Iringa. Kwa mujibu wa Msama, tamasha hilo baada ya kufanyika Dar es Salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu. Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane. Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000. Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi sita za Afrika ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya.

The Girl Empowerment Program” under the theme ” Build Your Future”, aimed at empowering Secondary school girls Saturday 10th March 2012, As part of our Corporate Social Responsibility initiative, Airtel Tanzania has today launch ”The Girl Empowerment Program” under the theme ” Build Your Future”, aimed at empowering Secondary school girls aged 14 to 18 years, in achieving their future career goals and build self confidence amongst young women. The Girl Empowerment Program is key to Airtel as it goes hand in hand with Airtel’s mission of educating the girl child and creating brand loyalty. Apart from the fact that they need clear rules, consistent consequences for breaking rules and encouragement to do their best, young girls need opportunities outside of school curriculum to learn and develop new skills and interests with other youth and adults. Speaking during the launch held at Canossa Girls Secondary School in Tegeta, Dar es Salam Airtel customer Care Director Adrianna Lyamba said ”Today we kick start the program this quarter with “Canossa Girls Secondary School in Tegeta, The Girl Empowerment Program will be an ongoing program which will be done quarterly to Girls Secondary Schools around Tanzania and in this program we will be covering different topics relating to career management, building self confidence and making the right decisions in life. We will be requesting our own employees to volunteer to speak in schools and share their career experiences and skills with the students. This will enable the students understand what it takes to build a career and select the right career path in life”. “There is the say that saying, when you educate a women you have educated the whole community, we therefore believe the knowledge acquired will be a great significance to girl’s destiny and for the upcoming generation. She added We are highly committed towards supporting Tanzanian community, apart from Girl empowerment program we have been supporting education sector through Shule yetu program were we provide books to Secondary schools in the country, our aim is to improve education level through availability books to secondary schools students. Since we started our books support programme, approximately seven years ago, we have reached more than 800 secondary schools that are spread across the country”

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Azam lililochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 72,731,000.
Jumla ya watazamaji 19,339 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati kwa VIP A ilikuwa sh. 15,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 11,303,932.20 kila timu ilipata sh. 14,726,592.20, uwanja sh. 4,908,864.07.
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,963,545.63, TFF sh. 4,908,864.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,454,432.03, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 490,886.41 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,908,864.07.
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. waamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, tiketi sh. 3,540,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata tena sh. 1,353,730 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata tena sh. 1,160,340.

Saturday, March 10, 2012

Mwamuzi Israel Mujuni pamoja na wasaidizi wake akitoka nje kwa kusindikizwa na askali wa kikosi cha kutuliza Ghasia FFU mara baada ya kupuliza kipenga cha mwisho kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliokutanisha timu ya Yanga ya Jangwani na timu ya Azam FC kutoka Chamazi ambapo Yanga imekandamizwa magoli 3-1 na wauza Sembe hao wa Chamazi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mwanzo ulikuwa ni mchezo mzuri uliokuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande lakini mambo yalibadilika mara baada ya Azam kuandika goli la kwanza, mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga alionekana kumlalamikia refa mara kwa mara jambo ambalo refa alimuonya mara kadhaa lakini, hata hivyo Niyonzima aliendelea baada ya muda, alitolewa nje kwa kadi nyekundu, jambo ambalo lilizua tafrani uwanjani huku makonde yakirushwa hovyo, baadae naye mchezaji Nadir Haroub Canavaro alipewa kadi nyekundu kutokana na vurugu hizo na kuzua tifu lingine uwanjani. Hali ilikuwa kama hivi angalia matukioo ya picha hizi.
Canavaro akitolewa nje huku huku akilia na kocha wake Papic akimtuliza.
Papic akiwatuliza wachezaji na baadhi ya maafisa wa benchi la ufundi
Canavaro akizuiwa na wenzake asimshushie kipondo refa huyo.
Polisi akiwa ameingia uwanjani ili kutuliza fujo hizo na kutoa ulinzi kwa refa huyo.
Mchezaji John Boko wa Azam FC akimtoka beki wa Yanga Haroub Nadir Canavaro.
Mashabiki wa Azam FC wakishangilia kwa furaha.
John Boko akishangilia mara baada ya kuipatia timu yake goli la kwanza.
Timu zikiingia uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo 

Mratibu wa Kitaifa Mradi wa athari za Mabadiliko ya tabia Nchi Bw Faraja Ngeregeza akitoa Mada kwa Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais juu ya athari za mabadiliko ya tabianchi leo Ukumbi katika wa Karimjee jijini Dar es Salaam[Picha na Ali meja]
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rasi wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Bw Richard Muyungi[Pichani hayupo]akitoa Mafunzo ya Utaratibu wa Utekelezaji wa Miradi ya Kupunguza Gesi joto huko kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.[Picha na Ali Meja]
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Tathimini na Ufuatiliaji Bi Grace Ngallu wakati wa Mafunzo ya Utaratibu wa Utekelezaji wa Mradi wa Kupunguza Gesi Joto Mafunzo hayo yalioandaliwa Kwenye Ukumbi wa Karimjee Mjini Dar es Salaam Katikati Naibu Katibu Mkuu Ofisiya Makamu wa Rais Eng Ngosi Mwihava[Picha na Ali meja]
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Idara ya Mazingira Bw Richard Muyungi akitowa Mafunzo ya Utaratibu wa Utekelezaji wa Miradi ya Kupunguza Gesi ya Joto kwa Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais yaliofanyika Leo Kwenye Ukumbi wa Karimjee Mjini Dar es Salaam.[picha na Ali Meja]

Baadhi ya washiriki wa semina maalum ya mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka nchi 20 duniani iliyofanyika hivi karibuni nchini Misri wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ofisi za gazeti la Serikali la Al Haram Jijini Cairo. Wa pili kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (Maelezo) Ismail Ngayonga na anayemfutia ni Afisa Habari wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Concilia Niyibitanga.
Afisa Habari wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Concilia Niyibitanga akiwa katika picha ya pamoja na watoto katika eneo la Tahrir Square Jijini Cairo nchini Misri hivi karibuni wakati wa kumbukumbu ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa vurugu katika sehemu hiyo ambazo zilimwondoa madarakani Rais wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak.
Afisa Habari wa Idara ya Habari (Maelezo) Ismail Ngayonga akitazama sehemu ya mitambo inayochapisha gazeti la Al Haram linalomilikiwa na Serikali ya Misri wakati wa ziara ya mafunzo kwa waandishi kutoka nchi 20 duniani iliyofanyika hivi karibuni nchini humo.
Afisa Habari wa Idara ya Habari (Maelezo) Ismail Ngayonga akiwa katika eneo la Tahrir Square Jijini Cairo nchini Misri hivi karibuni. Sehemu hiyo ni chimbuko la vuguvugu la wananchi katika kupinga na hatimaye kuung’oa madarakani utawala wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak.
Matumizi ya wanyama kazi kama farasi na punda Farasi na Punda ni makubwa sana katika nchi ya Misri. Pichani ni Farasi wakiwa wamebeba miti na kuwekwa pembeni mwa barabara katika mtaa wa Zamalek Jijini Cairo kama walivyokutwa na kamera yetu hivi karibuni nchini humo.
Waandishi wa habari na wapigapicha kutoka nchi 20 duniani wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni mara baada ya kuwasili katika piramidi za Misri zilizopo katika mji wa Giza nje kidogo ya Jiji la Cairo nchini Misri, aliyechumaa mstari wa mbele wa pili kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (Maelezo) Ismail Ngayonga. Piramidi za Misri ni miongoni mwa vivutio vya utalii ambavyo vipo katika orodha ya maajabu saba ya dunia.
(PICHA KWA HISANI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO)

Operations Manager, MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo awards Jane Mhina of Hotspot Media an HD PVR which she won in a lucky draw during DStv Customer Day.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa Kituo cha kimataifa cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Kambarage Nyerere kwenye Mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es salaam March 10,2012. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Kulia kwake ni Balozi wa China nchini, LV Youqing. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mzengo Pinda akijadili jambo na Waziri wa mamboya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kulia) , Balozi wa China Nchini, LV Youqing baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere , Mtaa wa Shaban Robert jijini Dar es salaam March 10,2012. Wengine pichani na wahadisi kutoka China wanaosimmia ujezi huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezitaka kampuni na taasisi zinazohusika na kutoa huduma muhimu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ziharakishe kufanya hivyo ili ujenzi wake ukamilike mapema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumamosi, Machi 10, 2012) mara bada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa kituo hicho na kukagua ujenzi wake katika mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.
Kampuni zinazotakiwa kufanya hivyo ni TANESCO kwa ajili ya umeme wa jengo hilo, Kampuni ya Simu (TTCL) kwa ajili ya mkonga wa mawasiliano na Idara ya Kodi ya Mapato (TRA).
Waziri Mkuu amesema ujenzi wa kituo hicho cha mikutano ni ishara ya urafiki wa muda mrefu ulikuwepo baina ya Tanzania na China na kwamba kukamilika kwake kutaboresha mandhari ya Jiji la Dar es Salaam.
Mapema, akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo ambalo litagharimu yen milioni 183.5 sawa na dola za Marekani milioni 30, Balozi wa China nchini Tanzania, Bw. Lv Youqing alisema ujenzi wa jengo hilo ulianza mara baada ya sherehe za uzinduzi Januari 15, 2010.
Awali, ujenzi wa jengo hilo ulitarajiwa kukamilika Aprili, 2012 lakini kutokana na uchelewashaji wa miundombinu hiyo muhimu hivi sasa linatarajiwa kukamilika Agosti, mwaka huu.
Litakapokamilika jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 1,000; litakuwa na kumbi ndogo ndogo nne zenye uwezo wa watu zaidi ya 20, ukumbi wa chakula wa watu zaidi ya 700 na ofisi za watumishi wa ukumbi huo. Vilevile, kutakuwa na ukumbi mmoja ambao unaweza kugawanywa (partitioned) na kutengeneza ofisi za muda kwa watu wanaoendesha mkutano mkubwa katika ukumbi huo.
Naye Mkurugenzi wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho, Bw. Huang Meiluan alisema ujenzi wa ghorofa ya chini umekamilika kwa asilimia 40 kwa sababu bado wanasubiri huduma muhimu zikamilike ili waanze kuweka sakafu. “Tunasubiri kuunganishwa na mkonga wa mawasiliano wa Taifa, bado hatujaweka njia kuu za umeme za kuingia katika jengo... kasi ya ujenzi imeathirika kutokana na kutokamilika kwa huduma hizi muhimu,” alisema.
Alisema ujenzi wa ghorofa ya kwanza na ya pili umekamilika kwa asilimia 90 na imebakia kazi ya kumalizia kuweka nakshi za ndani tu (interior decoration). “Kwa nje, kazi ya ujenzi imekamilika na tumeanza kuweka nakshi, kazi hii imekamilika kwa asilimia 75,” alisema.
Alisema wanakabiliwa na changamoto ya wizi wa vifaa vya ujenzi unaofanywa na vibaka kila mara na kwamba inawapa mtihani kwani itawalazimu kuagiza upya vifaa hivyo kutoka China. Aliomba polisi wawasaidie kuimarisha ulinzi katika eneo la ujenzi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe alimweleza Waziri Mkuu kwamba wizara yake imeanza kushughulikia upatikanaji wa kifaa muhimu cha umeme ambacho kilishindwa kupatikana hapa nchini.
Alisema vyuma vilivyotumika katika hatua za awali za ujenzi wa kituo hicho ni tani nyingi, na kwamba yanahitajika malori ya kuvisomba na kibali kutoka TRA ili yaweze kupelekwa katika eneo jingine kwa kuhifadhiwa. Alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba wizara yake inafuatilia suala hilo pia.
Kuhusu uwekwaji wa nyaya za mkonga wa mawasiliano ambao unapaswa kufanya na TTCL, waziri Membe aliomba apewe wiki moja zaidi kwani amekuwa akisumbuana nao kwa zaidi ya mwezi mmoja bila mafanikio yoyote. Suala la ulinzi pia alisema ameshaanza kulishughulikia.

Mbunge wa Arusha Godbless Lema akiwa amebebwa juu juu mara baada ya kuwasili hapo Meru Wilayani Arumeru ambapo mkutano mkubwa wa uzinduzi wa kampeni wa chama cha Deomkrasia na maendeleo CHADEMA unafanyika kuanzia muda huu katika viwanja vya Shule ya Msingi Leganza, Mwandishi Wetu ambaye yuko katika eneo la tukio, anasema "Tayari helkopta zilizowachukua viongozi kadhaa wa chama hicho zimeanza kutua katika viwanja hivyo tayari kwa uzinduzi na mkutano huo utarushwa moja kwa moja na televisheni kadhaa za hapa nyumbani.
Umati wa watu ukiwa unaelekea eneo la mkutano katika viwanja vya shule ya Msingi Leganza.
Waendesha pikipiki hawako nyuma kama wanavyoonekana katika picha hii. (PICHA KWA HISANI YA MJENGWABLOG)

Meneja Mkuu wa Multchoice Tanzania Bw. Peter Fuel akifurahia jambo na Meneja wa Uendeshaji Ronald Shelukindo wakati wa hafla ya wateja iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wateja wake, katika siku hii ya leo ving'amuzi vya DSTV vinauzwa kwa silingi 120.000 pamoja na kukuunganishia nyumbani kwako na ofaa hii ni ya leo tu.
Hafla hiyo inafanyika katika ofisi za Multichoice zilizopo Saint Peter Oysterbay jijini Dar es salaam. Mwanafunzi Diana Kimaro wa Chuo Kikuu cha Nilai Malasia akisomea masuala ya biashara ambaye yuko katika benki ya NMB kwa mazoezi akimpatia huduma mmoja wa wateja wa benki ya NMB aliyefika katika hafla hiyo, Benki ya NMB pia imeshiriki katika hafla hiyo kwa ajili ya kuwaelezea wateja wao huduma mbalimbali wanazozitoa.
Watoto wakicheza
Wanenguaji wa kiume wa bendi ya African Stars wakicheza katika hafla hiyo.
Mwimbaji wa bendi hiyo Lwiza Mbutu akiimba pamoja na wanamuziki wenzake katika hafla hiyo.
Meneja uendeshaji wa Multchoice Ronald Shelukindo akizungumza na wateja wa kampuni hiyo katika hafla hiyo.
Wateja mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo wapata burudani mbalimbali.
Baadhi ya wateja pia wameongozana na watoto wao katika kuonyesha upendo.
Kulia ni Ronald Shelukindo Meneja Uendeshaji, Barbara Kambogi Meneja Uhusiano na katikati ni Orest Kawau kutoka African Media Group.
Mdau Julio Batalia akitangaza bidhaa yake ya PayPoint katika hafla hiyo.
Wadau kutoka benki ya NMB nao wakiwa katika hafla hiyo tayari kwa kuelimisha wateja juu ya huduma zao.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara Jana (Machi 10 mwaka huu) amechangia sh. milioni moja kwenye uzinduzi wa akaunti ya Twiga Stars kupitia Tigo Pesa kuichangia timu hiyo ambayo inashiriki michuano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC).
Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam, Dk. Mukangara alisema ni jukumu la kila Mtanzania kuichangia Twiga badala ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuachiwa pekee mzigo huo wa kuendesha timu hiyo.
Wachangiaji wa Twiga Stars wanatakiwa kutuma mchango wao kwenda namba 13389 ambapo kiwango cha juu kinachoweza kutumwa kwa muhamala (transaction) mmoja ni sh. 500,000. Kwa Waziri Dk. Mukangara kuchangia sh. milioni moja alifanya mihamala miwili.
Naye Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani alisema Twiga Stars kwa sasa haina mdhamini na Shirikisho limekuwa likibeba mzigo wa kuhakikisha inashiriki katika mechi za kirafiki na mashindano mbalimbali kwa vile imekuwa ikifanya vizuri.
Twiga Stars inayofundishwa na kocha Charles Boniface Mkwasa iko kwenye raundi ya pili ya mashindano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) ambapo Mei 26 mwaka huu itacheza na Ethiopia jijini Addis Ababa.

Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa shirika la Millenium Challenge Account Tanzania Dar es Salaam(MCA-T Dsm) Bw. Bernard Mchomvu akimkabidhi zawadi ya Khanga yenye nembo ya shirika hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya walipoonana ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu (kulia) jana kujadili miradi ya barabara inayodhaminiwa na shirika la Millenium Challenge Cooperation (MCC) kupitia Tanzania Millenium Challenge Account (MCA-T Dsm). (Pichana Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa) Shirika hilo linafadhili ujenzi wa barabara kuu za lami zinazojengwa Mkoani Rukwa zenye jumla ya Km. 224 kwa miradi ya Tunduma-Ikana, Ikana-Laela, na Laela-Sumbawanga. Kwa mujibu wa Bwana Mchomvu miradi hiyo yote pamoja na changamoto zote kuzingatiwa itakuwa imekamilika ifikapo mwezi June 2013 na barabara zote zitakuwa zimekabidhiwa kabla ya mwezi wa nane 2013. Kwa upande wa Ruvuma shirika hilo linafadhili ujenzi wa barabara itokayo mjini Songea kuelekea Wilaya ya Mbinga ambapo ujenzi huo unaendelea na unategemewa kukamilika mwakani. Hata hivo Mkurugenzi huyo aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano wanaoutoa kuwaeleimisha wananchi wao juu ya umuhimu wa miradi hiyo na ulinzi wa vifaa vya ujenzi kwani umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza wizi wa vifaa vya ujenzi vilivyokuwa vinafanywa na baadhi ya wananchi na wafanyakazi wasiokuwa waaminifu. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya allishukuru shirika hilo kwa jitihada zao za kuchangia maendeleo nchini. Aliwashukuru pia kwa hatua za hivi karibuni walizochukua kujenga daraja la Laela ambalo ni kiunganishi muhimu kwa wananchi wa eneo hilo katika shughuli zao za kila siku hususani kuwaunganisha na kituo cha afya cha Laela.
Picha ya pamoja kati Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu, Injinia Stella Manyanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Tarimo na wawakilishi wa Jumuiya ya Millenium Challenge Cooperation (MCC) Bw. Carl Fickenscher Mkurugenzi Mkazi nchini (kushoto) na Bw. Bernard Mchomvu Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa shirika la Millenium Challenge Account Tanzania Dar es Salaam(MCA-T Dsm).
Kushoto Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa shirika la Millenium Challenge Account Tanzania Dar es Salaam(MCA-T Dsm) Bw. Bernard Mchomvu akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.

No comments:

Post a Comment