TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 4, 2013

Mbatia alitikisa Bunge Dodoma *Ni kuhusu hoja ya udhaifu sekta ya elimu *Wabunge wa CHADEMA, CCM wavutana Jahazi lazama Z'bar, 10 wahofiwa kufa *22 waokolewa, lilikuwa na abiria 32 Madiwani Kigamboni waponzwa na mwaliko wa Tibaijuka Pinda ataka amani itawale Mtwara Mvua yaua mwanafunzi, yajeruhi Mkakati wa kumtoa Ponda waandaliwa Sijaridhishwa na taarifa Waziri Pinda kuhusu gesi Hoja ya Mbatia imeona mbali ILALA YAANIKA MAFANIKIO YA RAIS KIKWETE Kaseba aapa kuonesha uwezo wake UZITO Ligi Kuu ya Grand Malt kuanza leo Azam yatamba kuendeleza vipigo Meru yazipa 'tafu' timu sita MICHEZO Kocha Stars aita wa kuivaa Cameroon *Amir Maftah, John Bocco watemwa TFF yatupa pingamizi zote zilizowekwa

Posted: 01 Feb 2013 02:01 AM PST

Rose Itono na Goodluck Hongo

MBUNGE wa kuteuliwa kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, jana aliwasilisha hoja binafsi iliyoainisha suala zima la udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini.
Alisema kukosekana kwa mitaala katika shule za msingi na sekondari kunachangia wanafunzi kufanya vibaya na utendaji mbovu wa kitengo cha kuandaa mitaala hiyo, kimeshindwa kufanya kazi zake ipasavyo na kusababisha usambazaji vitabu kunuka harufu ya rushwa.
Hoja hiyo iliyoibua mvutano mkali wa wabunge, iliwasilishwa bungeni mjini Dodoma. Baadhi ya wabunge walishauri iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchukuza udhaifu huo na wengine wakitaka hoja hiyo ifanyiwe kazi na Serikali.
Kutokana na hali hiyo, Spika wa Bunge Bi. Anne Makinda alilazimika kusimama na kujibu hoja za wabunge lakini kambi ya upinzani ilikuwa na msimamo wa kutaka iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchunguza udhaifu ulioainishwa na Bw. Mbatia.Wabunge wa CCM walipinga msimamo wa kambi ya upinzani
na kutaka hoja hiyo ifanyiwe kazi na Serikali wakidai Bw. Mbatia ameainisha mambo mengi ambayo kaamati haiwezi kuyafuatilia kwa wakati mmoja yakiwemo ya kisera.Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Simanjiro, mkoani Manyara, Bw. Christopher Ole Sendeka (CCM), alishauri hoja hiyo iachewe Serikali na kusisitiza kuwa, kikanuni kazi ya kuunda Kamati Teule hasa kwa suala la elimu linahitaji ujuzi na utaalamu wa hali ya juu.“Japo kuwa wabunge ni wasomi, hakuna ambaye ni mtaalamu wa masuala hayo hivyo jambo hili liachiwe Serikali ifanyie kazi hoja ambazo zimewasilishwa na Bw. Mbatia,” alisema.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha Bw. Joshua Nassari (CHADEMA), alisema inaonekana wabunge wameanza kukimbia majukumu ya kibunge kwa kukataa tume hiyo isiundwe.
Alisema kazi kubwa ya wabunge ni kuisimamia Serikali ambayo haiwezi kujisimamia yenyewe. “Katika Bunge hili, iliungwa Kamati Teule ikiongozwa na Dkt. Harrison Mwakyembe, kuchunguza sakata la Richmond...” alisema Bw. Nassari.
Mbunge wa Peramiho, mkoani Ruvuma, Bi. Jenista Mhagama (CCM), alisema kwa mtazamo wake wabunge wote wanajenga nyumba moja hivyo jambo la msingi ni kuangalia namna ya
kuiboresha hiyo iweze kufanya kazi zake vizuri.
Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), alisema elimu ni gharama hivyo lazima madudu yaliyomo ndani ya sekta hiyo yaondolewe na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
“Hoja aliyoitoa Bw. Mbatia ni ya msingi kwani elimu ni gharama kubwa hivyo lazima ijadiliwe kiundani na kukokotoa madudu yote, kazi ya bunge ni kuisimamia Serikali si vinginevyo,” alisema na kuongeza kuwa, kamwe Serikali haiwezi kujichunguza yenyewe.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, alisema Serikali imezingatia hoja zilizotolewa na Bw. Mbatia na kuahisi kuifanyia kazi ambapo hivi sasa wapo katika mapitio ya
sera ambayo yamechukua muda mrefu.
“Ieleweke kuwa, kuna mambo makubwa yanapaswa kuangaliwa ili ifikapo 2020, Taifa liweze kufikia hadhi ya kimataifa,” alisema.
Katika hoja yake, Bw. Mbatia alidai pamoja na mambo mengine, kuna kasoro nyingi kwenye mitaala wakati mwingine mtuzi wa vitabu anageuka kuwa Mhariri jambo ambalo si sahihi.

Jahazi lazama Z'bar, 10 wahofiwa kufa *22 waokolewa, lilikuwa na abiria 32
Posted: 01 Feb 2013 02:00 AM PST

Na Mwandishi Wetu

WATU 11 wanahofiwa kufa maji baada ya jahazi la Sunrise, ambalo lilikuwa likitokea mkoani Tanga kwenda Zanzibar kuzama katika eneo la Nungwi.
Habari zilizolifikia gazeti hili ambazo zimethibitishwa na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi Zanzibar, zilidai jahazi hilo lilibeba watu 32 ambapo hadi jana mchana, 21 walikuwa wameokolewa.
Inadaiwa kuwa, jahazi hilo mbali ya kubeba abiria pia lilikuwa na mizigo ambapo jitihada za kuwatafuta abiria wengine zinaendelea na hakuna taarifa za mtu aliyepoteza maisha hadi sasa
kutoka pangani kwenda kwenda zanzibar- abiria 27 na manahodha watano eneo la maziwe, jirani na Nungwi kati yao 21 wameokolewa wakiwa hai 11 hawjulikani walipopigwa
lilikuwa la kusafirisha mizigo kwenda zanzibar
Msemaji Mohamed Muhina msemaji wa Jeshi la Polisi wakati akihojiwa na idhaa ya kiswahili ya BBC alisema manahodha  wameokolewa baadhi yao hawajapatikana
"Ni Kweli taarifa za tukio hilo zipo lakini sina taarifa zaidi, labda unaweza kuwasiliana na Kamanda wa Polisi Kaskazini Unguja, aliyeko eneo la tukio anaweza kukupa taarifa zaidi," alisema mmoja wa maofisa wa polisi Zanzibar.
Juhudi za kumpata kamanda hiyo aliyetwa kwa jina moja la Ahamada hazikuweza kuzaa matunda kutokana na simu yake kutopokelewa muda. Kuzama kwa jahazi hilo na mfululizo wa ajali za baharini ambazo zimekuwa zikitokea katika habari ya Hindi na kusababisha vifo vya watu wengi.
Mwaka jana Meli moja inayomilikiwa na kampuni ya SEAGAL iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar Tanzania ilizama katika bahari ya Hindi baada ya kukumbwa na dhoruba kali na hatimaye kupinduka.
Kwa mujibu wa jeshi la polisi visiwani Zanzibar meli hiyo iliondoka Dar es Salaam mchana na imepatwa na ajali hiyo huku ndani yake kukiwa na abiria zaidi ya 200.
Kabla ya meli hiyo kuzama, meli nyingine iliyokuwa ikitoka Zanzibar kwenda Pemba ya MV Spice, ilizama kwenye mkondo wa Nungwe na kusababisha vifi vya watu karibu 200.
Posted: 01 Feb 2013 01:57 AM PST
Na Andrew Ignas

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Temeke, limemtaka Meya wa halmashuri hiyo, Bw. Maabadi Hoja, awachukulie hatua za kinidhamu madiwani wa Kigamboni waliokubali mwaliko wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Hali hiyo inatokana na madiwani hao kuridhia kuundwa kwa Kamati Maalumu ya kusimamia mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni bila kumshikilisha Mwenyekiti wa halmashauri hiyo na madiwani wa Temeke ili kutetea haki na masilahi ya wananchi.
Wakizungumza katika kikao cha baraza hilo kilichokuwa kikijadili ajenda mbalimbali za halmashauri, madiwani hao akiwemo Bw. Wilfred Kimati (Kata ya Kurasini) na Naibu Meya Bw. Noel Kipangule (Kata ya Chang'ombe), walisema umefika wakati wa Bw. Hoja kuonesha makucha yake kwa madiwani hao.
Walisema madiwani hao wameonesha usaliti mkubwa kwa kukubali mwaliko huo na kuridhia uundwaji wa kamati hiyo.
“Suala hili kama tutalifumbia macho, litaleta vita kwa sababu kama madiwani wa Temeke tumetelekezwa, itakuwa vigumu wananchi kupata taarifa za jambo hili ndio maana tunamuomba Meya
atoe adhabu kwa madiwani hawa,” walisema.
Waliongeza kuwa, licha ya kuundwa kamati hiyo bado Serikali ilitakiwa kuwashirikisha madiwani wa Temeke ili waweze kuzungumza na wananchi wao.
Diwani wa Kata ya Makangalawe, Bw. Victor Mwakasindile, Prof. Tibaijuka anapaswa kuandaa semina maalumu itakayoshirikisha madiwani ili waweze kutoa elimu kwa umma juu ya mradi huo
ili kuepukana vurugu kama zilizotokea mkoani Mtwara.
“Kama mradi utahusisha maeneo ambayo wananchi wanyamiliki kihalali, madiwani wanapoulizwa watashindwa kutoa majibu hivyo ipo hatari ya kutokea vurugu,” alisema Bw. Mwakasindile.
Posted: 01 Feb 2013 01:56 AM PST

Goodluck Hongo na Rose Itono

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, amesema Serikali haitawachukulia hatua viongozi wa Serikali na Jeshi la Polisi
wanaotuhumiwa kusababisha vurugu zilizotokea mkoani Mtwara, kusababisha vifo na uhalibifu mkubwa wa mali bali jambo la msingini kuhakikisha amani inatawala mkoani humo.
Vurugu hizo zilichangiwa na maandamano ya wananchi waliokuwa wakipinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Bw. Pinda aliyasema hayo katika kipindi cha maswali na majibu bungeni mjini Dodoma jana baada ya kuulizwa swali na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Bw. Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro.
Katika swali lake, Bw. Mbowe alitaka kujua hatua ambazo Serikali itazichukua kwa viongozi wa Serikali na Jeshi la Polisi ambao kauli zao zimechangia vurugu hizo kwa namna moja au nyingine.
Alisema kilichotokea mkoani humo ni matokeo ya mahusiano hafifu kati ya wananchi na Serikali ambapo hata kauli za viongozi wa CCM nazo zilichangia vurugu hizo je, kwanini wasichukuliwe hatua.
Msingi wa swali hilo ulitokana na malalamiko ya wananchi ambao waliitaka Serikali iwaondoe baadhi ya viongozi mkoani humo kwa kupingana na madai yao ya kutokana gesi hiyo isisafirishwe.
Akijibu swali hilo, Bw. Pinda alisema Serikali haiwezi kuwachukulia hatua ili kuepusha lawama hasa ukizingatia
kuwa, tayari kilio cha wananchi kimesikilizwa.
“Nilikwenda Mtwara nikakutana na viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini, Serikali na wananchi ambapo walitoa maoni yao bila kificho na kuitak Serikali iwaondoe baadhi ya viongozi ambao walikuwa kikwazo kutokana na kauli zao,” alisema Bw. Pinda ambaye majibu yake yalionekana 'kuwakuna' wabunge wa CCM.
“Niwaombe Watanzania wenzangu, viongozi na wanasiasa, jambo hili limekwisha hivi sasa tuongee lugha moja ya amani...kwani Tanzania ni moja,” alisema Bw. Pinda.
Alisema kutokana na vurugu hizo, baadhi ya kampuni ambazo zimewekeza mkoani humo zimeingiwa na hofu na nyingine kuomba kukaa miezi mitatu bila kufanya shughuli zao hadi watakaporidhika na hali ya utulivu.
Bw. Pinda alitomia fursa hiyo kutoa pole kwa watu waliofikwa na matatizo ambapo Serikali itaangalia uwezekano wa kuwasaidia.
Posted: 01 Feb 2013 01:55 AM PST
Na Yusuph Mussa, Korogwe

MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali imeleta maafa katika Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, baada ya kuua mwanafunzi mmoja wa sekondari, kujeruhi, kuezua paa za nyumba, mabweni
na madarasa ya Shule ya Sekondari Mkalamo iliyopo Kata ya Magamba-Kwalukonge, Tarafa ya Mombo.
Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Constantine Masawe, alisema tukio hilo limetokea juzi saa 11.45 jioni ambapo wanafunzi waliojeruhiwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya, Magunga.
Majeruhi hao ni Salma Bakari (15), ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Mkalamo aliyevunjika mguu wa kulia, Omar Haji (13) na Catherine Albert wa Shule ya Msingi Magamba- Kwalukonge na Asha Bakari wa Sekondari ya Mkalamo.
Albert aliumia kichwani, Haji (mgongo na mbavu) wakati Bakari  aliumia mguu wa kushoto baada ya kukimbilia katika nyumba ya Bw. Mustapha Abdallah ndipo walipopigwa na miti, mabati, kuangukiwa na ukuta.
Alisema bweni moja la wasichana katika Shule ya Msingi Magamba- Kwalukonge, limeanguka kabisa na jingine likitoa nyufa ambapo madarasa mawili ya Sekondari ya Mkalamo yameezuliwa paa zake.
“Inaaminika bado kuna nyumba nyingine zimeanguka au kuezuliwa paa zake na upepo lakini tutatoa taarifa kadiri muda unavyokwenda,” alisema Kamanda Masawe na kuongeza kuwa, inaaminika nyumba nyingine za wenyeji zimekwenda na upepo kwenye Kijiji cha Magamba Kwalukonge.
Wakati huo huo, mvua hiyo imesababisha kifo cha mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Semkiwa, iliyopo Mtaa wa Mtonga, mjini Korogwe, mkoani Tanga, Patrick Paul (14).
Mwanafunzi huyo amefariki dunia jana katika Hospitali ya Wilaya, Magunga wakati akiendelea kupatiwa matibabu baada ya upepo mkali ulioambana na mvua kumuangusha akiwa juu ya mti.
Mvua hiyo pia imeezua paa katika nyumba tisa zilizopo mitaa ya Mtonga na Kwamkole. Taarifa iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Kata ya Mtonga ambayo Majira inayo nakala yake, Bw. Maurice Kinyashi, ilisema tukio hilo limetokea juzi saa 12 jioni.
Alisema pamoja na mvua hiyo kusababisha kifo cha mtu mmoja, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Semkiwa, Rahim Ramadhani amejeruhiwa baada ya kuangukiwa na paa wakati mtoto wa miaka mitatu, Halifa Shabaan, alifunikwa na paa lakini hakuumia.
“Ukuta wa Kanisa la TAG nao ulianguka, hivi sasa waathirika wote wapo katika wakati mgumu wakiishi katika nyumba ambazo hazina paa,” alisema Bw. Kinyashi.
Posted: 01 Feb 2013 01:53 AM PST
Na Rehema Mohamed

WAKATI Katibu wa Taasisi za Jumuiya za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda na Shekhe Swaleh Mkadam, wakiendelea kusota rumande baada ya kunyimwa dhamana na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), wafuasi wao wamepanga kufanya kongamano maalumu la kujadili namna ya kuwatoa washtakiwa hao.
Shekhe Ponda na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na wizi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam ambapo dhamana zao zimefungwa kwa sababu za kiusalama.
Jana kesi hiyo ililetwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa na baada ya kuahirishwa, wafuasi hao walionekana wakigawana vikatarasi vilivyokuwa na ujumbe wa kufanya kongamano hilo.
Vikaratasi hivyo vilikuwa na ujumbe uliowataka Waislamu wote nchini kukutana Februari 3 mwaka huu, saa 8 mchana eneo la Temeke kwenye kiwanja cha Nurul Yaqiin (Uwanja wa Pumba) karibu na Uwanja wa Mwembeyanga.
Ujumbe huo uliongeza kuwa, kitendo cha washtakiwa hao kuendelea kunyimea dhamana ambayo ni haki yao, kinawafanya waendelee kuteseka kwa sababu ya kutetea mali za Waislamu ambazo
zinaendelea kuuzwa na kupolwa.
Pia ujumbe huo uliwataka Waislam wajumuike pamoja, kuonesha mshikamano wao na kutoa maamuzi ya pamoja juu ya nini cha kufanya ili haki itendeke kwani Muislamu wa kweli hawezi kukubali dhuruma yoyote dhidi yake.
Wakati huo huo, akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo, shahidi wa sita Bw. Hamis Mkangama (30), aliieleza mahakama hiyo kuwa Shekhe Ponda aliwakataza wasiendelee na ujenzi wa uzio katika kiwanja kinachodaiwa kuvamiwa.
Bw. Mkangama ambaye ni fundi mwashi, alisema yeye na wenzie 20 walikuwa wakichimba msingi wa uzio kwenye kiwanja cha Markaz ambapo Shekhe Ponda na wenzake, walikwenda eneo hilo na kuwahoji aliyewapa idhini ya kujenga eneo hilo.
“Tulimjibu kuwa bosi wetu Selemani ndiye aliyeturuhusu kujenga na kututaka tusitishe ujenzi akidai kiwanja husika kina mgogoro,” alidai shahidi huyo.
Aliongeza kuwa, pamoja na kuambiwa wasimamishe ujenzi wao waliendelea ndipo Shekhe Ponda, aliamua kupiga picha eneo hilo.
Alidai kuwa, walimweleza bosi wao juu ya suala la Shekhe Ponda ambaye aliwataka wasitishe ujenzi huo na kudai kuna matatizo yameanza kujitokeza.
Wakati Shekhe Ponda akiondoka katika viwanja vya mahakama hiyo akiwa ndani ya gari la Magereza, wafuasi wake walimuaga kwa kunyoosha mikono wakisema 'Takbirr -alahu akbar', wengine
wakilikimbiza gari hilo hadi barabarani.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 14 mwaka huu kwa
ajili ya kutajwa na Februari 18 kwa ajili ya kusikilizwa.
Posted: 01 Feb 2013 01:52 AM PST

Na John Mnyika

SIJARIDHISHA na taarifa ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na uamuzi wa Spika Anna Makinda bungeni jana kuhusu mgogoro wa gesi Mtwara, hatua ambazo zinadhihirisha kwamba nchi imefika hali hiyo kutokana na udhaifu wa Serikali na ombwe la kiuongozi na kiusimamizi ikiwemo wa kibunge.
Taarifa aliyoyatoa Waziri Mkuu jana imejibu baadhi tu ya madai ya wananchi, lakini pia imefafanua sehemu ndogo ya masuala ambayo niliyahoji bungeni Julai 27, 2012 lakini Serikali ikakwepa kutoa ufafanuzi.
Taarifa hiyo itawezesha kutuliza mgogoro kwa muda, lakini haijengi msingi wa ufumbuzi endelevu.
Sikubaliani na uamuzi wa Spika wa kubadili uamuzi wake wa awali alioutangaza wa kuunda kamati kufuatia maelezo ya Waziri Mkuu yasiyokuwa na vielelezo vyovyote kwa kuwa kufanya hivyo ni kulinyima bunge fursa ya kuisimamia Serikali ambayo ndio chanzo cha migogoro kuhusu gesi asili.
Spika alipaswa ikiwa amebadili uamuzi wa kuunda kamati ya kwenda Mtwara aunde Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ili ipitie vielelezo kubaini usahihi wa maelezo hayo ya Waziri Mkuu bungeni katika hali ya sasa ambayo nchi ina ombwe la kutokuwa na usimamizi wa kibunge kwenye sekta hizo nyeti kufuatia hatua yake ya kuvunja kamati iliyokuwepo bila kuunda kamati mbadala mpaka sasa.
Ikiwa hana nia ya kuunda kamati ya nishati na madini mpaka mwisho wa mkutano huu wa Bunge, basi anapaswa kurejea barua zangu nilizomwandikia na kutumia madaraka na mamlaka yake kuelekeza kamati nyingine ya Bunge kati ya kamati zilizopo hivi sasa iweze kukutana kwa haraka kuchukua hatua zinazostahili na kuwasilisha taarifa bungeni.
Kwa upande wangu, nafuatilia kumbukumbu rasmi za Bunge (Hansard) kupata nakala kamili ya ufafanuzi huo na nitaeleza hatua za ziada ambazo nitazichukua kama mbunge na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini.
Kwa ujumla, maelezo hayo hayana tofauti kubwa na yaliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Januari 2013, hivyo sikubaliani na Waziri Mkuu kueleza kuwa suala hilo limekwisha kwa maelezo matupu yasiyokuwa na vielelezo.
Maelezo hayo ya Waziri Mkuu yamedhihirisha kwamba iwapo Wizara ya Nishati na Madini ingetoa majibu bungeni kama nilivyohoji Julai 27, 2012, maandamano na migogoro iliyosababisha vifo na uharibifu wa mali Desemba 2012 na Januari 2013 yasingetokea hivyo ni muhimu waliosababisha hali hiyo wawajibishwe.
Maelezo hayo hayajaeleza hali halisi kuhusu kasoro katika ujenzi wa miundombinu ya gesi katika mradi unaoendelea hivi sasa kuhusu mitambo ya kusafisha gesi Madimba, ujenzi wa bomba kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam na mpango wa uzalishaji wa umeme mkoani Mtwara, na hivyo hatua zisipochukuliwa hivi sasa kurekebisha hali hiyo mgogoro utazimwa kwa muda mfupi lakini utaibuka mgogoro mkubwa zaidi baadaye.
Aidha, Waziri Mkuu hajatoa maelezo kamili kuhusu mipango ya matumizi ya gesi asili katika eneo la viwanda Bagamoyo na pia ujenzi wa Bandari ya Mbegani Bagamoyo, na mahusiano ya mipango hiyo na ile ya Mtwara na Dar es Salaam kuhusu matumizi ya gesi asili na bandari.
Ni muhimu maelezo ya ukweli, uwazi na ukamilifu yakatolewa. Katika muktadha huo, Bunge kwa niaba ya wananchi linapaswa kutokuridhika tu na maelezo ya Waziri Mkuu kwamba suala hili limemalizika, bali lipewe nafasi ya kutimiza wajibu wake wa kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 63 wa kuisimamia Serikali.
Spika wa Bunge atumie mamlaka yake kuelekeza Kamati mojawapo ya kudumu ya Bunge kushughulikia suala la gesi asili kama nilivyoomba katika barua zangu kwake za  Oktoba 2012 na Januari 2013 ambazo mpaka sasa hazijapatiwa majibu. Kamati hiyo ipitie maelezo hayo ya Waziri Mkuu na kuitaka Serikali kuwasilisha vielelezo ikiwemo mikataba ili kurekebisha kasoro zilizopo katika mipango na mfumo wa utekelezaji wa miradi ya utafutaji, uvunaji, usafirishaji, uendelezaji na utumiaji wa gesi asili.
Mwandishi ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Posted: 01 Feb 2013 01:46 AM PST

JANA Mbunge wa kuteuliwa kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, aliwasilisha hoja binafsi bungeni mjini Dodoma iliyoainisha suala zima la udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini.
Katika hoja hiyo, Bw. Mbatia alisema kukosekana kwa mitaala katika shule za msingi na sekondari, kunachangia wanafunzi kufanya vibaya. Alisema hali hiyo inachangiwa na utendaji mbovu wa kitengo cha kuandaa mitaala hiyo ambacho kimeshindwa kufanya kazi zake ipasavyo na kusababisha usambazaji vitabu kunuka rushwa.
Hoja hiyo iliibua mvutano mkali kwa wabunge ambao baadhi yao walishauri iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchukuza udhaifu huo na wengine wakitaka hoja hiyo ifanyiwe kazi na Serikali.
Ulimwengu mzima unatambua kuwa, hakuna nchi iliyowahi kuendelea bila wananchi wake kuwa na elimu bora. Kwa maana hiyo, maendeleo yote yametokana na elimu sahihi iliyojaa maarifa, ubunifu, uwezo mkubwa wa kufikiri na kuvumbua dhana mpya.
Elimu inayojenga ujuzi na ufundi wa aina mbalimbali, kudadisi, kujiamini na kutumia fursa zilizopo kutafuta masuluhisho ya matatizo ndiyo inayoleta maendeleo kwenye jamii.
Ni ukweli usiopingika kuwa, wafadhili wametoa pesa nyingi kusaidia nchi masikini ikiwemo Tanzania lakini umaskini bado unaendelea kuitafuna nchi yetu. Suala la kuwekeza katika elimu sahihi kwa kuwa na mitaala bora haliepukiki.
Hivi sasa, nchi mbalimbali zilizoendelea zinatafuta maarifa mapya ya kuibadili dunia wapendavyo kwa kurahisisha kila kitu wakitumia teknolojia na uvumbuzi mpya. Hii ndio nguvu ya elimu! Na hii inazaa changamoto nyingi katika sekta ya elimu, kama vile-
Sisi tunasema kwamba, mitaala tunayoitumia katika shule zetu haiwezi kumjenga mwanafunzi kupata maarifa, ujuzi na stadi  za aina mbalimabali zitakazowasaidia wanafunzi kuishi pindi wamalizapo shule.
Mitaala tuliyonayo haiwafundishi wanafunzi wetu na kuwapa uwezo wa kutatua matatizo yao au kupambana na changamoto zinazoikabili kwenye jamii. Mitaala yetu imetungwa na wataalamu wachache bila kuzingatia mahitaji wa jamii.
Hali hiyo inachangia wanafunzi wetu kukata tamaa na kuwa tegemezi wamalizapo shule na kibaya zaidi, ziara za mafunzo na kazi za nje zinazokazia maarifa hazifuatiliwi kabisa.
Mbinu za ufundishaji, haziwaelekezi wanafunzi kuwa na ari ya kujifunza, bali zinakaririsha tu. Walimu wengi wanatumia mfumo wa kuandika ubaoni na wanafunzi wananakili maelezo.
Mfumo huu unajulikana kama “ubao-chaki” ambao unawafanya wanafunzi kuwa vikapu vya kupokea maelezo ya mwalimu.
Katika karne hii ya maarifa na changamoto nyingi, mfumo huu haufai. Mbinu shirikishi zinazowapa muda na fursa wanafunzi kujadili wenyewe na kutoa mawazo yao kwa uwazi ndio sahihi.
Mbinu hizo zinaamsha ari ya wanafunzi kujifunza, kudadisi, ubunifu na fikra yakinifu za kukuza uhodari wa kutafuta maarifa hata kama hawapo shule.
Umefika wakti wa Serikali kuweka mikakati ya kifikra ya kuzifanya shule kuwa mahali salama pa kujifunza na kuibua vipaji vya watoto ambapo pengo hili bado halijafanyiwa juhudi za dhati ili kuzibwa.
Hivi sasa mtoto wa masikini anayelilia elimu imkomboe, anahitaji mfumo mzuri ambao utampa dira na dhamira ya kweli ili kuifanya elimu kuwa ni haki ya msingi kwa kila mtoto badala ya watoto wa viongozi pekee.
Posted: 01 Feb 2013 01:45 AM PST
Na Heri Shaaban
WILAYA Ilala imetoa taarifa ya Serikali ya awamu ya nne ya vitu walivyotekeleza kwa kipindi cha miaka saba,ikiwemo  miradi waliosimamia.Baadhi ya  mafanikio  hayo  kuongeza vituo vya afya,ujenzi wa daraja la Vingugunti,kujenga shule za sekondari 91 kwa kipindi cha miaka saba kuanzia  mwaka 2005 hadi 2013.
Hayo yalisemwa na Dar es Salaam jana, Mkuu wa Wilaya hiyo Raimond Mushi wakati wa kutoa taarifa ya Serikali ya awamu ya nne kwa kipindi cha miaka hiyo.Mushi alisema kuwa kati ya shule hizo 91 za sekondari zilizojengwa ambazo zinamilikiwa  na serikali 49 shule zisizo za seriklai 42 kufanya jumla 91."Shule za sekondari awali zilikuwa 11 zikaongezwa 80,shule kongwe Pugu, Azania,Tambaza juhudi zilifanyiwa ukarabati ya majengo ya mahabara na vyoo na kuzirudisha katika hadhi yake ya awali."alisema Mushi.
Pia alisema kuwa katika kipindi hicho wamefanikiwa kujenga nyumba za walimu 18 kutoka 52 na kufikia 70 mwaka 2012,Na madawati 9,330 yameongezeka kutoka 14,812 mwaka 2015 na kufikia 24,142  mwaka 2012. Alisema kuwa katika kipindi hicho pia katika sekta ya afya wamefanikiwa kujenga vituo saba kutoka 15 vya awali na kufikia 22 mwaka 2012 kati ya vituo hivyo vilivyojengwa ni Guluka Kwalala,Bonyokwa,Segerea,Zingiziwa ,Kivule,Gongo lamboto,na Kiwalani.
 Aidha alisema kuwa idadi ya zahanati zimeongezeka kutoka 13 mwaka 2005 na kufikia 20 na na kituo cha afya Mnazi Mmoja kimekarabatiwa,na kupata hadhi ya hospitali ambapo inatoa huduma za mama na mtoto (MHC)na upasuaji pia.
Kwa upande wa hospitali ya wilaya Amana imeongezewa wodi ya wazazi na kuwezesha kulaza wazazi kutoka 30 mwaka 2005 hadi 120 mwaka 2012,ujenzi wa jengo la mapokezi (OPD) ujenzi wa mahabara ya wilaya na jengo la mazoezi kwa wagojwa na mifupa.
Posted: 01 Feb 2013 01:44 AM PST
Na Mwali Ibrahim

BONDIA Japhet Kaseba, ameapa kuwaonesha Watanzania kilichomfanya bondia, Francis Cheka kumkimbia ulingoni katika pambano lake na Ramadhani Maneno.Pambano hilo linatarajia kufanyika Machi 2, mwaka huu kuwania ubingwa wa Taifa katika Ukumbi wa DDC Kondoa huku likishuhudiwa na Mbunge wa Kinondoni Idd Azan.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Japhet Kaseba alisema ameanza kujifua kwa ajili ya pambano hilo, ambapo anataka kuwaonesha Watanzania uwezo wake unaowatisha mabondia wengine na kumfanya wamkimbie, akimtolea mfano Cheka.
"Najua watu wanatamani kuona mpambano huu, ambapo kwa muda mrefu sijapanda ulingoni kutokana na kukosa mabondia wakupigana nao, kwani wamekuwa wakikwepa kupigana na mimi sasa basi pambano hili litadhihirisha hayo," alisema.Aliongeza kuwa anajifua katika gym yake iliyopo Mwananyamala, ambapo ana imani kwa kuanaza maandalizi mapema kutamsaidia kujiweka vizuri zaidi kwa mpambano huo.
Alisema zaidi anamtaka mpinzani wake ajiandae, ili ushindi huo kwani ana imani atauchukua.
Posted: 01 Feb 2013 01:43 AM PST

Bondia Selemani Kidunda wa Klabu ya Ngome, ambaye aliowakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic yaliyofanyika London nchini Uingereza mwaka jana akipima uzito, Dar es salaam kwa ajili ya mashindano ya Klabu bingwa yaliyoanza juzi katika Uwanja wa ndani wa Taifa, Dar es Salaam. Picha na Rajabu Mhamila Bondia Selemani Kidunda wa Klabu ya Ngome, ambaye aliowakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic yaliyofanyika London nchini Uingereza mwaka jana akipima uzito, Dar es salaam kwa ajili ya mashindano ya Klabu bingwa yaliyoanza juzi katika Uwanja wa ndani wa Taifa, Dar es Salaam. Picha na Rajabu Mhamila
Posted: 01 Feb 2013 01:38 AM PST
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Zanzibar maarufu zaidi kwa jina la Grand Malt Premier League, unatarajiwa kuanza leo kwa michezo miwili kati ya Mafunzo na KMKM zitakazokwaana Uwanja wa Amaan, huku Chipukizi na Falcon wakioneshana kazi Uwanja wa Gombani, Pemba
KMKM wanaingia uwanjani wakitaka kuendeleza ubabe wao, kwani mpaka sasa ndiyo wanaoongoza ligi hiyo wakiwa wamejikusanyia pointi 23, wakati Mafunzo ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 22.
Ugumu wa mchezo huo ni kuwa kila timu itataka kujiimarisha zaidi kwani kuteleza ni kujiweka katika mazingira magumu ya kutwaa taji na iwapo KMKM, itakubali kichapo, itaichia Mafunzo kushika usukani wa ligi hiyo yenye timu 12.
Chipukizi wao watataka kuutumia vyema uwanja wa nyumbani, kwani ikiwa nafasi ya tano kwa pointi 17 ilizonazo itataka kuhakikisha inashinda, ili kuzidi kupaa katika msimamo wa ligi hiyo ambayo kwa sasa imeongezeka mvuto kutokana na udhamini wa Grand Malt.
Hata hivyo wasitegemee mteremko kutokana na Falcon, nayo kutaka kujinasua kutoka nafasi za chini. Kwa sasa timu hiyo inashikilia nafasi ya tisa ikiwa na pointi 13.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho, kwa michezo miwili wakati Bandari na Malindi zitakapokwaana Uwanja wa Mao, huku Jamhuri na Duma zikioneshana ubabe Uwanja wa Gombani, Pemba na Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Zimamoto na Mtende zitakazocheza Uwanja wa Mao.
Timu inayoshika mkia mpaka sasa ni Mundu ikifuatiwa na Malindi. Timu zote hizi zina pointi saba kila moja.
Posted: 01 Feb 2013 01:37 AM PST

Na Shufaa Lyimo

KLABU ya Azam FC, umesema utaendeleza kipigo katika mchezo wa Ligi Kuu, dhidi ya Mtibwa Sugar.
Azam juzi iliinyuka Toto Africa ya Mwanza mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu mzunguko wa pili, iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jafari Iddi alisema kinachoifanya timu yake ifanye vizuri ni mshikamano uliopo, kati ya wachezaji na viongozi.
"Timu yetu itaendelea kufanya vizuri michezo yote na tunaahidi kuipa kipigo Mtibwa tutakapokutana," alisema.
Hata hivyo alisema ligi ya mwaka huu, ina ushindani mkubwa kwa kuwa kila timu imejipanga kupata ubingwa.
"Ligi hii kwa kweli ni ngumu kwani timu zote zimejiandaa kwa muda mrefu na kila moja, inataka ushindi," alisema.
Aliwataka mashabiki wao kuendelea kuwapa sapoti kila wanapocheza, ili waweze kufanya vyema na kupata matokeo mazuri.
Katika msimamo wa ligi, timu hiyo inakamata nafasi ya pili nyuma ya Yanga, inayoongoza.
Posted: 01 Feb 2013 01:37 AM PST

Na Queen Lema, Meru

WILAYA ya Meru, imetoa sh. milioni 8 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu sita za wilaya hiyo, lengo likiwa kuendeleza vipaji vya michezo ndani ya wilaya hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi wilayani hapa jana Mkuu wa wilaya hiyo, Munasa Nyirembe alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa kuna umuhimu wa wilaya yake kuhakikisha inaendeleza vipaji.
Munasa alisema fedha hizo zilitolewa na wilaya hiyo kwa kuwa imegundulika wachezaji wengi, hasa wa soka ambao wana vipaji lakini tatizo linaonekana ukosekanaji wa vifaa vya michezo.
Alisema fedha hizo zitaweza kunufaisha timu sita za wilaya hiyo, ambapo timu zao zitaweza kushiriki mashindano ya Kombe la CCM Wilaya ya Meru, ambayo yameanza na yanatarajiwa kumalizika Februari 5, mwaka huu.
“Tunaona Meru ni moja ya wilaya ambazo zina vipaji vingi, lakini kitu kimoja ni kuwa bado wachezaji wetu wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa, tumeona kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha tunawapa watu hawa fursa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi," alisema Munasa.
Pia alisema mbali na kuwapa vifaa vya hivyo timu sita za wilaya hiyo, lakini pia wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha wanapanga, ili kuandaa mechi za kirafiki ambazo zitasaidia kuibua vipaji zaidi.
Naye Ofisa Utamaduni wilaya hiyo, Senyaeli Palangyo alisema wamejipanga kuendelea zaidi katika michezo mbalimbali kwa kuwa vipaji vingi, vinaweza kuendelezwa ingawa awali hapakuwa na hamasa za kutosha.
Posted: 01 Feb 2013 01:36 AM PST
Waziri wa Fedha,Dkt Wiliam Mgimwa (kulia) akimkabidhi jezi na mpira,nahodha wa timu ya soka ya Vijana ya Kijiji cha Itagutwa,Sufian Mfilinge ikiwa ni juhudi za kuwahamasisha kuendeleza michezo.Picha na Eliassa Ally
Posted: 01 Feb 2013 01:29 AM PST
Na Elizabeth Mayemba

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars) inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini kesho kutwa kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimatifa, dhidi ya Cameroon 'Indomitable Lions'.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kim alisema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi, kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco, itakayofanyika Machi mwaka huu.
"Itakuwa mechi ngumu na kipimo kizuri kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi, kabla ya mechi na Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonesha wako tayari.
"Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015 kwa hiyo, mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko," alisema Kim.
Kocha huyo amerejea nchini juzi akitokea Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast, zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Taifa Stars itacheza na Morocco Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast, inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.
Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam), mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Said 'Cholo' (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).
Wengine ni viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakari (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba).
Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Posted: 01 Feb 2013 01:28 AM PST

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ambayo ilikutana Januari 30 mwaka huu imetupa pingamizi zote, zilizowekwa kwa wagombea wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hicho.
Kamati hiyo ilijadili pingamizi zilizowekwa, dhidi ya waombaji uongozi wa TFF na Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPL Board).
Wagombea waliowekewa pingamizi hizo ni Jamal Malinzi na Athuman Nyamlani wanaowania nafasi ya Rais, Michael Wambura (Makamu wa Rais), Yusuf Manji (Mwenyekiti TPL) na Said Mohamed (Makamu Mwenyekiti TPL).
Wengine waliowekewa pingamizi hizo, ambao wanawania nafasi za Ujumbe wa TFF ni Hamad Juma, Ephra Swai, Vedasus Lufano, Eliud Mvela na Athuman Kambi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura kwa niaba ya Katibu Mkuu wa chama hicho Angetile Osiah, ilieleza kwamba pingamizi za Malinzi na Nyamlani zimetupwa kwa kuwa walioweka pingamizi hizo, hawakutokea kutoa utetezi wao.
"Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF, Ibara ya 11(4) katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Januari 2013, ilijadili pingamizi zilizowekwa dhidi ya waombaji uongozi wa TFF na TPL Board na kutoa maamuzi," ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilieleza kwamba Malinzi aliwekewa pingamizi na Agape Fue, huku Nyamlani akipingwa na Mintanga Chacha.
Ilieleza kwamba pingamizi la Wambura, limetupwa kwa kuwa mpingaji mmoja Josea Msengi, hakutokea kutetea pingamizi lake wakati pingamizi alilowekewa na Said Rubeya, halikukidhi matakwa ya kanuni za uchaguzi.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa pingamizi aliyowekewa, Manji na Daniel Kamna na Juma Magoma yametupwa kwa kuwa nayo hayakukidhi matakwa ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment