TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, July 12, 2013

DARAJA LA KIGAMBONI LAFANYIWA UKAGUZI


Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) Dar es Salam jana kuhusu taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha tano katika shule za sekondari za Serikali na vyuo vya ufundi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi, Zuberi Samataba.
Mafundi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni linalojengwa na Kampuni za China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd na China Major Bridge Engineering Company wakipita na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli(hayupo pichani) baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo Dar es Salaam juzi.

Na Zourha Malisa
MSANII anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' ni miongoni mwa wanawake waliotajwa kunaswa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, ambapo msanii mwingine aliyekamatwa ametambulika kwa jina la Melisa Edward.
Inadaiwa wasanii hao kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam , Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzoa alithibitisha kukamatwa kwa wasanii hao nchini huko ambapo aliwataja kuwa ni Agnes Masogange pamoja na Melisa.
Alisema wasanii hao walikamatwa Julai 5, mwaka huu nchini humo na bado wanashikiliwa na jeshi la polisi la nchi hiyo kwa ajili ya uchunguzi.
"Hadi sasa taarifa rasmi bado hazijafika hivyo, hatujajua ni aina gani ya adhabu wanaotumikia tunasubiri taarifa rasmi kutoka huko," alisema Nzoa.
Alisema Jeshi la Polisi nchini kwa upande wake, linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu, ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
Habari zilienea katika mitandao ya kijamii Jumapili iliyopita za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine, zenye thamani sh. bilioni sita nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Taarifa hizo zilionesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, uliopo eneo la Kempton Park Ijumaa iliyopita wakitokea Tanzania.
Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takriban kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama 'Tik' zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.
Wasanii 'Bongo' wanaswa na dawa za kulevya A. Kusini

No comments:

Post a Comment