TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, July 11, 2013

MV KIGAMBONI HAPATOSHI FELI DAR ES SALAAM ASUBUHI NA JIONI

 Taifa linaitaji vijana wenye vipaji ili kutuwezesha kujikomboa na janga la kuishia kuwa wasindikizaji katika mashindano ya kimataifa, pichani watoto wakiwa katika moja ya mazoezi ya awali ili kufikia malengo ya kuitwa timu ya Taifa kama walivyokutwa hivi karibuni na mpiga picha wetu Kibaha Dar es Salaam..
 Watumishi wa Kanisa la Kristo, wanafunzi wa masomo ya Kwaya ya jumapili, wakiwa katika maandalizi ya kujiweka sawa kwa ajili ya kutumika wakati wa sala ya jumapili kanisa katoliki, kama walivyokutwa na Mpiga picha wetu Kibamba Dar es Salaam juzi.
 Wachezaji wa Timu ya Vijana wa eneo la Kibamba wakijiweka sawa kujiwinda na michezo ya kirafiki katika uwanja wa kibamba Hospitali.
 Mjasilia mali Mkazi wa Mbezi akiwa katika heka heka za kuhakikisha Mzigo unafika mahala pake, kutokana na kukosekana soko la Ajira Vijana wengi wameendelea kujiajiri kama alivyokutwa kijana huyu ambaye hakufahamika jina lake Kimara Dar es Salaam.
 Wakazi wa Eneo la Kigamboni wanaendelea kuwa watumwa wa Usafiri wa kuvuka Kigamboni, hadi hapo Daraja litakapokuwa limekamilika, hali hii ya msongamano wa abiria imekuwa ni tatizo linalosababisha msongamano mkubwa majira ya asubuhi na jioni kama walivyokutwa ikiwa majira ya jioni.
Wakati wa Kufungua shule Wanafunzi wa jiji la Dar es Salaam umewadia, kama wanavyoonekana watoto hawa wakiwa katika mwelekeo wa kwenda shule katika kijiji cha Kibamba Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment