TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, October 23, 2014

INDA AZINDUA TOLEO LA JARIDA LA FIRST LINALOINADI TANZANIA

PG4A6350 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Mwenyekiti na Muasisi wa Kampuni ya Invest Africa ya Uingereza, Bw. Robert Hersov kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Savoy,London Oktoba 20, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A6406Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama Jarida la  First baada ya kukabidhiwa nakala  ya toleo la  jaridai hilo na Muasisi wake, Rupert Goodman  (kulia) kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza uliopo London , Oktoba 21, 2014. Jarida  hilo limesheheni  makala zenye kuinadi Tanzania na vivutio vyake nje ya nchi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A6421Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza wakati alipozindua toleo la  Jarida la First lenye makala mbalimbali za kuinadi Tanzania na Vivutio vyake nje ya nchi katika hafla iliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Oktoba 22, 2014. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe  na kulia ni Mwanzilishi wa jarida hilo, Rupert Goodman. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A6487 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya watanzania wanaosoma nchini Uingereza kwenye ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo London Oktoba 21, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A6499Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya watanzania wanaosoma nchini Uingereza kwenye ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo London Oktoba 21, 2014.Watatu kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
===================================================================

Waajiriwa wapya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo watakiwa kuwa waadilifu

1 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiongea kwa msisitizo kuhusu maadili ya Utumishi wa Umma wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa Wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam.
2Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasirimali Watu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Barnabas Ndunguru akifafanua jambo wakati wa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa Wizara hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa mikutano uliopo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
4Mwajiriwa mpya katika kada ya Afisa Habari akichangia mada wakati wa semina elekezi ya waajiriwa wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
5aBaadhi ya Waajiriwa wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatilia mada wakati wa mafunzo elekezi kwa ajili ya kuwajengea uwezo kujua taratibu za Kiutumishi wa Umma semina iliyofanyika leo jijini5b Baadhi ya Waajiriwa wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatilia mada wakati wa mafunzo elekezi kwa ajili ya kuwajengea uwezo kujua taratibu za Kiutumishi wa Umma semina iliyofanyika leo jijini6Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waajiriwa wapya na baadhi ya viongozi wa wizara hiyo mara baada ya kufungua mafunzo kwa watumishi wapya leo jijini Dar es Salaam.

APIGWA FIMBO NA KUTEKETEZWA KWA MOTO MKOANI KATAVI

index 
Na Kibada Kibada-Katavi
Siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya mauaji Mkoani Katavi vitendo vinavyoashiria kuwepo ukiukwaji wa sheria na kujichukulia sheria mkono kinyume na taratibu za sheria. Matukio hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara Mkoani Katavi,mwishoni mwa wiki Mkazi wa kijiji Nsemlwa Mathias Kameme (35)mkulima aliuwawa kwa kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha mwili wake kuchomwa moto na kuteketea kabisa. Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Kamishina Msaidizi wa Polisi Dhahiri Kidavashari anaeleza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa wananchi wasiojulikana waliamua kujichukulia sheria mikononi kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe. Kamanda Kidavashari alieleza kuwa tukio hilo lilitokea mnamo oktoba 17 majira ya saa mbili usiku kitongoji cha malebwe kijiji cha mnyamasi Kata ya Ugalla Halamsahuri ya Nsimbo Wilayani Mlele. Akaeleza kuwa siku ya oktoba 16 mwaka huu majira ya mchana marehemu aliondoka nyumbani kwake na kuelekea na kuelekea kusikojulikana na alirejea oktoba 17 majira ya saamoja mke wake aitwaye Fotonatha Raphael miaka (26)mkazi wa Nsemlwa alimuuliza marehemu unatoka wapi muda huo .marehemu alijibu kuwa yeye ni mwanamke hapaswi kumuhoji. Ilipofika majira ya saa mbili usiku wakiwa ndani wamelala walisikia vishindo vya watu wengi wakiizunguka nyumba huku wakisema MATHIAS toka nje na alipotoka nje walianza kmsahambulia huku wakimuuliza nyama ya ng’ombe aliyoiba na kuchinja ipo wapi?. Kamanda akaeleza kuwa ndipo marehemu alimuelekeza mke wake ilipo na aliifuata nyama hiyo nyuma ya nyumba na alipoileta ndipo watu hao wasiofahamika walikotoka waliendelea kumshambulia hadi kufa na kisha mwili wake kuuchoma moto na kutokomea kusikojulikana. Hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini na kuwatia nguvuni wale wote waliohusika katika mauaji hayo kisha kuwafikisha mbele ya mahakamani ili kujibu tuhuma hizo na sheria ichukue mkondo. Katika tukio jingine huko wilayani mpanda Kijiji cha Mpandandogo Tarafa ya Kabungu mtoto mwenye umri wa miaka mitano jina linahifadhiwa alinajisiwa na mtu anayejulikana kwa jina la Rashidi Mbogo (62) na kumsababishia maumivu makali, mtuhumiwa huyo yuko chini ya ulinzi wa polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma hizo. Katika hatua nyingine Kamanda Kidavashari ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkono na badala yake wajenge tabia ya kutoa taarifa za matukio katika mamlaka husika za kisheria ziweze kuchukua nafasi yake.Akashukuru wananchi wanaoendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mapambano dhidi ya uharifu kwa kuwataka waendelee na moyo huo huo ili Mkoa uwendele kuwa salama na Taifa kwa ujumla.
===============================================================

MILIONI 16/- ZATOLEWA NA CIP TRUST UJENZI WA MADARASA

IMG-20141017-WA0009Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi, (mwenye mgorore wa bluu) akishiriki kutoa burudani na kikundi cha uhamasishaji cha kijiji cha Kinyamwenda kwenye sherehe ya kukabidhi vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu wa shule ya kijiji hicho.
Na Nathaniel Limu, Singida
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Community Initiatives Promotion Trust Fund (CIP Trust), limetumia zaidi ya shilingi 16 milioni, kugharamia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu, katika shule ya msingi Kinyamwenda kata ya Itaja.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa shirika la CIP Trust,Affesso Ogenga,wakati akitoa taarifa ya ujenzi huo kwenye hafla ya kukabidhi vyumba hivyo na ofisi ya walimu ambayo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi.
Alisema fedha hizo zimetolewa na serikali ya Austria kupitia asasi ya Sister Cities Singida Salzurg (SCSS).
Ogenga alisema asasi yao iliombwa na uongozi wa shule ya msingi Kinyamwenda kusaaidia kukamilisha mradi huo ambao tayari wananchi waliisha changia nguvu kazi.
IMG-20141017-WA0012 
Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,akiwa amevikwa nguo na kukabidhiwa zana za ushujaa na wananchi wa kijiji cha Kinyamwenda,kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mchapa kazi wa kupigiwa mfano katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
“Tunatarajia kwamba baada ya uzinduzi wa majengo haya, tatizo la msongamano wa wanafunzi darasani,litakuwa limepungua kwa kiasi kikubwa.Pia walimu watakuwa na ofisi nzuri kwa ajili ya kazi zao za kila siku”,alifafanua Ogenga.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika makabidhiano hayo,mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,aliwapongeza wananchi wa kijiji cha Kinyamwenda chini ya mwenyekiti wao na madiwani wa kata ya Itaja kwa kuupokea mradi huo na kuchangia nguvu kazi.
“Nitumie fursa hii kuipongeza asasi ya CIP Trust kwa msaada wao wa kuijengea shule ya msingi Kinyamwenda vyumba viwili vya madarsa na ofisi ya walimu.Hongereni sana kwa kuiunga mkono serikali katika juhudi zake za kuboresha sekta ya elimu”,alisema Mlozi.
IMG-20141017-WA0014 
Aidha,DC huyo aliangiza uongozi wa serikali ya kijiji kumaliza uhaba wa madawati 25 kabla ya januari mwakani.
Dc Mlozi aliendesha harambee kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara ya sekondari ya kata ya Itaja na kufanikiwa kukusanya shilingi 450,000.Fedha hizo zilitumika kununulia mifuko 25 ya saruji.
IMG-20141017-WA0015Vyumba viwili vya madarasa ya shule ya msingi Kinyamwenda wilaya ya Singida.Vyumba hivyo na ofisi moja ya walimu,ujenzi wake umegharamiwa na shirika la Community Initiatives Promotion Trust Fund kwa gharama ya shilingi 16 milioni.(Picha na Nathaniel Limu).
============================================================

South Sudan’s SPLM warring factions ink CCM-brokered framework agreement to address conflict causes

Factions of the ruling party in South Sudan, the Sudan Peoples’ Liberation Movement (SPLM), on Monday 20th October, 2014 signed a framework agreement aimed at addressing root causes of the conflict that erupted in mid-December and plunged the country into violent crisis. 
The signing ceremony, held at the Ngurdoto Mountain Lodge in the outskirts of Arusha, was witnessed by the two principal rival leaders – President Salva Kiir Mayardiit, Chairman of SPLM in government and Mr. Riek Machar Teny, former vice president and leader of the SPLM-in-Opposition, as well as the SPLM faction of former detainee, who also participated in the talks. 
The Chairman of the Tanzania’s  ruling party, Chama Cha Mapinduzi (CCM), President Jakaya Kikwete, CCM Secretary General Mr Abdulrahman Kinana, Tanzania Minister for Foreign and Internationa Relations Mr Bernad Membe, and Former Tanzania Vice President and Prime Minister Mr John Samwel Malecela, who chaired the talks, also witnessed the occasion.
Delegates of the three rival groups of the South Sudanese ruling party met in Arusha from 12th to 18th of this month to try to come up with the framework of the intra-SPLM dialogue which is being facilitated by CCM.
However, it said the process is distinct from the peace talks which take place in Addis Ababa, Ethiopia. 
 “The parties recognize that the Arusha process is essentially an intra-SPLM dialogue and is separate and distinct from the IGAD mediated peace talks among South Sudanese stakeholders. 
“Yet the parties are fully aware that the two processes, although separate, are mutually interdependent and reinforcing,” partly reads a communiqué. 
It further calls for “unity of SPLM as a safeguard against fragmentation of the country along ethnic and regional fault lines.”
 “Initiate measures to stop the war, lead the government and the people of South Sudan towards peace, stability and prosperity,” it further urges. 
Both leaders expressed their commitment to the intra-party dialogue that would reunite the divided historical party. 
The document was signed by senior officials of the rival factions, namely Daniel Awet Akot, Peter Adwok Nyaba and Pagan Amum Okech, representing SPLM in government, SPLM-in-Opposition and SPLM former detainees, respectively. 
The governance crisis within the SPLM gave birth to the 15 December violence which has unfortunately plunged the country into the current national crisis or civil war. 
The intra-party dialogue provides a supplement to the peace talks in Addis Ababa to try and address the root causes of this conflict within the ruling party. 
The framework agreement has also recognized the need to “revitalize, reorganize, strengthen and restore the SPLM to its vision, principles, political direction and core values.
Analysts say the dialogue, could provide an avenue for progress on key issues, including deep divisions between South Sudanese party leaders, if respected.
CCM Chairman President Jakaya Mrisho Kikwete walks to the conference hall with the two principal rival leaders – President Salva Kiir Mayardiit, Chairman of SPLM in government and Mr. Riek Machar Teny, former vice president and leader of the SPLM-in-Opposition, ready for the Monday 20th October, 2014 ready for the signing ceremony of the framework agreement aimed at addressing root causes of the South Sudan conflict that erupted in mid-December and plunged the country into violent crisis. 
CCM Chairman President Jakaya Mrisho Kikwete leads  to the high table  the two principal rival leaders – President Salva Kiir Mayardiit, Chairman of SPLM in government and Mr. Riek Machar Teny former vice president and leader of the SPLM-in-Opposition
CCM Chairman President Jakaya Mrisho Kikwete and CCM Secretary General Abdulrahman Kinana at  the high table  with  President Salva Kiir Mayardiit, Chairman of SPLM in government and Mr. Riek Machar Teny 
Mr Pagan Amum Okech, representing SPLM in government, makes his opening remarks
Part of the conference hall during the ceremony
Malecela, who chaired the talks, is introduced
A relaxed atmosphere as the CCM Chairman President Jakaya Mrisho Kikwete and CCM Secretary General Abdulrahman Kinana engage in pep talks before the start of the proceedings at  the high table  with  President Salva Kiir Mayardiit, Chairman of SPLM in government and Mr. Riek Machar Teny as Former Tanzania Vice President and Prime Minister Mr John Samwel Malecela, who chaired the talks
A relaxed atmosphere as the CCM Chairman President Jakaya Mrisho Kikwete and CCM Secretary General Abdulrahman Kinana engage in pep talks at  the high table  with  President Salva Kiir Mayardiit, Chairman of SPLM in government and Mr. Riek Machar Teny as Former Tanzania Vice President and Prime Minister Mr John Samwel Malecela, who chaired the talks
Mr. Pagan Amum Okiech of  the SPLM-in-Opposition makes his remarks
Mr. Pagan Amum Okiech of  the SPLM-in-Opposition makes his remarks
Mr Daniel Awek Okot of the SPLM-in-Government delivers his statements
Tanzania Minister for Foreign and Internationa Relations Mr Bernad Membe steers the meeting
CCM Secretary General Mr Abdulrahman Kinana makes his statements
CCM Secretary General Mr Abdulrahman Kinana addresses the delegates
CCM Secretary General Mr Abdulrahman Kinana speaks on
STATE HOUSE PHOTOS.
====================================================

NI SHIDAAAA: WAKIMBIZI WAGONJWA KUTOKA CONGO DRC WATELEKEZWA DAR ES SALAAM,WAKOSA CHAKULA WAANZA KUNYONYOKA NYWELE, SHIME WATANZANIA TUJITOKEZE KUWASAIDIA

Mgonjwa, Mwalihoba Nyasa, anaye sumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya titi, sasa ameanza kunyonyoka nywele zake kwa madai ya kukokosa chakula kutokana na kutumia dawa kali lakini hapati chakula.
Mtoto Josephiner Obeid aliyepooza miguu ni miongoni mwa wagonjwa hao wanaoteseka katika nyumba ya kulala wageni ya Bosco iliyopo Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam kwa kukosa chakula kwa madai ya kutelekezwa na Taasisi ya Redeso.
Mtoto Maulid Yunus anayesumbuliwa na ugonjwa wa kukatika vidole na vidonda miguuni ni miongoni mwa wagonjwa walio katika adha hiyo ya kukosa chakula. 
Mtoto Lucy Angela ambaye anajisaidia kwa kutumia mpira baada ya kutobolewa tumboni naye ni miongoni mwa wagonjwa hao wanaoteseka katika nyumba hiyo ya wageni kwa kukosa chakula ‘hakika ukikutana na ndugu zetu hawa unaweza kutokwa na machozi kwani inauma na kutia uchungu’
Mama huyu naye yupo katika mateso hayo, hakika inaumiza.
Watoto hawa nao hawajui cha kufanya wapo katika mateso.
Dada huyu ambaye ni mgonjwa hana la kufanya zaidi ya kumuachia mungu.
Ndugu zetu hawa ambao ni  wakimbizi kutoka Jamhuri ya Watu wa Congo (DRC), ambao ni wagonjwa ambao wanadai wametelekezwa na Taasisi ya Msaada wa Maendeleo ya Jamii (Rudeso), yenye makao yake Kinondoni, wakiwa nje ya nyumba ya kulala wageni ya Bosco iliyopo Ilala Mchikichini Dar es Salaam leo. Inadaiwa kuna zaidi ya wakimbizi 100 waliopo jijini wanaishi katika mazingira ya shida baada ya kutelekezwa na taasisi hiyo.
…………………………………………………………………………………..
Dotto Mwaibale
WAKIMBIZI zaidi ya 100 wanaokabiliwa na magonjwa mbalimbali, wametelekezwa na Taasisi ya Msaada na Mandeleo ya Jamii (Redeso) ambayo ni wakala wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), baadhi yao wameanza kunyonyoka nywele kutokana na kukosa chakula, kwa muda wiki moja sasa.
Mtandao wa www. habari za jamii.com leo ulifanikiwa kuwatembelea wakimbizi hao ambao wapo katika Hotel mbalimbali zilizopo Ilala na Kinondoni katika nyumba za wageni Eritex na Bosco ambapo wamehifadhiwa hapo wametokea Kambi ya Nyarugusu Mkoani Kigoma kwa lengo la kupatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Wakiongea kwa nyakati tofauti na mtandao huo wakimbizi hao ambao ni wagonjwa walisema wamekuwa wanateseka kwa muda sasa jambo ambalo wanaliona kuwa linahatarisha maisha yao.
Walisema pamoja na kutoa taarifa kwa wahusika ambao ni Redeso hadi sasa hawajapatiwa msaada wowote hivyo kujikuta wakinywa dawa bila kula chakula hali ambayo inawaletea madhara.
Mgonjwa, Mwalihoba Nyasa, anaye sumbuliwa na ugonjwa wa kansa titi alisema ameanza kunyonyoka nywele zake kwa madai ya kukokosa chakula kutokana na kutumia dawa kali.
“Hii si afya yangu na sikuwa hivi siwezi kubeba chochote na afya yangu imeendelea kuteteleka na nywele zangu zimeanza kunyonyoka kutokana na kukosa chakula” alisema Nyasa.
Mmoja wa wakimbizi hao alisema baadhi yao wanamagonjwa ya kansa, kupoza, ukoma na magonjwa mengine ambayo ni hatari iwapo hakutakuwa na utaratibu mzuri wa kuwapatia chakula ili dawa ziweze kufanya kazi.
Baadhi ya wakimbizi hao ambao ni wagonjwa ni Sango Nyasa (36), Josephiner Obeid (15), Kashindi Alfan (47), Andhurin Elisha (5), Muhambo Msana (7), Maulid Yunus (5), Jane Kabeza (30), Lucy Kashindi (11) na Mwalihoba Nyasa (37) ambaye anasumbuliwa na kansa ya titi.
“Jamani tunaomba msaada kwani hali zetu ni mbaya mmoja wetu ameshapoteza maisha kutokana na tatizo hilo tunaomba msaada hata kwa serikali ya Tanzania,” alisema.
Aidha alisema wanawaomba wasamaria wema wengine kujitokeza kuwasaidia msaada wa chakula kwani kwa sasa hawakopeki kutokana na kukosa fedha.
Alisema wanapaswa kupata shilingi elfu 70 kila mmoja kwa wiki kwa ajili ya chakula lakini hali hiyo imekuwa kinyume kwa takribani wiki nzima.
Mkimbizi huyo alisema iwapo hakuna juhudi ambazo zitachuliwa upo uwezekano mkubwa wakimbizi hao kupoteza maisha.
Akizungumza kuhusu jambo hilo mmoja wa maofisa wa Taasisi ya Redeso, Neema Malulu alisema yeye sio msemaji na kumtaka mwandishi awaulize UNHCR kwani wao ndio wanatoa fedha.
“Mimi sio msemaji, kazi yangu ni kuwapatia fedha wakimbizi hao baada ya kupewa na UNHCR hivyo ni vema ukawaulize wao,” alisema Malulu.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Ame Silima alisema mimi ndio nampa taarifa hizo na kudai kuwa suala hilo linawahusu UNHCR hivyo waulizwe wao.
“Upo uwezekano wa kuwepo hapa kama ulivyosema ila wanao husika na watu hao ni UNHCR nadhani itakuwa vema ukiwauliza wao kwanini hawawapatii chakula wakimbizi hao,” alisema Silima.
Jitihada za kuwapata watu wa UNHCR kwa ufafanuzi ziligonga ukuta kwani kila simu yao ilipokuwa ikipigwa walikuwa wahawapokei simu.
Ndugu zetu hawa katika kupigania maisha yao awali walikuwa wakienda kukopa vyakula katika maduka ya jirani na wanapoishi lakini baada ya kuona hawalipi wenye maduka hayo wamesitisha kuwasaidia ambapo baadhi yao wanadaiwa kuanzia shilingi 45,000 hadi 50,000.
Ndugu wasomaji wa mtandao huu wa www. habari za jamii.com kwa yeyote atakayeguswa na kupenda kuwasaidia ndugu zetu hawa ambao licha ya kuwa katika hali ya ugonjwa hasa hao watoto ambao wanapita katika kipindi kigumu kutokana na taasisi hiyo kushindwa kuwapatia chakula kwa wakati unaweza kwenda katika nyumba ya kulala wageni ya Bosco wanapo jihifadhi kwa ajili ya kupeleka chochote ulichonacho iwe matunda, nguo, unga, sabuni, mafuta ya kula na vitu vingine ambavyo utaona vinafaa kwani kutoa ni moyo na si utajiri. Okoa maisha ya wapendwa wetu hawa kwa kutoa ulichonacho kwani mpendwa wao mmoja aitwaye Maua tayari ametangulia mbele za haki kwa kile walichodai ni kukosa chakula. Kama utapenda kupata maelezo zaidi wasiliana na Mwandishi wa mtandao huu, Dotto Mwaibale kwa namba ya simu 0712-727062,0786858550 na 0754-362990.
====================================================================

Mbunge wa Jimbo la TemekeMh.Abbas Mtemvu azindua vicoba

 Mbunge wa Jimbo la TemekeMh.Abbas Mtemvu alipowasili katika Viwanja vya TCC Club, Dar es Salaam, (kushoto ni) Naibu meya na Diwani wa Miburani Juma Mkenga, na kulia ni Mwenyekiti wa Temeke Jogging, Mussa Mtulya.(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
 Baadhi ya wanachama wa Vilab kumi vya Jogging Jimbo la Temeke wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu wakati alipofanya kazi ya kuzindua Vikoba  katika viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam na kuchangisha zaidi ya shilingi  milioni 1.8.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu,   akizindua vikoba  na kupitisha Harambee ambapo zaidi ya Sh. milioni 1.8 zilipatikana katika harambe hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu, kulia na Mwenyekiti wa Temeke Jogging, Mussa Mtulya , wakati mbunge huyo alipokuwa akizindua vikundi zaidi ya  kumi vya Vicoba.
 Pendo Masigati , alipofunguwa kinywaji cha Shampeni katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Vikoba hivyo katika Viwanja vya TCC Clob ,Dar es Salaam
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu  (kulia), akimkabidhi Sh. Laki moja , Mwenyekiti wa Jogging Sports Club ya Mikocheni Dar es Salaam,  Muhamed Husseni kwa ushiriki wao baada ya kukubali mwaliko bila kujali umbali, wanao shuhudia katikati kushoto ni Diwani Hamisi Mzuzuri na anayefuatia ni Naibu meya na Diwani wa Miburani Juma Mkenga
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu, akiongea na wana Habari baada ya uzinduzi wa Vicoba.
=====================================================

TANZANIA KUANIKIZA MAFANIKIO YA LFI KWA MATAIFA 8

DSC_0012Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na mfuko huo katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam).

Na Mwandishi wetu
MATAIFA manane yaliyopo katika nchi zinazoendelea zitaanikizwa mafanikio ya Tanzania katika utekelezaji wa programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) inayosimamiwa na Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF).
Pamoja na upelekaji wa maarifa yaliyopatikana nchini Tanzania katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi huo ambao ulianza mwaka 2012 na kumalizikia 2015, Watanzania ndio watakaotumika kupeleka maarifa mapya.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa UNCDF, Peter Malika wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu warsha ya siku tatu inayofanywa na UNCDF iliyolenga kuwaelimisha wadau mbalimbali wanaohusika na programu hiyo.
Wadau hao ni waandaaji wa miradi, watoa fedha na wasimamizi wanaofanya maamuzi.
Alisema baada ya mafanikio ya mradi huo, UNCDF imemua Tanzania kuwa makao makuu ya LFI na kwamba watanzania baada ya kuonesha uwezo wa dhana za LFI, mafanikio hayo katika mataifa mengine.
Mataifa yaliyoelezwa kupelekewa utaalamu wa watanzania kuanzia awamu ya pili inayotarajiwa kuanza mwakani hadi mwaka 2017 ni Uganda, Benin, Senegal na Bangladesh.
DSC_0081Majadiliano ya nchi nyingine tatu bado yanaendelea na zitapatikana baada ya serikali hizo kukubali kuwepo kwa mradi huo, alisema Malika.
Alisisitiza kwamba program ya LFI inatekelezwa kwa kushirikiana na serikali na hapa Tanzania inafanyika kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI).
Katika utekelezaji wa program hiyo LFI imesaidia miradi kadhaa yenye kipaumbele inayogusa miundombinu ya nishati, kilimo na mawasiliano.
Kwa mujibu wa Malika kuna miradi 25 yenye maslahi kwa umma ambayo imewezeshwa kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Akifafanua zaidi alisema miradi hiyo 25 ya miundombinu iliyoanzishwa na wawekezaji wa umma na binafsi iko katika hatua mbalimbali za uendelezaji.
Aidha alisema miradi hiyo imetawanyika katika sekta mbalimbali zikiwemo za usindikaji bidhaa za kilimo, nishati, miundo mbinu ya utoaji huduma za jamii, mawasiliano na uzalishaji viwandani katika mikoa 10 kote nchini.
DSC_0125Mtaalamu wa nishati mbadala na mshauri wa masuala ya kifedha wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Michael Feldner akitoa mada yenye kuainisha zana za ubunifu zikiwemo masuluhisho wakati wa uhaba wa fedha, mkakati ya kukabili athari, mtiririko wa uandaaji mikataba na masharti na kanuni za msingi zinazoweza kujitokeza katika kila mkataba kwenye warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandazi wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na mfuko huo katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo.
Hadi kufikia Septemba mwaka huu miradi mitano iliyopiga hatua kubwa zaidi ilitarajiwa kufikia kikomo cha bajeti yake katika miezi sita hadi tisa ijayo ambapo dola milioni 26 za mtaji wa ndani katika muundo wa mkopo na misaada ipatayo dola milioni 3 ilihamasishwa.
Msaada wa LFI kwa miradi iko katika muundo wa utaalamu wa kiufundi, kutoa amana, misaada ya kifedha na aina nyingine ya mikopo ambayo inahitajika sana kwa miradi midogo na ya kati ya miundombinu ili ivutie uwekezaji.
LFI imeundwa kuhamasisha ukuaji endelevu, jumuishi na wenye usawa kwa kufungua fursa za uwekezaji ili kuleta mabadiliko chanya na kusaidia miradi kupata fedha kupitia sekta binafsi na hasa masoko ya mitaji.
UNCDF yenye jukumu la pekee kuhusiana na fedha katika mfumo wa Umoja wa Mataifa, shirika hili limelenga kutoa msaada wa mtaji wa kuwekeza na wa kiufundi katika seklta ya umma na binafsi.
Aidha imepewa uwezo wa kutoa fedha za uwekezaji katika muundo wa misaada, mikopo na uwezeshaji wa ukopaji na utaalamu wa kiufundi katika kuandaa taarifa ya mradi kuhusu uendelevu na kujenga uwezo wa kuondoa hatari ya kuporomoka.
DSC_0095Kazi ya UNCDF ni kuhakikisha pia watu katika mikoa na maeneo yote wananufaika na ukuaji wa uchumi kwa kushughulikia changamoto zao hasa maeneo ya pembezoni mwa mji na vijiji.
Na katika hilo Malika alisema lengo kuu ni kuhakikisha kwamba miundombinu hasa ya maeneo ya vijijini ambayo haiwezi kupata kirahisi ridhaa ya taasisi za kifedha au utekelezaji wa serikali kuu inawezeshwa kwa kuitafutia andiko madhubiti na kuelekeza namna ya kupata fedha za utekelezaji.
“Kwa maneno mengine, miradi ile ambayo pengine isingekopesheka athari zake zinapunguzwa na kuingizwa katika hatua ya kuwa tayari kupokea uwekezaji ambapo inaadaliwa ili ipate mtaji wa kibiashara” alisema Malika.
DSC_0210Mkurugenzi wa Nelwa’s Gelato wauzaji wa watengenezaji wa Ice Cream, Bi. Mercy Kitomari akiuliza swali muwasilishaji mada Mtaalamu wa nishati mbadala na mshauri wa masuala ya kifedha wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Michael Feldner wakati wa warsha hiyo.
Matokeo ya jumla ya LFI, kwa mujibu wa Malika ni kuongezeka kwa ufanisi wa rasilimali fedha kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi ya hapa nchini kupitia uhamasishaji kwanza kabisa wa mtaji binafsi kutoka nchini na masoko ya mitaji ili kuwezesha na kuhamasisha maendeleo ya mahalia yaliyo jumuishi na endelevu.
Akizungumzia warsha hiyo ya siku tatu ambayo imeanza leo, Malika alisema kwamba zaidi ya watu 120 watashiriki wakiwamo waandaaji miradi na taasisi za kifedha.
Mafunzo ya leo ambayo yalihusu waandaaji miradi waliwezeshwa na mtaalamu nishati mbadala Michael Feldner ambaye pia ni mshauri wa masuala ya kifedha wa UNCDF.
Mtoa mada huyo aliainisha zana za ubunifu zikiwemo masuluhisho wakati wa uhaba wa fedha , mkakati ya kukabili athari, mtiririko wa uandaaji mikataba na masharti na kanuni za msingi zinazoweza kujitokeza katika kila mkataba.
Mafunzo mengine yatagusa watu wa fedha wanaopokea maandiko na kuyafanyia tathmini, ambayo yatafanyika kesho na kuishia na watoa maamuzi katika taasisi hizo kuhusu mikopo iliyoombwa.
DSC_0228Mtaalamu wa masuala ya fedha wa programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) Abraham Byamungu akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam.
DSC_0117Kutoka kushoto ni Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika, Bw. Imanuel Muro wa UNCDF pamoja na Ofisa Msaidizi anayeshughulikia masuala ya fedha Program ya LFI kutoka UNCDF, Bw. Oscar Kanyenye wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Mtaalamu wa nishati mbadala na mshauri wa masuala ya kifedha wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Michael Feldner (hayupo pichani).
DSC_0083Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na mfuko huo katika hoteli ya Serena mjini Dar es salaam.
DSC_0138
DSC_0120
DSC_0122Washiriki wa warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) wakisikiliza mada katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam .
DSC_0209Mshiriki kutoka Ileje Mbeya, Bw. Joseph Mchome akitoa maoni yake kwenye warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo.
DSC_0187Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akizungumza na waandishi wa habari kuhusu warsha ya siku tatu inayofanywa na UNCDF iliyolenga kuwaelimisha wadau mbalimbali wanaohusika na programu hiyo.
DSC_0168Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akibadilishana mawazo na Mtaalamu wa nishati mbadala na mshauri wa masuala ya kifedha wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Michael Feldner kwenye warsha hiyo.
====================================================================

RITA YAFANIKIWA KUSAJILI WANAFUNZI ELFU 15 MANISPAA YA ILALA.

01Meneja Masoko, Mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bw. Josephat Kimaro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam kuhusu Mafanikio ya Mkakati wa Usajili na Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Manispaa ya Ilala.
02Meneja Masoko, Mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bw. Josephat Kimaro akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani)  jijini Dar es Salaam kuhusu kueneza Mkakati wa Usajili na Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Manispaa ya Kinondoni na Temeke baada ya kumaliza Manispaa ya Ilala. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum 03Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza taarifa ya mafanikio kutoka kwa Meneja Masoko, Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bw. Josephat Kimaro leo jijini Dar es Salaam.
Picha na MAELEZO.
……………………………………………….
Na Fatma Salum- Maelezo Jumla ya wanafunzi 15,120 wa shule za Msingi na Sekondari katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameweza kusajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa kupitia Mkakati wa Usajili na Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa unaotekelezwa na Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini (RITA). Hayo yamesemwa na Meneja Masoko, Mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bw. Josephat Kimaro wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. “Mkakati huu umeonesha mafanikio makubwa kwani mpaka sasa wanafunzi 15,120 wamepata vyeti vya kuzaliwa wakiwemo wasichana 7,712 na wavulana 7,408 kutoka shule 201 za Manispaa ya Ilala ambapo 201 ni shule za Msingi na 96 ni Sekondari.” Alisema Kimaro. Akifafanua zaidi kuhusu mkakati huo uliozinduliwa mwezi Aprili mwaka huu Kimaro alisema umelenga kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kuwapatia wanafunzi vyeti vya kuzaliwa wakiwa shuleni badala ya wazazi kuvifuata kwenye Ofisi za RITA. Aidha umesaidia kuongeza uelewa kwa wanafunzi, wazazi na walezi kuhusu umuhimu wa cheti cha kuzaliwa kwani wazazi wengi wameshawishika kufanya usajili na kupata vyeti kwa ajili ya familia nzima. Pia Kimaro aliongeza kuwa baada ya mkakati huo kufanikiwa katika Manispaa ya Ilala RITA inatarajia kuendeleza katika Manispaa za Temeke na Kinondoni mnamo mwezi Januari 2015 zikifuatiwa na Manispaa nyingine za Tanzania Bara. Akitoa wito kwa wazazi na walezi Kimaro amewataka kutumia fursa hiyo kuwapatia vyeti watoto wao wanaosoma katika shule ambazo program inatekelezwa kwani hutumia mfumo rahisi kwa gharama nafuu na mtoto hupata cheti halisi.

No comments:

Post a Comment