TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, October 23, 2014

MAOFISA WA UN WAHAMASISHA WANAFUNZI WA JANGWANI KUTEKELEZA AJENDA ZA UMOJA WA MATAIFA

DSC_0132Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani akiwa ameambatana na maafisa wenzake wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa unazishwe. Kushoto kwa Bi Ledama ni Albert Okal (ILO).
Shamrashamra za maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa uanzishwe zimeanza nchini, na leo jumatano maofisa waandamizi wa UN walitembelea shule ya sekondari ya Jangwani na kuwahabarisha wanafunzi hao juu ya shughuli za Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Mjadala kati ya maofisa hao Phillemon Mutashubirwa, Programme Manager wa UN Habitat, Usia Nkhoma Ledama, Afisa habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Albert Okal (ILO),Greta Sayungi (UNICEF), ulijikita katika masuala ya HIV/AIDS, EBOLA, Usafi na umuhimu wakuosha mikono ili kujikinga na maradhi, elimu ya ujasiriamali, ajira kwa vijana, kazi za kujitolea, malengo ya Milenia na malengo ya Umoja wa Mataifa kwa ujumla wake.
Ijumaa wiki hii Umoja wa Mataifa utaadhimisha mkiaka 69 toka uanzishwe na kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
DSC_0106
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule yasekondari Jangwani jijini Dar. Kutoka kushoto ni Phillemon Mutashubirwa (UN Habitat), Greta Sayungi (UNICEF) pamoja na Dr Bwijo Bijo (UNDP)
DSC_0094Pichani juu na chini ni Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani wakiwasiliza maafisa wa Umoja wa Mataifa waliowatembelea shuleni hapo.
DSC_0083

 =============================================

Rais Kikwete akutana na Mabalozi wa Afrika nchini China

unnamedRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilkisha nchi zao nchini China wakati alipokutana nao jijini Beijing China leo asubuhi.Rais Kikwete yupo nchini China kwa ziara ya kiserikali(picha na Freddy Maro)unnamed3

================================================

Shirika la ndege la Flydubai lenye makao yake makuu Dubai lazindua njia mbili mpya za ndege


Makamu wa Rais mwandamizi katika shughuli za kibiashara wa shirika la ndege la FlyDubai ,Bwa.Sudhir Sreedharan akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wana habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) katika hafla fupi ya uzinduzi wa njia mbili mpya za shirika la ndege hiyo kutoka Dubai kuja jijini Dar es salaam na Zanzibara (nchini Tanzania). Bwa.Sudhir amesema kuwa shirika hilo la Flydubai liliingia katika soko la kibiashara kuanzia mnamo mwaka 12009,ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kuongeza njia mpya sita (six new routes ) .

Mgeni rasmi,Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Mh Samia Suluhu akizungumza mapema leo katika uzinduzi wa njia mbili mpya za ndege ya FlyDubai aina ya Boieng 737-800,uliofanyika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar.

Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo wa njia mpya ya shirika la ndege la Flydubai lenye makao yake makuu Dubai..

 Wageni waalikwa wakishangilia jambo.

Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo .
========================================================

PUSH MOBILE MEDIA LTD, PARTNERS WITH APALYA TECHNOLOGIES FOR OTT VIDEO STREAMING TECHNOLOGY

unnamedPush Mobile Managing Director, Freddie Manento (L) exchange documents contract with Apalya Technologies International Business, Rishabh Gunjal, Apalya to provide best-in-class mobile video solutions across East and Central Africa.
By Our Reporter
Dar es Salaam. Tanzania’s leading interactive mobile communications technology provider, Push Mobile has partnered with Apalya Technologies, South Asia’s leading technology platform provider to enhance mobile video and live TV streaming experience in Tanzania and into other markets across the region.
Freddie Manento, Push Mobile Managing Director, speaking at the signing ceremony held at Push Mobile offices said the partnership serves to cement Push’s vision and mission of being the mobile communications market leader in East Africa and the international sphere and a provider of high quality products and services.
 “Our partnership with Apalya Technologies is in line with our strategy to expand our video and Live TV streaming technology to new markets around the region and they are the right technology partners to take us there.” said Manento.
On his part Rishabh Gunjal, Apalya Technologies’ AVP – International Business said “Apalya Technologies is excited to partner with Push Mobile in their drive to provide best-in-class mobile video solutions across East and Central Africa. Apalya’s leadership across the emerging markets of India and South Asia as well as their 8 year track record in working with some of the biggest global telecom brands will be a great leverage in helping Push Mobile serve the growing mobile market in this region.”
He said that the firm partnership promises the best platform in terms of technology and content offering providing an opportunity to mobile network operators to monetize their mobile data network with best possible consumer experience.
Television stations and production houses can use this platform to create new revenue stream in digital media space. Consumers will also have access to best of local and international content at an affordable price across all video streaming supported devices like feature phones, smart phones, tablets and PCs.
========================================================================

NHIF NA MPANGO WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOANI

1 1.0     UTANGULIZI
Pamoja na kutekeleza mpango wa kusogeza huduma karibu na wanachama na wadau kwa maana ya kufungua ofisi mikoani, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanzisha mpango wa kupeleka huduma za Madaktari Bingwa mikoani.
Mpango huu unawahusisha Madaktari Bingwa ambao ki-ukweli ni wachache kutoka katika hospitali zifuatazo:-
  1. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili;
  2. Taasisi ya Mifupa MOI;
  • Hospitali ya Bugando.
Madaktari Bingwa hao wanafanya kazi katika hospitali za mikoa kwa kushirikiana na madaktari waliopo huko mikoani.
Madaktari hao ni mabingwa wa:-
  1. Magonjwa ya Moyo
  2. Magonjwa ya Wanawake
  • Magonjwa ya Watoto
  1. Upasuaji na
  2. Mabingwa wa Dawa za Usingizi.
  • LENGO LA KUANZISHA MPANGO HUO:
Lengo la kuanzisha mpango huo ni:-
  1. Kuwapeleka Madaktari Bingwa katika mikoa yenye uhaba mkubwa wa madaktari bingwa na kuwatumia wataalamu hao wachache kitaifa;
  2. Kuwapunguzia wananchi gharama za usafiri kufuata huduma za madaktari bingwa katika miji mikubwa;
  • Kurahisisha utaratibu wa kumwona daktari bingwa ambao wanaonwa kwa ahadi maalum;
  1. Kuwapa fursa ya kujifunza na kuwajengea uwezo wa kiutendaji madaktari walioko kwenye hospitali za mikoa hiyo.
4.0     MAFANIKIO YA MPANGO HUO:
Mpango wa kupeleka Madaktari Bingwa mikoani umekuwa na mafanikio makubwa kwa maana ya kuwafikia walengwa ambao wana mahitaji makubwa ya huduma za madaktari hao. Maisha ya watanzania yameokolewa kwa huduma zitolewazo na Madaktari Bingwa unaofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Mikoa ya Lindi, kigoma, Katavi na Rukwa imeshafikiwa na mpango huo na idadi ya wananchi waliopata huduma hiyo ya madakatari bingwa ni kama ifuatavyo:-
SN MKOA WAGONJWA WALIOONWA WALIOFANYIWA OPERESHENI
1 Lindi 258 6
2 Kigoma 754 37
3 Katavi 1276 37
4 Rukwa 1410 18
  Jumla 3,698 98
Mpango huu umepokelewa kwa mtizamo chanya na wadau wetu wakiwemo wanachama na wananchi wa mikoa husika kwa kuwa wengi wao hawana uwezo wa kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa ambazo nyingi ziko mbali na maeneo wanayoishi.
5.0 RATIBA YA MIKOA INAYOFUATA
Mikoa inayofuatiwa kupelekewa huduma hii ya madaktari bingwa ni Mara,Tabora, Manyara na Mtwara.
MKOA TAREHE MAHALI HUDUMA ZITAKAPOTOLEWA
Mara 3/11/2014-8/11/2014 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara
Tabora Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa)
Manyara Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa)
Mtwara Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa)
  • CHANGAMOTO ZA MPANGO WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOANI:
Pamoja na nia njema ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuwapeleka madaktari Bingwa karibu zaidi ya wananchi wengi wenye mahitaji ya huduma zao, bado zoezi hilo linakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo:
  • Idadi ndogo ya Madaktari Bingwa ikilinganishwa na wananchi wanaohitaji huduma hizo.
  • Uhaba wa vifaa tiba vya kisasa, kama vile vipimo katika hospitali za mikoa ya pembezoni na
  • Uhaba wa vitendea kazi na madawa ili kufanikisha zoezi hili.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unaamini kuwa mpango huu utaokoa maisha ya Watanzania wengi ambao walikwishakata tamaa ya kupata tiba kutokana na gharama kubwa za kufuata matibabu hayo katika hospitali walizopewa rufaa.
6.0 MIPANGO YA BAADAYE YA MFUKO.
Mfuko utaendelea kupeleka Madaktari Bingwa katika maeneo mbalimbali ya nchi baada ya kufanya upembuzi wa mahitaji ya huduma na utaalamu katika maeneo husika.
Kauli mbiu yetu ni “ Afya Bora Ndiyo Mambo Yote.”
======================================================================

Mahakama ya Tanzania imedhamiria kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote

1
Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza akiwaeleza waandishi wa (hawapo pichani) mikakati iliyoweka iliyowekwa na Mahakama ya Tanzania ili kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote na kwa wakati kwa vitendo, kwa kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa mahakamani, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi. Mary Gwera. Picha na Hassan silayo-maelezo
………………………………………………………………………………..
Na Georgina Misama-MAELEZO.
Mahakama ya Tanzania imedhamiria kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote ili kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri na rufaa kukaa Mahakamani kwa muda mrefu. Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi Mary Gwera wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Akizitaja hatua zilizochukuliwa na Mahakama Bi Mary alisema, kuboresha bajeti ya kushughulikia mashauri kupitia mfuko wa mahakama toka bilioni 57 kwa mwaka 2012/13 mpaka bilioni 88 mwaka 2014/15, Idadi ya vikao vya Mahakama ya Rufani vimeongezeka kutoka 26 mwaka 2012 hadi 34 mwaka 2013/14. Aidha, Bi Mary alisema kuwa hatua nyingine ni pamoja na kuanzisha kitengo cha Mahakama Kuu Dar es Salaam kitakachoshughulikia masuala ya utatuzi wa mashauri kwa njia ya suluhu muafaka, pia uundwaji wa kamati ya kanuni za Mahakama itakayosaidia kutunga au kurekebisha kanuni ili kuhakikisha kuwa kanuni zinazotumika Mahakamani si chanzo cha kuchelewa mashauri Mahakamami Naye, Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza alisema kuwa Mahakama imeanza kuchukua hatua za kuimarisha ukaguzi wa shughuli za Mahakama na maadili ya watumishi kwa kuanzisha kurugenzi ya ukaguzi na maadili. Aidha, Bw Kahyoza alivitaja viwango ambavyo kila hakimu au Jaji anatakiwa kuvitimiza kwa mwaka na muda ambao mashauri yanatakiwa kuwa Mahakamani kuwa ni Mh. Jaji wa Mahakama Kuu analenga kumaliza kesi 220, Mahakimu wa Mahakama za Wilaya na Hakimu Mkazi kesi 250 na Mahakimu wa Mahakama za mwanzo kesi 260 Mahakama Kuu inatoa rai kwa Watanzania kufika Mahakamani kwa Tarehe zinazopangwa ili kuisaidia Mahakama kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa Mahakamani.
=======================================================================

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania imeanzisha masomo ya jioni ya diploma ya ukutubi

1
Mkuu wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Bw. Comfort Komba akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) Kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Ofisi hiyo ikiwamo ujenzi wa majengo ya chuo cha ukutubi na uhifadhi wa nyaraka kilichopo Bagamoyo na uzinduzi wa maktaba za wilaya za Kibaha, Chunya, Ruangwa, Ngara, Rulenge, Masasi na Mbulu, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bi. Georgina Misama.
………………………………………………………..
Na Hassan Silayo-MAELEZO Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania imeanzisha masomo ya jioni ya diploma ya ukutubi katika Kampasi ya Dar es Salaam katika mwaka wa masomo 2014/2015. Hatua hiyo inatokana na kuongezeka kwa maombi ya wanafunzi wanaohitaji kuendelea na masomo baada ya kuhitimu mafunzo ya cheti. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Bw. Comfort Komba wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Comfort alisema kuwa masomo hayo kwa awali yalikuwa yakitolewa katika kampasi ya Bagamoyo lakini kutokana na kuongezeka kwa uhitaji wa masomo hayo ambapo mpaka sasa kuna wanafunzi wapya 130 “Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania imeamua kuanzisha masomo ya jioni ya diploma ya ukutubi katika Kampasi ya Dar es Salaam katika mwaka wa masomo 2014/2015 na utaratibu huu tunautekeleza kutokana na kuwepo kwa ongezeko la uhitaji wa wanafunzi” Alisema Comfort. Aidha Comfort alisema kuwa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania kwa kushirikiana na halmashauri za Wilaya na Mikoa imefanikiwa kuanzisha maktaba katika wilaya mbalimbali ikiwemo Kibaha, Chunya, Ruangwa, Ngara, Rulenge, Masasi na Mbulu. Akizungumzia kuhusu uhufadhi wa machapisho ya kitaifa, Comfort alisema kuwa Ofisi hiyo imefanikiwa kuhifadhi jumla ya vitabu 1,300,000 pamoja na majarida 950,000 tangu Bodi hiyo ilipoanzishwa katika ngazi ya Mikoa, Wilaya hadi Tarafa. Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania ni Shirika la umma lililopo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
==============================================================

Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Rubella Manispaa ya Ilala yavuka lengo.

01 Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Manispaa ya Ilala imevuka lengo la kutoa chanjo ya ugonjwa wa Surua na Rubella kwa watu 468,297 ambapo awali lengo lao lilikuwa kutoa chanjo hiyo kwa watu 445,801 wakati wa wiki ya kutoa chanjo hiyo nchini. Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Ilala Dkt. Willy Sangu leo jijini Dar es salaam alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya zoezi la chanjo hiyo linalofanyika nchi nzima. Dkt. Sangu alisema kuwa zoezi la kutoa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Surua na Rubella linaendelea vizuri katika Manispaa ya Ilala kama ilivyopangwa ambapo linafanyika kwa muda wa wiki moja katika kote nchini. “Ninawaomba watu wote ambao hawajajitokeza kupata chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Surua na Rubella, wafike kwenye vituo vya kutolea chanjo hiyo ili kuokoa maisha ya watoto, akina mama wajawazito, akiba baba na vijana” alisema Dkt. Sangu. Dkt. Sangu alisema kuwa idadi ya watu walioitikia wito wa kupata chanjo hiyo imekuwa kubwa katika Manispaa ya Ilala suala ambalo linawapa faraja ambapo watu wa rika zote wamejitokeza kupata huduma. Ili kutoa huduma ya chanjo kwa wakati kulingana na ratiba, Dkt. Sangu amesema kuwa imewalazimu kuongeza vituo 30 ambapo timu ya wahudumu kutoka kwenye vituo mama inatoka ili kuwafuata wananchi waliko. Awali Manispaa ya Ilala ilitenga vituo 236 vya kutoa chanjo hiyo kwa wananchi ndani ya Manispaa hiyo. Dkt. Sangu amesema kuwa mafanikio idadi kubwa hiyo ya mwitikio wa watu kupata chanjo katika manispaa ya Ilala yanatokana na sifa ya kuwa katikati ya jiji ambapo watu wengi hupata huduma mbalimbali za kijamii. Kwa upande wake Afisa Muuguzi Hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo Ilala Queen Lutufyo amesema kuwa mwitikio wa watu kuja kupata chanjo ni mzuri na hawajakosa wateja muda wote wakati wa kutoa huduma hiyo kituoni hapo. Aidha, katika zoezi la kutoa chanjo hiyo magonjwa ya Surua na Rubella wahudumu pia wanatoa dawa za magonjwa ya matende, mabusha, minyoo na matone ya vitamin ‘A’. Muda wa kutoa huduma hiyo ya chanjo vituoni ni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni licha ya kwanba wakati mwingine huduma hiyo hutolewa hadi saa 1:00 usiku kulingana na idadi ya wateja waliopo katika kituo wakati huo kuanzia Oktoba 18 hadi 24 mwaka huu. Zoezi la kutoa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Surua na Rubella nchini linaongozwa na kauli mbiu inayosema “Linda, Okoa, Zuia ulemavu- Kamilisha Chanjo” na kusimamiwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa ufadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Kusaidia Watoto (unicef), Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Misaada la Marekani (UNSAID) na Muungano wa watoa chanjo duniani (Gavi).
================================================================

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

indexWATU WATATU WASIOFAHAMIKA MAJINA WALA MAKAZI YAO, JINSI ZA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 25 -29, WALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI, FIMBO, MAWE KUTOKANA NA TUHUMA ZA UVUNJAJI.
TUKIO HILO USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:51 HUKO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA MBEYA, KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, WANANCHI HAO WAISHIO KATIKA ENEO LA FOREST MPYA NYUMA YA HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA WALIWAKAMATA WATU HAO WAKIWA NA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUVUNJIA VIKIWEMO NONDO, PLAIZI PAMOJA NA MISUMARI NA NDIPO WALIAMUA KUWASHAMBULIA KWA KUWAPIGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI.
WATU HAO WALIFARIKI DUNIA WAKIWA NJIANI KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA ASKARI WA KIKOSI CHA KUZUIA NA KUPAMBANA NA UJAMBAZI CHA WILAYA YA MBEYA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA UTAMBUZI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA KANGAGA WILAYANI MBARALI AITWAYE FUNGO KIFANGA (50) ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 21.10.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANGAGA, KATA YA MAWINDI, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOMVI WA ARDHI KATI YA MAREHEMU NA WATU HAO AMBAO BADO KUFAHAMIKA. AIDHA, WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA MAHOJIANO ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. CLEMENCE KIBIKI, (28) MKAZI WA KANGAGA 2. IMANI KIBIKI (23) MKAZI WA KANGAGA NA 3. FIDELIS KIBIKI (34) MKAZI WA KANGAGA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBARALI KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA AMANI NA UTULIVU ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MBIGILI WILAYA YA RUNGWE AITWAYE AMANI LIKENEME MWAKYOMA (50) ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.10.2014 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBIGILI, KATA YA RWANGWA, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA RUNGWE.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO/WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. Imesainiwa na: [BARAKAEL N. MASAKI – ACP] KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
=====================================================================

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA RAIS WA MMI BINGWA WA MASUALA YA UTAWALA NA UONGOZI KUTOKA BAHAMAS, DKT. MYLES MUNROE

4 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akigana na Rais wa MMI Bingwa wa Masuala ya Utawala na Uongozi kutoka Bahamas, Dkt. Myles Munroe, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR 3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa MMI Bingwa wa Masuala ya Utawala na Uongozi kutoka Bahamas, Dkt. Myles Munroe, na ujumbe wake baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam. Picha na OMR 2 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais wa MMI Bingwa wa Masuala ya Utawala na Uongozi kutoka Bahamas, Dkt. Myles Munroe, wakati alipofika ofosini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, juzi Oktoba 20, na kufanya mazungumzo. Picha na OMR 1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha, Rais wa MMI Bingwa wa Masuala ya Utawala na Uongozi kutoka Bahamas, Dkt. Myles Munroe, na ujumbe wake wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, juzi Oktoba 20, 2014 akiwa na ujumbe wake na kufanya mazungumzo. Picha na OMR
=======================================================================

SOS VILLAGES IKISHIRIKIANA NA MONTAGE INAWALETEA CHAKULA CHA HISANI

MONTAGE
SOS VILLAGES IKISHIRIKIANA NA MONTAGE INAWALETEA CHAKULA CHA HISANI KATIKA KAMPENI YAO YA ‘NIJALI, MCHANGO WAKO TUMAINI LA MAISHA YANGU’ KWA AJILI YA WATOTO WA SOS VILLAGES ITAKAYOFANYIKA TAREHE 24/10/2014 PALE HOTEL YA SERENA MJINI ZANZIBAR KUANZIA SAA MOJA USIKU

MGENI RASMI ATAKAWA MHESHIMIWA MAKAMU WA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR MOHAMMED GHARIB BILAL, TICKET ZINAUZWA SHILLING LAKI MBILI ZA KITANZANIA AU SHNG MILION MBILI KWA MEZA YA WATU KUMI, PIGA SIMU NO 0756-860231 AU 0715-003355 UNAWEZA PIA CHANGIA KWA KUPITIA EASY PESA NO 0774 022270 AU TIGO PESA 0652 475847

 ==============================================

Chuo Kikuu Ardhi kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na taka ngumu

1Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mpango wa chuo hicho wa kuendelea na jitihada za kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na tanga ngumu ikiwemo ujengaji wa miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji na gesi asili ya kupikia, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa chuo hicho Prof. Gabriel Kassenga.
2Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye pia ndiye mtaalam wa teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka (waste treatment facilities) Dkt. Shabaan Mgana Akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna Teknolojia hiyo ya kubadili taka ngumu na maji taka inavyotumika na kuwasaidia wananchi walioonesha nia ya kuitumia ikiwamo kupata mboji kwa ajili ya mazao, mimea pamoja na kupata gesi asili ya kupikia, ambapo mpaka sasa kiasi cha nyumba 100 za awali katika mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na nyumba mia moja katika Chuo Kikuu cha Ardhi zimeshaunganishwa katika Mradi huo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idrissa Mshoro
3Mkemia Mkuu wa Kiwanda cha Mansoor Daya Chemicals Bw. Benedict Mtenga Akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi wanavyoendelea kunufaika na teknolojia hiyo ya kibiolojia ikiwemo kutumika kusafisha maji taka yanayozalishwa na kiwanda hicho na kuepusha uharibifu wa mazingira,wakati wa ziara iliyofanywa katika kiwanda hicho ili kuona jinsi teknolojia inavyofanya kazi.
4Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo na kutembelea maeneo ilipojengwa miundombinu ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili taka ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji.
5 7Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi Bi. Minza Selele hayupo pichani akiwaeleza waandishi wa habari jinsi mtambo wa kuzalisha gesi asili inayotokana na mabaki ya chakula, taka za jikoni na mbogamboga, wakati wa ziara iliyofanywa chuoni hapo kujionea jinsi teknolojia ya kubadili taka ngumu na kuzalisha gesi asili ya kupikia inayofanya kazi. 9Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi Bi. Minza Selele akiwasha karatasi kwa kutumia Gesi Asili iliyozalishwa na Mtambo huo. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

No comments:

Post a Comment