TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 11, 2015

Kinondoni Revival yachomoza Tamasha la Krismasi



Na Mwandishi Wetu

KWAYA mahiri ya nyimbo za Injili, Kinondoni Revival ni mojawapo ya watakaosindikiza Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanaendelea kufanyika kupitia kamati yake.
Msama alisema waimbaji kadhaa wameshathibitisha kushiriki kufikisha ujumbe wa neno la Mungu ambao ni wa Shukrani baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Msama alisema kabla ya uchaguzi Mkuu aliandaa Tamasha la Kuombea Amani uchaguzi Mkuu , lililofanyika Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

"Tunaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi katika tamasha la Krismasi ambalo linalwenda sambamba na shukrani kwa Mungu baada ya kupita kwenye uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu, tukio ambalo limefanikishwa kupitia maombi ya waimbaji na viongozi wa dini waliopiga magoti kumuomba Mungu," alisema Msama.

Aidha Msama aliwataja waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ni pamoja na Rebecca Malope, Ephraim Sekeleti, Sarah K, Rose Muhando, Upendo Nkone, Christina Shusho, Kwaya ya Wakorintho Wapili na Joshua Mlelwa.

No comments:

Post a Comment