TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, March 22, 2013

Bunduki yatumika kuombea rushwa *Wananchi walalamika kubambikiwa kesi na polisi *Viongozi CCM wataka iundwe tume kuchunguza Papa asimikwa,atoa ujumbe mzito Kikwete aomboleza kifo cha trafiki Hukumu wafuasi a ponda Kituo kikubwa cha kuzalisha gesi kujengwa nchini KATUNI

MAJIRA - GAZETI HURU LA KILA SIKU:

Posted: 19 Mar 2013 11:41 PM PDT
Na Mwandishi Wetu, Tabora

BAADHI ya wananchi katika Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora, wamelalamikia kitendo cha baadhi ya askari wa vituo vya polisi Usinge na Kaliua, kuomba rushwa kwa mtutu wa bunduki.
Kutokana na hali hiyo, wananchi hao wamemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kusikiliza kilio chao na wachukulia hatua baadhi ya askari wanaofanya vitendo hivyo ili waweze kuishi kwa uhuru na amani.
Wananchi hao kutoka Vijiji vya Ugansa, Shela, Kombe, Maboha na Usinge, walitoa malalamiko hayo katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa Kata ya Usinge, Bw. Titus Kilomba.

Mkutano huo ulifanyika hivi karibuni kwenye Kijiji cha Ugansa, ambapo wananchi hao walidai kuwa, mbali ya kutishiwa kwa silaha ili kutyoa rushwa pia wamekuwa wakibambikiziwa kesi na askari.
“Tunamuomba Dkt. Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, atusaidie kutatua mgogoro kati ya askari na wananchi ambao umeanza kuvunja mahusiano wetu,” walisema.
Walidai kwamba askari hao wamekuwa wakiwanyanyasa wananchi hususani jamii ya wafugaji kwa kuwabambikia kesi kubwa kwa lengo la kutaka wapewe rushwa.
Mkazi wa Kijiji hicho, Bw. Ngidingi Lusumisha (67), alidai yeye walimbambikia fuvu la kichwa cha mtu na askari aliowataja katika mkutano huo (majina tunayo), ambao walikwenda nyumbani kwake na kudai wanamtilia shaka kuwa anamiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria.
“Siku hiyo ilikuwa asubuhi, askari walikuja nyumbani kwangu wakaniambia nipo chini ya ulinzi wakidai wan mashaka na mimi hivyo wanahitaji kufanya upekuzi.

“Wakati wakiendelea kunihoji, kuna mtu ambaye nadhani alikujana na fuvu la kichwa cha mtu na kukiweka katika zizi langu la ngo’mbe ambapo wakati wakiendelea kunihoji, askari mmoja alitokea zizini akiwa na kichwa fuvu hilo na kudai nimekitoa wapi,” alisema.
Alisema askari hao walianza kumtisha na kumwambia “Wewe mzee sasa utaozea jela maana adhabu ya kukutwa na fuvu la binadamu mahakamani ni kunyongwa hivyo kama nina sh. milioni tano, wamuachie kwani kesi yake ni nzito sana.
Aliongeza kuwa, kutokana na maelezo ya askari hao aliogopa sana hadi kulazimika kuwalilia wakamshawishi awape sh. 200,000. ambazo alizito na kuwapa.

Hata hivyo, Bw. Lusumisha alidai kumshukuru Mwenyekiti wake wa Kijiji cha Shela, Bw. Martin Juma kwa kumshauri alifikishe suala hilo kwa Bw. Kilomba ili aweze kulifuatilia zaidi.
Kwa upande wake, Bw. Kilomba alisema, amekuwa akipokea malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi kuhusu
vitendo askari wa Kituo cha Polisi Kata ya Usinge ambao
wanadaiwa kuwanyanyasa raia na kuwalazimisha kutoa
rushwa kwa mtutu wa bunduki.

Mkazi mwingine wa Kijiji cha Kombe, wilayani humo, Bw. Ikungile Mwandu, alidai mtoto wake Bw. John Ikungile (25), alipigwa risasi na askari wa Kituo cha Kaliua, kwa madai ya kuchunga ng'ombe katika shamba la jirani la kusababisha hasara ya sh. milioni 150.

Alisema baada ya askari hao kufika nyumbani kwake, walimuweka mtoto wake chini ya ulinzi, kumfunga pingu ambapo wakiwa njiani kumpeleka Kituo cha Polisi, walimtaka anyooshe mikono juu na kumpiga risasi katika mkono wake wa kulia.

Akizungumzia mkasa huo, Bw. Ikungile alisema “walinipiga risasi katika mkono wa kulia, baada ya kuanguka na kutowa damu nyingi walinifungua pingu na kukimbia wakiwa na pikipiki.

“Baba aliporudi alinipeleka polisi ili tukachukue PF3 ili niweze kwenda kutibiwa hospitali lakini baada ya kufika kituoni hapo, waliniambia tukienda hospitali nisiseme kuwa nimepigwa risasi eti, niwaambie nimechomwa na kitu chenye ncha kali,” alisema.

Mkuu wa Mkoa huo, Bi. Fatuma Mwassa, alipoulizwa kuhusu sakata hilo alikiri kupokea malalamiko hayo na kuwa, tayari amemuagiza Kamanda wa Polisi mkoani humo, Anthony Rutta ashughulikie suala hilo ili wahusika waweze kukamatwa na kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya kijeshi.

“Taarifa hiyo ninayo...tayari nilishamwagiza RPC awachukulie hatua askari wote wanaotuhumiwa kufanya vitendo hivyo,” alisema.

Naye Kamanda Rutta alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo alidai kuwa, hana taarifa yoyote kuhusu hivyo kupingana maelezo ya Bi. Mwassa ambaye alisema tayari alishampa maagizo.

“Nani kakuambia taarifa hizo...mimi sifahamu chochote kuhusu jambo hilo ndio kwanza unanipa taarifa ngoja nizifanyie kazi” alisema Kamanda Rutta.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani humo, Bw. Iddy Amme, alisema chama hicho hakiwezi kuvumilia vitendo vya aina hiyo vinavyofanywa na askari wanaokiuka madili ya kazi zao.

Alisema baada ya kupata taarifa hizo, alishituka sana na kuahidi kulifikisha suala hilo katika uongozi wa CCM Taifa ili liweze kushughulikiwa kikamilifu.

Katibu wa CCM wilayani Kaliua, Bw. Simon Yaawo, alipendekeza iundwe tume ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo kwa wahusika.

“Mimi nipo tayari kutoa ushahidi sehemu yoyote kama nitahitajika maana tumechoka na matukio kama haya, mimi mwenyewe nilimuona yule kijana aliyepigwa risasi (Ikungile).
Posted: 19 Mar 2013 11:35 PM PDT
ROME, Italia

KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis I, jana amesimikwa rasmi kutumikia wadhifa huo na kutumia fursa hiyo kuwataka viongozi mbalimbali, kuwalinda wanyonge na masikini.

Papa Francis I, alitoa wito huo katika misa maalumu iliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Roma ambapo katika misa hiyo, alivalishwa pete ikiashiria sasa amekuwa Baba Mtakatifu wa 266.

Kwa mujibu wa Kituo cha Utangazaji cha CNN, Papa Francis I, alizunguka katika viwanja hivyo akiwa kwenye gari la wazi na baada ya kuteremka, aliwabariki mahujaji mbalimbali.

Hata hivyo, inakadiriwa zaidi ya watu milioni 1.6  waliudhuria sherehe hiyo huku mamilioni wakiifuatilia kupitia vyombo vya habari wakiwemo viongozi 130 kutoka duniani kote.

Papa huyo alichaguliwa na Mkutano wa Makadinali wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Papa Benedict XVI aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo Februari 28, mwaka huu.

Papa Benedict XVI alikuwa papa wa kwanza kujiuzulu katika miaka 600 ya historia ya kanisa hilo akidai umri wake wa miaka 85, asingeweza kutekeleza kikamilifu majukumu yake.

Katika hatua nyingine, Papa Francis I, anaonekana kuwa na mtazamo tofauti na watangulizi wake.
Posted: 19 Mar 2013 11:34 PM PDT
Na Jesca Kileo

RAIS Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, kuomboleza kifo cha askari WP 2494 Koplo Elikiza ambaye amepoteza maisha kwa kugongwa na gari juzi mchana katika eneo la Bamaga, Dar es Salaam.

Koplo Elikiza aligongwa wakati akimsimamisha dereva gari ambalo alijiunga na msafara wa Rais Kikwete na kupewa amri ya kusimama badala yake akamgonga na kusababisha kifo chake.

“Nimepokea taarifa za kifo hiki kwa mshtuko na huzuni nyingi, nimejulishwa kuwa aligongwa na gari akiwa kazini katika eneo la Bamaga, Dar es Salaam, wakati akiongoza msafara rasmi.

“Ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha kwa Koplo Elikiza kupoteza maisha akiwa kazini kwenye utumishi wa jeshi lake
na nchi yake wakati Taifa bado linaendelea kuhitaji sana
nguvu kazi yake,” alisema Rais Kikwete.

Alimtaka IGP Mwema kumfikishia salamu zake kwa familia ya marehemu kuwa yupo pamoja nao.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema bado linaendelea kumsaka dereva aliyesababisha kifo cha askari huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Posted: 19 Mar 2013 11:32 PM PDT
Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kesho inatarajia kutoa hukumu ya washtakiwa wa kesi ya kufanya maandamano haramu kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), inayowakabili wafuasi 53 wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Sundi Fimbo, anayesikiliza ambapo upande wa mashtaka ulikuwa ukiwakilishwa na wakili wa Serikali, Bernad Kongola, wakati upande wa utetezi unawakilishwa na wakili Mohamed Tibanyendela.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi saba na vielelezo mbalimbali ambapo upande wa utetezi, washtakiwa hao walijitetea wenyewe.

Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya maandamano haramu Februari 15 mwaka huu kwenda kwa DPP, licha ya Jeshi la Polisi kukataza kufanyika kwa maandamano hayo.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, washtakiwa hao wanadaiwa kufanya maandamano haramu kwenda katika Ofisi ya DPP ili kumshinikiza atoe dhamana kwa Shekhe Ponda na mwenzake Shekhe Mukadamu Swalehe.

Katika maelezo ya awali, washtakiwa hao walidaiwa kuwa awali polisi walitoa zuio la maandamano hayo lakini walikaidi ambapo siku ya tukio, polisi waliwaamuru kutawanyika katika mikusanyiko waliyokuwa wakiifanya na kukaidi ndipo wakakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Katika maelezo hayo, mshtakiwa wa kwanza Bw. Salum Makame, alikiri kukutwa na kisu na kipaza sauti lakini akakana kuwa hakuwa mfuasi wa Shekhe Ponda.

Posted: 19 Mar 2013 11:31 PM PDT

OSLO, Norway

KAMPUNI za Statoil na BG Group, zinatarajia kutumia dola za Marekani bilioni 10 kujenga kituo cha kuzalisha na kusafisha
gesi ya asili nchini Tanzania ili kuiuza Asia.

Hatua hiyo inatokana na Kampuni ya Statoil kutoka nchini Norway, kugundua uwepo wa gesi nyingi Pwani mwa Tanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Uchimbaji wa kampuni hiyo, Bw. Tim Dodson, aliyasema hayo juzi kutokana na utafiti waliofganya kwenye Bahari ya Hadi na kugundua uwepo wa gesi yenye
ujazo wa trilioni nne hadi sita.

“Tunafanya kazi na BG ili kuja na makubaliano ambayo yataweka mambo sawa katika maeneo husika, tunapaswa kukubaliana na mamlaka husika nchini Tanzania wakati tunaingia katika hatua
ya pili,” alisema Bw. Dodson wakati akizungumza na Shirika
la Habari Reuters.

Aliongeza kuwa, gesi waliyoigundua katika bahari hiyo huenda ikawa na ongezeko kubwa kwani rasilimali hiyo inaonekana ni nyingi nchini Tanzania ambapo kwa mujibu wa Reuters, BG imevutiwa na ushirikiano uliopo kati ya kampuni hiyo na nyingine ya Ophir Energy.

Mwanzoni mwa wiki hii, Kampuni ya BG ilitangaza utafiti wake umefikia katika hatua nzuri za uchimbaji wa gesi Tanzania.

Katika hatua nyingine, Wanajeolojia kutoka nchini Marekani wanadai gesi ya asili inapatikana kwa wingi katika mwambao wa Tanzania, Kenya na Msumbiji kuliko Nigeria ambayo ni nchi kubwa kwa uzalishaji wa nishati ya mafuta.

Reuters liliongeza kuwa, Afrika Mashariki imeanza kuvutia watu katika sekta ya mafuta kutokana na uhitaji mkubwa wa gesi katika Asia.

“Statoil na BG katika ujenzi wa kiwanda hicho, tutakuwa tunapitia japo hatua mbili, kwanza kuiandaa gesi katika kitalu namba mbili kinachosimamiwa na Statoil na kitalu namba moja cha BG kwa nyongeza kutokana na ujazo wa 10-13 (tcf) ambao tunao.

“Kama ujazo huo utafikia 20 (tcf), wataangalia nini kifanyike ili
gesi hiyo iweze kuandaliwa vizuri, kiasi hicho cha fedha kitatumika katika shughuli hiyo na uwekezaji utafanyika ndani ya miaka mitatu, kabla ya mwaka 2016,” alisema Bw. Dodson.

Wakati huo huo, Mwandishi Peter Mwenda anaripoti kuwa, Wizara ya Nishati na Madini, imeingia mkataba wa utafiti wa gesi, mafuta na Kampuni ya JACKA Resources Ltd ya Australia.

Waziri wa Wazara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo, aliyasema hayo Dar es Salaam jana na kuongeza kuwa, watafiti hao wameingia mkataba wa miaka 11 ambao umegawanyika sehemu tatu.

Alisema utafiti  huo utafanyika katika eneo la Ruhuhu mkoani Ruvuma, Njombe na utakuwa wa miaka minne kwa kila awamu.

Aliongeza kuwa, awamu ya kwanza ya mradi huo kama mafuta na gesi itagundulika, kampuni hiyo itachukua asilimia 50 ya mapato na serikali ya Tanzania asilimia 50.

Alifafanua kuwa, baada ya hapo Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania nchini (TPDC), nayo italipa kodi asilimia 30 na kampuni hiyo italipa asilimia 30 ambazo zitatokana na mapato yao ya asilimia 50.

Awali akizungumza katika mkataba huo, Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw. Scott Spencer, alisema wao ni wazoefu katika kazi hiyo kwani waliwahi kufanya utafiti katika Bara la Afrika na kufanikiwa kugundua mafuta ya petrol kwenye Ziwa Albart nchini Uganda.

Alisema mradi huo utagharimu dola milioni 20 hadi 50 ambazo ni sawa na fedha za Tanzania sh. bilioni 80.
Posted: 19 Mar 2013 11:29 PM PDT

Thursday, March 21, 2013

WASANII NYOTA WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA WAKIENDELEA KUPAKAZIA KATIKA TAMASHA LA KABANG na TIGO. hivi karibuni

Tigo na Kabang yazidi kutikisa Anga

 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Mr.Blue akifafanua Jambo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Tigo Kabang hivi karibuni.
Msanii akizungumzia Kabang inavyozidi kutikisa
 Chege akifafanua jambo
 Mwandishi wa Habari Ahamad Michuzi akiziweka hewani habari hizi za Kabang na Tigo

 Wasanii wakishangaa jambo kuhusiana na huduma ya Kabang na Tigo
Picha Zote kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania.

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAM CHADHAMINI FAINALI YA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13

Chuo Kikuu cha Dar es salaam ni miongoni mwa taasisi mbalimbali nchini zilizoitikia wito wa kudhamini fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 ikiwa ni baada ya kupata taarifa ya kuwapo kwa mapungufu mbalimbali ambayo yamepelekea kusogezwa mbele fainali zake kutokana na upungufu na ufinyu wa bajeti kiasi cha shilingi milioni 170 zilizotokana na kushindwa kwa baadhi ya wadhamini kutimiza ahadi zao.
udhamini huo ambao unalenga moja kwa moja kwa washindi, ni pamoja na kulipiwa gharama za ada ya masomo katika musimu wa 2013/14  kozi ya uandishi wa habari  katika chuo kikuu cha dar es salaam ,school of journalism and mass communication( sjmc).
akizungumza jijini dar es salaam kuhusu udhamini huo , rais wa miss utalii tanzania, gideon chipungahelo alisema kwamba ni jambo la kupendeza kwa kuwa kuna  ufinyu wa bajeti katika kukamilisha fainali za taifa za miss utalii tanzania.
“tunashukuru kuona taasisi kama chuo kikuu cha dar es salaam kinajitokeza kuunga mkono juhudi za miss utalii tanzania katika harakati za kufanikisha fainali za taifa za miss utalii tanzania 2012/13 ambazo zinalenga kuutangaza utalii wa tanzania, ikiwa ni pamoja na chuo kikuu cha dar es salaam ambacho kina historia ukilinganisha na vyuo vingine katika ukanda wa afrika mashariki na kati, hivyo nazidi kusisitiza kwa wadau, taasisi na makampuni binafsi kujitokeza kuunga na kusaidia juhudi hizi ili fainali za mwaka huu ziwe tofauti na fainali za miaka ya nyuma” alisema chipungahelo
Na kuongza kwamba ahadi kwa wadau na wapenzi wa mashindano haya iko pale pale, kwa kuwa dhamira ipo na nia ya kulifanya shindano la Miss Utalii Tanzania kuendelea kuwa bora na lenye mafanikio makubwa kuliko jingine lolote nchini na afrika iko pale pale, na hili litadhihirika wakati wa fainali kuu ya mashindano  mwishoni mwa mwezi huu, hivyo wadau,wafanyabiashara, makampuni binafsi na ya umma, hasa ya kizalendo watakaojitokeza siku hiyo watashuhudia burudani ya aina yake kutoka kwa Warembo mbalimbali wanaowakilisha Mikoa yao,na wawakilishi wa Kanda za Vyuo Vikuu Tanzania bara na Zanzibar.

Miss Utalii Katavi akionekana mwenye Furaha wakati akipozi kwa ajili ya Picha

Wednesday, March 13, 2013

Washtakiwa kesi ya uchochezi, wizi wakana waelezo ya awali

Posted: 12 Mar 2013 12:12 AM PDT

Rehema Mohamed na Rehema Maigala

WASHTAKIWA wa kesi ya wizi na uchochezi inamkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Issa Ponda na wenzake, jana waliendelea kujitetea baadhi yao wakikana maelezo ya awali waliyotoa katika Kituoa cha Polisi Mabatini, Kijitonyama.

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wametoa utetezi wao kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Victoria Nongwa wakiongozwa na wakili wao, Bw.Juma Nassoro.
Mshtakiwa Alawi Musa, alikana maelezo yake na kudai kuwa, alikwenda katika Msikiti wa Changombe Markaz, kwenye ibada ya Itikafu kwa ajili ya kukomboa eneo la Waislamu lililouzwa. Alawi alikana maelezo ya kuhusika kujenga Msikiti wa muda
katika eneo la Markaz, linalomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd, wakati wakati akihojiwa na wakili wa Serikali Tumaini Kweka. Katika maelezo aliyotoa polisi, mshtakiwa huyo alidai yeye ni mzaliwa wa Zanzibar, Kijiji cha Ole na alikuja Dar es Salaam mwaka 2008, lakini wakili huyo alipomuhoji kuhusu  maelezo hayo pia aliyakana. Kwa upande wake, mshtakiwa Ramadhani Rashidi katika maelezo aliyotoa polisi, alidai kuwa yeye ni mkazi wa Mlandizi na alipata taarifa za kusaidia ujenzi wa Msikiti katika kiwanja cha Chang'ombe Markaz kutoka kwa imamu wake wa Msikiti wa Nuruh.
Katika maelezo hayo, alidaikuwa baada ya kupata taarifa hizo alikuja Dar es Salaam na kwenda Chang'ombe Markaz, Oktoba 15,2012 na walikamatwa na polisi Oktoba 16 mwaka huo usiku. Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana maelezo hayo na kudai polisi walimuhoji jina lake, umri na anapoishi ambapo suala la kwenda Chang'ombe Markaz, kujenga msikiti halijui hivyo huenda polisi wamejiandikia. Shekhe Ponda na wenzake wanakabiliwa na makosa matano  ambapo Oktoba 12 ,2012 wanadaiwa kula njama na kuvamia kiwanja kinachomilikiwa na Kampuni ya Agritaza Ltd  kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali.
Katika kosa la uchochezi, inadaiwa Shekhe Ponda na Salehe Mkadam wakiwa katika eneo la Chang'ombe Markaz na viongozi
wa taasisi hiyo, waliwashawishi wafuasi wao ambao ni washtakiwa katika kesi hiyo kutenda makosa hayo.
Posted: 12 Mar 2013 12:11 AM PDT

Na Yusuph Mussa, Korogwe

MKUU wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Bw. Mrisho Gambo, ameungana na vyama vya upinzani kuikataa taarifa ya Kaimu Ofisa Elimu Sekondari wilayani humo Bw. Shabaan Shemzigwa, kuhusu chanzo cha kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2012 na kudai haina mashiko.

Akizungumza mwishoni mwa wiki kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC), Kaimu Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), wilayani humo, Bw. Ibrahim Abdillah, alisema taarifa hiyo haioneshi matatizo yaliyochangia wanafunzi kufanya vibaya zaidi.
“Mwenyekiti (DC), naomba tuikatae taarifa ya Ofisa Elimu kwani haioneshi tatizo lililofanya wanafunzi kufeli zaidi ya kuja na asilimia ya watoto waliopata sifuri, pia hawaoneshi ni jitihada gani ambazo watafanya ili kumaliza tatizo hili,” alisema Bw. Abdillah.
Kwa upande wake, Bw. Shemzigwa alijitetea na kudai kuwa, alipata taarifa kikao hicho siku moja kabla hivyo ameshindwa kuingiza vitu vingi kwenye ripoti yake na kukiri kasoro hizo lakini alimtibua Bw. Gambo baada ya kusema kuwa, tatizo la kufeli ni la kitaifa.
Bw. Gambo alimwambia Bw. Shemzigwa kuwa, asilete taarifa ambazo zinazungumzia Taifa katika kikao hicho bali yeye anapaswa kusema ni nambna gani wataweza kumaliza tatizo la watoto kufeli wilayani humo.
“Taarifa iliyotolewa na Ofisa Elimu inaonesha kama funika kombe mwanaharamu apite, haioneshi mkakati au jitihada gani zitafanyika kupunguza matokeo mabaya kwa wanafunzi... taarifa hii ni sawa na utani, dharau na mazoea.
“Acha kusema wanafunzi kupata sifuri ni tatizo la Taifa, kwani mimi, mke wangu na mtoto wangu tumepata zero...zungumzia nini kifanyike ili kuondoa tatizo hili, kama ningekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ningemuandikia barua Ofisa Elimu ya kujieleza kwa nini asishushwe cheo,” alisema Bw. Gambo.
Aliongeza kuwa, anaungana mkono msimamo wa vyama vya upinzani kuikataa taarifa hiyo na kumtaka Bw. Shemzigwa aiondoe kwenye kumbukumbu za DCC na kuiwasilisha wakati ujao.  Alisema kama Watanzania tunataka ufaulu mzuri kwa watoto wao, wanapaswa kuacha kuingiza siasa na haki za binadamu kwenye masuala ya elimu kwani kuacha kuwachapa viboko wanafunzi kupunguza nidhamu shuleni ambayo ndio msingi wa mafanikio. taarifa hiyo ilisema wanafunzi 1,727 waliomaliza kidato cha nne wilayani humo mwaka 2012, walipata sifuri sawa na asilimia 83.269. 
Akizungumza na gazeti hili baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wilayani humo, Dunstan Mdoe, alisema kuwe na masharti magumu kwa wakuu wa shule za sekondari kuwa atakayeshindwa kufikia
kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wake afukuzwe.
Posted: 12 Mar 2013 12:10 AM PDT
Na Kassim Mahege

SIKU moja baada ya Waziri wa Mambo ya ndani Dkt.Emmanuel Nchimbi kuwasimamisha kazi maofisa wa Jeshi la Polisi kwa tuhuma mbalimbali, Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party(DP) Mchungaji Christopha Mtikila amempongeza kwa hatua hiyo na kumtaka asiishie hapo.
Akizungumza na gazeti hili jana alisema kuwa hatua hiyo inaonyesha ishara nzuri kwa Jeshi la polisi lakini Dkt Nchimbi anatakiwa achimbuwe mizizi ya uhalifu kwa jeshi hilo na hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa watakaobainika.
"Kuwasimamisha kazi pekeyake haitoshi tunataka ukweli ukibainika kwa maofisa hao hatua kali sana za kisheria zifanyike dhidi yao,maana hao ndio wanaolipaka matope Jeshi la Polisi."na kuongeza kuwa hao ndio wanaowaumiza wananchi."alisema Mtikila.
Akitolea mfano wa aliyekuwa waziri wa fedha Basil Mramba,Amatus Liyumba na Yona wa benki kuu mahakama yenyewe ilithibitisha kuwa hakuna makosa yoyote ya wizi walioyafanya ispokuwa makosa yao yalikuwa ni kutumia vibaya madaraka yao na kuongeza kuwa leo hii watu hao wanasota kisutu,hivyo anataka na maofisa hao pia wapelekwe mahakamani ili iwe fundisho kwa wengine.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt.Wilbroad Slaa alisema haoni kama kuna jipya kutokana na hatua hiyo.
"Mimi sitaki kuzungumzia uamuzi huo wa Dkt.Nchimbi kwa sababu ni dhahiri kuwa kuna double standard,Nchimbi aliwahi kuunda tume kwa ajili ya kufuatilia mauaji ya Mwangosi lakini hakuna hatua yoyote alioichukua mimi sioni kama kuna jambo jipya."alisema Slaa.
Alisema hatua hiyo imechelewa kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uhalifu kwa jeshi la polisi na kutolea mfano kuwa Dkt.Nchimbi aliwahi kuunda tume yake kwa ajili ya kuchunguza mauaji ya mwangosi,Ripoti zote zilizotolewa zilionyesha kuwa Jeshi la polisi lilitumia nguvu isio ya lazima na kuongeza kuwa mpaka hivi leo Nchimbi hajasema chochote.
Posted: 12 Mar 2013 12:09 AM PDT

Na David John

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James
Mbatia, amemshauri aliyekuwa mgombea urais nchini Kenya
kwa tiketi ya Chama cha Muungano CORD, Bw. Raila Odinga kuheshimu matokeo ambayo ndio maamuzi ya wananchi.
Alisema kinachohitajika baada ya Bw. Uhuru Kenyatta kushinda nafasi ya urais nchini humo kwa tiketi ya Chama cha Muungano
wa Jubilee ni kukaa mezani ili kuijenga nchi hiyo kwa pamoja. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana, Bw.  Mbatia alimpongeza Bw. Kenyatta kwa ushindi alioupata na kusisitiza kuwa, Wakenya wamefanya uamuzi mgumu ambao haukutarajiwa na watu wengi. “Hali nii inatokana na ukweli kwamba, Bw. Kenyatta anakabiliwa
na kesi mahakamani lakini bado wananchi wameendelea kumuamini na kumpa nchi ili aweze kuwaongoza kama rais wao.
“Ni vyema Bw. Odinga akaachana na nia yake ya kutaka kwenda mahakamani kuweka pingamizi la matokeo yaliyotangazwa badala yake aheshimu maamuzi ya Wakenya ambayo wameyafanya kwa kumchagua Bw. Kenyatta,” alisema.
Alisema Wakenya wameandika historia mpya duniani hasa katika Bara la Afrika inayopaswa kuigwa na mataifa mengine na kufafanua kuwa, kama Bw. Odinga atakwenda mahakamani kuweka pingamizi ajue wazi huko ni kutaka kuwagawa Wakenya, kuhatarisha amani ambayo tayari wameionyesha, kusababisha machafuko na chuki.
Bw. Mbatia aliongeza kuwa, ushindi wa Bw. Kenyatta ni kielelezo kuwa si kila kitu watakacho wazungu, waafrika wakifanye lakini ufike wakatiAfrika iweze kufanya maamuzi yake wenyewe bila kuingiliwa na taifa lolote duniani. “Namuomba Bw. Odinga na wagombea wengine walioshindwa katika uchaguzi huu waheshimu makubaliano ya kulinda amani ambayo walikubaliana ili kuivusha Kenya kwenye demokrasia
ya ukomavu,” alisema Bw. Mbatia.
Katika hatua nyingi, Bw. Mbatia alizungumzia mchakato wa Katiba Mpya unaondelea nchini na kusisitiza nchi inapaswa kujifunza kwa yale mazuri ambayo Wakenya wameweza kuyatumia katika Katiba yao ambayo wameipata miaka michache iliyopita.
Posted: 12 Mar 2013 12:06 AM PDT

KUJIAJIRI ni suala linalopewa kipaumbele na mamlaka mbalimbali nchini pamoja na mataifa yaliyoendelea. Mabadiliko makubwa katika mifumo ya uchumi, yamechangia
wananchi wengi kukosa kazi za kuajiriwa ambapo ajira binafsi 
ndizo zinazoonekana kushika kasi katika maeneo mengi. Nchini Tanzania, idadi kubwa ya wananchi wameamua kujiajiri wenyewe wakiwemo wastaafu kwa kufungua vitega uchumi mbalimbali  pamoja na kufanya biashara ndogondogo ili waweze kujipatia kipato. Cha kukidhi mahitaji yao.
Kujiajiri katika biashara ni jambo jema lakini sisi tunaona kuwa, tatizo kubwa linalowasibu wadau wengi wanaofanya shughuli hizo ni kukosa mafunzo ambayo yatawawezesha kuendesha biashara pamoja na kukuza mitaji yao.
Wafanyabiashara wengi nchini hawabadiliki kwa sababu shughuli wanazofanya ni zile za mazoea bila kuwa na ujuzi wa namna ya kuziendesha hivyo upo umuhimu wa Serikali, kubeba jukumu hilo ili kuwawekea msingi mzuri wa maisha.
Baadhi ya wastaafu waliopewa viinua mgongo na kuwekeza kwenye biashara, wanakabiliwa na wakati mgumu wa kutafuna mitaji yao kwa sababu ya kufanya biashara zisizoendelea. Wanaofanya biashara ya kuuza maandazi na vitumbua, hawana mtazamo wa kutunza ziada wanazopata kwa kufungua akaunti bali wanachokipata kinakwenda tumboni bila kujua senti 50 inayobaki, ilipaswa kuwekwa akiba ili kuendeleza biashara zao.
Hili ni jambo hatari sana, wafanyabiashara kama hawa mbali ya kufanya biashara hizo kila siku, bado wataendelea kubaki maskini bila mafanikio yoyopte kama Serikali haitachukua hatua za haraka kuwasaidia kwa kuwapatia mafunzo ya kuendesha biashara zao.
Ni wajibu wa Serikali na wadau wengine, kutambua kundi hili ni watu wenye vipato vidogo na vile vya kati ambao hawawezi kulipa maelfu ya pesa kugharamia mafunzo ya uendeshaji biashara.
Wito wetu kwa Serikali ibuni mkakati wa kushirikisha wadau wengine na kuandaa mpango maalumu wa kutoa mafunzo ya usimamizi na uendeshaji shughuli za ujasiriamali bure
kwa wananchi waishio mijini na vijijini.
Kwa kufanya hivyo, italeta mwamko kwa wajasiriamali kujua namna ya kuendesha shughuli zao na kuwapa ubunifu zaidi wa biashara mpya tofauti na sasa.
Hivi sasa, wajasiriamali wengi wanafanya biashara kwa kumwiga mwenzake, utakuta kila mahali biashara ni saloon, grosari, maduka ya dawa, chakula na nguo. Je, hivi hizi ndio huduma pekee wanazohitaji wananchi?