TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, July 23, 2014

Bweni la shule ya Sekondari Erikisongo Wilayani Monduli lateketea kwa moto

Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo (Jumatano) asubuhi.

Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako darasani.

Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea. Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kilifika wakati tayari mabweni hayo yameshateketea.

Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh Edward Lowassa  ametembelea shule hiyo na kuahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati  utaratibu unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida.

Gharama za kuwasafirisha wanafunzi hao ni shilingi laki Saba. Aidha Mh Lowassa amesema kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.
Kikosi Cha zimamoto kikijaribu kupambana na moto ulioteketeza mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli yaliyoteketea kwa moto, akiongozana na mkuu wa shule hiyo mwalimu Agnes Nyange.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo Monduli mjini yaliyoteketezwa kwa moto.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa afisa elimu wa Monduli mwalimu Shaaban Mgunya wakati alipotembelea mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli yaliyoteketea kwa moto.

MKUTANO MKUU WA BRN WAFANYIKA JIJINI DAR.

    Gavana  wa  Benki   Kuu  ya  Tanzania,  Prof.  Benno  Ndulu   akichangia   hoja   wakati  wa mkutano  wa  kupitia  taarifa  ya  mwaka mmoja ya utekelezaji  wa  Mpango  wa  Matokeo  Makubwa  sasa (BRN) uliofanyika  leo  Jumatano   Julai  23,  2014  katika  ukumbi   wa Mwalimu  Nyerere  Jijini  Dar es  Salaam.  Kulia  ni  Katibu   Mkuu  wa Wizara  ya Maji  na  Umwagiliaji  Mhandisi  Bashir Mrindoko
Katibu  Mkuu  Kiongozi  Balozi   Ombeni  Sefue  akichangia  hoja  wakati mkutano wa kupitia taarifa  ya  mwaka  mmoja  ya  utekelezaji  wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa uliofanyika leo Jumatano   Julai  23,  2014  katika ukumbi   wa Mwalimu  Nyerere Jijini  Dar es  Salaam. Kulia  ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Asha- Rose  Migiro   na (katikati)  Mtendaji  Mkuu  wa  Ofisi  ya  Rais-  Usimamizi  wa  Utekelezaji  wa  Miradi  (PDB),  Bw. Omari Issa.
 Naibu  Waziri  wa Viwanda  na Biashara, Mhe. Janet Mbene akichangia  hoja  wakati mkutano wa kupitia taarifa ya  mwaka  mmoja  ya  utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa uliofanyika leo Jumatano   Julai  23,  2014  katika ukumbi   wa Mwalimu  Nyerere Jijini  Dar es  Salaam. Kushoto  ni Katibu  Mkuu Ofisi  ya Waziri Mkuu Tawala  za  Mikoa  na Serikali  za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Jumanne Sagini.
 .       Naibu  Waziri  wa  Katiba  na  Sheria, Mhe. Angellah Kairuki (katikati)  akichangia  hoja  wakati mkutano wa kupitia taarifa ya  mwaka  mmoja  ya  utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa uliofanyika leo Jumatano   Julai  23,  2014  katika ukumbi   wa Mwalimu  Nyerere Jijini  Dar es  Salaam.
1.       Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe  (kulia) akichangia akichangia  hoja  wakati mkutano wa kupitia taarifa ya  mwaka  mmoja  ya  utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa uliofanyika leo Jumatano   Julai  23,  2014  katika ukumbi   wa Mwalimu  Nyerere Jijini  Dar es  Salaam. Kutoka  kushoto  ni  Waziri  wa  Elimu na Mafunzo  ya Ufundi,  Mhe. Shukuru  Kawambwa,  Naibu  Waziri  wa Fedha  na Uchumi, Mhe.  Mwigulu Nchemba,  na Katibu  Mkuu wa  Wizara  ya Nishati  na Madini,  Eliakim Maswi.

(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

Rais Kikwete afungua nyumba za Watumishi wa Afya Matemanga, Tunduru, zilizojengwa na Mkapa Foundation

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua mradi wa nyumba za watumishi wa afya zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation katika hafla iiyofanyika katika kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma leo.

Jumla ya nyumba 480 zinajengwa katika halmashauri 48 nchini na miongoni mwa nyumba hizo 40 zipo katika mkoa wa Ruvuma.Taasisi ya Benjamin Mkapa iliingia mkataba na Wizara ya Afya kutekeleza mradi wa miaka mitano(2011-2016) wa uimarishaji wa mifumo ya Huduma za afya chini ya ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kupambana na ukimwi,kifua kikuu na Malaria(Global Fund).

Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin W.Mkapa Dkt.Ellen Senkoro, Mbunge wa Jimbo la Tunduru Mhandisi Ramo Makani, Meneja wa Portfolio, Mfuko wa Dunia wa Kupambana na ukimwi,kifua kikuu na Malaria Bi. Tatajana Peterson, Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof.Anna Tibaijuka, Naibu Waziri wa TAMISEMI Aggrey Mwanri, Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Kebwe Stephen  Kebwe, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Saidi Mwambungu. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kiwete akiteta jambo na mkazi wa kijiji cha Ligela wilayani Namtumbo Bwana Edwin Ngonyani wakati alipokuwa anahitimisha ziara yake wilayani humo.Bwana Ngonyani ambaye alipata ulemavu baada ya kupoteza miguu yote miwili katika ajali ya moto alimweleza Rais kuwa anapata taabu ya kutafuta riziki kwakuwa anatambaa kwa taabu.Rais Kikwete alitoa ahadi ya kumsaidia mlemavu huyo ili aweze kujikimu kimaisha.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa kijiji cha Matemanga wakati wa hafla ya uzinduzi nyumba 480 za watumishi wa umma zilizojengwa na Taaasisi ya Benjamin W.Mkapa kwa ushirikiano na Wizara ya Afya
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin w.Mkapa Dkt  Ellen Mkondya Senkoro(kushoto) akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete michoro na ramani za nyumba za watumishi wa afya zilizojengwa na taasisi hiyo wkati hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo uliofanyika katika kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru leo.Watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na wane kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka.Picha na Freddy Maro

VIUNGO VYA BINADAMU SASA YAIBUKA MENGI, HOFU YATANDA BAADA YA SIRI KUFICHUKA UTUPAJI WA VIUNGO VYA MAITI YA BINADAMU KUBAINIKA, MAABARA YA CHUO KIKUU CHA INTERNATIONAL MEDICAL AND TECHONOLOGICAL UNIVERSITY YATAJWA KUHUSIKA JIJINI DAR ES SALAAM.

Makamu Mkuu wa Chuo cha International Medical and Technological University (IMTU), Profesa PV Prabhak Rao (mwenye koti la blue) na viongozi wengine wakisindikizwa na polisi kuingia kwenye Kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na upatikanaji wa viungo vya binadamu eneo la Mpigi Bunju. Picha na Rafael Lubava


Dar es Salaam.
 

Wakati ikibainika kuwa viungo vya miili ya binadamu vilivyookotwa juzi katika Bonde la Mto Mpiji nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam vilitoka katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), jana Jeshi la Polisi liliwatia nguvuni watumishi wanane wa chuo hicho kuhusiana na sakata hilo.

Kukamatwa kwa watumishi hao kumeelezwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kuwa ni baada ya uchunguzi wa awali kubaini kuwa viungo hivyo kwa mara ya mwisho vilikuwa katika maabara ya IMTU.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi jioni eneo la Bonde la Mbweni Mpiji ambako iligundulika mifuko ya plastiki 85 yenye mabaki ya viungo vya binadamu.

Kutokana na tukio hilo, Polisi imeunda jopo la wapelelezi saba likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu, Jafari Mohamed kusaidiana na daktari wa jeshi hilo kufanya uchunguzi wa miili hiyo.

“Katika uchunguzi wetu tulibaini kuwa hivyo viungo vya binadamu vilitolewa katika Chuo cha IMTU na kusindikizwa na mfanyakazi wa ngazi ya juu kwa ajili ya kutupwa eneo la Bonde la Mbweni Mpiji,” alisema Kova.

Alisema mifuko hiyo ilikuwa myeusi ikiwa na viungo vya aina mbalimbali vikiwamo vichwa, miguu, mikono, moyo, mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali.

“Viungo hivyo havikuwa na harufu wala uvundo wa aina yoyote na vilionekana vimekaushwa na kukakamaa,” alisema.

Alisema katika eneo hilo walikuta vifaa vinavyotumika hospitali kama glovu, nguo maalumu (apron) 20 na karatasi mbili zenye maswali ya kujibu.
Kova alisema viungo hivyo vilichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Alisema jeshi hilo limefungua jalada la uchunguzi ili kujua sheria gani imevunjwa na kwa nini viungo hivyo vilitupwa hapo na kwa nini wasitumie utaratibu mzuri wa kuhifadhi na kwamba endapo kuna makosa ya kisheria, hatua zitachukuliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Muhimbili wapokea mabaki
Meneja Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema jana kuwa hospitali hiyo imepokea vifurushi 40 vyenye mabaki ya miili ya binadamu na kuhifadhiwa wakisubiri maelekezo ya polisi... “Hili ni suala la polisi, ninachoweza kusema ni kweli tumepokea vifurushi hivyo jana (juzi) usiku.”

IMTU yakiri kuhusika
Wakati Kova akisema hayo, uongozi wa IMTU ulikiri kuhusika na mabaki ya miili hiyo yaliyotupwa katika mto huo usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita.
Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho, Dk Fariji Mtango alisema jana kwamba anaamini miili hiyo inaweza kuwa ni ile iliyotoka katika chuo hicho, ambayo imekuwa ikifanyiwa mazoezi na wanafunzi kwa kuwa walihitaji kuiteketeza na walishatoa agizo hilo.

Alisema walitoa agizo kwamba mabaki hayo yapelekwe Muhimbili kwa mujibu wa utaratibu wao kwa kuwa hayakuwa na matumizi tena, kwa kuwa ndiyo sehemu yenye uwezo wa kuyateketeza na kutoa jukumu hilo kwa mmoja wa wakufunzi wa chuo hicho ambaye jana alikuwa safarini.

“Sasa zaidi hatujui kilichoendelea lakini tulipoangalia jana (Jumatatu) tulikuta sehemu yalipohifadhiwa imesafishwa, hivyo inawezekana ni sehemu ya vile vilivyoondolewa hapa. Hatukutarajia kwamba vingetupwa katika eneo lisilokuwa sahihi kama ilivyofanyika,” alisema.
Dk Mtango alisema hiyo ilikuwa moja ya hatua za kupisha wakaguzi ambao walitarajiwa kukuta maeneo yote ya kufundishia yakiwa katika hali ya usafi na unadhifu.
“Hawa wakaguzi wanapokuja wanatakiwa waone vitu vyote vikiwa sawa. Hata kama wangeona hayo mabaki ya miili ya binadamu isingekuwa tatizo, bahati nzuri wamekuja jana na wamefanya kazi yao vizuri,” alisema.
Muda mfupi baada ya kutolewa kauli hiyo, viongozi tisa wa chuo hicho na walinzi wawili walikamatwa mnamo saa 7.30 mchana na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay ambako wanashikiliwa, lakini baadaye Kova alisema waliokamatwa ni wanane.
Jana mchana eneo la chuo cha IMTU lilikuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi waliotanda kuanzia getini, mapokezi na kwenye bustani za chuo hicho na wengine waliovalia sare maarufu kama ‘tigo’ ambao walikuwa wakishika doria mbele ya chuo hicho.


Hatua kuchukuliwa
Dk Mtango alisema uongozi wa chuo hicho umeshtushwa na kutupwa kwa mabaki hayo katika utaratibu usiokubalika na utafanya uchunguzi na kuchukua hatua kwa wote waliohusika.
“Tunaanza na huyu ambaye tulimpa hili jukumu. Yeye ndiye aliyetakiwa kusimamia na anaujua wazi utaratibu wetu. Kwa sasa hajafika hapa na hata simu yake haipatikani. Tunaarifiwa kwamba amekwenda Zanzibar,” alisema.


Jinsi ilivyotokea
Juzi jioni, ilitokea taharuki baada ya wananchi kubaini viungo hivyo na taarifa kuanza kusambaa katika mitandao ya kijamii na baadaye vyombo vya habari na hadi jana mjadala kuhusu suala hilo ulikuwa mzito na wananchi wakihoji miili hiyo ni ya watu gani, imetoka wapi na imetupwa na watu gani.
Shuhuda wa tukio hilo, Mariam Nkumba alisema mara ya kwanza aliona mifuko yenye viungo hivyo Jumapili alipokwenda kuponda kokoto katika eneo hilo lakini hakubaini kulikuwa na nini.
Siku hiyo, Nkumba alisema aliondoka katika eneo hilo saa 12 jioni bila kujua nini kilikuwa ndani ya mifuko hiyo na siku iliyofuata (Jumatatu), alikwenda kuchukua mfuko mmoja ili ahifadhie kokoto zake, ndipo aliposhtuka kuona viungo vya binadamu.
“Mifuko ilikuwa mingi kweli, yote ilikuwa imejaa viungo vya binadamu. Mpaka sasa sijala na sina hamu ya kula. Ukiiona ile miili huwezi kula chakula,” alisema.
Mfanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya Skol iliyopo karibu na eneo hilo, Supery Kaijunga alisema mara alipopata taarifa kutoka kwa Nkumba alianza kutoa taarifa kwa wananchi wengine ili kwa pamoja wajue la kufanya.
Baadaye walitoa taarifa polisi ambao walifika saa mbili usiku na kukusanya mabaki yote na kuondoka nayo.
Hata hivyo, Kaijunga alieleza wasiwasi wake kuhusu wingi wa miili hiyo na kuhoji walikuwa watu gani na walitoka maeneo gani.

“Tukio hili siyo la kawaida na halijawahi kutokea huku kwetu. Tunakuwa na wasiwasi sana labda nasi maisha yetu yatachukuliwa kama hawa; polisi wafanye uchunguzi wa kina kubaini ukweli wake,” alisema Kaijunga.MWANANCHI

TOFAUTI ZA DINI ZISIWAGAWE WATANZANIA –MWINYI.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Karimjee kuhudhuria Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kushoto) kwa watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam. Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova (katikati) akifafanua jambo kwa viongozi wa mkoa wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema (kushoto) wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa huo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahmani Kinana wakijumuika katika Futari hiyo.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO. 

Rais mstaafu wa awamu ya pili , Ali Hassan Mwinyi ,amewataka watanzania kuwa makini kwa kutoruhusu tofauti za dini zilizopo hapa nchini kuwa chanzo cha mgawanyiko miongoni mwao.

Kauli hiyo ameitoa jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki kwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari hiyo amesema kuwa kila Mtanzania bila kujadili itikadi na dini aliyonayo ana wajibu wa kulinda na kutunza amani iliyopo kwa kuendelea kudumisha upendo na ukarimu kwa wenzake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyomo katika vitabu vitakatifu.

“Nawasihi Watanzania wenzangu tuendelee kupendana, tuwe wamoja katika kushirikiana, kamwe tusiruhusu wala kukubali mgawanyiko wa dini wala itikadi zetu” Amesisitiza.

Amewashukuru viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Saidi Meck Sadiki kwa uamuzi walioufanya wa kuandaa Futari iliyowaunganisha watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali bila kujadili itikadi na dini zao ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu walio nao.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza wakati wa Futari hiyo aliyowaandalia wageni hao amesema kuwa serikali ya mkoa inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ukarabati na ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya wakati wa msimu wa mvua jijini Dar es salaam.

Bw. Sadiki ameziagiza Halimashauri za Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni na Wakala wa Barabara (TANROAD) mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanarejesha hali ya kupitika kwa barabara iliyokuwepo mwanzo ili kuwaondolea kero ya usafiri wananchi.

Amezitaka mamlaka hizo kutumia fedha za ndani na zile zilizotolewa na Serikali Kuu kukamilisha ukarabati wa miundombinu hiyo yakiwemo madaraja yaliyosombwa na maji kwa muda muafaka ili kuruhusu magari kuweza kufika katika maeneo hayo.

Katika hatua nyingine Bw. Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kushiriki kikamilifu katika suala la usafi na uhifadhi wa mazingira kwa kujenga utaratibu wa kusafisha mazingira ya jiji ili kulinda heshima ya jiji huku akisisitiza kuwa dini zote zinamtaka mwanadamu awe mwadilifu na mwenye kuzingatia usafi.

Amezitaka mamlaka zinazosimamia utekelezaji wa sheria za kuhifadhi mazingira jijini Dar es salaam kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuhakikisha maeneo yote ya jiji yanaendelea kuwa katika hali ya usafi. Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum akuzungumza wakati wa Futari hiyo ameeleza kuwa viongozi wa dini na serikali kote nchini wanalo jukumu kubwa la kuwaongoza wananchi kutenda mema na kuendelea kuvumilia.

TRAFIKI & DEREVA USO KWA USO, JEKI MKONI


Trafiki akimdhibiti dereva wa gari dogo aina ya Toyota Pick up.
SEKESEKE la aina yake kati ya dereva wa gari dogo aina ya Toyota Pick up na trafiki ambao majina yao hayakujulikana mara moja liliibuka na kuzua maswali mengi kwa mashuhuda huku mambo ya rushwa yakitajwatajwa.  Tukio hilo lilizozua maswali mengi liliibuka, Bamaga, Mwenge jijini Dar jirani na kituo cha mafuta cha Bamaga.
Katika tukio hilo, dereva huyo na trafiki walikuwa wakikunjana, ambapo dereva alikuwa akilalamika kuonewa (Haikujulikana kivipi) wakati askari huyo wa usalama barabarani akisisitiza kuwa jamaa huyo alivunja sheria.


Gari aina ya 'Land Rover' (break down) lililotumika kuvuta gari la aina ya Toyota Pick up la dereva huyo.
 ILIKUWAJE?
Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers, kikiwa katika pitapita zake za kusaka matukio na kuhakikisha maadili hayavunjwi ndipo kilipokutana na kisanga hicho cha kushangaza.
Trafiki alisikika akimwambia dereva kuwa amevunja sheria za barabarani huku gari lake likiwa bovu hivyo aliamuru gari hilo kuvutwa hadi kituoni kwa ajili ya ukaguzi lakini dereva huyo alikataa.


...ilikuwa ni vigumu sana kwa dereva huyo kukubali gari lake kukamatwa.
 DEREVA
Pamoja na kuelezwa kuwa gari lake lilikuwa na matatizo na mahali alipoegesha hapakuwa sahihi, dereva huyo alipayuka: “Nawajua nyie trafiki, kazi yenu ni kuonea watu sasa mimi sitoi kitu hapa, labda mniue.“Siendi popote, mkiondoa gari nalala mbele yake ili mnigonge nife, mimi nimesema silitoi.”


...dereva akizidi kubisha kwa uamuzi uliochukuliwa na afisa usalama wa barabarani 'trafiki' 
 TRAFIKI
Trafiki huyo aliyeonekana kuwa makini na kazi yake, hakuwa na makuu, zaidi alitaka gari livutwe hadi kituoni huko sheria ingefuata mkondo wake baada ya ukaguzi.
 Mashuhuda wa tukio hilo, waliliambia Ijumaa kuwa, kilichohitajika ilikuwa ni busara ya masikilizano kuliko kuvutana kwa maneno na afisa wa polisi.



Afisa usalama wa barabarani akisisitiza kulichukua gari la dereva huyo kwa ukaguzi zaidi.
 “Sasa kama gari lake anajua ni zima, anabishana nini na polisi? Ikiwa anajiamini kuwa aliegesha sehemu sahihi, hofu yake ni nini? Kama kweli anajua yupo sawa, anatakiwa kukubali kwenda polisi, gari likakaguliwe. “Wakati mwingine unaweza kuwalaumu tu askari, kumbe ni tabia ya watu kukataa kutii sheria bila shuruti. Sasa anafikiri kwa maneno makali anayotoa kwa huyo askari atamwachia?

Raia wakishuhudia mkasa huo uliotokea katika kituo cha mabasi yaendayo Mwenge cha Bamaga.
 “Anasema eti hatoi kitu, kwani kaombw TWENZETa rushwa pale au anadhani kila trafiki anayemkamata dereva aliyevunja sheria anataka rushwa?” alisikika shuhuda mmoja akihoji kwa jazba.
Hata hivyo, pamoja na mkwara wa jamaa huyo, gari lake lilifanikiwa kuvutwa kuelekea polisi ambapo jamaa huyo alipanda gari lingine kulifuata.

700 pound Snake pulled out of Lake in North Carolina?

Giant 700 pound snake caught in lake in Proctor, North Carolina. The giant man eating python was measured at 98 feet long.
Police were contacted to see if there have been any recently filed missing person reports as a snake this big could have surely eaten a human.

Giant Snake Found in American Lake?

This giant snake is massive and just gorgeous, but it didn’t take long to find out that the STORY behind it… was fake, just another hoax.
While the image is indeed real, I think the size of the giant snake could have been exaggerated due to the camera angle
Nevertheless, this snake is still huge, but where did it come from? The markings on it’s skin looks similar to that of a reticulated python native to Southeast Asia.
After playing around with a little Google translate, the mystery was finally solved.
giant-snake
Looks like a type of Boa.. Red-tail boa perhaps?
This giant python came from Indonesia and after some rough translating, it turns out that it was discovered this last Thanksgiving near the village of Belinyu City.
It was found by accident by a group of construction workers who severely injured the reptile while knocking down a large dead tree in which the python was sleeping inside of.
The workers put the dying snake out of it’s misery and buried it.
It’s sad to see such an incredible animal killed, especially one that could have been a new world record size. I wish there were more pictures so we could get a better idea of just how large it was.

WATANZANIA KUTIBIWA KITEKNOLOGIA ZAIDI

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Ceragem, Africa Mashariki, Nam Chae Woo,(kulia) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Dafa Ceragem, Edmund Mndolwa jinsi mashine mpya ya Ceragem V3 inavyofanya kazi , wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo inayotumia teknolojia ya hali ya juu katika kutibu magonjwa mbalimbali bila ya mgonjwa kumeza dawa au kuchomwa sindano katika vituo vya Dafa Ceragem vilivyopo sehemu mbalimbali hapa nchini . Anaeshuhudia ni Patricia Mndolwa.
 Mzee Fransis Kavishe na Bi Ashura Salum,wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kansa wakifunua kitambaa, kuashiria uzinduzi wa Mashine mpya ya Ceragem V3  inayotumia teknolojia ya hali ya juu katika kutibu magonjwa mbalimbali bila ya mgonjwa kumeza dawa au kuchomwa sindano katika vituo vya Dafa Ceragem vilivyopo sehemu mbalimbali hapa nchini,pamoja nao katika picha ni Mkurugenzi wa Dafa Ceragem, Edmund Mndolwa,Mkurugenzi wa Kampuni ya Ceragem, Africa Mashariki, Nam Chae Woo, na Patricia Mndolwa.
 Mzee Fransis Kavishe na Bi Ashura Salum,wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kansa wakikata utepe, kuashiria uzinduzi wa Mashine mpya ya Ceragem V3 inayotumia teknolojia ya hali ya juu katika kutibu magonjwa mbalimbali bila kumeza dawa wala kuchomwa sindano katika vituo vya Dafa Ceragem vilivyopo sehemu mbalimbali hapa nchini,Pamoja nao katika picha ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ceragem, Africa Mashariki, Nam Chae Woo, Mkurugenzi wa Dafa Ceragem, Edmund Mndolwa.
 Baadhi ya Wagonjwa na wafanyakazi wa Kampuni ya Ceragem, Africa Mashariki wakifuatilia hotuba ya Uzinduzi waMashine mpya ya Ceragem V3  inayotumia teknolojia ya hali ya juu katika kutibu magonjwa mbalimbali bila ya mgonjwa kumeza dawa au kuchomwa sindano katika vituo vya Dafa Ceragem vilivyopo sehemu mbalimbali nchini.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Ceragem, Africa Mashariki, Nam Chae Woo, akizungumza na baadhi ya wagonjwa na wafanyakazi wa Dafa Ceragem wakati wa Uzinduzi wa Ceragem V3 inayotumia Teknoloji ya hali ya juu katika kutibu Magonjwa mbalimbali bila kumeza dawa wala kuchomwa sindano katika vituo vya Dafa Ceragem vilivyopo sehemu mbalimbali hapa nchini.Katika picha kutoka kushoto, Patricia Mndolwa,  Mkurugenzi wa Dafa Ceragem, Edmund Mndolwa, na Mgeni Mualikwa Bi. Lydia Mushumbusi.

WAZIRI WA BIASHARA VIWANDA, NA MASOKO ZANZIBAR AZUNGUMZA NA WANAHABARI KUHUSU UZINDUZI WA MPANGO WA ELIMU KWA WANANCHI

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akijibu maswali ya wandishi wa Habari (hawapo pichani), kulia Naibu Waziri wake Thuwaiba Edington Kisasi na (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Julian Raphael.
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Julian Raphael akimkaribisha Waziri Mazrui (hayupo pichani) azungumze na wandishi wa Habari katika sherehe ya uzinduzi wa mpango wa elimu kwa wananchi kuhusu kuanzishwa kwa Sheria ya Biashara Zanzibar No. 14 ya mwaka 2013 katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na wandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa mpango wa elimu kwa wananchi kuhusu kuanzishwa kwa sheria ya Biashara Zanzibar No. 14 ya mwaka 2013. Sherehe hiyo imefanyika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
Mwandishi wa Habari Abdallah Pandu wa Star tv akiuliza swali juu ya uanzishwaji wa sheria hiyo.
Baadhi ya wandishi wa Habari waliofika katka sherehe ya uzinduzi wa mpango wa elimu kwa wananchi kuhusu kuanzishwa kwa sheria ya Biashara Zanzibar No. 14 ya mwaka 2013 wakifuatilia maelezo ya Waziri Mazrui (hayupo pichani) Sherehe hiyo iliofanyika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar . (Picha na Makame Mshenga -Maelezo Zanzibar).

REGGAE AMBASSODOR JHIKOMAN AFUNIKA KWA KISHINDO ONYESHO LA 5th INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN,UJERUMANI

Tubingen,Ujerumani,

Mfalme  wa muziki wa reggae barani Afrika Jhikoman alifanikiwa kufunika kwa kishindo kikubwa katika maonyesho ya 5th International African festival Tubingen,  siku ya jumapili 20 julai 2014 mjini Tubingen,Ujerumani.
 
Katika maonyesho hayo mwanamuziki Jhikoman kwa sasa ndiye nyota inayong'aa kutoka Afrika katika muziki wa reggae aliuthiirishia ulimwengu kuwa Tanzania ni moto wa kuotea mbali kimuziki ,akishagiliwa na umati wa maelefu ya washabiki waliofika katika maonyesho Jhikoman anatajwa ndie mfalme na nyota mpya ya muziki wa reggae kutoka Afrika,Jhikoman mwenye maskani yake Bagamoyo mkoani Pwani,Tanzania amepata bahati ya kukubalika na kupata mkataba na kutumbuiza katika maonyesho mengi barani ulaya.
 
(picha kwa niaba ya Afrika Festival Tubingen)