Mkurugenzi Mkuu wa Nawina Resort ya Mbagala jijini Dar es Salaam, amesema kuwa wakazi wa mbagala kuu mwanzoni mwa mwezi wa kumi na moja kutatelemshwa shoo kabambe ya muziki wa Dansi chini ya vijana watatu(Mapacha) chini ya Mwanamuziki nyota Khalid Chokolaa.
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mama Komba amesema kuwa huo ni mwanzo tu isipokuwa kutakuwa kukifanyika maonyesho mbalimbali ikiwa ni kuwaweka sawa vijana na wakazi wa maeneo hayo ili kusaidia kupunguza ongezeko la vijana kukaa vijiweni.
"Utaratibu huu ilikuwa uanze siku nyingi, isipokuwa niliamua kusitisha kwanza kupisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, na pengine niseme kuwa sasa wakati umewadia hivyo natamka rasmi kuwa Ukumbi wa NAWINA RESORT ni kwa ajili ya wakazi wa Mbagala na Maeneo ya jirani, hivyo karibuni katika matamasha na shoo zote zitakazoandaliwa hapa NAWINA" amesema mama Komba
Ukumbi huo ambao kwa namna moja ni wa kisasa pia zinapatikana Huduma Mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vyakula, Vyumba kwa ajili ya kupumzika wageni, huku kukiwa na maonyesho ya mikanda mbalimbali ya CINEMA pamoja na matukio ya LIVE yanayopatikana kupitia mitandao ya DSTV na STAR TIME.
Burudani hizo ambazo zitakuwa zikifanyika katika kumbi za NAWINA RESORT iliyoko Mbagala na ule wa NIT CLUB ulipo Mabibo kwenye Chuo cha Usafirishaji jijini Dar es Salaam.
Mwisho kabisa amewatakia na kuwapa pole wote waliopatwa na ajali ya MV-SPICE iliyotokea Zanzibar .