Ibla Joldan(katikati) akiwa na kaka zake ambao pia ni wakazi wa Mji wa mwanza
|
Ibla Joldan akiwa kwenye moja ya maonyesho yake wakati wa hafla za mji wa Mwanza hivi karibuni | |
|
Ibla Joldan akiwa katika pozi Mjini Shinyanga, alizaliwa katika jiji la Mwanza miaka kumi na saba iliyopita(17) akiwa ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia yenye watoto Watatu, yeye pamoja na wadogo zake Omary Komba, Abubakari Komba,Elimu yake ya Msingi alipata katika Shule ya Nyakato iliyopo jijini Mwanza na kuhitimu katika mwaka wa 2012, ambapo akiwa katika shuke hiyo anasema ndipo alipoanza kufanya shuguli ya uigizaji baada ya kujikuta na kipaji kikubwa cha fani hiyo," nilijikuta nikipenda kuigiza baada ya kufurahishwa na Shalomilionea, Mzee Majuto, Kinyambe, na wengine wengi, " nilipozungumzia matarajio yake alisema kuwa ni kuwa msanii Mkubwa ambaye ataisaidia Tanzania na Mji wa Mwanza kwa Ujumla. "napenda siku moja niweze kuwa kivutio kikubwa sana katika Nchi yangu ya Tanzania, Ususani Mkoa wangu wa Mwanza, kwani siku zote nina ndoto ya kuwa Mmoja wa wasanii Wakubwa. Kuhusu wazazi wake na Sanaa yake ya Uigizaji Ibla anasema kwamba" kwangu siyo tatizo kwani wazazi wangu pia wanapenda kuniendeleza katika sanaa hii ya Uigizaji, zaidi nampenda sana baba Yangu Dkt. Komba ambaye siku zote ananipa msaada mkubwa ninapokwama, ni tofauti kabisa na wazazi wengi ambao wanawazuia vijana wao kujiendeleza katika Vipaji vyao, ila mimi kweli baba yangu namshukuru sana ana mambo ya wazee wengine, utakuta mzee anamzuia kijana kufanya shuguli kama hizi kisa eti ni uhuni, nani kasema uigizaji ni uhuni? pia hata mama yangu Bi. Fatma Komba, siku zote ananishauri kujiendeleza.aidha anawashauri wazazi kuwaruhusu vijana wao kufanya fani wazipendazo kwani Ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa sayansi na Teknolojia, ambapo kuna mabadiliko mengi ya mifumo ya utafutaji katika mafanikio. lakini pia anaomba wadau Wakubwa wa Sanaa kumuunga Mkono ikiwa ni pamoja na kumshirikisha wakati wa Uigizaji, Watu ama makampuni kumpa sapoti ya mialiko wakati wa matamasha yao Popote.kingine ni Misaada ya Udhamini kwa ajili ya kuwezeshwa kipato kwa ajili ya kufanya maanadalizi ya kazi zake za Sanaa, Ibla anasema kuwa matarajio kwa mwaka huu wa 2013 ni kuingia katika sokom la Filamu(Cinema) ambayo kwa sasa anafanya Mipango ya Kushiriki kwenye Sinema kadhaa za Mkoa wa Mwanza ikiwa ni pamoja na Filamu za Mazingira na nyinginezo nyingi.aidha ibla naomba kwa yeyote atakayemuitaji kwa mawasiliano +255-769-11-77-09 | | |
| | |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
|
|