Na Hassan Silayo na Lorietha Laurence
…………………………………………………….
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete anatarajia kufungu
a mkutano wa Kilimo wa Umoja wa Nchi za Kusini mwa Africa, utakaofanyika tarehe 13 hadi 14 Mei mwaka huu .
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkutano wa Vyama vya Kilimo vya
Kusini mwa Afrika (SACAU), Ishmael Sunga wakati akiongea na waandishi
wa habari kuhusu mkutano huo utakao fanyika katika hoteli ya White sands
iliyopo jijini Dare s salaam.
Alisema kuwa kipaumbele katika kipindi hiki ni kupambana na changamoto ya kilimo,na usalama wa chakula ili kufanya sekta ya kilimo kukua , kustawi na kufanya kilimo kuwa biashara badala ya kufikiri katika kuondoa umaskini.
Alisema kuwa kipaumbele katika kipindi hiki ni kupambana na changamoto ya kilimo,na usalama wa chakula ili kufanya sekta ya kilimo kukua , kustawi na kufanya kilimo kuwa biashara badala ya kufikiri katika kuondoa umaskini.
“Lengo
litakuwa ni kubadilisha mtazamo wa watu kuwa, kilimo ni kwa ajili ya
kumfanya mkulima ajikimu mahitaji ya kawaida na kuondoa umaskini, bali
ni kumfanya mkulima kupata faida na kutajirika kupitia kilimo katika
ngazi zote za kilimo”, alisema Sangu.
Aliongeza
kuwa mkutano huo una malengo ya kuwasaidia na kuwaongezea nguvu
wakulima pamoja na kutoa taarifa za kilimo kwa wadau wa sekta hiyo kwa
niaba ya wakulima wote wanachama wa umoja huo ili kuleta tija katika
sekta hiyo muhimu ya kilimo.
Naye
Mkurugenzi wa Baraza la Kilimo Tanzania Janet Bitegeko alisema baada ya
mkutano huo washiriki watapata fursa ya kutembelea wakulima wa mpunga
katika kijiji cha Bagamoyo ili kujionea changamoto na nini wakulima hao
wanafanya na kutoa ushauri ili kuweza kuboresha zaidi zao hilo.
Janet aliongeza kuwa umoja huo utatoa taarifa za utekelezaji za mwaka pamoja na kufanya ukaguzi wa hesabu za mwaka za umoja huo.
Mkutano
huo utahudhuriwa na washiriki kutoka nchi 14 wakiwemo wakurugenzi na
wenyeviti kutoka nchi za kusini mwa afrika, wawakilishi zaidi ya 10 wa
muungano wa wakulima pamoja na taasisi za kifedha.
Kauli
mbiu ya mkutano huo ni kusaidia kilimo cha biashara na maendeleo ya
biashara yanayolenga mkakati maendeleo ya kilimo katika nchi za kusini
mwa afrika, ambapo waziri wa kilimo wa Nigeria atatoa kauli.
No comments:
Post a Comment