
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Jimbo la Lindi Mjini, Salum Baruany amewashauri watu waliowahi kusoma katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania kushirikiana katika kufanikisha tamasha la kuchangia maendeleo ya elimu kwa ajili ya mikoa hiyo.
Baruany aliyasema hayo juzi katika kikao cha maandalizi ya tamasha la kuchangia maendeleo ya elimu kwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kilichofanyika Ukumbi wa Imasco, Temeke jijini Dar es Salaam.
Akiwa mmoja wa waalikwa wa vikao hivyo vya kila wiki, Baruany alielezea kukunwa kwake na ubunifu wa baadhi ya wanafunzi walioamua kuwahamasisha wenzao kukumbuka walikotoka kielimu, kwa lengo la kuwainua wengine.
“Nawapongeza sana. Ni wachache wanaoweza kukumbuka walikotoka, hasa kielimu. Hapa mmelenga, mikoa ya kusini iko nyuma kielimu, naamini wa kusaidia kupandisha hadhi ni ninyi wenyewe mliosoma kule na wadau wengine wanaoguswa na suala hili.
“Msikate tamaa, mtafanikiwa. Cha msingi ni kuwashirikisha na kuwashawishi wengine waliosoma ana kuwa karibu na mazingira ya kielimu ya mikoa hii. Nchi hujengwa na wananchi wenye moyo, nanyi kwa kuguswa kwenu, naamini elimu ya kusini itainuka kwa sababu ni vigumu mtu mmoja mmoja kuchangia na bado maendeleo ya kweli yakaonekana, bali kupitia mshikamano kama wenu,” alisema mbunge huyo.
Naye Mratibu wa tamasha hilo, Asanterabbi Mtaki, licha ya kumshukuru mbunge huyo kwa nasaha zake, aliwataka wadau wa elimu nchini kuungana na waliosoma mikoa ya kusini ili kufanikisha azma ya kuiinua kusini kielimu.
“Tangu awali tumeelezea hali ya elimu ya mikoa ya Kusini, kwa kweli si nzuri na inahitajika nguvu ya ziada, ndiyo maana tumeungana kuhakikisha tunafanikisha kitu kwa ajili ya shule za kusini na wanafunzi wake, hasa yatima, walemavu na wasiojiweza ili wapate haki ya kupata elimu bora,” alisema Mtaki.
Alisisitiza kuwa, kasi ya maandalizi ya tamasha hilo inaridhisha na kuongeza kuwa, nafasi ya waliosoma kusini kuchangia mawazo bado ipo, hasa kupitia vikao vya kila mwisho wa wiki vinavyofanyika ukumbi wa Imasco.

Na Gladness Mushi, Arusha Taasisi ya maendeleo ya jamii hapa nchini (CDTF) imefanikiwa kutoa msaada wa kimaendeleo, ambapo imechangia zaidi ya milioni 43 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili pamoja na ofisi ya walimu wa shule ya walemavu iliopo katika eneo la Ilboru Mjini hapa Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi vyumba hivyo vya madarasa pamoja na ofisi ya walimu ambayo itatumika kwa watoto hao ambao ni walemavu Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bw Hendry Mgingi alisema kuwa watoto ambao ni walemavu kwa kuwa nao wana nafasi kubwa sana ndani ya jamii ya watanzania aidha aliendelea kusema kuwa wao kama taasisi ya maendeleo wamefikia uamuzi huo mara baada ya kuona kuwa watoto ambao ni walemavu wana nafasi kubwa sana ya kuweza kusaidika hata kama wanaulemavu wa aina mbalimbali. aliongeza kuwa kama jamii ya watanzania itaweza kuwasaidia watoto hao ambao ni walemavu basi wataweza kufanya hata idadi ya wanafunzi ambao wana ujuzi mbalimbali kuongezeka kwa hali ya juu sana hapa nchini. "unajua endapo kama baadhi ya taasisi zitaweza kuona mchango ambao wanao hawa watoto walemavu basi hawa watoto wataweza kukua kwa kiwango cha hali ya juu sana na hata kama hawataweza kufanya kazi ngumu basi wanaweza kufanya kazi ambao ni raisi na hivvyo kusaidia jamii katika kutatua tatizo la ajira"aliongeza Bw Hendry hataivyo alisema kuwa walemavu wanaweza kuibua mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuweza kutengeneza ajira ambazo zimo kwenye jamii kwa kuwa mpaka sasa baadhi ya walemavu wameonekana kuwa wabunifu wa hali ya juu sana. alisisitiza kuwa ubunifu huo ambao wanao baadhi ya walemavu utaenda sanjari na upokeaji wa vipaji kutoka kwa walemavu hao ambapo kama jamii ya leo itaweza kuwasaidia ni wazi kuwa kazi mbalimbali za walemavu zitakubalika na jamii ya watanzania. 'leo kuna baadhi ya walemavu ambao wapo tu lakini cha ajabu ni kwamba bado hawajaweza kusaidika lakini huu ndio wakati muafaka wa kila mwananchi kuweza kuwasaidia hawa walemavu kwa kuwa kwa kutowasaidia basi asilimia kubwa ya walemavu hao wanashindwa kutimiza ndoto za kuondokana na umaskini"alisema Bw Hendry. Alimalizia kwa kusema kuwa walemavu hao wanatakiwa kuhakikisha kuwa elimu ambayo wanapata wanaitumia vema katika kazi zao na masomo kwa kuwa ili napo waweze kufanikiwa ni lazima kwanza kuwepo na mipango mikakati ya elimu bora.
Maandali ya kuujenga Mkoa mpya wa Njombe
Jamii maskini kwa kawaida huwa na vipaumbele vingi. Matokeo yake ni kushindwa kuvitekeleza. Wananchi wa mkoa mpya wa Njombe ambao ni wachapa kazi kweli kweli wameikataa falsafa hiyo na wamejiwekea vipaumbele vichache na vya uhakika ili kuujenga mkoa wao. Vipaumbe vya wananjombe ni:
1. Elimu- Kwa kujitolea wananchi wa vijiji na kata za Katulila, Madobole, Miva, Lusitu, Mtila, Mbega, Matola, Luponde, Itulike, Ramadhani, Kihesa, Utalingolo, Ihalula, Nolle, Mamongoro, Makowo, Ng’elamo, Yakobi, Igominyi, Idunda, Idihani, Lugenge na Kiyaula wameamua kujikita katika suala zima la elimu kwa shule za awali, msingi na sekondari. Majenfo mzuri ya ya kisasa yako katika hatua mbali mbali. Ombi lao ni waalimu wa kutosha.
2. Afya: Ili kuimarisha afya wananchi hao wako katika mpango wa kuwa na zahanati katika kila kata. Tayari kwa kujitolea wameanza ujenzi wa zahanati hizo. Ombi lao ni kupatiwa wauguzi wa kutosha.
3. Kilimo: kutokana na hali ya hewa nzuri ya nyanda za juu kusini, wananjombe hawa wamejizatiti katika kilimo cha chai, mahindi, viazi mviringo na misitu ya mbao.
4. Miundombinu: kwa sehemu kubwa wananjombe wamejitahidi sana kutengeneza barabara za ndani na wanaamini ni kwa barabara nzuri wataweza kufaidika na fursa zitokanazo na migodi ya machimbo ya chuma na mkaa wa mawe ya Mchuchuma na Liganga

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein jana amefanya uteuzi wa nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee Rais amewateuwa Sheikh Saleh Omar Kabhi kuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar,Sheikh Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar ambapo Sheikh Hassan Othman Ngwali kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.
Aidha Dk Shein amemteuwa Muumin Khamis Kombo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Zanzibar,Khalifa Hassan Choum kuwa Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo Zanzibar, Abdulrahman Mwinyi Jumbe kuwa Mshauri wa Rais Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi .Pia Mwinyi Jumbe ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar.
Vile vile Rais amewateuwa Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa kuwa Mshauri wake katika mambo ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uwekezaji. Ramia aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Sweden na India pia alikamata nafasi mbali mbali za Uwaziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Burhani Saadati Haji ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makaazi. Kabla ya Uteuzi huo Burhani aliwahi kuwa Waziri wa Kilimo pia Waziri wa Ardhi,Maji na Nishati.Pia Dk Shein amemteuwa Issa Ahmed Othman kuwa Mshauri wa Rais Utalii. Issa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza juzi

Hatimaye lile shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Mara katika maswala ya utalii, litafanyika Ijumaa ya tarehe 07/10/2011, katika ukumbi wa Bwalo la Magereza mjini Musoma, ambapo takriban warembo 15 watapanda jukwaa moja kuchuana kumpata muakilishi wa mkoa katika mashindano yan Miss Tourism Lake Zone yatakayofanyika baadae mwezi december. Kampuni ya Stoppers Entertainment inayoandaa mashindano hayo, imejipanga kuyapa hadhi mashindano hayo ambapo warembo mbali na kupita jukwaani, watashiriki katika shughuli za kijamii, kuimba na kucheza ngoma za makabila ya mkoa wa Mara. Hata hivyo waandaji wamewaomba wadhamini kuendelea kujitokeza kudhamini shindano hilo, kutokana na kugusa utalii, utamaduni na uchumi wa nchi yetu, yote kwa minaajili ya kuitangaza Tanzania. Shindano la Miss Tourism Mara 2011, litasindikizwa na burudani kutoka kwa Ditto na Linah wote kutoka jumba la vipaji THT. Pia burudani za ngoma za asili zitakuwepo.
Na Mwandishi wetu
TIMU ya Leaders Club imeisambaratisha timu ya Bongo Movie bao 1-0 katika mchezo maalum wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Leaders Club jana.
Mchezo huo ulikuwa mkali na wa kusisimua kutokana na wachezaji wote kuonyesha viwango vya hali ya juu.
Leaders Club ikiongozwa na Doyi Moke, Adam Sapi, Christopher Semi, Baraka, Makoye, Juma Pinto, Idd Janguo, Abdul Tall, Michael, Kibwana Matephone na Charles Nyarusi walitawala mchezo huo ambao ulivuta mashabiki wengi kutoka kona mbali mbali za jiji.
Bongo Movie iliongozwa na Jacob Steve, (JB), Masoud Bitebo, Steven Nyerere na Vincent Kigosi ‘Ray’ ilishindwa kumudu kasi ya timu ya Leaders.
Baada ya kosa kosa nyingi, Leaders Club ilipachika bao la ushindi kupitia kwa Juma Tall kufutia ushirikiano mzuri na Adam Sapi na Juma Pinto.
Bao hilo liliwachangaya zaidi Bongo Movie ambao walipoteza ‘network’ uwanjani na kuanza kumvamia mwamuzi kila wakati wanapocheza faulo.
Tofauti na mchezo wa soka, mchezo huo ulionekana kuwa wa upande mmoja zaidi kutokana na uwezo mkubwa wa Leaders Club.
Baada ya mchezo, timu ya Bongo Movie iliondoka mapema uwanjani hapo tofauti na awali kwani mara kadhaa huwa wanadumu uwanjani hapo kwa vinywaji na vitafunwa vingine.

Na mwandishi wetu

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WIZARA YA Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imejipanga kwa makini ili kuhakikisha kuwa maeneo yote ya wazi yanarudishwa kwa wananchi ambapo matumizi yake yatakuwa kwa manufaa ya watanzania wote.
Aidha wizara hiyo imesema kuwa itatoa muda maalum kwa watu wote walivamia maeneo hayo kuondoka wenyewe na utakapokwisha muda uliopangwa itakuja kubomoa hivyo hakutakuwa na msamaha.(hakuna cha msalie mtume).
Kauli hiyo ilitolewa (leo) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Maliasili na Mazingira, Abdulkarim Shah, wakati akifunga maonesho ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ya wizara hiyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa, Mnazimmoja, jijini Dares Salaam.
Shah alitoa kauli hiyo ikiwa ni matazamio ya miaka 50 ijayo ya wizara hiyo huku akisema maeneo hayo yamepangwa kwa faida ya wananchi wote.
“Napenda kusisitiza kwamba taaluma ya upangaji miji inahitajika kutiliwa maanani na serikali haitakubali mipango hiyo kubadilishwa matumizi kiholela. Natoa rai hii kwa jamii kushirikiana na serikali kulinda maeneo ya wazi yaliyoko katika maeneo yao,” alisema Shah.
Aliwataka watendaji husika hasa wa halimashauri kutobalidilisha matumizi ya ardhi .
Aliongeza kuwa wizara hiyo imeandaa mikakati ya kuwa na mipango shahidi ya uendelezaji miji itakayokidhi mahitaji ya idadi kubwa zaidi ya watu watakaoishi mijini.
Pia kuwa na mipango itakayowezesha ujenzi wa miji nadhifu, ya kisasa na endelevu,kuzijengea uwezo halimashauri kusimamia na kudhibiti uendelezaji wa miji na kuwa na mipango ya matumizi ya ardhi kwa kila eneo la makazi nchini.
“ Wizara imedhamiria kuongeza kasi ya upimaji wa ardhi nchini kwa matumizi mbalimbali pamoja na kupunguza gharama za upimaji, ambapo nchi itakuwa imejenga kituo cha kupokea na kusambaza picha za saltillite, vituo vingi zaidi cha upimaji vitajengwa,” alisema.
Makamu Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa wizara hiyo itaanza kutunza kumbukumbu za upimaji na ramani kwa kutumia teknolojia ya kisasa, ambapo sasa inatumika mikoa 15 baadae itakuwa mikoa yote hadi wilayani kulingana na uwezo wa bajeti.
Alisema ili kuwawezesha wananchi kutumia ardhi kama mtaji wizara itahakikisha kuwa mashamba ya wananchi vijijini kote nchini yanabainishwa yanapimwa na wamiliki wake wanapewa hatimiliki za kimila.
Alisema kwa upande wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) limejipanga kujenga nyumba 150,000 katika kipindi cha miaka 50 ijayo na kujenga nyumba kwa ubia kwa kuwashirikisha wawekezaji wengine.

akiondoka New York kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya Marekani ambapo alihudhuria mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa na wa Diapora jijini New York na Virginia, Washington DC.
Picha na Ikulu

akiondoka New York kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya Marekani ambapo alihudhuria mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa na wa Diapora jijini New York na Virginia, Washington DC.
IMBA YASHINDA 1-0 DHIDI YA MTIBWA SUGAR YA MANUNGU


