TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, November 1, 2014
CCM YAVUNA MAVUNO YAKE KUTOKA CHADEMA NGORONGORO
Na Gladness Mushi, Ngorongoro
CHAMA cha Mapinduzi, CCM, kimezidi kujiimarisha baada ya
kukisambaratisha Chama cha Chadema wilayani Ngorongoro, kufuatia hatua
ya mwenyekiti wake ,Revocatus Parapara,na viongozi wa kata na matawi
kubwaga manyanga na kujiunga CCM.
Tukio hilo limetokea jana kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha
Mapinduzi, uliokuwa ukihutubiwa na Katibu wa CCM, mkoa, Alphonce
Kinamhala,aliyekuwa kwenye ziara ya kujitambulisha kwa wananchi
uliofanyika kijiji cha Waso wilayani Ngorongoro, na viongozi hao
kujiunga rasmi na Chama cha mapinduzi.
Akihutubia mkutano huo , Katibu wa CCM, Kinamhala, amewataka madiwani wasijiingize kwenye uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa na badala yake wawaache wananchi wachague viongozi wawatakao .
Amewataka madiwani kutokujiingiza kwenye Zabuni mbalimbali za
serikali kazi zao ni kusimamia wakandarasi ili kuhakikisha miradi
yote inayotekelezwa kwenye vijiji na kata inatekelezwa kwa kiwango
kinachotakiwa.
Amesema hasara ni kubwa iwapo wao watajiingiza kwenye Zabuni
watashindwa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo na mradi usipotekelezwa kwa kiwango na muda wake serikali na Chamna cha
mapinduzi ndio watakaonyoshewa vidole na kulaumiwa na wao watashindwa kutetea na huko ni kukiuka majukumu yao.
.Kuhusu mchakato wa KATIBA, Katibu Kinamhala, amewaambia wananchi
wasikubali kudanganywa kwamba mchakato huo uliporwa na CCM, Katiba
hiyo sio ya Chama cha Mapinduzi, bali ni ya wananchi na ndio maana
imepitishwa kwenye bunge la katiba maalum, Na CCM, haijawa
Awali katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, CCM, mkoa wa Arusha, Joseph Izack ,amewataka wanaotaka kuvuruga amani ya nchi hii kwa kisingizio cha siasa kuacha mara moja vinginevyo watashughulikiwa kokote pale walipo.
Ameongeza kuwa katiba inatoa fursa kwa wanawake kugombea uongozi
ngazi mbalimbali ambapo sasa wanayo nafasi ya 50 kwa 50 kila nafasi
ya uongozi na haya ni mafanikio makubwa .
MFUKO WA WANAFUNZI WALIOHITIMU SHULE KONGWE ILBORU WATARAJIA KUTUMIA ZAIDI YA MILIONI 20 KUKARABATI MAJENGO
Na Gladness Mushi,Arusha
MFUKO wa wanafunzi waliohitimu zamani katika shule kongwe ya vipaji
maalum ya Ilboru(Ilboru Alumni Foundation)wanatarajia kutumia kiasi
cha zaidi ya shilingi milioni 20 hadi ifikapo desemba mwaka huu kwa
ajili ya kukarabati majengo ya shule hiyo ili kuweza kuirejesha
katika mazingira mazuri .
Aidha kwa sasa shule hiyo pamoja na kuwa ni ya vipaji maaluma lakini
mazingira yake hayako katika hali nzuri hali ambayo iliwafanya
wanafunzi hao waliomaliza miaka ya nyuma kuungana ili kuikarabati na
kuirejeshea mzingira yake ya miaka ya nyuma kwa lkuwa mazingira mabaya yanachangia kufelisha wanafunzi.
Hayo yalisemwa na mtendaji mkuu katika mfuko huo ambaye ni dr Daniel
Maro alipokuwa akikabidhi rasmi funguo za darasa moja lililomalizika
kukarabatiwa katika mahafali ya 25 ya kidato cha nne ya shule hiyo
ambapo darasa hilo limegharimu kiasi cha zaidi ya milioni 4 .
Dr Maro alisema kuwa shule hiyo imekuwa ikizalisha wataalamu mbali
mbali sana lakini bado ina changamoto nyingi ambazo zinawahitaji wadau wa elimu kuziunga mkono ili kuhakikisha kuwa watoto wanasomea katika mazingira mazuri.
“sisi tumeungana kwa pamoja tuliosoma kwa kipindi cha kuanzia 1999
katika kuhakikisha kuwa tunarejesha mzingira ya nyuma kwani mazingira ya sasa nay a kipindi tulichokuwa tunasoma yalikuwa ni tofauti sana na mzingira mabaya yanasababisha hata watoto kutosoma vizuri”aliongeza dr Maro.
Alifafanua kuwa hadi sasa wameshafanikiwa kukarabati darasa moja na
wana mpango wa kuendelea na madarasa mengine manne ambayo kila moja
litagharimu zaidi ya milioni nne ambapo wanatarajia hadi ifikapo
desemba wawe wameshakamilisha mchakato wa kukarabato majengo hayo
ambayo yamekuwa chakavu mno.
Aidha dr Maro alisema kuwa mara baada ya kumaliza kukarabati majengo
hayo bado wataendelea kutatua changamoto nyinginzo zinazoikabili shule hiyo huku akiwataka wale wote waliomaliza katika shule
KULUVYA UNITED YAIFUNGA SINZA STAR 3-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI YA MICHUANO YA DK. MWAKA SPORTS EXTRA NDONDO CUP 2014
Kikosi cha Kiluvya United kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi kamili cha timu ya Snza Star kikiwa katika picha ya pamoja.
Beki
wa tmu ya Kiluvya United, Mwita Enoshi (kushoto) akiwania mpira na
mshambuliaji wa Sinza Stars katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports
Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi
Makurumla Dar es Salaam. Kiluvya ilishinda 3-0 na kutinga hatua ya robo
fainali ya mchuano hiyo.
Mshambuliaji
wa timu ya Kiluvya United, Haji Zege (kushoto) akichuana na beki wa
Sinza Stars Charles Kaembe katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports
Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi
Makurumla Dar es Salaam. Kiluvya ilishinda 3-0 na kutinga hatua ya robo
fainali ya mchuano hiyo.
Kikosi
cha Kiluvya United kikifanya mazoezi mepesi kabla ya mechi yao ya Ligi
ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 katika Uwanja wa Makurumla
dhidi ya Sinza Star. Kiluvya United ilishinda 3-0.
Kikosi cha Kiluvya United kikifanya mazoezi mepesi kabla ya mechi yao na Sinza Star. Kiluvya United ilishinda 3-0.
Wachezaji wa Sinza Star wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mchezo wao na Kiluvya United.
Wachezaji
wa Kiluvya United wakisalimiana na wachezaji wa Sinza Stara kabla ya
mchezo wao wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Dk. Mwaka Sports Extra
Ndondo Cup 2014 uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Makurumla
jijini Dar es Salaam. Kiluvya United ilishinda 3-0 na kuingia hatua ya
robo fainali ya michuano hiyo.
Baraza l;a madiwani laitaka REA kukamilisha umeme kwa wakati
BARAZA la madiwani wa halmashauri ya Arusha limemtaka wakala wa
usambazaji wa umeme vijijini (REA)kuhakikisha kuwa vijiji vyote
vilivyoko kwenye mpango wa kupatiwa umeme vinapata kwa wakati kwani
kwa sasa mashimo yalichimbwa yanahatarisha maisha ya wananchi.
Mbali na baraza hilo kuwataka REA kufikisha umeme kwa wakati vijijini
lakini pia wanatakiwa kuifanya jamii iweze kuwakubali tofauti na sasa ambapo wamechimba mashimo ya kusimamamishia nguzo na wameyaaacha.
Akiongea na katika baraza hilo la madiwani lililofanyika
jana mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Saimon Saningo alisema kuwa
ni muda mrefu sasa umepita toka wakala hao wachimbe mashimo na
kuyaacha kama yalivyo jambo ambalo limewafanya wananchi kubaki na
malalamiko.
Amedai kuwa,mashimo hayo yanahatarisha sana maisha ya wananchi lakini pia hata mifugo ambayo ipo vijijini humo na kwa hali hiyo wananchi wamebaki wakiwa na manunguniko makubwa.
Ameongeza kuwa endapo kama muda wa kufikisha umeme vijijini haujafika basi REA wanatakiwa kwenda kufukia mashimo hayo na pindi watakapokuwa tayari basi watayafukua na kisha kusimamisha nguzo kwa ajili ya umeme.
Hataivyo ameitaka REA kuhakikisha kuwa wanashirikiana na madiwani
waliopo kwenye kata husika kwani takwimu za halmashauri hiyo
zinaonesha kuwa bado asilimia kubwa ya madiwani hawajui mradi huo
Amesema kuwa wakati mwingine wananchi wanashindwa kupenda na
kuthamini mradi huo kwa kuwa hawana hamasa kutoka kwa madiwani hao
hali ambayo wakati mwingine inasababisha fujo zisizo za lazima hasa
maeneo ambayo mradi huo umepita.
NHC watathmini utekelezaji wa ujenzi wa miradi
Meneja
wa NHC Mkoa wa Tabora, Erasto Chilambo akiwasilisha ripoti ya
utekelezaji wa mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Isikizya zilizopo
wilayani Uyui mkoani Tabora kwenye semina ya mameneja na wakurugenzi
wa NHC inayoendelea katika Hoteli ya Tanga Beach Resort.
Meneja wa NHC Mkoa wa Dodoma,
Itandula Gambalagi akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa mradi wa nyumba
za gharama nafuu za NHC Mnyakongo, Kongwa Dodoma kwenye semina ya
mameneja na wakurugenzi wa NHC inayoendelea katika Hoteli ya Tanga Beach
Resort.
Washiriki wa Semina hiyo
Wenceslaus Tillya, Meneja wa NHC mkoa wa Temeke, Nehemia Msigwa, Meneja
wa NHC Katavi na Daniel Nkya wakifuatilia kwa kina somo lililokuwa
likitolewa na Wataalamu
Washauri wa Delloite Touche juu ya mapitio ya Mpango Mkakati wa Shirika
unaomalizika mwakani, ili kuuboresha kwa kipindi kijacho. Somo hilo
lilitolewa kabla ya mawasilisho ya mameneja wa mikoa.
Meneja
Mshauri Taasisi inayojishughulisha na mambo ya uchumi
ya Deloitte Bw.Frederick Nsemwa, Mkurugenzi wa Watushi Housing Limited,
Dk Fred Nsemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu wakifuatilia somo hilo
Wataalamu washauri wa semina hiyo
wakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu, James Rhombo na
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki Benedict Kilimba wakifuatilia semina
hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Susan Omari akifuatilia kwa kina soma hilo la Delloite Touche.
Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa
Ndani, Fatuma Chillo akisisitiza jambo katika semina hiyo huku
Mkurugenzi wa Fedha, Felix Maagi na Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara,
David Shambwe wakifuatilia.
Julius Ntoga wa Shirika la Nyumba
la Taifa, William Genya, Joseph Mwanasenga, Ramadhani Macha, Elias
Msese, Pauline Mrango , Hamad Abdallah na Ladislaus
Bamanyisa wakifuatilia kwa kina somo lililokuwa likitolewa na Wataalamu Washauri wa Delloite Touche.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akisisitiza jambo katika semina hiyo.
Humphrey Kishimbo, Meneja wa NHC,
Iringa, George Magembe, Meneja Miradi wa NHC na Mektilda Mihayo, Meneja
wa Mahusiano kwa Wateja wakifuatilia somo katika semina hiyo.
Washiriki wakifuatilia mada iliyotolewa na Wataalamu wa Afrika Kusini kutoka kampuni ya Hydraform.
Wataalamu wa Afrika Kusini kutoka kampuni ya Hydraform.wakiwa na mdau kutoka Hydraform Tanzania wakifuatilia semina hiyo
MABONDIA WAZIPIGA MAZOEZINI
Bondia Shabani Kaoneka kushoto
akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Obago Kamata wakati wa
mazoezi .
Bondia Shabani Kaoneka kulia
Bondia Shabani Kaoneka kushoto
akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Obago Kamata wakati wa
mazoezi.
Bondia Jumaa Rashid akioneshana
ubavu na Juma Biglee wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika uwanja wa
Shule ya Uhuru uwanja wa basket Dar es salaam jana.
HOTUBA YA WAZIRI WA UCHUKUZI Mhe. Dkt. Harrsion Mwakyembe KATIKA MKUTANO WA SITA WA MAMENEJA WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA ULIOFANYIKA HOTEL YA DOUBLE TREE DAR ES SALAAM
Awali ya yote napenda nichukue
fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kujumuika pamoja leo
hii katika tukio hili muhimu linalohusu mkutano mkuu wa sita wa
mameneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Aidha nichukue nafasi hii pia kuipongeza Menejimeti ya TAA
pamoja na wafanyakazi wote kwa kufanikisha maandalizi ya mkutano huu na
kunipa heshima hii kubwa ya kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano
huu. Kwa hili nawashukuru na kuwapongeza sana.
Ndugu Wajumbe,
Pamoja na shukrani zangu za awali, nimefarijika sana kuona
Mkutano huu unawajumuisha Viongozi wa Menejimenti na Mameneja wote wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini kote wapatao sitini (60) kama
Mkurugenzi Mkuu alivyoeleza katika hotuba yake. Katika mkusanyiko huu,
ni matarajio yangu kwamba Mkutano huu ulikuwa ni fursa nzuri ya
kubadilishana mawazo kwa ukaribu zaidi na kutafuta ufumbuzi wa matatizo
na changamoto zinazohusiana na shughuli za utoaji huduma katika Mamlaka
yenu. Aidha, hii ni njia mojawapo ya ushirikishwaji na uwajibikaji
katika uendeshaji wa Taasisi hii.
Sambamba na pongezi zangu za awali, nichukue fursa hii pia kwa
kuwapongeza tena juu ya kauli mbiu ya mkutano mliyoichagua ambayo
inaendana na mabadiliko ya huduma za makampuni yaliyoanza kutoa huduma
za usafiri wa anga kwa gharama nafuu ambayo yatakuwa chachu ya ukuaji wa
sekta ya Anga Tanzania. Ukuaji wa “low cost carriers” kwa sasa na kwa
siku zijazo ni wa uhakika, hivyo nawaasa kuwa TAA kama mdau mkuu katika
ukuaji huo, ihakikishe kwamba inajipanga vizuri kwa kuweka mazingira
yanayowezesha kukabiliana na changamoto zitakazotokana na ukuaji huo.
Bila shaka na kama nilivyoarifiwa,
mada mbalimbali zilizoandaliwa zilijadiliwa kwa kina na ufasaha
kutokana na kwamba zote zilijikitika katika kufanikisha lengo la mkutano
huu, ambazo zimeainishwa vizuri katika kauli mbiu yake.
Ndugu Wajumbe,
Wizara tunajivumia sana mafanikio ambayo TAA imeyapata tangu
kuanzishwa kwake, ni dhahiri kwamba mafanikio hayo si tu kwamba
yatatokana na mipango mizuri mliyojiwekea bali pia yanatokana na
usimamizi wenu wa karibu juu ya malengo hayo kwa kuwashirikisha kwa
karibu wafanyakazi walioko chini yenu. Dunia ya sasa ya karne ya 21
katika viwanja vya ndege, inatawaliwa zaidi na utoaji huduma ulio bora
ukilenga kuwavutia wateja na hili linaweza tu kufikiwa iwapo wafanyazi
watahamasishwa na kupewa mafunzo ambayo yatawaongezea ujuzi ukiwemo wa
kiteknolojia, weledi na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii zaidi. Na ili
ushirikishwaji huo utoe matunda yanayostahili, mnaaswa mhakikishe kwamba
wafanyakazi hao wanahamasishwa na kupewa mafunzo stahiki na hasa katika
kusimamia miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa sasa katika viwanja
vyenu, inayokuja na inayotarajiwa.
Sanjari na hili mnaaswa pia
mhakikishe kuwa ili kujua na kupima utendaji wao wa kazi, watumishi hao
wapimwe juu ya utendaji wao wa kazi wa kila siku kwa kutumia mfumo ulio
wazi wa kupima utendaji wa kazi wa watumishi wa serikali yaani OPRAS.
Nimefahamishwa kuwa upimaji wa utendaji kazi chini ya OPRS umekuwa na
changamoto nyingi. Hata hivyo, siamini kama changamoto hizo
hazitatuliki, hivyo kwa weledi mlio nao, naomba muendelee kuboresha
mfumo huo kwa lengo la upimaji bora wa watumishi hatimaye ulete matunda
ya pamoja kwa utendaji ulio bora kwa Mamlaka.
Friday, October 31, 2014
BEN KIKO AMEFARIKI DUNIA
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania Dar
es salaam(RTD) ambayo sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo au maarufu
Ben Kiko (pichani) amefariki duania.
Mwandishi huyo mkongwe nchini Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Ben Kiko alihamishiwa katika hosptali ya Muhimbili kutokea hosptali ya Jeshi ya Milambo ya mkoani Tabora ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki mbili.
Atakumbukwa kama mmoja wa watangazaji mahiri ambao walijipatia umaarufu mkubwa ambapo katika enzi za uhai wake alifanya makubwa wakati wa Vita vya Kagera kwa kuleta matukio mbalimbali kutoka uwanja wa vita. Pia aliupaisha sana mkoa wa Tabora alikokuwa akifanyia kazi kwa habari na visa mbalimbali katika kipindi cha RTD cha Majira.
MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA, AMIN
Mwandishi huyo mkongwe nchini Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Ben Kiko alihamishiwa katika hosptali ya Muhimbili kutokea hosptali ya Jeshi ya Milambo ya mkoani Tabora ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki mbili.
Atakumbukwa kama mmoja wa watangazaji mahiri ambao walijipatia umaarufu mkubwa ambapo katika enzi za uhai wake alifanya makubwa wakati wa Vita vya Kagera kwa kuleta matukio mbalimbali kutoka uwanja wa vita. Pia aliupaisha sana mkoa wa Tabora alikokuwa akifanyia kazi kwa habari na visa mbalimbali katika kipindi cha RTD cha Majira.
MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA, AMIN
Halmashauri zashauri kutenga maeneo ya uwekezaji.
Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stela
Manyanya akikagua bidhaa za wajasiliamali na waoneshashi kwenye viwanja
vya maonesho ya SIDO yaliyojumuisha mikoa mitano ya Njombe,Mbeya,Rukwa
,Katavi na Kigoma sanjali na kongamano la uwekezaji kwa mikoa ya ukanda
wa ziwa Tanganyika ambayo,Katavi Rukwa na Kigoma yanayoendelea kwenye
uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa
……………………………………………………………..
Na Kibada Kibada –Rukwa.
Halmashauri za Wilaya zimeshauriwa kutenga maeneo ya uzalishaji
na kuendeleza maeneo maalum kwenye baadhi ya mipaka ili kuweza kupata
sehemu bora za kuuzia bidhaa za wananchi zinazozalishwa katika maeneo hayo.
Ushauri huo ulitolewa na waziri wa Viwanda na Biashara
Dkt Abdalah Kigoda katika Hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stela Manyanya wakati wa ufunguzi wa maonesho
ya kumi na mbili ya Kanda ya Nyanda za Juu kusini ya wajasiliamali
wadogo na kati Mjini Sumbawanga.
Dkt Kigoda ameeleza kuwa bidhaa kwenye maeneo maalum na ya pamoja hususani ya mipakani kunasaidia katika kuleta ushindani na uboreshaji wa bidhaa.
Akasema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kulitumia
soko la AGOA na masoko mengine ambayo Serikali imeridhia ambayo ni Afrika Mashariki AECna lile la kusini mwa Afrika SADC.
Akashauri kufanya biashara halali na nchi jirani na kutunza kumbukumbu sahihi ya biashara zinazofanyika nchi za jirani na nchi ya Tanzaznia ili kuweza kuandaa sera mahususi za kuwasaidia.
Waziri Kigoda Katika Hotuba yake akasisitiza kwa Halmashauri
zote nchini kushiriki moja kwa moja katika Program ya SIDO ya ’Wilaya
moja Bidhaa moja’ ambayo inasisitiza kuwa kila wilaya iwe inatambulika
kwa uzalishaji wa bidhaa moja itakayotiliwa mkazo zaidi kuliko nyingine
zilizopo kwenye wilaya husika.
Hii ikiwa na maana kutoa kipaumbele kwenye upande wa kuendeleza
bidhaa kwa kuipa huduma zaidi kwenye upande wa kupata mafunzo
teknolojia,masoko na mikopo,lengo ikiwa ni kuongeza mapato na ajira kwa
vijana katika maeneo husika.
Pia Wafanya biashara, wajasiliamali na wasindikaji wa bidhaa wa
Mikoa ya Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini na ule wa kanda ya ziwa
Tanganyika wametakiwa kuwa wabunifu katika kubaini nini kinahitajika na
mahali gani na lini wakati wa kuzalisha kadiri ya mahitaji ya soko.
Mikoa mitano ya Kanda ya nyanda za juu na ukanda wa ziwa
Tanganyika imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi na hali ya hewa nzuri
inayovutia na kufaa katika kuzalishaa bidhaa na kutoa huduma mbalimbali.
Ambapo bidhaa zinazotokana na maliasili,mifugo,na mazao ya
kilimo ambayo mikoa yote mitano ya kandahii imejaliwa ambayo ni Njombe
Mbeya, Rukwa Katavi na Kigoma ambapo Serikali inajitahidi kuweka
miundombinu ili kuwezesha huduma na bidhaa kusafiri kwa urahisi kutoka
mikoa hiyo kwenda kwenye mikoa mingine na nchi jirani za Zambia,Jamhuri
ya Kidemkrasi ya Kongo DRC,Burundi, Malawi na Rwanda, kwa kutumia
barabara na majini Maziwa Tanganyika,Rukwa na Nyasa, Ambapo ili kutumia
fursa hiyo wanatakiwa kuwa wabunifu katika kubaini mahitaji.
SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI-DKT.BILALI
Makamu
wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali (watatu kutoka kulia) akiwa kwenye
picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya afya nchini mara baada ya kufungua
Kongamano la wadau hao leo jijini Dar es salaam.Wengine kushoto ni
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid.Picha zote na Frank Mvungi-MAELEZO_Dar es salaam.
Makamu wa Rais Dk. Mohemed Gharib Bilali akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii
Dk Seif Rashid leo Jijini Dar es salaam wakati wa Kongamano la wadau
wa Sekta ya Afya lililofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Wadau wa Kongamano la wadau wa Sekta ya Afya wakiwa wanamsikiliza
mgeni rasmi ambaye ni makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali (hayupo
pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………….
Na Frank Mvungi-MAELEZO
Serikali imesema itaendelea kuboresha huduma za afya hapa nchini
kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hosipitali za Rufaa zote nchini ili
kuhakikisha wananchi wanapata matatibu bora na yanayoridhisha.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Makamu wa Rais
Dkt. Mohamed Gharib Bilali wakati akifungua Kongamano la wadau wa Afya
nchini.
Amesema kuwa Serikali inayo dhamira ya dhati katika kuhakikisha
kuwa kila Mtanzania anapata huduma bora za afya ili apate muda mzuri wa
kuchangia shughuli nyingine za maendeleo akiwa mzima.
Dkt. Bilali ameongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa motisha kwa
watumishi wa Sekta ya afya ili waendelee kutoa huduma bora za afya kwa
wananchi.
Kwa upande wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif
Rashid amesema Tanzania ni moja kati ya nchi nne barani Afrika
zilizoweza kufikia lengo namba 4 la malengo ya millennia katika utoaji
wa huduma bora za afya.
Amesema kuwa hatua imefikiwa baada ya Wizara hiyo kuamua
kuanzisha idara maalum itakayohusika kuangalia ubora wa huduma
zinazotolewa hapa nchini ili kuongeza tija katika Sekta ya Afya kwa
kuwapa Wananchi huduma bora zinazokidhi vigezo.
Ameongeza kuwa kwa wale wanaofanya vizuri katika kutoa huduma za Afya watatambuliwa kwa mchango wao katika kutoa huduma bora.
Dkt. Rashid ametaja vigezo vinavyotumika katika kuwapata watoa
huduma za afya kuwa ni kutoa huduma inavyotakiwa,kutumia utaalamu sahihi
katika kutoa huduma hiyo na kuzingatia viwango vilivyowekwa katika
kutoa huduma za afya.
Aidha Dkt. Rashid ametoa wito kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa
kupitia mfuko huo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma
bora za afya.
Kongamano la wadau wa Sekta ya Afya limehusisha wadau zaidi ya
300 kutoka katika Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Kiserikali
na linafanyika kwa muda wa siku mbili ambapo baadhi ya wadau
walitambuliwa kwa kutoa huduma bora za Afya ni kama vile Hosipitali ya
Rufaa Mbeya,KCMC, na Bugando.
Subscribe to:
Posts (Atom)