Meneja
wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, Mkoa wa
Katavi Seneti Lyatuu akiwaonesha timu ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda. Nyuma yake
(mwenye suti nyeusi) ni Mhandisi Caroline Mntambo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya
Ndenge Tanzania, Makao Makuu, Dar es Salaam.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda Bw. Seneti Lyatuu akifafanua jambo wakati timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipotembelea kiwanja hicho.
Timu ya ukaguzi ikitazama barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda
Barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoani Katavi
Mhandisi Caroline Mntambo (mwenye suti nyeusi) akifafanua jambo kwa timu ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Uwanja wa ndege wa Mpanda umekarabatiwa na kupanuliwa hivyo , kuwa katika hali nzuri kwa matumizi ya ndege zote za binafsi na biashara

Na Mwandishi wetu, Mpanda
Serikali imekamilisha
ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoa wa Katavi na hivyo
kuufanya uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na
biashara.
Meneja wa Uwanja wa Ndege
wa Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza
kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile ndege kubwa
zinaweza kutua kwa dharura.
Aliiambia timu ya ukaguzi
wa miradi ya maendeleo kutoa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango iliyotembelea uwanja
huo mwishoni mwa wiki kuwa uwanja huo umeongeza idadi ya wasafiri mara dufu
kutokana na ukarabati na upanuzi uliofanyika.
Meneja wa Uwanja huo
alisema idadi ya abiria imeongezeka kutoka abiria 285 mwaka 2009 hadi 2,390
mwaka 2013/14.
Bw. Lyatuu alisema kuwa uwanja
huo umekarabatiwa na barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango
cha lami kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa
mita 1,820 na upana wa mita 30.
Alisema maeneo mengine
yaliyokarabatiwa ni pamoja na kujenga uzio na mifereji ya kupitishia maji ya
mvua.
“Kwa sasa kiwanja kipo
vizuri na ndege za aina zote zinaweza kutua hapa uwanjani hivyo,
tunawakaribishwa wadau wote kuutumia uwanja huu” alisema Bw Lyatuu.
Eng. Caroline Mntambo
kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Makao Makuu Dar es Salaam alisema kuwa
tayari wamealika mashirika ya ndege yanayofanya biashara hapa nchini kuanzisha
safari katika uwanja huo. Mashirika hayo ni pamoja na ATC, Precision Air, Fast
jet nk.
Eng Mntambo alisema kwa
sasa shirika la ndege la Auric Air
tayari limeanzisha safari za kwenda Mpanda ambapo linasafirisha abiria kutoka
Dar- Mpanda – Mwanza mara tatu kwa wiki.
Alisema ndege zingine
zinazotua uwanjani hapo kwa sasa ni pamoja na za UNHCR, ndege za kukodi na
ndege za serikali.
-Mwisho-
No comments:
Post a Comment