Mke wa Rais wa China aipa msaada Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama
Na Anna Nkinda – Beijing, China Mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan ameahidi kutoa vifaa vya shule vikiwemo vya maabara pamoja na vitabu kwa ajili ya shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama ili wanafunzi hao waweze kusoma vizuri masomo ya sayansi. Mama Liyuan aliitoa ahadi hiyo jana wakati akiongea na mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika ukumbi maarufu wa watu (Great hall of the People) uliopo mjini Beijing.
“Nina mapenzi na Taasisi ya WAMA, nakupongeza kwa kazi unayoifanya ukiwa Mke wa Rais ya kuwainua wanawake kiuchumi na kuwasaidia watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi ambao nao wanapata elimu sawa na watoto wengine”.
Najua kitaaluma wewe ni mwalimu na unapenda shule mwaka huu nitakuunga mkono zaidi katika masuala ya shule, hii itawasaidia wanafunzi kusoma vizuri. Pia nitakuwa na ushirikiano endelevu na Taasisi ya WAMA”, alisema Mama Liyuan.
Kwa upande wake Mama Kikwete alishukuru kwa msaada huo na kusema kila kwenye maendeleo changamoto hazikosekani alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ambazo ni upungufu wa maabara, kutokuwepo kwa wataalamu wa maabara na walimu wa masomo ya sayansi wa kutosha.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema katika upande wa elimu Serikali kwa kushirikiana na wananchi wamejitahidi kujenga shule nyingi za Sekondari lakini bado kuna upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi , kutokuwa na maabara za kutosha, kutokuwa na vifaa vya maabara na upungufu wa wataalamu wa maabara .
“Ninaomba kuwe na ubadilishanaji wa ujuzi wa kazi (Exchange Program) kwa walimu wetu wa nchi hizi mbili hii itawasaidia kupata utaalamu zaidi katika fani zao na kutoa mfano wa wataalamu wa maabara ambao wakija nchini watasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafundisha wanafunzi masomo ya sayansi kwa njia ya vitendo”, alisema Mama Kikwete.
Shule hiyo ambayo inamilikiwa na Taasisi ya WAMA wanafunzi wake ni watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani iko kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
Hii ni mara ya pili kwa Mama Liyuan kuiunga mkono Taasisi ya WAMA ambapo mwaka 2013 alipotembelea nchini alitoa Yuan milioni moja sawasawa na shilingi milioni 250 za kitanzania na mabegi ya shule 100 kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama na vyerehani 20 kwa ajili ya Umoja wa Vikundi vya WAMA (UVIMA).
Mama Kikwete ameambatana na mumewe Rais Prof. Jakaya Mrisho Kikwete nchini China kwa ziara ya kikazi ya siku sita.
===============================================================
Dk. Shein Azungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya Zanzibar Ikulu.
=============================================================
KAMPUNI YA KARIATI YAKABIDHI WAKULIMA MATREKTA MANNE LEO, JIJINI DAR ES SALAAM
Kampuni
ya Kariati Matracktor Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma,
Omary Kariati, leo imekabidhi matrekta manne kwa wakulima wa wilaya ya
Kondoa (matrekta matatu) na Mbarali (trekta moja), katika hafla
iliyofanyika leo asubuhi, kwenye Ofisi za Kariati Matrektor, Kinondoni,
Dar es Salaam. Zinazofuatia ni picha za hafla hiyo. Picha/Maelezo na
Bashir Nkoromo

Kariati akikata uatepe kuzindua makabidhiano ya trekta hizo


=============================================================
Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira yatembelea kiwanda cha Mifuko ya Plastiki (East African Industy)
================================================================
Dr Slaa akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na TCD.
====================================================================
Mwandosya amuwakilisha JK Sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Zambia
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe William Ruto wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Mhe. Mwandosya alimuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe hizo.
Picha na Mpiga Picha wetu
================================================================
ZIARA YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NCHINI POLLAND
==================================================================
MKUTANO WA KUANDAA RAMANI YA MJI WA ZANZIBAR WAFANYIKA
==============================================================
Tanzania and China Marks 50 Years of Diplomatic Relations
===========================================================
Benki ya Exim yasaini mkataba wa mwaka mmoja na Stand United FC
Mkuu
wa matawi wa Benki ya Exim Kanda ya Ziwa, Bw. Justus Mukurasi (wapili
kushoto) akibadilishana mkataba na Mwenyekiti wa Timu ya Mpira wa Miguu
ya Stand United, Bw. Amani Vicent (wapili kulia) wakati wa hafla fupi
iliyofanyika mkoani Shinyanga jana. Mkataba huo utaiwezesha benki
kuidhamini timu hiyo katika ligi kuu ya mpira wa miguu ya Vodacom (VPL)
katika msimu wa 2014/2015. Wakishuhudia wa kwanza kushoto ni Meneja
Msaidizi Tawi la Shinyanga, Bw. Hatunga Nicodemus na Katibu wa kamati ya
Fedha, Bw. Bakari Salum (Wa kwanza kulia). Picha na mpiga picha wetu.
Benki ya Exim imesaini makubaliano ya kuifadhili timu ya mpira wa miguu ya Stand United FC ya mkoani Shinyanga. Hii ni timu ya kwanza kupata ufadhili toka Benki ya Exim. Ufadhili huo wa mwaka mmoja utaisaidia timu hiyo kushiriki katika ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu wa 2014/2015.
“Makubaliano haya yanaikutanisha Benki ya Exim na mchezo mkubwa kuliko yote Tanzania,” alisema mkuu wa matawi ya Benki ya Exim kanda ya ziwa, Bw. Justus Mukurasi jana katika hafla fupi iliyofanyika mkoani Shinyanga. Aliongeza kuwa hakuna mchezo wenye watazamaji, wafuatiliaji na mashabiki wengi zaidi nchini kama mpira wa miguu.
“Timu ya Stand United inanguvu kubwa ya kuunganisha mashabiki wa kanda ya ziwa. Hivyo ni jambo stahiki kwa Benki ya Exim kuisaidia timu hii ambayo mashabiki wake ni miongoni mwa wateja wa Benki ya Exim,” alisema Bw. Mukurasi.
Mukurasi aliongeza kuwa pande hizo mbili zilifanikiwa kuingia katika makubaliano ambayo yataiwezesha benki hiyo kuifadhili timu ya Stand United toka Ligi Kuu Tanzania bara ilipoanza.
“Kwetu sisi udhamini tuliofanya sio tu wa nembo, nbali ni ufadhili wa muda mrefu utakaozinufaisha pande zote mbili,” alisema Mukurasi.
”Tunatumai kuwa kila mmoja wetu ataweza kujifunza kutoka kwa mwenzake ili kupata matokeo mazuri kwa pamoja. Exim itasaidia kukuza na kuundeleza mchezo wa soka na hivyo kuiwezesha benki yetu karibu zaidi na wateja wake,” alisema Bw. Mukurasi.
Naye, Mwenyekiti wa Stand United FC, Bw. Aman Vicent alisema kuwa timu yake inayofuraha kubwa kuingia katika makubaliano na Benki ya Exim. “Tunadhamiria kuimarisha uhusiano huu ili kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu,” alisema Bw. Vicent.
“Kwa niaba ya Stand United FC, ningependa kuishukuru Benki ya Exim kwa jitiada zao za kusaidia wachezaji wetu na timu kwa ujumla. Tunafanya kazi kubwa kuhakikisha tunainua vipaji vya wachezaji wetu ili na wao waweze kufika mbali zaidi,” aliongeza Bw. Vicent.
No comments:
Post a Comment