TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, August 2, 2014
Dunia nzima lazima iifuate Azam Mbagala
By DORIS MALIYAGA
(email the author)
Posted Agosti2 2014 saa 12:13 PM
Posted Agosti2 2014 saa 12:13 PM
KATIKA kujiweka sawa, Mabingwa wapya wa Ligi Kuu
Bara klabu ya Azam FC, itakipiga na Zesco ya Zambia Uwanja wa Azam
Complex Agosti 10 na imetamka rasmi kuwa itacheza mechi zake zote za
Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wao na siyo Taifa.
Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassor ameliambia
Mwanaspoti kuwa: “Baada ya mechi yetu na Mtibwa, tutacheza mechi ya
kirafiki na Zesco ya Zambia siku hiyo mipango yote imeshakamilika.”
Muivory Coast wa Azam, Kipre Tchetche
ameondolewa kikosini kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya shingo na
anatarajiwa kuanza mazoezi na wenzake, wiki ijayo.
Pia Mhaiti Leonel Saint-Preux anasumbuliwa na
majeruhi kwenye mguu wa kulia. Omog amesema: “Tchetche nimempumzisha
hadi wiki ijayo, anamatatizo mgongoni kwenye shingo na Leonel hayuko
vizuri nafikiri ataanza mazoezi na wenzake kesho (leo),”alisema Omog.
Azam leo itafanya mazoezi ya ufukweni Coco.
TWIGA AFA BAADA YA KUJIGONGA DARAJANI
Na: FICHUO Tz
Shirika la kutetea haki za wanyama la Afrika Kusini limeanza uchunguzi
kuhusiana na kifo cha twiga baada ya kuumia wakati akisafirishwa kwenye
gari. Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema twiga mmoja kati ya wawili
waliokuwa kwenye lori, aligonga kichwa chake katika barabara moja mjini
Johannesburg.
Gari
hilo baadaye liliharibika na kulazimika kusubiri kwa saa kadhaa kabla ya
kutengenezwa. Wanyama wote wawili walipelekwa kwa daktari wa wanyama,
lakini shirika la kutetea haki za wanyama la NSPCA limesema twiga mmoja
alikufa.
Tukio hilo limeleta mjadala mkubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Meneja
wa NSCPA Rick Allen amethibitisha kuwa twiga huyo alipata majeraha ya
kichwani lakini amesema uchunguzi ni muhimu ufanyike kutafuta sababu
hasa ya kifo hicho.
WENGER: MESSI ALIMFANYA SANCHEZ AHANGAIKE BARCELONA KAMA ILIVYO KWA NEYMAR
NA BARAKA MPEJA
ASERNE
Wenger anaamini Alexis Sanchez aliathirika kama anavyoathirika Neymar
wakati akiwa Barcelona kutokana na uwepo wa Lionel Messi.
Asernal
ilitumia Euro milioni 40 kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Chile
majira haya ya kiangazi na leo hii anatarajia kucheza mechi yake ya
kwanza ya maandalizi ya msimu mpya.
Licha
ya kucheza kama winga akiwa Barca, Alexis atachezeshwa kama
mshambuliaji Emirates na Wenger anaamini atang`ara zaidi katika nafasi
hiyo kutokana na kutokuwepo kwa ‘mchawi’ wake Messi.
“Kwa
mara ya kwanza alitinga katika rada zangu alipokuwa Udinese na baadaye
Barcelona”. Alisema Mfaransa huyo alipozungumza na The Dail Mirror.
“Ni
mshambuliaji. Ni mmaliziaji mzuri ambaye alikuwa na kiwango kizuri
Italia. Nilimuona pale na alikuwa amesimama vizuri. Lakini mambo
yalikuwa magumu alipoenda Barcelona kama ilivyo kwa Neymar sahizi”.
“Unapomuona
Neymar wa Brazil na Neymar wa Barcelona sio mtu mmoja. Naamini kuwa
Alexis anaweza kucheza kushoto, kulia na mbele na ndio maana
nilimfuata”.
MBUNGE NASSARI ASHIRIKI MDAHALO ULIOANDALIWA MAKAO MAKUU YA BENKI YA DUNIA.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua
Nassari (wa pili toka
shoto) akiwa ni miongoni mwa wawasishaji wa mada katika mdahalo maalumu
uliofanyika Makao Makuu ya Benki ya Dunia.
BREAKING NEWS: BASI LA HOOD LAUA WATANO ARUSHA
Ajali
iliyohusisha basi la HOOD na daladala maeneo ya Usa River mkoani Arusha
muda huu...Ambapo dereva wa dala dala kafariki hapo hapo
|
TETESI ZA SOKA ULAYA
Friday, August 1, 2014
MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA AYOUB MLAY KWA BASTOLA AMBROSIA CLUB AONJA JOTO YA JIWE MAHAKAMANI KISUTU.
|
Mtuhumiwa wa kesi ya Mauaji, Conrad Leo (33)akiwa chini ya ulinzi wa polisi mara baada ya kuachiwa na kukamatwa tena katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana.Mtuhumiwa huyo anashitakiwa kwa kosa la kumuua kwa kutumia silaha Ayubu Mlai. |
Mtuhumiwa wa kesi ya Mauaji, Conrad Leo (33)akiwa ndani ya gari ya polisi akipelekwa Mahabusu baada ya kuachiwa na kukamatwa tena katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam .Mtuhumiwa huyo anashitakiwa kwa kosa la kumuua kwa kutumia silaha Ayubu Mlai |
Mtuhumiwa wa kesi ya Mauaji, Conrad Leo (33)akizibitiwa na Polisi
Rais Kikwete awasili Washington kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Amerika na Africa (US-Africa Leaders summit)
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya maafisa waliofika
kumpokea wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles
tayari kwa Mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Amerika
na Africa (US-Africa Leaders summit) uliondaliwa na Rais Barack Obama wa
unaotaraji kuanza Agosti 4-hadi 6, 2014, ambao utatanguliwa na mikutano
mingine ya maendeleo ya sekta mbalimbali na uwekezaji (2-3 Agosti,
2014) jijini Washington DC. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini
Marekani,Balozi Liberata Mulamula.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakisalimiana na
baadhi ya maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakati
walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles.PICHA NA
IKULU.
Maadhimisho ya siku ya Mwanamke wa Afrika yaliyo ratibiwa na -WiLDAF yafana jijini Dar es salaam
Maadhimisho
ya siku ya Mwanamke wa Afrika yaliyo ratibiwa na Women in Law and
Development in Africa-WiLDAF yafana jijini Dar es salaam. Ni siku ya
Mwanamke wa Afrika na husheherekewa kila mwaka tarehe 31 July toka
ilipotamkwa rasmi mwaka 1963 July 31 na wanawake wa Pan African
waliokutana Dar es Salaam kwa wakati huo.Mada mbalimbali zilitolewa
ikiwemo mchakato mzima wa katiba mpya na changamoto zake. Kulikuwa na
watoa mada mbalimbali wakiwemo Dr Khoti Kamanga na Mh. Getrude Mongela.
Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa akabidhi kombe kwa washindi wa shindano la Airtel Rising Stars
Mbunge wa jimbo la Ukonga
Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Ilala Academy
Maisala Adam baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa
kisoka wa Ilala juzi.
Mbunge wa jimbo la Ukonga
Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Temeke All Stars
Maulid Jamal baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa
kisoka wa Temeke juzi.
Mbunge wa jimbo la Ukonga
Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Kinondoni
Academy Jafali Said baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars
mkoa wa kisoka wa Kinondoni juzi.
CHUO CHA CBE CHAZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 JIJINI DAR, WADAU MBALIMBALI WAPONGEZA UBORA WA ELIMU INAYOTOLEWA
Mbunge
wa Ilala Mh. Mussa Zungu ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Uzinduzi
wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam
(CBE) akikata utepe kuashiria uzindunzi wa maadhimisho ya chuo hicho
kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika leo
jijini Dar es salaam.
Viongozi
mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50
ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiangalia moja ya
picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho Januari, 1965. Kutoka kushoto ni
Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel Mjema, Mh. Musa Zungu (Mb) jimbo la
Ilala,Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda,Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo
hicho Prof. Mathew Luhanga na Prof.Eliuta Mwageni Makamu Mkuu wa Chuo
Utawala na Fedha.
Viongozi
mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50
ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiwa katika picha ya
pamoja wakiongozwa na Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu na Mke wa Waziri
Mkuu, Mama Tunu Pinda (katikati). Nyuma ni bango lenye picha ya
kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa
wakati akifungua Chuo hicho mwaka 1965.
Mke wa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kwa
niaba ya wanafunzi waliosoma katika chuo cha Elimu ya Biashara Dar es
salaam akizungumza na wadau na wanajumuiya wa Chuo hicho wakati wa
uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho jijini Dar es salaam.
MH ZITTO KABWE ATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU KATIBA NA UKAWA..
Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha
PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari
vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo
wangu kuhusu mchakato wa Katiba.Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala
kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi
linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu
Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala
egemezi kwa Washirika wake. Pili, Mimi niliunga mkono ‘protest’ ya
baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na
lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile
niliunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana
na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde
Warioba.
Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tatu,
kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora. Mkwamo
unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande
zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na Viongozi wa Bunge la Katiba
badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo
kamwe haliwezi kujenga mwafaka.Ushauri wangu ni kuahirisha
mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama
ifuatavyo;
i) Tume
ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa
watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia
uchaguzi
ii) Kuruhusu mgombea binafsi
iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze
mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu
vilivyopo upande huo wa Muungano
Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano
utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha
za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini.
MARAIS WASTAAFU THABO MBEKI, FESTUS MOGAE NA BENJAMIN MKAPA WAKUTANA DAR ES SALAAM
Marais
wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Festus Mogae wa Botswana
wakiigia kwenye chumba cha Mkutano katika hoteli ya Serena jijini Dar es
salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa Africa Readership Forum
ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es salaam ambao
ulikuwa unajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi za Afrika na
kuangalia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za kushughulikia
changamoto hizo.
Rais
mstaafu wa wa Afrika Kusin Thabo Mbeki akizungumza katika mkutano huo
uliojumuisha viongozi mbalimbali wa afrika na taasisi mbalimbali kweye
hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
Marais
wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini katikati ,Festus Mogae wa
Botswana kushoo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa
wakiwa wakiongoza mkutano huo.
Baadhi ya viongozi kutoka taasisi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.
Mbunge
wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe katikati ni mmoja wa viongozi
waliohudhuria katik mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena
jijini Dar es salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye kulia ni Mh. Balozi Ali Karume
walikuwa ni miogoni wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo pia.
Thursday, July 31, 2014
RAIA WANNE WAPOTEZA MAISHA JIJINI MBEYA, YUMO ALIYEANGUKIWA NA KIFUSI. WATU WANNE WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 51 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI MATUNDASI- CHUNYA
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 31.07.2014.
WATU WANNE WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 51 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI MATUNDASI WILAYANI CHUNYA.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI JIJINI MBEYA.
MTOTO WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MCHANGA WILAYANI CHUNYA.
MTOTO WA MIAKA KUMI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA NA SHOTI YA UMEME.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU WANNE WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. PAULO MWASANGA (18) MKAZI WA KITONGOJI CHA MATUNDASI ‘B’ 2. WEDI ANGOLWISE (21) MKAZI WA MATUNDASI 3. SALOME MWAKIBETE (13) MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI SAMBILIMWAYA NA 4. OBEDI MWAKAMELA (25) MKAZI WA MATUNDASI WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.595 CHU AINA YA FUSO TIPPER LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA KIPINDUKA KATIKA KIJIJI CHA MATUNDASI WILAYANI CHUNYA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MATUNDASI “B”, KIJIJI CHA MATUNDASI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA CHUNYA/MAKONGOLOSI.
GARI HILO LILIKUWA LIKITOKEA KIJIJI CHA SAMBILIMWAYA KUELEKEA KIJIJI CHA MATUNDASI LIKIWA LIMEBEBA WACHEZAJI WA MPIRA WA MIGUU NA MASHABIKI. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU 51 WALIJERUHIWA, KATI YAO 26 WALITIBIWA NA KURUHUSIWA NA WENGINE 25 WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA CHUNYA WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA WILE PETER AMBAYE ALIKUWA ABIRIA KATIKA PIKIPIKIAMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI DFP 0036 AINA YA BENZ MALI YA SHIRIKA LA UMEME TANESCO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA PATRICK MHAGAMA (46) MKAZI WA ILOMBA JIJI MBEYA KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE NA KUSABABISHA KIFO KWA ABIRIA HUYO.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 31.07.2014 MAJIRA YA SAA 16:45 JIONI HUKO NZOVWE, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITATU ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA PASCALIA JIFULA NGASA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KUFUNIKWA NA KIFUSI CHA MCHANGA KATIKA KITONGOJI CHA CHIZYA WILAYANI CHUNYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA 08:300 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA CHIZYA, KIJIJI CHA MWAMBANI CHINI, KATA YA MWAMBANI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA, MTOTO HUYO ALIKUWA AKICHEZA NA WATOTO WENZAKE KWENYE GEMA LA MCHANGA NA NDIPO KIFUSI KUMUANGUKIA NA KUMFUNIKA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUANGALIA MAZINGIRA YA MAENEO YAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
KATIKA TUKIO LA NNE:
MTOTO WA MIAKA KUMI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JERRY JESTED, MWANAFUNZI NA MKAZI WA MLOWO WILAYANI MBOZI ALIKUTWA AMEKUFA CHUMBANI KWAKE BAADA YA KUPIGWA NA SHOTI YA UMEME.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI BAADA YA MAREHEMU KULAMBA NYAYA ZA UMEME AMBAZO ZILIKUWA KARIBU NA KITANDA CHAKE HALI ILIYOPELEKEA KUPIGWA SHOTI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUANGALIA MAZINGIRA YA MAENEO YAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA MBALI VITU VYA HATARI KWA WATOTO.
Imetolewa na kusainiwa na:
[BARAKAEL .N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Mahenge azindua tovuti ya mabadliko ya tabia nchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mh. Dkt.
Eng Binilith Satano Mahenge akizindua rasmi tovuti ya mabadiliko ya tabianchi
itakayotumika kutoa taarifa mbalimbali za utunzaji wa Mazingira.
Mheshimiwa Eng Dkt. Binirithi S. Mahenge
(mbunge) Waziri wa nchi ofisi ya
Makamu wa Rais (mazingira) azindua tovuti
ya mabadiliko ya tabia nchi. Katika hotuba yake fupi ya uzinduzi wa tovuti hiyo,
aliyoandaliwa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark Mh. Binirithi Mhenge amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya
nchi huangaliwa kwa muda wa miaka 30 hivyo kwa kipindi hiki chote kumekuwa na
madhara mengi yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia Nchi ikiwa ongezeko
la joto, kina cha bahari kuongezeka pamoja na ongezeko la majanga ya mvua
zisizo na viwango, kutoka na shughuli za
binadamu katika uzalishaji hasa viwanda vikubwa
Alisema kwa tovuti inayozinduliwa ina umuhimu mkubwa kwani
inaelezea maeneo ya hali ya mabadiliko ya tabia
nchi na juhudi za serikali katika kukabiliana na athari zinazoletwa na
mabadiliko hayo.
“ziko sababu za kuungana na wenzetu ili kuondoa tatizo hili la mabadiliko ya nchi ambapo
tovuti hii WWW.climatechange.go.tz
inatuunganisha na tovuti mbali mbali katika kupunguza gesi joto hapanchini pia
inaelezea fursa zilizopo katika miradi na program mbali mbali. Alisisitiza”
Alibaini kuwa tovuti hii itachangia kwa kiasi kikubwa
kuongeza uelewa na weledi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi nchini kwa wananchi na wadau kwa ujumla.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mh. Dkt.
Eng Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto) akizungumza na wandishi wa
habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa mkutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais leo jijini Dar es
Salaam, wakati wa uzinduzi wa "tovuti ya mabadiliko ya tabianchi" huku
akieleza malengo ya tovuti hiyo. kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais Bw. Julius Ningu.
sehemu ya wadau waliyoudhulia katika mkutano huo kushuhudia
makubaliano ya mkataba huo.
Mkuu Msaidizi wa Chuo cha kilimo SUA Prof. Gerald Monella (aliyesimama)
akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali kuhusu mkataba
huo unaofanyika baina ya Ofisi ya Makamu wa Rais na chuo cha SUA.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (wa kwanza
kushoto) na Mkuu Msaidizi wa Chuo cha SUA Prof. Gerald Monella wakisaini
mkataba wa uwanzishwaji wa kituo cha Taifa cha kukusanya na kuratibu takwimu za
hewa ukaa uliofanyika katika ukumbi wa mkutano
Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula wakipeana Mkataba na mkuu msaidizi wa wa
chuo cha kilimo SUA Prof. Gerald Monella baada ya kusaini.
Sehemu ya waandishi wa habari waliyoudhulia katika uzinduzi
huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)