TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, July 26, 2014

Jezi ya James Rodriguez yaingiza pato la 345,000 kwa masaa 48 tu.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au Tupigie n amba +255767869133/ +255-713-869133
 

James Rodriguez  

Ni kama ajabu, lakini ndiyo hivyo baada ya jezi yenye namba 10 aliyokabidhiwa staa huyo kuuzwa kama njugu ndani ya saa 48 tu tangu alipotambulishwa rasmi Jumanne iliyopita kuwa ni mchezaji wa Real Madrid.
REAL Madrid imepiga bao. Imetoa pauni 63 milioni kumnasa James Rodriguez na hata kabla hajaanza kucheza mechi yoyote kuleta mataji klabuni hapo, pesa zao zimeanza kurudi.
Ni kama ajabu, lakini ndiyo hivyo baada ya jezi yenye namba 10 aliyokabidhiwa staa huyo kuuzwa kama njugu ndani ya saa 48 tu tangu alipotambulishwa rasmi Jumanne iliyopita kuwa ni mchezaji wa Real Madrid.
Ripoti zinabainisha kwamba Real Madrid hadi sasa tayari imesharudisha kiasi cha pauni 21 milioni baada ya mauzo ya jezi 345,000 za Rodriguez ndani ya saa 48 tu.
Mashabiki wa timu hiyo wameonekana kupagawa na usajili wa Rodriguez, ambaye amepewa jezi iliyokuwa ikivaliwa na Mesut Ozil (kabla hajabadili na kuvaa namba 11) na mwaka jana kutimkia Arsenal.
Kwa mujibu wa gazeti moja la michezo la Hispania, kampuni ya wataalamu wa masoko ya kibiashara michezoni ilifanya hesabu na kugundua kwamba jezi hizo 345,000 zilizouzwa kwa saa 48 ni sawa na mauzo ya jezi 7,188 kwa saa. Hii ni rekodi.
Real Madrid haijawahi kusumbuka juu ya mauzo ya jezi za mastaa wao wanaowasajili kwa pesa nyingi, lakini nyota huyo aliyetamba kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil mauzo ya jezi zake zimeweka rekodi.
Kwenye utambulisho wake uliofanyika uwanjani Bernabeu Jumanne iliyopita zaidi ya mashabiki 44,000 walijitokeza kumshangilia mchezaji huyo huku wengine 900 tayari walionekana kuvaa jezi za mchezaji wao huyo mpya.
Kwa mauzo hayo ya siku mbili tu ya jezi za Rodriguez, tayari Real Madrid imebakiza pauni 3 milioni tu kurudisha pesa walizomsajili kiungo Toni Kroos, aliyejiunga na timu hiyo kwa pauni 24 milioni kutoka Bayern Munich.

Special Thanks from Ngoma Africa band

We are taking this opportunity to thank our entire fans around the globe for your support to this band. It is your support that makes the Ngoma Africa band prosper, without you there will be no success!
Please, we ask you again to keep on supporting and let the band be on the top most position in every event, festival, media etc.
Let others around you join the band at www.ngoma-africa.com, here they will have the opportunity to enjoy music at www.ngoma-africa.com  or http://www.ngoma-africa.com
Yours Sincerely

RAIS KIKWETE ATUNUKU WAHITIMU WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI KATIKA MAHAFALI YA KOZI YA PILI

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security and Strategic Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki tisa wa kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi walitoka Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe. Jumla ya wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. 

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali C.L. Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika  mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.Jumla ya wahitimu 30 wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka  nchi za nje ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia na Zimbabwe.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni zamu yao kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.
Picha ya Pamoja.PICHA NA IKULU

HII NDIYO MBINU ILIYOTUMIKA KUMKAMATA MWIZI KATIKA JIJI LA TANGA., SIMU YAMWOKOA MTOTO WA MAIAKA 4 ALIYEIBWA JIJINI DAR ES SALAAM,,


Mama mzazi wa Marylin Repyson (kulia), Elida Fundi, akiwa amembeba mwanawe huku akiomba jana baada ya kuwasili nyumbani kwake Changanyikeni jijini Dar es Salaam. Picha na Fidelis Felix.
HATIMAYE kinara wa wizi wa watoto jijini Dar es Salaam, Amir Juma, amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa mkoani Tanga.
Juma anadaiwa kumuiba mtoto, Merlin Repyson (4) katika eneo la Changanyikeni siku nane zilizopita.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo akiwa wilayani Korogwe.
“Ni kweli mtuhumiwa huyo amekamatwa huko Korogwe na polisi wetu kwa kushirikiana na wenzao waliotoka Dar es Salaam,” alisema Kamanda Massawe.
Alisema tayari mtuhumiwa alisafirishwa jana asubuhi kupelekwa Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

MAMA ASIMULIA
Mama mzazi wa Merlin, Elida Fundi katika mahojiano maalumu na MTANZANIA alianza kwa kusema: “Mungu ni mkubwa nashukuru kwa maombi yenu, Merlin alipotea siku nane zilizopita lakini amepatikana akiwa mzima.
“Ni jambo la kumshukuru Mungu, watoto wengine wakipotea wanakutwa wametobolewa macho, lakini kwa uwezo wa Mungu na maombi yenu mwanangu amepatikana mzima,” alisema Elida.
Alisema mwanaye alipatikana juzi saa 9:30 alasiri na kupigiwa simu na polisi wa kituo cha Oysterbay wakitaka aende Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Alisema baada ya kufika Hospitali ya Mnazi Mmoja, alikutana na askari polisi aliyekuwa amevaa nguo za kiraia huku akiwa amembeba Merlin ambaye alikuwa anafanyiwa vipimo kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Alisema baada ya kukamilika kwa vipimo vyote, majibu yalipotoka yalionyesha Merlin hana tatizo lolote linalomsumbua.
“Pamoja na kumuona mwanangu akiwa hana ugonjwa wowote, nilishtuka mno kwa sababu alikuwa amelegea kama vile alikuwa na njaa kali,” alisema Elida.
Alisema baada ya kukabidhiwa mtoto wake, aliamua kumbadilisha nguo alizokuwa amevaa kwani siku alipoibwa alikuwa na nguo tofauti na hizo.
“Baada ya kumbadilisha zile nguo niliamua kuzichoma moto pale pale hospitali, nikiamini hazifai kuvaliwa na mwanangu… kama unakumbuka mwanangu aliibwa Julai 15, mwaka huu mpaka nakabidhiwa jana (juzi) Julai 23,” alisema.
MTANZANIA lilifika nyumbani kwa Elida katika eneo la Changanyikeni juzi saa 11:30 jioni baada ya kupata taarifa za tukio hilo na kushuhudia ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamekusanyika.
Ilipofika saa 3:30 usiku msafara wa magari mawili madogo ulionekana ukiingia ndani ya uzio wa nyumba ya mama Merlin, huku shangwe vigelegele vikitawala kwa ndugu na jamaa waliokuwepo nyumbani hapo.
Baada ya muda mfupi, alishuka mama Merlin akiwa na mwanaye ambaye alionekana kuwa katika hali ya kawaida.
Tukio hilo lilipokelewa kwa vigelegele, nderemo na nyimbo za kuabudu zikitawala.
Baada ya kushuka kwenye gari Merlin ndugu na jamaa walimzunguka huku kila mmoja akiwa na shauku kubwa ya kutaka kumbeba na kupiga naye picha.
Baada ya shamra shamra hizo, Elida alishika kitabu cha sala za novena na kuanza kufanya maombi na kuimba nyimbo za mapambio wakishirikiana na wana ndugu.
Baada ya sala ya awali, alifika Mwinjilisti wa Kanisa Katoliki Ubungo, Michael Kobelo na kuanza kusali tena kwa mara ya pili huku akimshika Merlin kichwani na kumuombea.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kumalizika shughuli zote, Elida alisema kwa siku nane za kupotea mwanaye aliishi katika maisha magumu.
“Nimeishi katika wakati mgumu mno, sijawahi kupotelewa na mwanangu kiasi hiki…tumesali na kufunga siku zote nane ili Merlin apatikane akiwa katika afya njema.
“Hali ilikuwa mbaya nilisimamisha shughuli zangu zote hakuna aliyekuwa anakula chakula, familia nzima kwa kushirikiana na waumini wenzangu tulifunga novena ya siku tisa na leo (juzi) ni siku ya tano, tutaendelea mpaka zitakapoisha kwa sasa tutakuwa tunamuombea afya na kumuepusha mambo yote mabaya ambayo yataweza kumtokea baada ya hili,” alisema Elida.
Alisema familia kwa kushirikiana na waumini wa Kanisa Katoliki Changanyikeni, walikuwa na utaratibu wa kusali novena kila siku kuanzia saa 2:30 usiku.
Akisimulia kupatikana kwa mtoto wake, anasema: “Nilipigiwa simu na mume wangu ambaye naye alipigiwa na polisi kuwa mtoto amepatikana katika eneo la Tandale kwa Mtogole,” alisema Elida.
“Nilifurahi sana nilivyomuona mwanangu lakini alikuwa amechoka mno, kitu kingine nilichokikuta tofauti ni nywele, alikuwa na nywele fupi lakini sio hizi wamempunguza tena tofauti na ilivyokuwa mwanzo, nilimuuliza ulikuwa wapi akanijibu kuwa alikuwa kwa bibi,” alisema Elida.
Kuhusu Juma ambaye anadaiwa kumuiba mtoto huyo, Elida alisema aliwahi kufanya kazi katika moja ya biashara za mume wake zilizopo eneo la Mwenge.
Alisema Juma alimchukua Merlin na kumpeleka kwa mama aliyekuwa akiishi na mtoto huyo siku zote mpaka polisi walipofanikiwa kumuona.
“Mimi nimeshangaa sana, hivi watu wanaishi dunia gani nasikia uko Tandale muda wote aliokuwepo alikuwa anatoka nje na anacheza na watoto wenzie kama kawaida,” alisema Elida.
Elida alilimwagia sifa MTANZANIA kwa kuandika ukweli wa taarifa hiyo uliosaidia kupatikana kwa mwanaye.
Merlin azungumza
Merlin alipoulizwa na MTANZANIA alikuwa wapi alijibu hivi:
“Nilikuwa nakaa na bibi mbali, nilikuwa nakula chipsi na juisi wakati nipo kwa bibi,” alisema Merlin.

MTUHUMIWA
Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, zinasema mawasiliano ya simu ndiyo yaliyosaidia alipo mtuhumiwa.
Taarifa hizo zinasema siku ya tukio mawasiliano yalionyesha Juma alikuwa eneo la Changanyikeni na baadaye Tandale kwa Mtogole.
Baada ya hapo mawasiliano yalionyesha Juma alikuwa Manzese kabla ya kupiga simu ambayo ilionyesha yuko Magomeni.
Baada ya kutoka Magomeni, alielekea Mbagala na baadaye Tandika kabla ya kuanza safari ya kwenda Korogwe mkoani Tanga ambako alikamatwa.

MAJIRANI TANDALE
Baadhi ya majirani waliokuwa wanaishi na mama Mwanahamisi aliyekuwa akiishi na Merlin nyumbani kwake Tandale Kwamtogole, wamesema hawakuwa na taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake, mmoja wa wanafamilia ambaye ni mtoto wa dada wa mtuhumiwa alisema kipindi chote tangu Merlin alipopelekwa hawakuwa na taarifa yoyote kama ameibwa.
“Kwa kweli huyo mtoto tangu alipoletwa na Juma zimepita kama siku tano hivi na huyo kijana aliomba aishi hapa na sisi na baada ya siku tatu atakuja kumchukua ampeleke kwao Tanga.
“Alituambia Merlin ni mwanaye ambaye alimzaa nje ya ndoa, hivyo endapo angempeleka nyumbani kwake angeweza kusababisha ugomvi mkubwa na mkewe.
“Juma alikuwa anakuja mara moja moja wakati wa usiku kumjulia hali Merlin akiwa na mfuko wa chips, jambo ambalo lilisababisha tuamini ni mwanaye,” alisema.
Alisema siku ya tukio Amir alifika nyumbani kwao jioni akiwa na mtoto huyo na kumkabidhi kwa mama yao mdogo.
Alifafanua kuwa muda wote ambao Merlin alikuwapo nyumbani hapo, alikuwa mchangamfu kwa watu na watoto wenzake.
Alieleza Merlin alikuwa tofauti kimuonekano na watoto wengine wa mtaani hapo kwa kuwa yeye anaonekana kalelewa katika familia ya kifahari.
“Alikuwa tofauti sana na wenzake wakiwa wanacheza utaona kabisa yeye ametokea katika familia ya watu wanaojiweza, wakati mwingine katika maongezi na watoto wenzake alikuwa akisema kuwa anasoma Don Bosco,” alisema dada huyo.
MWENYEKITI
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtogole, Ramadhani Kabanga, alisema baada ya kupokea taarifa hizo jana jioni, alifanya uchunguzi na kubaini kuwa Juma alikuwa akiishi eneo hilo.
Alisema taarifa alizokuwa nazo ni kwamba, Juma aliamua kumuiba Merlin kwa sababu wazazi wa mtoto huyo walimdhulumu fedha zake wakati akiwafanyia kazi.
“Sijapata taarifa kamili kuwa ni kiasi gani cha fedha ambacho alikuwa anadai huyo kijana hadi ikafikia hatua ya kuamua kumchukua mtoto kinyemela wakati akijua ni

CHAMA CHA NGUMI ZA KULIPWA TPBC CHATOA MAFUNZO KWA MAREFARII

Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' kushoto akiwaelekeza baadhi ya marefarii waliojitokeza katika mafunzo hayo yaliyo andaliwa na chama cha ngumi za kulipwa TPBC yaliyoanza Ilala CCM Dar es salaam juzi na kumalizika jumamosi  hii .
Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' kulia akisisitiza jambo kwa wakati wa mafunzo hayo uku marefarii waliojitokeza wakimsikiliza kwa makini kutoka kushoto ni Kondo Nassoro, Sako Mtlya na Buchato Michael .
Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' akitoa maelekezo kwa mabondia na marefarii kabla ya kupigana wakati wa mafunzo kwa vitendo ya urefarii wa mchezo huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

BAADHI YA MAREFARII WALIOSHILIKI KATIKA KOZI HIYO KUTOKA KUSHOTO NI BUCHATO MICHAEL,PEMBE NDAVA,HAMISI KIMANGA,RAJABU MHAMILA 'SUPER D' ALLY BAKARI,Ayubu Tezikoma NA SAKO MTLYA

NDEGE YA SUNWIN IKIWA ANGANI NA ABIRIA 181 , NUSURA YATOKEE MENGINE




Tayari mpaka sasa abiria zaidi ya 300 wamepoteza maisha kwenye ajali tatu za ndege zilizotokea ndani ya wiki moja kuanzia wiki iliyopita ambazo ni ndege ya Malaysia, nyingine huko Taiwan na nyingine iliyoanguka Mali.


Matukio ya ndege yanaendelea kukaa kwenye wino wa vichwa vya habari baada ya hili jingine la ndege ya Sunwing ambayo ililazimika kukatisha safari na kurudi ilikotoka baada ya maneno ya kijana wa miaka 25 raia wa Canada kuongea na mhudumu wa ndege na kusema anataka kuilipua Canada.
 
Ndege hiyo iliyoruka saa 1 asubuhi siku ya Ijumaa July 25 2014 ikiwa na abiria 181 kutokea Toronto Canada kuelekea Panama City ambapo kijana huyu aliongea na Mhudumu aliekuwa anapita na kumwambia jinsi sigara zilivyo bei ghali nchini Canada na kwamba anaichukia nchi hiyo.

Baada ya hapo kijana huyu aliongea kwa kujiamini na kwa sauti ya msisitizo na ishara za mikono kwamba anataka kuilipua Canada.

Muda mfupi baada ya hiyo kauli Mhudumu wa ndege alitoa taarifa na ndege hiyo ikaamrishwa kugeuza kurudi ilikotoka wakati huo huo pia ikiwa inasindikizwa na ndege mbili za kivita zilizopewa amri kuifatilia zikiwa zinafaya mazoezi.

Baada ya kutua tu saa mbili na dakika 55 ikabidi Polisi waingie ndani wakiwa na silaha na kumchukua kijana huyu aitwae Ali Shahi na kuanza kumuhoji hapo hapo uwanja wa ndege ambapo alitarajiwa kupelekwa Mahakamani saa tatu kamili asubuhi.

Hata hivyo baada ya taarifa kuenea, baba wa huyu mtoto amejitokeza na kusema mwanae amekua na matatizo ya akili toka akiwa na umri wa miaka 16 hivyo alichosema hakuwa anamaanisha

MKURANGA KUTEKELEZA MIRADI YAKE, MWENGE WAZINDUA MIRADI YA BILIONI MOJA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au piga namba +255767869133. 
Mkimbiza mwenge kitaifa, Rachael Kassanda
Mkimbiza mwenge kitaifa, Rachael Kassanda, amezindua miradi 13 ya maendeleo, katika wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani, yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja .
Alizindua miradi hiyo katika kijiji cha Mkiu ikiwamo mnada na matenki ya maji katika kijiji cha Kiramba, katika shule ya msingi Kimanzichana na maabara katika shule ya sekondari Tambani.
Alisema lengo la kuizundua miradi hiyo ni kuwasaidia wananchi kupata maendeleo na kuwaongezea kipato.
Akiwahutubia wakazi hao aliwataka wajitokeze katika kuchangia maoni ya upatikanaji wa katiba mpya  ambayo itawasaidia kupata haki katika mambo mbalimbali yanyoizunguka jamii.
Alisema bila ya kujitokeza katika masuala ya katiba na kutoa maoni wanaweza kupata katiba ambayo italalamikiwa kutokana na kutokuwa na mahitaji yao.
Aliwataka vijana kujituma kwa kufanya kazi ambazo zitawaingizia vipato badala ya kujiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya.
Akizungumzia ugonjwa wa Ukimwi, Kassanda alisema kuwa hauna kinga na umeteketeza idadi kubwa ya vijana ambao ndiyo taifa la kesho na kuwataka vijana kutoshiriki ngono zembe na kujenga utamaduni wa kuangalia afya zao mara kwa mara.
Mkuu wa wilaya hiyo, Mercy Sila, ambaye aliupokea mwenge huo katika kijiji cha Njopeka ukitokea Rufiji, alisema lengo la kuzindua miradi hiyo ni njia mojawapo ya kutumiwa na wakazi wa wilaya hiyo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo, sambamba na kuwaongezea kipato.
Mwenge huo baada ya kuzindua miradi katika Wilaya hiyo, umekabidhiwa na Sila katika Wilaya ya Kisarawe.
CHANZO: NIPASHE

'PSPF' MFUKO WA PESHENI KWA WATUMISHI WA UMMA ,WATOA SEMINA KWA WASANII WA BONGO MOVIE

   Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu kushoto akisalimiana na msanii Rose Ndauka wakati wa semina iliyoandaliwa na mfuko huo kwa ajili ya kutoa elimu na kujiunga katika mfuko huo Dar es salaam juzi kulia ni msanii Ester Kiama picha na mpiga picha wetu
 Baadhi ya wasanii wakijadiliana jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na mfuko wa wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF'
  Mwigizaji na Mchekeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Bongo Movie Unity, Steven Mengere a.k.a 'Steve Nyerere' kushoto akizungumza wakati wa semina kwa ajili ya wasanii iliyoandaliwa na mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' juzi makao makuu ya mfuko huo Dar es salaam juzi picha na mpiga picha wetu
Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu kushoto akizungumza na wasanii Rose Ndauka wakati wa semina iliyoandaliwa na mfuko huo kwa ajili ya kutoa elimu na kujiunga katika mfuko huo Dar es salaam juzi kulia ni msanii Ester Kiama.

 Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu wa pili kushoto akizungumza na wasanii baada ya kufungua semina kwa ajili ya wasanii mbalimbali .
 
 Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Adam Mayingu kushoto akisalimiana na kocha wa timu ya simba msimu uliopita Jamuhuri Kiweru 
wakati wa semina iliyoandaliwa na mfuko huo kwa ajili ya kutoa elimu na kujiunga katika mfuko huo Dar es salaam juzi katikati ni Afisa Masoko wa mfuko huo Rahma Ngassa picha na mpigapicha wetu
BAADHI YA WATU WALIOHUDHULIA SEMINA HIYO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au Tupigie n amba +255767869133.

PSPF YAZAWADIA MADAWATI 90 KWA SHULE ZA TUNDURU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au namba +255767869133. 
Mfuko wa Pensheni kwa Umma (PSPF)
Mfuko wa Pensheni kwa Umma (PSPF) umetoa msaada wa madawati 90 yenye thamani ya shilingi milioni tano kwa ajili ya kusaidia kupunguza tatizo la madawati katika baadhi ya  shule za msingi za Wilaya ya Tunduru.
Akikabidhi msaada huo jana, Mwakilishi wa mfuko huo Mkoa wa Ruvuma, Deogratius Njuu, alisema, PSPF ni mdau mkubwa wa elimu wamegushwa na tatizo hilo hivyo wameona wasaidiane na halmashauri hiyo ili kupunguza tatizo hilo.
Njuu ameongeza kuwa, mfuko huo unaamini kuwa taifa lolote lenye maendeleo lazima libebwe na elimu na ndiyo maana nao wamepanga kusaidia katika kuinua kiwango cha elimu katika maendeleo mbali mbali nchini.
Aidha, amewashauri kuyatunza madawati hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu na kuwasaidia wanafunzi wote.
 
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Tunduru Kaskazini, Ramo Makani, amewapongeza PSPF kwa kutoa msaada huo kwa kuwa utasaidia kupunguza tatizo la  madawati na kuwataka wadau wengine watakao sikia waige mfano mzuri na bora  uliofanywa na mfuko huo.
 
Alisema, bado halmashauri inakabiliwa na changamoto nyingi kama upungufu wa madawati ambapo watoto wa shule za msingi wanakaa chini, upungufu wa matundu ya vyoo, meza, viti pamoja na miundombinu, hivyo amewaomba watu wenye uwezo wasaidiane na halmashauri kutatua matatizo hayo. 
 
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Kenneth Haule, alisema  kuwa halmashauri hiyo ina upungufu wa madawati 4537 ili kufanikisha utoaji elimu bora kwa watoto ni muhimu kuwapo kwa miundombinu na samani za kutosha zenye viwango kwa wanafunzi na walimu.
 
Alisema, wilaya hiyo inaupungufu mkubwa wa miundombinu na samani za kielimu vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, vyoo  pamoja na madawati ambapo jitihada kubwa za kupunguza tatizo hilo kwa kushirikiana na serikali kuu na jamii husika bado zinaendelea  kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi  wanaosajiliwa kila mwaka.
 
Aidha, alisema bado wilaya ina upungufu mkubwa wa samani za shule hivyo ameomba waendelee kusaidia kila wanapopata fursa ili kuendeleza sekta ya elimu nchini.
CHANZO: NIPASHE

SERIKALI HAINA MPANGO WA KUPUNGUZA MAFAO YA PENSIONI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au  namba +255767869133
 
Chama cha Walimu Tanzania (CWT)
 
Serikali imesema kuwa haina mpango wa kupunguza mafao ya pensheni kwa wanachama wa Mfuko ya Hifadhi ya Jamii na kwamba maamuzi yote yanayohusu mafao yao yanafanyika kwa uwazi.
 
Hivi karibuni Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) walitoa taarifa kupitia vyombo vya habari wakieleza kuwa serikali ina mpango wa kupunguza mafao ya pensheni ya wanachama wa mifuko ya LAPT na PSPF.
 
Tamko hilo la serikali lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kamishina wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamko lililotolewa na CWT pamoja na THTU na kueleza kuwa tuhuma hizo siyo za kweli kwani wanapotosha umma.
 
Alisema kuwa Wizara ya Kazi na Ajira ndiyo yenye dhamana ya sekta ya hifadhi ya jamii Tanzania na ndiyo maana wameamua kutolea ufafanuzi suala hilo ili jamii iweze kuelewa kwa kina dhidi ya upotoshaji huo.
 
"Wizara Kazi na Ajira inachukua nafasi hii kukanusha vikali taarifa zilizotolewa na CWT na THTU ambazo kwa namna moja au nyingine zinalenga katika upotoshaji," alisema
"Tunaomba wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii na umma kwa ujumla, uelewe wazi kuwa si SSRA wala serikali zimetoa tamko lolote kuhusiana na upunguzaji wa mafao ya pensheni kwa wanachama wa mifuko ya PSPF na LAPF," alisema Kinemela
 
Kinemela alisema kinachoendelea ni majadaliano ya wadau wa sekta ya hifadhi ya jamii yenye lengo la kuboresha mafao ya wastaafu. Hata hivyo, majadiliano hayo hakuna maamuzi wala tamko lolote lililotolewa kuhusiana na upunguzwaji wa mafao ya wanachama.
 
Hata hivyo, alisema CWT na THTU ni moja kati ya wadau wa sekta ya hifadhi ya jamii, wanayo haki kikatiba ya kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali  yakiwemo mifuko hiyo ya kijamii na siyo vizuri wakafanya upotoshaji kuhusu jambo hilo muhimu.
 
Alisema serikali inachukua fursa hiyo kuwatoa hofu wastaafu na wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii, hususani wale wa PSPF na LAPF na walimu wote kwa ujumla kuwa maamuzi yoyote kuhusiana na mafao yao yanafanyika kwa uwazi na kuwahusisha wadau wote.
CHANZO: NIPASHE

UTAFITI WAFICHUA MTANDAO WA WIZI UNAOFANYWA NA MAWAZIRI, WABUNGE NA MADIWANI KWA KUHUJUMU MALIASILI YA TANZANIA, WAZIRI NYALANDU ANAJISUMBUA ?.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.

Dar es Salaam. 
Wakati Serikali ikiahidi kuongeza nguvu vita dhidi ya watu wanaoharibu maliasili za taifa, utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa baadhi ya mawaziri, wabunge na madiwani wanahujumu nchi kwa kufanya biashara ya mazao ya misitu nchini.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa mawaziri wanafanya biashara hiyo kwa asilimia 39, watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama asilimia 61, maofisa misitu asilimia 43, wabunge asilimia 23, madiwani asilimia 72 na wakurugenzi watendaji kwa asilimia 25.

Ripoti ya Kitengo cha Udhibiti na Utafiti katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iliyotolewa hivi karibuni na kuwekwa kwenye tovuti, inasema kuwa mawaziri wanajihusisha zaidi na biashara ya magogo na mbao kwa asilimia 12.5, mkaa asilimia 6.3, milango na madirisha asilimia 5.1 na vinyago asilimia 2.1.

Wabunge wanafanya biashara ya magogo kwa asilimia 2.1, mbao asilimia 8.3, mkaa asilimia 8.2, milango na madirisha asilimia 2.1 na vinyago asilimia 2.2. Madiwani na asilimia zao kwenye mabano kama ifuatavyo, magogo (2.1), mbao (16.7), mkaa (33.3), milango na madirisha (16.7) na vinyago (2.3).

Wakurugenzi watendaji wanafanya biashara ya magogo kwa asilimia 3.5, mbao asilimia 8.3, mkaa asilimia 4.2, milango na madirisha asilimia 6.3 na vinyago kwa asilimia 2.1.

“Imeelezwa na waliohojiwa kuwa baadhi ya askari polisi wasio na maadili wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa na kuwaachia watuhumiwa badala ya kuwakamata na kuwakabidhi kwa maofisa misitu kwa hatua za kisheria au kuwafikisha mahakamani,” inaeleza ripoti hiyo.

Ripoti hiyo iliyowahoji watu 776 katika mikoa 10 ya Tanzania Bara, inaeleza kuwa pamoja na kwamba sheria ya misitu haijakataza wanasiasa, watumishi wa sekta ya misitu na watumishi wengine wa umma kushiriki katika biashara ya mazao ya misitu, ushiriki wao unasababisha migongano ya kimaslahi huku rushwa ikishika asilimia 63.4.

Pia, inaeleza kuwa upungufu mkubwa wa watumishi na vitendea kazi katika sekta ya misitu umeathiri usimamizi endelevu wa rasilimali ya misitu nchini huku asilimia 82 ya watu waliohojiwa walisema uvunaji haramu wa mazao ya misitu unachochea biashara hiyo.

Vilevile, imebainika kuwa asilimia 71.9 ya misitu inavunwa bila vibali, huku maeneo yasiyoruhusiwa ni asilimia 70.3, uvunaji wa miti isiyokomaa asilimia 73.4 na miti inayozidi kiasi kilichopangwa kuvunwa asilimia 67.2.

Mikoa ya Kigoma, Pwani, Ruvuma na Tabora imetajwa kukithiri wa uvunaji haramu wa misitu ya asili. Asilimia 73.7 ya mazao ya misitu yamesafirishwa kwa njia za panya na matumizi ya kibali kimoja cha kusafirishia zaidi ya mara moja kwa asilimia 64.4.

Utafiti huo unaeleza kuwa asilimia 56 ya mazao ya misitu husafirishwa ndani au nje ya nchi. Kutokana na sababu hizo, inakadiriwa kuwa, nchi inapoteza hekta 403,000 kila mwaka.

Mikoa 10 iliyofanyiwa utafiti ilikidhi vigezo vya uwepo wa misitu ya asili na misitu ya miti ya kupandwa katika mashamba ya Serikali kwa wingi ukilinganishwa na mikoa mingine. Mikoa inayoongoza kwa usafirishaji wa mazao ya misitu kinyume na sheria ni Kigoma, Pwani, Ruvuma na Lindi.

Waziri azungumza.
Akizungumzia ripoti hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema viongozi wanaojihusisha na biashara hiyo wanajiingiza kwenye mgogoro wa kimaslahi, jambo linalowafanya washindwe kuwajibika ipasavyo.
Alisema zipo sheria na taratibu zitakazotumika iwapo watendaji hao watabainika kufanya makosa.

“Ripoti ya Takukuru itakuwa sahihi kwa sababu wao ni wataalamu. Sikatai kuwa wapo wanaoweza kuwa wamehusika, kama wamekiuka kanuni na taratibu za kazi watachukuliwa hatua,” alisema.

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Ester Bulaya alisema hivi sasa dunia inazungumzia kupunguza uharibifu wa mazingira kwa kuhifadhi misitu, kwa hiyo ni jambo la kushangaza kusikia kundi fulani la viongozi linaongoza kwa kufanyabiashara ya mkaa.

Pia, alisema wananchi wanaposikia viongozi wao wanajihusisha na biashara, hata kama ni halali wanajiona wanyonge kwa sababu wanaamini madaraka yanatumika kufanikisha shughuli hiyo.

Mfanyabiashara wa mkaa katika Mtaa wa Bojonga, Kijichi, Mwanahamisi Kondo alisema ripoti hiyo inatoa majibu ya maswali ambayo wananchi wamekuwa wakijiuliza kwa nini kuna watu wanasafirisha mkaa bila ya vibali na hakuna kiongozi anayewasumbua.

“Kuna msimu ambao vibali vyote vya kusafirisha mkaa hufungwa, lakini kitu cha kushangaza utakuta wenzetu wanaendelea na biashara wakati sisi tumezuiwa. Hii inaonyesha kuwa wakubwa wanahusika,” alisema.MWANANCHI

Rais Kikwete afungua ujenzi wa barabara Tunduru - Mangaka matemanga,pia azindua mradi wa maji Nalasi -Tunduru

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) na balozi mdogo wa Japan nchini Kazuyoshi Matsunaga (wa tatu kushoto) wakishirikiana kukata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Tunduru-Mangaka Matemanga mradi unaojengwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa serikali ya Japan kupitia shirika lake la kimataifa la maendeleo JICA.Wengine pichani toka kushoto ni ni Mbunge wa Nanyumbu Dunstan Mkapa,Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Kapten Mstaafu Joseph Simbakalia,Waziri wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Wairi wa Ardhi nyumba na mendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa TAMISEMI,Hawa Ghasia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza balozi mdogo wa Japan Kazuyoshi Matsunaga muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Tunduru-Mangaka Matemanga mradi unaojengwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa serikali ya Japan kupitia shirika lake la kimataifa la maendeleo JICA.Kushoto ni mbunge wa Nanyumbu Dunstan Mkapa, wapili kushoto ni Waziri wa ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kulia ni Wairi wa Ardhi nyumba na mendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua maji katika kisima kuashiria kuzindua rasmi mradi wa maji katika kata ya Nalasi wilayani Tunduru.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Chande Bakari Nalicho,Wapili kulia anayepiga makofi ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu na kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata ya Nalasi Rehema Kassim Yakubu wakati alipokwenda kuzindua mradi wa maji katika kata hiyo iliyopo katika wilaya Tunduru leo.(picha na Freddy Maro)